KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, July 31, 2014

AZAM ACADEMY BINGWA KOMBE LA ROLLINGSTONE



AZAM FC imetwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa nchi za Maziwa Makuu, maarufu kama Rollingston baada ya kuichapa timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ya Mgulani Twalipo bao 2-0 katika fainali jioni hii Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Jamil Mchaulu ‘Balotelli’ aliyefunga bao la kwanza dakika ya tatu, baada ya kuwatoka vizuri beki wa kulia wa Twalipo, Ally Mbonde na beki wa kati Ally Athumani kisha kumtungua kipa wao, Kulwa Baumba.


Twalipo ilipoteza mwelekeo mapema tu baada ya bao hilo, na wachezaji wake kuanza kucheza rafu nyingi, badala ya kutengeneza mipangop ya kusawazisha bao.

Azam walitumia mwanya huo kucheza mpira wa kuachiana pasi za haraka uwanjani kuwakwepa ‘wapiga kiatu’ wa jeshini na kufanikiwa kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa wanaongoza 1-0.

Kipindi cha pili, mchezo ulizidi kunoga, Twalipo wakisaka bao la kusawazisha na Azam wakitafuta mabao zaidi- hali iliyosababisha mashambulizi ya pande zote mbili.

Alikuwa ni Adam Omar Soba aliyeihakikishia Kombe la kwanza la Rollingston Azam FC baada ya kufunga bao la pili dakika ya 88.

Katika mchezo wa kwanza wa kuwsaka mshindi wa tatu, Champion ya Kawe ilitwaa ubingwa wa U17 kwa kuifunga Bom Bom ya Ilala kwenye Uwanja huo huo, Karume.

TAIFA STARS YAENDA AFRIKA KUSINI



Msafara wa watu 27 wa kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kimeondoka nchini juzi saa 10 jioni kwa ndege ya Air Tanzania kwenda Afrika Kusini ambapo kitapiga kambi ya siku mbili kabla ya kuingia Maputo kuikabili Msumbiji (Mambas).

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iliwasili Afrika Kusini saa 9 asubuhi jana kwa ndege ya Fastjet, na baadaye jioni kuunganisha safari ya Afrika Kusini.

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itachezwa Agosti 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa uliopo Zimpeto nje kidogo ya Jiji la Maputo.

Msafara huo wa Taifa Stars kwenda Afrika Kusini unajumuisha wachezaji 19 na waliobaki ni maofisa wa Benchi la Ufundi lililo chini ya Kocha Mkuu Mart Nooij kutoka Uholanzi.

Wakati kiungo Mwinyi Kazimoto ametua leo (Julai 29 mwaka huu) nchini kuungana na wenzake, washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wao wataungana na wenzao kesho (Julai 30 mwaka huu) jijini Johannesburg wakitokea Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Wakati huo huo, Serengeti Boys imewasili salama jana (Julai 28 mwaka huu) jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 dhidi Afrika Kusini (Amajimbos).

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto kuanzia saa 9 kamili mchana kwa saa za Afrika Kusini.

Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Serengeti Boys inahitaji ushindi kwenye mechi hiyo au aina yoyote ya sare ya mabao ili ifuzu kwa raundi ya tatu.

Monday, July 28, 2014

MANJI AUNDA KAMATI MPYA YA UTENDAJI YANGA, AMUINGIZA KUNDINI TARIMBA ABBASI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

1. Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Sports Club (YANGA) kwa
mamlaka waliyopewa na Wanachama,kubadilisha, kupunguza au kuongeza Mjumbe yeyote kwenye
Kamati ya Utendaji wakati wowote,kulingana na changamoto wanazoziona zinazoikabili Klabu ya
YANGA, Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa YANGA wanapenda kutoa taarifa rasmi, kuwa
Kamati ya Utendaji ya YANGA na Kamati zote ambazo ziko chini ya Kamati ya Utendaji zitavunjwa
kuanzia tarehe 31 Julai, 2014.

2.Vile vile, Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa YANGA wanapenda kuwashukuru Wajumbe wote
wa Kamati ya Utendaji ya YANGA kwa juhudi zao za kutekeleza shughuli za Klabu.

3. Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Klabu ya YANGA Bw.Yusuf Manji na naibu wake Bw.Clement

Sanga wanatangaza Kamati ya Utendaji mpya ya Young Africans Sports Club ambayo itakuwa
madarakani kuanzia 1 Agosti, 2014 kama inavyoelezwa na kila Mjumbe anavyotajwa hapo chini anakuwa
na majukumu ya msingi ya kusimamia kama inavyoonyeshwa pembeni ya jina lake.

WAJUMBE WAPYA WA KAMATI YA UTENDAJI YA YANGA NI HAWA WAFUATAO:
1.Bw.Abubakar Rajabu - Mradi wa Jangwani City
2.Bw.Sam Mapande - Sheria na Utawala Bora
3.Bw.George Fumbuka - Uundwaji wa Shirika
4.Bw.Waziri Barnabas - Vibali vya Hatimiliki na Mahusiano na Wafadhili
5.Bw.Abbas Tarimba - Mipango na Uratibu
6.Bw.Isaac Chanji na Bw.Seif Ahmed - Uendelezaji wa Mchezo
7.Bw.Musa Katabalo - Mauzo ya Bidhaa
8.Bw.Mohammed Bhinda - Ustawishaji wa Matawi
9.Bw.David Ndeketela Sekione - Uongezaji wa Wanachama
10.Bw.Mohammed Nyenge - Utangazaji wa Habari, Taarifa, Matangazo n.k.

WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI ILIYOUNDWA UPYA WATASIMAMIA KIMSINGI
KAMATI NDOGO ZIFUATAZO:
•Kamati ya Maadili - Bw.Sam Mapande
•Kamati ya Nidhamu - Bw.Sam Mapande
•Kamati ya Uchaguzi - Bw. Sam Mapande
•Kamati ya Uchumi na Fedha - Bw.George Fumbuka na Bw.Waziri Barnabas
•Kamati ya Mashindano - Bw.Seif Ahmed & Bw.Isaac Chanji
•Kamati ya Soka la Vijana na Wanawake - Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac Chanji
•Kamati ya Ufundi - Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac Chanji

5. Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa YANGA wanamategemeo makubwa kuwa waliotajwa hapo
juu watahakikisha wana timiza malengo yaliyokusudiwa na YANGA ili“DAIMA MBELE, NYUMA
MWIKO” mpaka hapo itakapoamuliwa kubadilishwa au kutenguliwa vinginevyo.

6. Mwisho,tunawaomba ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha kuwa YANGA inapiga hatua mbele na
inafanikiwa katika kufikia malengo na mipango yake ya maendeleo ya muda mfupi na ya muda mrefu
kwa manufaa ya Klabu, Timu na wana YANGA popote walipo duniani.

“MUNGU AIBARIKI YANGA.”
(BENO NJOVU)
KATIBU MKUU- YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB.

AZAM YATINGA FAINALI KOMBE LA ROLLINGSTONE,YAWATOA WABABE WA YANGA




AZAM FC imeingia fainali ya michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa nchi za Maziwa Makuu, maarufu kama Rollingston baada ya kuifunga mabao 2-0 EMIMA, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.


Kwa matokeo hayo, Azam FC iliyoitoa Simba SC katika Robo Fainali, itakutana na Twalipo katika fainali ya timu za Manispaa ya Temeke tupu kesho Chamazi.

EMIMA iliyoitoa Yanga SC katika hatua ya 16 Bora na Mwambao ya Bagamoyo mkoani Pwani katika Robo Fainali, leo ilimalizwa mapema tu kipindi cha kwanza na Azam FC.

Jamil Mchaulu ‘Balotelli’ ndiye aliyeifungisha virago timu hiyo ya Tabata kwa mabao yake dakika za 18 na 44 na kufikisha jumla ya mabao matatu katika mashindano haya.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Mcameroon Joseph Marius Omog kama kawaida yake alikuwepo uwanjani kuangalia vipaji vya akademi na baada ya mechi akasema; “Nina furaha, huu ni msingi mzuri kwetu, vipaji na uwezo katika akademi, inafurahisha sana,”alisema Omog.

