KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, January 3, 2013

SAJUKI KUZIKWA KESHO DAR


MAZISHI ya msanii mahiri wa tasnia ya filamu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ yanatarajiwa kufanyika kesho (Ijumaa) mchana katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba amesema leo kuwa mazishi hayo yatasimamiwa na shirikisho hilo na wadau wa tasnia ya filamu

“Tumeamua kulichukua jukumu la kumzika msanii mwenzetu Sajuki na familia wabaki na shughuli nyingine kwa sababu amemwacha mke na mtoto, ambao kwa vyovyote watahitaji kuishi kwa hiyo kama kuna kidogo basi kiwasaidie, kwa hiyo tayari kuna kamati inayoshughulikia hilo,”amesema Mwakifwamba.

Rais wa TAFF alimedai kuwa bajeti ya awali kuanzia leo hadi siku ya mazishi gharama au fedha inayohitajika ni milioni saba, ambazo wadau mbalimbali na wasanii bado michango inahitajika hivyo amewaomba wanaoguswa na msanii huyo hata kama si wasanii, wafike msibani na kuwakilisha michango hiyo.

No comments:

Post a Comment