Mapema katika Nusu Fainali ya kwanza, Twalipo iliitoa Ashanti United ya Ilala kwa bao 1-0, Uwanja huo huo wa Azam Complex.

Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika bila bao na ilibaki moja tu kutimia dakika 30 za nyongeza mchezo uhamie kwenye penalti kuamua mshindi, lakini Suleiman Bofu akamaliza kazi.

Mshambuliaji huyo hatari alimalizia shambulizi la kushitukiza kuipatia bao lililoipeleka fainali Twalipo.

EMIMA na Ashanti zitamenyana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu pia kesho Chamazi.

AZAM YAITOA SIMBA KOMBE LA ROLLINGSTONE



AZAM FC imetinga Nusu Fainali ya michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa nchi za Maziwa Makuu, Rollingston baada ya kuitoa Simba SC, zote za Tanzania kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.


Makocha wakuu wa vikosi vya kwanza vya timu hizo za Dar es Salaam, Mcameroon Joseph Marius Omog wa Azam ya Chamazi na Mcroatia Zdravko Logarusic wa Simba ya Msimbazi wote walikuwepo kushuhudia mchezo huo.

Shujaa wa Azam FC alikuwa ni kipa wao, Hamad Juma aliyepangua penalti mbili za wachezaji wa Simba SC, Dadi Yunus na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wakati penalti ya Haruna Abdallah iliota mbawa.

Waliofunga penalti za Simba SC ni Ibrahim Hajibu na Omary Hussein wakati penalti za Azam zilifungwa na Kassim Kisengo, Reyna Mngungila na Adam Omar.

Kipa wa timu ya taifa ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Peter Manyika alipangua penalti mbili pia za Shirazy Abdallah na Masoud Abdallah, lakini akaangushwa na wachezaji wake waliokosa penalti.

Kipa wa Azam FC, Hamad Juma alichomoka kwa shangwe baada ya kupangua mkwaju wa mwisho wa Tshabalala aliyesajiliwa kwa ajili ya kikosi cha kwanza cha Simba SC kutoka Kagera Sugar msimu huu.

Peter Manyika aliyefanya kazi nzuri ya kuokoa michomo mingi ya hatari ndani ya dakika 90 na akaenda kucheza penalti mbili baadaye aliangua kilio baada ya mchezo huo.

Kwa ujumla mchezo ulikuwa mzuri na timu zote zilishambuliana kwa zamu, huki wachezaji wakionyesha vipaji vya hali ya juu. Kwa kutolewa, Simba SC imeungana na watani wao, Yanga SC ambao jana walitolewa katika hatua ya 16 Bora. Nusu Fainali zinatarajiwa kuchezwa kesho.

Sunday, July 27, 2014

SERENGETI BOYS KWENDA AFRIKA KUSINI KESHO



Msafara wa watu 25 wa kikosi cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) unaondoka kesho (Julai 28 mwaka huu) kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos).

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto, Johannesburg kuanzia saa 9 kamili mchana kwa saa za Afrika Kusini.

Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Mshindi atacheza raundi ya mwisho ya michuano hiyo ya Afrika na mshindi wa mechi kati ya Misri na Congo Brazzaville.

Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitafanyika mwakani nchini Niger.

Wachezaji wanaounda kikosi cha Serengeti Boys katika msafara huo utakaoondoka saa 2 usiku kwa ndege ya Fastjet ni Abdallah Jumanne Shimba, Abdulrasul Tahil Bitebo, Abutwalibu Hamidu Msheri, Adolf Mtsigwa Bitegeko, Ally Aziz Mnasi, Ally Shaban Mabuyu na Athanas Enemias Mdamu.

Wengine ni Badru Haji Othman, Baraka Yusuph Baraka, Issa Backy Athuman, Juma Ally Yusuph, Kelvin Longnus Faru, Martin Kiggi Luseke, Metacha Boniface Mnata, Mohamed Mussa Abdallah, Omary Ame Omary, Omary Natalis Wayne, Prospal Alloyce Mushin na Seif Said Seif.

Benchi la Ufundi linaongozwa na Kocha Mkuu Hababuu Ally Omary akisaidiwa na Stewart John Hall (Mshauri wa Ufundi), Peter Manyika (Kocha wa makipa), Richard Yomba (Daktari), na Edward Venance (Mtunza vifaa).

Msafara wa timu hiyo itakayorejea nyumbani Agosti 4 mwaka huu unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Khalid Mohamed Abdallah.

Wednesday, July 23, 2014

JAMES RODRIGUEZ ATAMBULISHWA RASMI REAL MADRID




 
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Colombia, James Rodriguez, juzi alitambulishwa rasmi na klabu yake mpya ya Real Madrid ya Hispania.

James amemwaga wino wa kuichezea Real Madrid kwa miaka sita na uhamisho wake umeigharimu klabu hiyo pauni milioni 60 za Uingereza na kuwa mchezaji ghali wa nne duniani.

Maelfu ya mashabiki wa Real Madrid walifurika kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu wakati nyota huyo wa Kombe la Dunia alipokuwa akitambulishwa na Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez.

Utambulisho huo uliingia doa baada ya shabiki mmoja, anayesadikiwa kuwa ni kutoka Colombia, alipovamia ndani ya uwanja na kwenda moja kwa moja kumkumbatia James kabla ya kutolewa na polisi.

Rekodi ya mchezaji ghali duniani kwa sasa inashikiliwa na Gareth Bale, ambaye uhamisho wake uliigharimu Real Madrid pauni milioni 80, akifuatiwa na Cristiano Ronaldo, aliyenunuliwa pia kwa pauni milioni 80. Luis Suarez anashika nafasi ya tatu kutokana na uhamisho wake kuigharimu Barcelona pauni milioni 75.

Real Madrid imemuhamisha James kutoka Monaco ya Ufaransa. Wakati wa utambulisho wake, Perez alimpeleka mchezaji huyo kwa nyota wa zamani wa klabu hiyo, Alfredo Di Stefano, ambaye pia alihamishwa kutoka Colombia.

WACHEZAJI 10 GHALI DUNIANI
£80m - Gareth Bale (Tottenham to Real Madrid)
£80m - Cristiano Ronaldo (Manchester United to Real Madrid)
£75m - Luis Suarez (Liverpool to Barcelona)
£60m - James Rodriguez (Monaco to Real Madrid)
£59m - Zlatan Ibrahimovic (Inter Milan to Barcelona)
£56m - Kaka (AC Milan to Real Madrid)
£55m - Edinson Cavani (Napoli to PSG)
£51m - Radamel Falcao (Atletico Madrid to Monaco)
£50m - Fernando Torres (Liverpool to Chelsea)
£50m - David Luiz (Chelsea to PSG)

YANGA KUFUNGUA DIMBA NA RAYON KOMBE LA KAGAME


YANGA imepangwa kufungua dimba la michuano ya soka ya Kombe la Kagame kwa kumenyana na wenyeji, Rayon Sports kwenye dimba la Amahoro mjini Kigali.


Ratiba ya michuano hiyo iliyotolewa juzi na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), inaonyesha kuwa mechi hiyo itapigwa Agosti 8 mwaka huu.

Wawakilishi hao wa Tanzania Bara wamepangwa kundi A pamoja na timu za Rayon, Coffee ya Ethiopia, Atlabara ya Sudan Kusini na KMKM ya Zanzibar.

Kundi B litakuwa na timu za APR ya Rwanda, KCC ya Uganda, Flambeau Del Est ya Burundi, Telecom ya Djibouti na Gor Mahia ya Kenya.

Timu zilizopangwa kundi C ni Vital'O ya Burundi, El Merreikh ya Sudan, Police ya Rwanda na Banadir ya Ethiopia.

Kwa mujibu wa ratiba, mbali na mechi ya ufunguzi kati ya Yanga na Rayon, mechi zingine za ufunguzi zitazikutanisha Atlabara na KMKM na kati ya Gor Mahia na KCC.

DIARA AONGOZA KWA MABAO AZAM


MSHAMBULIAJI Ismaila Diara kutoka Mali ameendelea kufanya vizuri zaidi ya wachezaji wenzake wapya wa kigeni kwa kufunga mabao Azam FC.

Azam FC imesajili washambuliaji wapya watatu wa kigeni, Didier Kavumbangu kutoka Burundi, Leonel Saint-Ptreux kutoka Haiti na Diara wanaoungana na Kipre Herman Tchetche wa Ivory Coast, kinara wa mabao wa timu hiyo kwa misimu miwili iliyopita.

Diara jana alifikisha jumla ya mabao matatu aliyoifungia Azam FC katika michezo mitatu ya kujipima nguvu aliyoichezea akifunga bao moja katika ushindi wa 2-1 dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza, Friends Rangers.

Bao lingine la Azam FC, lilifungwa na Gaudence Mwaikimba wakati bao la kufutia machozi la Rangers lilifungwa na Yussuf Mgwao.

Awali, Diara aliifungia Azam FC mabao mawili katika ushindi wa 3-2 dhidi ya kombaini ya Jeshi, bao lingine likifungwa na Mudathir Yahya.

Leonel ana bao moja tu alilofunga dhidi ya Polisi Morogoro katika ushindi wa 1-0, wakati Kavumbangu ana bao moja pia alilofunga katika ushindi wa 2-1 dhidi ya JKT Ruvu, bao lingine likifungwa na Kipre Tchetche.

Azam FC leo itaendelea na mazoezi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wakati kesho itacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja huo.

VODACOM KUDHAMINI ZIARA YA ZIARA YA REAL MADRID


VODACOM Tanzania ni miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza kudhamini ziara kikosi cha wachezaji nyota waliowahi kutamba Real Madrid ya Hispania, maarufu kama Real Madird Legends ambao watazuru nchini mwezi ujao.


Meneja ziara ya magwiji wa Real Madrid, Dennis Ssebo amewaambia Waandishi wa Habari asubuhi ya leo katika hoteli ya New Africa, Dar es Salaam kwamba, mbali na Vodacom, wadhamini wengine wa ziara hiyo ni Fastjet, Tropical, Pembe Flower, Lake Gas, EFM Radio na Ladger Plaza Bahari Beach.

Wachezaji waliotamba kuanzia La Liga, wakacheza ligi nyingine za Ulaya, Kombe la Ulaya, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia waliowahi kuchezea Madrid watakuja nchini Agosti 22.

Katika ziara hiyo, pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi maalum cha wachezaji nyota wa Tanzania, pia watafanya utalii katika vivutio mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro.

Real Madrid inakuja nchini kwa mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Farough Baghozah.

Miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kuja na Real nchini ni pamoja na Wanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Mfaransa Zinadine Zidane, Mreno Luis Figo na Mbrazil, Ronaldo Lima.

Magwiji hao wa Real tayari wamekwishafanya matangazo ya ziara yao nchini wakisema wana hamu mno ya kukanyaga ardhi ya Tanzania.

LOGA AMWAGA WINO SIMBA MIAKA MIWILI


KOCHA Mkuu wa Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic amesaini Mkataba mpya wa mwaka mmoja na kusema kwamba timu hiyo itakuwa bora msimu ujao, ubingwa wa Ligi Kuu ikiwa lengo la kwanza.


Akizungumza makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi baada ya kusaini Mkataba huo, kocha huyo wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya amesema kwamba amefurahi kusaini kandarasi mpya na sasa anaelekeza nguvu zake kwenye kazi.

Loga amesema Simba SC itakuwa timu bora msimu ujao na lengo lake kuu ni kuhakikisha inatwaa ubingwa.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliyesaini Mkataba na kocha huyo amesema kwamba sasa msalaba mkubwa wa Loga ni kuhakikisa Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu msimu ujao linatua Msimbazi.

Kaburu pia amesema Kocha Msadizi, Suleiman Matola ‘Bin Laden’ naye alisaini Mkataba wa miaka miwili tangu Novemba mwaka jana.

Loga alijiunga na Simba SC Desemba mwaka jana kwa Mkataba wa miezi sita, lakini uongozi wa klabu hiyo umeridhishwa na kazi yake na kumuongeza mwaka mmoja mwingine.

Tuesday, July 22, 2014

USAJILI LIGI KUU WAONGEZWA KWA WIKI MBILI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza muda wa usajili kwa wiki mbili ili kuzipa klabu nafasi ya kukamilisha taratibu zinazotakiwa. Hivyo hatua ya kwanza ya usajili inakamilika Agosti 17 mwaka huu badala ya Agosti 3 ya awali.

Kutokana na marekebisho hayo, kipindi cha uhamisho kinakamilika Agosti 17 mwaka huu wakati pingamizi itakuwa kati ya Agosti 19 hadi 26 mwaka huu.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itathibitisha usajili kati ya Septemba 1 na 2 mwaka huu.

Uhamisho wa kimataifa, usajili wa wachezaji huru, na utatuzi wa dosari za usajili unatakiwa uwe umekamilika kufikia Septemba 7 mwaka huu. Uthibitisho wa hatua ya mwisho ya usajili utafanywa Septemba 15 mwaka huu.

Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015 itaanza Septemba 20 mwaka huu, na ratiba itatolewa mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi hiyo.

TAIFA STARS KUWEKA KAMBI MBEYA NA AFRIKA KUSINI



Kikosi cha Taifa Stars kinatarajia kuondoka keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Mbeya ambapo kitapiga kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Msumbiji.

Mechi hiyo ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco itafanyika wikiendi ya Agosti 2 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka nchini Julai 31 mwaka huu kwenda Johannesburg, Afrika Kusini ambapo itafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kutua Maputo kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto.

…MECHI YAINGIZA SHILINGI MILIONI 158
Mechi ya michuano ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas) iliyochezwa juzi (Julai 20 mwaka huu) imeingiza sh. 158,350,000 kutokana na washabiki 19,684 walioingia kwa kiingilio cha sh. 7,000 na sh. 30,000.

Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 24,155,084.75, gharama za tiketi (MaxMalipo) sh. 19,684,000, gharama za mchezo sh. 22,902,183, uwanja sh. 11,451,092, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 5,725,546 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 74,432,095.

Tunawashukuru washabiki wote waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa kuishangilia Taifa Stars katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

STEVEN GERRARD ATANGAZA KUSTAAFU SOKA YA KIMATAIFA



Asema Beckham, Rooney na Terry walikuwa wachezaji bora aliowahi kucheza nao England.
Asema alicheza na wachezaji wenye kiwango cha juu kwenye kikosi cha England
Awataja Beckham, Rooney, Terry, Lampard na Scholes kuwa ni wachezaji aliokuwa akipenda kuchati nao kwenye chumba cha wachezaji
Nahodha huyo wa Liverpool alisema Beckham, aliyestaafu soka 2013, alimsaidia kufikia uamuzi wa kustaafu soka ya kimataifa.
Asema Kocha Roy Hodgson alimruhusu kutimiza ndoto aliyokuwa nayo tangu akiwa mdogo ya kuvaa kitambaa cha unahodha wa England
Ameuelezea uamuzi wake wa kustaafu soka ya kimataifa kuwa ulikuwa mgumu katika maisha yake kisoka
Gerrard asema kwa sasa akili yake ipo kwenye klabu ya Liverpool, kuliko kujiunga na klabu nyingine
Tayari Gerrard anayo leseni ya ukocha na sasa anapigania kupata daraja C
Ana hakika atafanya tena kazi kwenye kikosi cha England katika miaka kati ya 20 hadi 40 ijayo.




Monday, July 21, 2014

TFF YAIOMBA AIRTEL KUDHAMINI UNDER 20




Meneja Mutukio wa Airtel Tanzania Rebeca Mauma akizungumza wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya washiriki wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars wakifutilia kwa makini moja ya mada zilizowasilishwa kwenye semina hiyo iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa akisisitiza jambo wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiteta na Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi na Mwenyekiti wa DRFA Almasi Kasongo.


Katibu Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Selestine Mwesigwa amesisitiza umuhimu wa programu za vijana kwa maendeleo ya soka nchini na kuitaka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kuangalia uwezekano wa kuwa wadhamini wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20.

Akifungua semina elekezi kwa makatibu wakuu wa mikoa inayoshiriki mashindano ya vijana ya Airtel Rising Stars (ARS) iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi Julai 19, 2014 Mwesigwa alisema hali halisi inaonyesha kwamba miaka michache ijayo wachezaji wengi watakaounda timu ya taifa ya U-20 watatokana na ARS hivyo ni vema kampuni ya Airtel ikawa mdhamini mkuu wa timu hiyo.

Alisema kuwa suala la programu za vijana ni agenda namba moja ya TFF na kuzitaka timu za ligi kuu kuzingatia maagizo ya shirikisho hilo la kuwa na timu za vijana. “Klabu ya Simba imefanikiwa sana katika suala hili na ni vema timu nyingine za ligi kuu zikaiga mfano huo”, alisema Mwesigwa na kuipongeza Airtel kwa kuwekeza katika soka la vijana.

“Wachezaji wanapolelewa na klabu tangu wakiwa wadogo inakuwa ni rahisi kwao kuendana na maadili ya klabu hiyvo kuwa na wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu tofauti na wachezaji waosajiliwa kutoka sehemu mbali mbali wakiwa na umri mkubwa”, alisema.

Aliwataka makatibu hao wa mikoa kuzingatia kanuni ikiwa ni pamoja na umri ili kuwafanya vijana watakaoshiriki mashindano ya Airtel Rising Stars kuwa na ushindani ulio sawa. Mashindano ya ARS yanashirikisha vijana chini ya umri wa miaka 17.

Mwesigwa aliungwa mkono na Mwenyekiti wa kamati ya vijana ya TFF Ayoub Nyenzi aliyesema kuwa programu za vijana e.g. ARS ndiyo mkombozi wa kweli wa soka popete pale duniani.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika ngazi ya mkoa Julai 27 na kushirikisha mikoa ya Mbeya, Morogoro, Mwanza, Ilala, Kinondoni na Temeke kwa upande wa wavulana huku timu za wasichana zikitoka mikoa ya Mwanza, Mbeya, Zanzibar, Ilala, Kinondoni na Temeke.

Akiongea katika semina hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando aliwapongeza viongozi wa mikoa kwa kazi nzuri iliyoiwezesha Tanzania kutwaa ubingwa wa mashindano ya kimataifa ya ARS (wasichana) yaliyofanyika Nigeria na kuzawadiwa USD 10,000, medali na vikombe.

“Vile vile timu ya wavulana ilifanya vizuri sana na ni imani yangu kwamba mwaka huu Tanzania itashinda vikombe kwa wasichana na wavulana”, alisema na kusisitiza nia thabiti ya Airtel kuendelea kuboresha mashindano hayo.

Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi aliwataka makatibu hao kufanyakazi kwa karibu na kamati ya vijana ya TFF inayosimamia mashindano hayo

MISS KANDA YA MASHARIKI AGOSTI 8 MORO



Mashindano ya kumsaka mrembo kanda ya Mashariki ( Redds Miss Eastern Zone 2014) yatafanyika siku ya sikukuu ya Nanenane kwanue ukumbi wa Nashera Hotel, mkoani Morogoro.

Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14 kutoka mikoa minne ambayo ni Pwani, Lindi, Mtwara na mwenyeji, Mkoa wa Morogoro chini ya udhamini wa Redds Original, Zanzi Cream Liquer, Pepsi, Usambara Safari Lodge, Kitwe General Traders, Starwing Lodge, Nashera Hotel, CXC Africa, Sykes Travel, Sasa Saloon, Grand Villa Hotel, Shabibi Line na Clouds FM.

Mratibu wa masindano hayo, Alex Nikitas aliwataja warembo watakaoshindana siku hiyo kuwa ni Lucy Julius Diu, Prisca Mengi, Tarchisia Noback Mtui na Angel Shio ambao wanatoka Morogoro.

Warembo wengine ni Elizabeth Tarimo, Lilian Andrew na Leila Abdul Ally ambao wanatoka mkoa wa Lindi ambapo kutoka Mtwara ni Nidah Fred Katunzi, Lightness Mziray na Nelabo Emmanuel.

Pia warembo kutoka Pwani ni Khadija Ramadhan Sihaba, Irene Rajabu Soka, Mary Mpelo na Arafa Shaban. Nikitas alisema kuwa warembo hao watakuwa kambini kuanzia Julai 29 kwenye hotel ya Usambara Safari Lodge chini ya Miss Kanda ya mashariki mwaka jana, Diana Laizer.

JAJA AMWAGA WINO YANGA MIAKA MIWILI



Jaja akipokea nakala ya mkataba wake kutoka kwa Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu leo maraa baada ya kusaini kuitumikia kwa miaka miwili


Hatimaye mshamabuliaji Geilson Santos Santana "Jaja" raia wa Brazil leo amesaini mkataba wa miaka miwili (2014-2016) kuitumikia timu ya Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.

Katibu mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema usajli wa Jaja unakua ni wa pili msimu huu kwa wachezaji wa kimataifa baada ya awali kumsajili kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho ambaye pia ni raia wa Brazil.

"Kazi yetu uongozi ni kutekeleza maelekezo ya kocha mkuu pamoja na benchi la ufundi, walitoa mapendekezo ya usajili kabla hawajaanza kazi na mengine baada kuwasili yote tunajitahidi kuyatekeleza ili kila kitu kiende safi" alisema Beno.

Jaja ambaye alizaliwa tarehe 21 Septemba 1985 na kukulia katika mji wa Aracaju nchini Brazili mpaka anasajiliwa na timu ya Young Africans alikuwa akiichezea timu ya Itabaina FC iliyopo nchini Brazil.

Mshambuliaji huyo mwenye mwili uliojaa vizuri tayari alishaanza mazoezi tangu katikati ya wiki iliyopita chini ya Kocha Mkuu Marcio Maximo na msaidizi wake Leonado Neiva ambao wanaendelea kukinoa kikosi cha Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali.

TAIFA STARS YABANWA MBAVU NA MSUMBIJI



MSHAMBULIAJI Thomas Ulimwengu wa Taifa Stars akimtoka beki wa Msumbiji jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
MSHAMBULIAJI Mbwana Samatta wa Taifa Stars akiwafungisha tela mabeki wa Msumbiji
KIPA Deogratius Munishi 'Dida' wa Taifa Stars akishangilia bao la pili la timu hiyo kwa kuonyesha maandishi kwenye fulana yake.

TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars jana ililazimishwa kutoka sare ya mabao 2-2 na Msumbiji katika mechi ya michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Sare hiyo imeiweka Taifa Stars katika mazingira magumu ya kusonga mbele kwa vile italazimika kushinda mechi ya marudiano mjini Maputo kwa idadi yoyote ya mabao ama kuomba ipate sare ya mabao zaidi ya matatu.

Taifa Stars, inayofundishwa na Kocha Mart Nooj kutoka Uholanzi, ilicheza soka ya kuvutia kipindi cha kwanza na kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la Msumbiji.

Msumbiji ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 47 lililofungwa na Elias Pelembe kwa mkwaju wa penalti baada ya beki Kevin Yondan kumchezea vibaya Helder Pelembe ndani ya eneo la hatari.

Kiungo wa Taifa Stars, Mcha Khamis aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mrisho Ngasa, alifunga bao la kusawazisha dakika ya 60, akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Thomas Ulimwengu.

Mcha aliwainua tena vitini mashabiki dakika ya 71 baada ya kuifungia Taifa Stars bao la pili kwa njia ya penalti baada ya Samatta kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Zikiwa zimesalia dakika tatu pambano hilo kumalizika, Isac de Carvalho aliisawazishia Msumbiji kutokana na uzembe wa mabeki wa Taifa Stars.

Saturday, July 19, 2014

TAIFA STARS MIKONONI MWA MAMBA WA MSUMBIJI KESHO, KIINGILIO BUKU SABA




Viingilio kwa mechi ya Taifa Stars na Msumbiji itakayochezwa keshokutwa (Jumapili) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni sh. 7,000 na sh. 30,000 kwa viti maalumu 4,500 tu.

Kuanzia kesho asubuhi (Jumamosi) tiketi za kielektroniki zitauzwa pia katika magari maalumu kwenye vituo vya Buguruni Shell, Dar Live Mbagala, Ferry Magogoni, Kigamboni, OilCom Chang’ombe, OilCom Ubungo, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa (Kariakoo), TCC Club Chang’ombe na Uwanja wa Taifa.

Aidha tiketi zinapatikana kupitia M-PESA kwa kupiga *150*00# kisha bonyeza 4, bonyeza tena 4 kisha weka namba ya kampuni 173399 kisha ingiza 7000 kama namba ya kumbukumbu ya malipo, kisha andika tena 7000 kwenye weka kiasi, kasha weka namba ya siri na baadaye bonyeza 1 kukubali.

Utapokea ujumbe wenye orodha ya vituo vya MaxMalipo vya kuchukua tiketi ukiwa na namba ya uhakiki wa malipo yako.

Vituo vya MaxMalipo vya kuchukulia tiketi ni mgahawa wa Steers uliopo mtaa wa Samora/Ohio, maduka makubwa ya Uchumi Supermarket (Quality Centre, Tabata Segerea na kituo cha daladala Makumbusho), Sheer Illussions (Millennium Tower na Mlimani City), maduka makubwa ya TSN Supermarket (City Centre, Kibo Tegeta na Upanga).

Vodashop (Ubungo na Mill Pamba), Shop Mwenge (Born to Shine), Puma Petrol Station (Mwenge na Uwanja wa Ndege), Engen Petrol Station (Mbezi Beach), Big Bon Petrol Station (Kariakoo, Sinza Mori, Mbagala na Temeke), YMCA (Posta Mpya), City Sports Lounge (Posta), Uwanja wa Taifa) na Uwanja wa Karume.

Wakati huo huo, Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Msumbiji hatua za awali Kombe la Mataifa ya Afika (AFCON).

Nooij ambaye amewahi kuifundisha Msumbiji amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari hoteli ya Coutyard, eneo la Sea View, Dar es Salaam kwamba wachezaji wake wote wapo fiti kwa mchezo huo.

“Nafahamu sana mchezo utakuwa mgumu, hii ni timu yangu na timu yenu pia, naamini mshindi ni yule ambaye atacheza kitimu zaidi Jumapili,”amesema.

Amesikitika kiungo Jonas Mkude ameshindwa kuhusika na mchezo wa Jumapili kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti, hata hivyo amesema ana matumaini mchezaji huyo wa Simba anaweza kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

Ametaja kikosi alichoteua kwa ajili ya mchezo wa kesho, kuwa ni makipa Deo Munishi ‘Dida’ na Aishi Manula, mabeki Said Mourad, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Aggrey Morris, Kevin Yondan na Edward Charles, wakati viungo ni Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Shaaban Nditi, Simon Msuva, Himid Mao, Mwinyi Kazimoto, Khamis Mcha, Ramadhani Singano ‘Messi’, Haroun Chanongo, Amri Kiemba na washambuliaji Mrisho Ngassa, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na John Bocco,

Kwa upande wake, Nahodha wa Taifa Stars Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kwamba anaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi Uwanja wa taifa mjini Dar es Salaam kuisapoti timu yao.

“Tunashukuru hadi kufika hapa, ni matunda ya kupambana kwa juhudi na pia sapoti yenu, kwa hivyo tunaomba muendelee kuwa nasi Jumapili, watu waje kwa wingi wasapoti timu, ifanya vizuri,”amesema Cannavaro.

Aidha nahodha huyo wa taifa Stars amesema bado ana kumbukumbu za kipigo walichokipata dhidi ya Msumbiji mwaka 2007,wakati Nooij akiwa kocha mkuu wa Mambas, na kwa maana hiyo hivi sasa akiwa chini yake atafanya kila juhudi kwa faida ya Watanzania na yeye mwenyewe binafsi.

Stars itamenyana na Msumbiji Jumapili katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mwisho wa mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya AFCON mwakani nchini Morocco, ambao kiingilio cha chini kitakuwa Sh. 7,000.

Stars ilifika hatua hii baada ya kuitoa Zimbabwe kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 1-0 Dar es Salaam na kwenda kulazimisha sare ya 2-2 Harare.

Timu itakayofuzu hatua hii itaingia kwenye Kundi C ambalo lina timu za Zambia, Cerpe Verde na Niger zilizofuzu moja kwa moja hatua hiyo, kuwania tiketi ya Morocco mwakani.

Katika kuwania tiketi ya AFCON ya mwaka jana nchini Afrika Kusini, Tanzania ilitolewa na Msumbiji kwa penalti 5-4 baada ya sare ya jumla ya 2-2 Dar es Salaam na Maputo, Stars ikiwa chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen.

Stars inaonekana kuwa na maandalizi mazuri safari hii chini Mholanzi, Nooi na uongozi mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Rais Jamal Malinzi.

Baada ya kuitoa Zimbabwe, wachezaji walipata mapumziko ya wiki moja, kabla ya kwenda Botswana kuweka kambi ya wiki, na waliporejea Mbeya kuweka kambi ya wiki moja na ushei.

Nchini Botswana, pamoja na mazoezi, pia Stars ilipata mechi tatu za kujipima nguvu, ambazo

walifungwa mbili, moja dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Botswana mabao 4-2 na nyingine dhidi ya timu ya jeshi la nchini humo, BDF walishinda moja 3-1 na kufungwa moja 2-1.

Tanzania imewahi kushiriki mara moja tu AFCON, mwaka 1980 nchini Nigeria ambako ilitolewa katika hatua ya makundi, ilipokuwa pamoja na wenyeji Nigeria, Ivory Coast na Misri, Kundi A. Ilifungwa 3-0 na Nigeria, 2-1 na Misri na kutoa sare ya 1-1 na Ivory Coast.

SERENGETI BOYS YABANWA MBAVU NA AFRIKA KUSINI


Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM


TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imelazimishwa sare ya bila kufungana na Afrika Kusini, Amajimbos katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika, uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Matokeo hayo yanamaanisha, Serengeti Boys itahitaji sare ya mabao katika mchezo wa ugenini, au kushinda kabisa ili kuingia hatua ya mwisho ya mchujo katika kuwania tiketi ya Fainali zitakazopigwa Niger mwakani.

Amajimbos waliuanza mchezo vizuri wakilitia kwenye misukosuko lango la Serengeti kwa dakika takriban 20 za mwanzo, lakini taratibu mchezo ulianza kubadilika na wenyeji wakageuza kibao.

Serengeti ilipoteza nafasi mbili za wazi za kufunga kipindi cha kwanza na nafasi nyingine mbili zaidi za wazi pia za kufunga kipindi cha pili, ambacho watoto wa nyumbani walitawala zaidi mchezo.

Kocha wa Serengeti, Hababuu Ali alisema kwamba vijana wake waliuanza mchezo kwa kuelemewa kutokana na woga wa kucheza mbele ya umati wa mashabiki kwa mara ya kwanza. “Lakini walipozoea hali, wakatulia na kuanza vizuri,” amesema Hababuu.

Kuhusu wapinzani wao, Hababuu amesema kwamba Amajimbos si wazuri kiufundi zaidi wana nguvu na kasi na kwa sababu hiyo ana matumaini ya kupata matokeo mazuri ugenini.

Kikosi cha Serengeti Boys; Mitacha Mnacha, Abdallah Jumanne/Mashaka Ngujiro dk23, Issa Baky, Adolph Mutasingwa/Kelvin Farrel dk10, Martin Kiggi, Omar Wayne, Athanas Mdam, Ali Mabuyu, Abdul Bitebo/Mohamed Mussa dk86, Prosper Mushi na Baraka Yussuf.

Amajimbos; Mondili Mpoto, Nelson Maluleke, Simon Nqoi, Notha Ngcobo, Keanu Cupido, Tendo Mukumela, Katlego Mohamme, Athenkosi Dlala, Sibongankonke Mbatha/Felix Noge, Luvuyo Mkatshana/Vuyo Mantjie na Khanyiso Nayo.   IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BIN ZUBEIRY.

SIMBA KUJIPIMA UBAVU NA ISMAILI TAMASHA LA SIMBA DAY



SIMBA SC itacheza na Ismailia ya Misri au Zesco United ya Zambia katika tamasha maalum la klabu hiyo la kila mwaka, maarufu kama Simba Day Agosti 9, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema leo katika mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi kwamba, kipaumbele cha kwanza ni Ismailia na iwapo itashindikana Zesco itachukua nafasi.

Kaburu amesema mchakato wa usajili unaendelea na jana mchezaji wa Burundi amewasili wakati kesho Kamati ya Usajili itakutana naye kwa mazungumzo.

Simba SC inaendelea na mazoezi Dar es Salaam
Beki Mrundi, Kaze Gilbert ameomba aandikiwe barua ya ruhusa ya kwenda kujiunga na klabu yake ya zamani, Vital’O, wakati beki chipukizi Hassan Hatibu anatakiwa na Kagera Sugar.

Kaburu amesema wamekubali maombi yote la Kaze na Kagera Sugar na watawaidhinishia wachezaji hao, ambao kwa sasa hawana nafasi kwenye kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi.

Amesema klabu hiyo pia imeridhia mshambuliaji wake Betram Mombeki kujiunga na JKT Ruvu, maana yake imefuta mkataba wake.

Kuhusu kocha wa timu hiyo, Mcroatia Zdravko Logarusic aliyemaliza Mkataba wake, Kaburu amesema kwamba wanatarajia kumpa Mkataba mpya wiki ijayo kabla ya timu kwenda kambini visiwani Zanzibar kujiandaa na msimu mpya.

Simba SC pia imetangaza nafasi za kazi kwa Katibu, Msaidizi wake na Ofisa Habari na Kaburu ameomba watu watume maombi ili kuiwezesha klabu kufanya uteuzi. Katibu wa Simba SC kwa sasa ni Ezekiel Kamwaga, wakati Ofisa Habari ni Asha Muhaji

IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BIN ZUBEIRY

Friday, July 18, 2014

AZAM YATOA DOZI



AZAM FC imeshinda mechi ya tatu mfululizo ya kirafiki, baada ya jana kuilaza mabao 2-1 JKT Ruvu Stars Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, wachezaji wa kigeni wakiendelea kuibeba timu.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, walikwenda kupumzika wakiwa tayari wanaongoza tayari kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Mrundi Didier Kavumbangu na Kipre Tchetche kutoka Ivory Coast.

Kipindi cha pili, kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog alibadilisha karibu wachezaji wote walioanza na JKT Ruvu ya Freddy Felix Minziro ilitumia mwanya huo kujipatia bao la kusawazisha lililofungwa na Hassan Bilal, aliyemalizia kazi nzuri ya Betram Mombeki.

Mshambuliaji mpya wa Azam FC kutoka Haiti, Leonel Saint- Preux alicheza vizuri na ndiye aliyetoa pasi ya bao la pili, wakati Ismaila Diara kutoka Mali alikuwa jukwaani kabisa kutokana na mejeruhi.

Chipukizi waliopandishwa kutoka akademi, Abdul Mgaya, Bryson Raphael, Malik Farid, Dizana Issa na Mudathir Yahya ambao walianza kipindi cha kwanza, wote walicheza vizuri.

Awali, Azam FC ilizifunga kombaini ya Jeshi 3-2, mabao yake yakifungwa Ismaila Diara mawili na Mudathir Yahya moja, kabla ya kuilaza Polisi Morogoro 1-0, bao pekee la Leonel Saint- Preux.

MSUMBIJI KUTUA DAR LEO





Timu ya Taifa ya Msumbiji (Mambas) inawasili Dar es Salaam leo kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mambas itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7.30 mchana kwa ndege ya LAM ikiwa na msafara wa watu 37 ambapo kati ya hao, 25 ni wachezaji.

Wachezaji kwenye msafara huo ni Almiro Lobo, Apson Manjate, Bone Mario Uaferro, Dario Ivan Khan, Edson Sitoe, Eduardo Jumisse, Gelicio Aurelio Banze, Helder Pelembe, Josemar Machaisse, Elias Pelembe, Isac Carvalho na Jeffrey Constatino.

Wengine ni Manuel Fernandes, Manuel Uetimane, Mario Sinamunda, Momed Hagi, Reginaldo Fait, Reinoldo Mandava, Ricardo Campos, Saddan Guambe, Simao Mate Junior, Soares Victor Soares, Stelio Ernesto, Vando Justino na Zainadine Junior.

Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya Accomondia, na itaondoka Jumapili mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Mahmoud Ashour.

LINA KESSY AUTEULIWA KUWA OFISA MICHEZO AU
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Lina Kessy ameteuliwa kuwa Ofisa Michezo wa Umoja wa Afrika (AU).

Uteuzi huo umefanywa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Nkozasana Dlamini-Zuma, na Lina atatumikia nafasi hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu katika makao makuu ya AU yaliyopo Addis Ababa, Ethiopia.

Lina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) amewashukuru wote ambao kwa michango yao ya hali na mali imemwezesha kufika hapo.

Ameishukuru TFF kwa kumlea na kumjenga. Shukrani nyingine amezitoa kwa Serikali kupitia Kurugenzi ya Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).

TFF inampongeza kwa uteuzi huo, na tunaamini ataipeperusha vyema bendera ya Tanzania ikiwemo kuwa chachu ya maendeleo ya michezo kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

TAIFA STARS YAREJEA DAR, SAMATTA, ULIMWENGU, KAZIMOTO NDANI


Kikosi cha Taifa Stars kimerejea jijini Dar es Salaam leo kutoka Mbeya ambapo Jumapili (Julai 20 mwaka huu) kitapambana na Msumbiji (Mambas) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Benchi la Ufundi la Taifa Stars pamoja na wachezaji kesho (Julai 19 mwaka huu) saa 5 asubuhi watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea Courtyard iliyopo Upanga Seaview jijini Dar es Salaam.

Naye mchezaji Mwinyi Kazimoto amewasili leo 1.30 asubuhi kwa ndege ya Qatar Airways kutoka Qatar ambapo anacheza mpira wa miguu katika klabu ya Al Markhiya ya huko. Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi katika hoteli ya Protea Courtyard.
  Washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu waliwasili nchini juzi asubuhi (Julai 16 mwaka huu) kutoka Tunisia kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao wamefikia hoteli ya Courtyard, Seaview Upanga na juzi walifanya mazoezi kwa programu maalumu waliyopewa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij wakati wakiwasubiri wenzao.

Naye kiungo Mwinyi Kazimoto anayecheza mpira wa miguu katika klabu ya Almarhiya ya Qatar aliwasili nchini jana asubuhi kwa ndege ya Qatar Airways.

RAIS MALINZI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi leo atakuwa na mkutano na waandishi wa habari.

Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

FIFA KUWANOA WAAMUZI 30 DAR



Semina na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa waamuzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na baadhi ya wale wa daraja la kwanza wenye kiwango cha juu (elite) itafanyika jijini Dar es Salaam.

Waamuzi 30 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watashiriki kwenye semina hiyo itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Julai 21 hadi 26 mwaka huu.

Mkufunzi wa FIFA kwa Kanda ya Kusini mwa Afrika, Carlos Henriques kutoka Afrika Kusini ndiye atakayeendesha semina hiyo akisaidiwa na Watanzania Charles Mchau kutoka Kilimanjaro, Juma Ali David (Zanzibar), Joan Minja (Dar es Salaam) na Riziki Majala (Pwani).

Waamuzi na waamuzi wasaidizi wa FIFA watakaoshiriki semina hiyo ni Ferdinand Chacha (Mwanza), Hamisi Chang’walu (Dar es Salaam), Israel Mujuni (Dar es Salaam), Jesse Erasmo (Morogoro), John Kanyenye (Mbeya), Josephat Bulali (Zanzibar), Kinduli Ali (Zanzibar), Oden Mbaga (Dar es Salaam), Ramadhan Ibada (Zanzibar), Samwel Mpenzu (Arusha) na Waziri Sheha (Zanzibar).

Kwa upande wa waamuzi wa daraja la kwanza ni Abdallah Kambuzi (Shinyanga), Agnes Pandaleo (Arusha), Ahamada Simba (Kagera), Arnold Bugado (Singida), Charles Simon (Dodoma), Dalila Jafari (Zanzibar), Frank Komba (Pwani), Helen Mduma (Dar es Salaam), Issa Bilali (Zanzibar) na Issa Haji (Zanzibar).

Wengine ni Janeth Balama (Iringa), Jonesia Rukyaa (Kagera), Lulu Mushi (Dar es Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mary Kapinga (Ruvuma), Mbaraka Haule (Zanzibar), Mfaume Ally (Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga) na Soud Lila (Dar es Salaam).

Washiriki wa semina hiyo na wakufunzi wanatakiwa kuwasili jijini Dar es Salaam, Julai 20 mwaka huu.

SERENGETI BOYS MIKONONI MWA AFRIKA KUSINI LEO



TIMU ya soka ya Taifa ya vijana wa chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inashuka dimbani leo kumenyana na Afrika Kusini katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Shelisheli na kiingilio kitakuwa sh. 2,000.

Waamuzi hao ambao waliwasili nchini juzi usiku kwa ndege ya Kenya Airways ni Allister Barra, Gerard Pool, Jean Joseph Felix Ernest na Nelson Emile Fred.

Kamishna wa mechi hiyo Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar pia ameshawasili.

Afrika Kusini (Amajimbos) ilitua nchini juzi ikiwa na msafara wa watu 37 na imefikia hoteli ya Sapphire. Amajimbos ilifanya mazoezi jana jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Kikosi cha Serengeti Boys chini ya kocha Hababuu Ali Omari kipo kambini kwa zaidi ya wiki mbili sasa kikijiandaa kwa mechi hiyo. Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Agosti 1 na 3 nchini Afrika Kusini.

Wakati huo huo, Alfred Kishongole Rwiza wa Tanzania ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya marudiano ya michuano hiyo ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Rwanda na Uganda.

Mechi hiyo itachezwa nchini Rwanda kati ya Agosti 1 na 3 mwaka huu. Waamuzi wa mechi hiyo watatoka Burundi wakiongozwa na Pacifique Ndabihawenimana.

MBRAZIL MWINGINE ATUA YANGA


Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Brazil Geilson Santos Santana "Jaja" amewasili

leo mchana jijini Dar es salaam akitokea jijini Sao Paul tayari kwa kuanza kazi ya
kuitumikia klabu ya Young Africans Sports Club kwa msimu wa 2014/2015.

Jaja ambaye alikua akichezea timu ya Itabaina FC nchini Brazil, anakuwa ni mchezaji wa
pili kuungana na kikosi cha Young Africans baada ya Andrey Coutinho kuwa mchezaji
wa kwanza kujiunga na kikosi cha kocha Marcio Maximo.

Usajili wa wachezaji hawa ni muendelezo wa uongozi wa Young Africans kuhakikisha
msimu ujao unakua na kikosi bora ambacho kitaweza kufanya vizuri kwenye michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya Kombe la Shrikisho Barani Afrika.

Jaja anaungana na makocha wabrazil Marcio Maximo na Leonardo Neiva na kiungo
Andrey Coutinho katikaa msimu huu ambapo kwa pamoja ushirikiano wao na wachezaji
wengine wazawa wataisaidia Young Africans kufanya vizuri.

Kesho asubuhi Jaja anatarajiwa kuanza mazoezi katika shule ya sekondari Loyola ikiwa
ni sehemu ya maandaliz ya michuano mbalimbali itayowakabili

Thursday, July 10, 2014

SERENGETI BOYS KUJIPIMA NA AZAM -20 KESHO



Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boyz) inacheza mechi ya kujipima nguvu kesho (Julai 11 mwaka huu) dhidi ya Azam U-20 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mechi hiyo ambayo ni maalumu kwa benchi la ufundi la Serengeti Boyz likiongozwa na kocha Hababuu Ali Omari kuangalia kikosi chao itaanza saa 2 kamili asubuhi.

Serengeti Boyz itacheza mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos) siku ya Ijumaa, Julai 18 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Azam Complex kuanzia saa 10 kamili jioni.

Wachezaji wanaounda kikosi cha Serengeti Boyz ni Abdallah Shimba, Abdulrasul Bitebo, Abutwalibu Mshery, Adolf Bitegeko, Ally Mabuyu, Ally Mnasi, Amin Noren, Athanas Mdamu, Badru Othman, Baraka Baraka, Hatibu Munishi na Issa Athuman.

Wengine ni Juma Yusuf, Kelvin Faru, Kelvin Kamalamo, Martin Luseke, Mashaka Ngajilo, Mechata Mnata, Mohamed Abdallah, Mussa Vicent, Nazir Barugire, Omary Omary, Omary Wayne, Prosper Mushi, Seif Seif na Yahya Hafidh.

LIGI KUU BARA KUANZA KUTIMUA VUMBI SEPTEMBA 20



Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2014/2015 itaanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu.

Awali michuano hiyo ilikuwa ianze Agosti 24 mwaka huu, lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limelazimika kuisogeza mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupitisha michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).

Michuano ya Kombe la Kagame inayoshirikisha mabingwa wa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itafanyika Agosti mwaka huu nchini Rwanda.

Timu 14 zitashiriki Ligi Kuu msimu huu. Timu hizo ni mabingwa watetezi Azam, Coastal Union, JKT Ruvu Stars, Kagera Sugar, Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Ndanda FC, Polisi Morogoro, Ruvu Shooting, Simba, Stand United, Tanzania Prisons na Yanga.

Ratiba ya ligi hiyo itatolewa mwezi mmoja kabla ya michuano hiyo kuanza kutimua vumbi.

Wednesday, July 9, 2014

MAXIMO SASA KUTETA NA WANAHABARI KILA IJUMAA, AKERWA KULISHWA MANENO


Kocha mkuu wa timu ya Young Africans SC Mbrazil Marcio Maximo amesema atakua akiongea na waandishi wa habari kila siku ya Ijumaa asubuhi mara tu baada ya mazoezi katika shule ya sekondari Loyola ili kuwapa nafasi na fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na maandalizi ya kikosi chake msimu ujao.


Akiongea na mtandao rasmi wa klabu ya Young Africans Maximo amesema, ameamua kufanya hivyo ili kupunguza kuwepo taarifa tofauti kuhusiana na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wake katika maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015.

Unajua utendaji wa kazi umebadilika, nafasi yangu kwenye klabu na nilipokua timu ya Taifa ni tofauti, hivyo nimekubaliana na uongozi na umeniruhusu kuwa naongea na vyombo vya habari kwa pamoja kila siku ya Ijumaa mara tu baada ya mazoezi ya asubuhi "alisema Maximo"

Waandishi wa habari, Vyombo vya Habari mnaombwa kuhudhuria kila siku ya ijumaa shule ya sekondari Loyola ili mpate nafasi ya kuongea na kocha Maximo na kumuuliza maswali, kwani kwa sasa yeye ndie atakayekua akiongelea timu, wachezaji pamoja na benchi lake la ufundi.

Maximo ameanza kazi ya kukinoa kikosi cha Young Africans tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwatuvia wapenzi, washabik na wanachama ambao wamekua wakijitokeza kwa wingi kushuhudia ufundishaji wa kocha huyo mwenye mvuto mkubwa kwenye soka la Tanzania.

KIINGILIO STARS, MSUMBIJI BUKU SABA


KIINGILIO cha chini cha mechi kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas)
itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 7,000.

Tiketi zinapatikana kwa mfumo wa elektroniki kupitia M-PESA. Kiingilio hicho kwa ajili
ya viti vya rangi ya rangi ya chungwa, kijani na bluu. Viingilio katika maeneo mengine
vitatangazwa baadaye.

Mshabiki ili apate tiketi anatakiwa kutumia M-PESA kwa kupiga *150*00# kisha
bonyeza 4, ingiza namba ya kampuni 173399 kisha weka 7000 kwenye namba ya
kumbukumbu ya malipo, na weka 7000 kama kiasi cha bei ya tiketi na mwisho weka
namba yao ya siri.

Baada ya hapo utapokea ujumbe wenye orodha ya vituo vya MaxMalipo kwa ajili ya
kuchukulia tiketi ukiwa na namba ya uhakiki wa malipo yako.

Vituo vya kuchukulia tiketi ni mgahawa wa Steers uliopo mtaa wa Samora/Ohio, maduka
makubwa ya Uchumi Supermarket (Quality Centre, Tabata Segerea na kituo cha
daladala Makumbusho), Sheer Illutions (Millennium Tower na Mlimani City), maduka
makubwa ya TSN Supermarket (City Centre, Kibo Tegeta na Upanga).

Vodashop (Ubungo na Mill Pamba), Shop Mwenge (Born to Shine), Puma Petrol
Station (Mwenge na Uwanja wa Ndege), Engen Petrol Station (Mbezi Beach), Big Bon
Petrol Station (Kariakoo, Sinza Mori, Mbagala na Temeke), YMCA (Posta Mpya), City
Sports Lounge (Posta), Uwanja wa Taifa) na ofisi za TFF (PPF Tower).

TAIFA STARS YAINGIA KAMBINI TUKUYU


Wakati Taifa Stars inaingia kambini Tukuyu mkoani Mbeya kesho (Julai 9 mwaka huu),
kocha Mart Nooij amesema kambi ya wiki mbili nchini Botswana imekisaidia kikosi
chake kujiandaa kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo (Julai 8 mwaka huu) kuhusu maandalizi ya timu
hiyo, Nooij amesema timu yake inafanya mazoezi kwenye maeneo ya baridi kwa sababu
za kitaalamu, hivyo kambi ya Tukuyu kama ilivyokuwa ya Botswana itawasaidia kwa
mechi dhidi ya Msumbiji.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka kwa ndege
kwenda Mbeya ikiwa na kikosi cha wachezaji 25, na itarejea jijini Dar es Salaam siku tatu
kabla ya mechi hiyo.

Wachezaji walioko kwenye msafara huo ni Aggrey Morris, Aishi Manula, Amri Kiemba,
Benedictor Tinoko, Deogratius Munishi, Edward Charles, Emmanuel Namwando,
Erasto Nyoni, Haruni Chanongo, Himid Mao, John Bocco na Jonas Mkude.

Wengine ni Joram Mgeveke, Kelvin Friday, Kelvin Yondani, Khamis Mcha, Mrisho
Ngasa, Mwagane Yeya, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Ramadhan
Singano, Said Juma, Said Moradi, Shabani Nditi, Shomari Kapombe, Simon Msuva,

Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za
Afrika (AFCON) dhidi ya Msumbiji itafanyika Julai 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.

Tuesday, July 8, 2014

AIRTEL YAMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA JUKWAA LA WAHARIRI






Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akimkabithi Nahodha wa timu ya wahariri Bwana Kulwa Karedia , vifaa vya michezo kwaajili ya mechi kati ya timu ya Jukwaa la wahariri na timu ya waandishi wa mkoa wa Mtwara itakayofanyika siku ya Ijumaa tarehe 11 Julai mkoani Mtwara

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetoa msaada wa vifaa vya michezo wenye thamani ya Sh milioni 1.1 kwa timu ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema uamuzi wa kutoa msaada huo umefikiwa kutokana na kutambua mchango wa vyombo vya habari nchini.

“Tunafaurahi kuwaambia kwamba leo (jana),tunakabidhi msaada wa vifaa vya michezo ndugu zetu wahariri ambao wanajiandaa na mchezo wa kirafiki mkoani Mtwara Jumamosi hii.

“Kama kwa vile wahariri ni watu ambao wanakuwa na majukumu mengi ya kila siku kwenye vyumba vya Habari, tunaamini baada ya mkutano wao, watapata fursa ya kucheza mchezo wa soka pale Mtwara ili kuweka miili yao sawa,”alisema Mmbando.

Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni pamoja na jezi seti moja,mipira mitano, filimbi tatu,fulana na traksuti tano.

“Hii ni sehemu tu ya msaada mdogo,tunategemea vitawasaidia jamaa zetu kuonyesha makekeo yao,”alisema Mmbando.

Akipokea msaada huo, Nahodha wa timu ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Kulwa Karedia aliishukuru Airtel kwa msaada huo na kusema umekuja wakati mzuri.

“Unajua mawasiliano bila waandishi wa habari hayapo, nadhani ndiyo maana Airtel wameona umuhimu wa kutoa msaada huu na sisi tunasema hatutawaangusha,”alisema Karedia.

Alisema timu yake inatarajia kuondoka kesho kuelekea Mtwara ambako Jumamosi hii watacheza na timu ya waandishi wa habari mkoa wa Mtwara.

Kikosi cha TEF kinaundwa na wachezaji kama Theopil Makunga,Revocatus Makaranga,Jesse Kwayu,Manyerere Jackton,Ansbert Ngurumo,Salehe Mohamed,Neville Meena,Mnaku Mbani,Salim Said Salim, Wallace Maugo na Erick Anthony ‘Chinga’.

LOWASSA ATOA SOMO KWA UONGOZI MPYA SIMBA



WAZIRI Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ameutaka uongozi mpya wa Simba kutolipiza kisasi au kufukua maovu ya uongozi uliopita, badala yake ujikite katika kuweka mikakati ya kuendeleza klabu.

Lowassa alisema hayo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam jana alipotembelewa na Rais mpya wa Simba, Evans Aveva.

Lowassa amemtaka Aveva kuunganisha wanachama wa Simba kwa manufaa ya soka ya Tanzania.

Aidha aliwataka viongozi wa klabu kubwa nchini kusajili zaidi wachezaji wa
nyumbani na kuachana na tabia ya kukimbilia kusajili wachezaji wa kigeni kwani hiyo inadhoofisha uimara wa timu ya taifa.

Lowassa alitolea mfano timu ya taifa ya Uingereza ilivyofanya vibaya katika Kombe la Dunia, akisema inatokana na klabu nyingi za ligi kuu ya nchi hiyo kuwa an wachezaji wengi wa kigeni kuliko wale wa ndani.

Kwa upande wake,  Rais huyo wa Simba alisema uongozi wake umejipanga kuwekeza katika soka ya vijana ili kupunguza gharama za kusajili wachezaji wapya kila msimu.

Pia alimueleza Lowassa kuwa wanatarajia kufungua hosteli katika kipindi kifupi kijacho katika eneo jipya la klabu hiyo huko Bunju.

Alisema awamu ya pili ndiyo itakuwa ya ujenzi wa uwanja ambapo alimuomba Lowassa kukubali mualiko wa kufanya harambee ya kukusanya fedha za ujenzi wa uwanja huo wakati ukifika.

DK BILAL, MZEE MWINYI WATEMBELEA GYM YA AZAM


Mkurugenzi wa Makampuni ya SSB, Said Mohamed, (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa

viongozi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati walipokuwa
wakitembelea kujionea Uwanja na Gym ya mazoezi ya timu ya Azam FC iliyopo kwenye
Uwanja wa Azam Complex, unaomilikiwa na timu ya hiyo, Chamazi.

WASANII WA TANZANIA WATIA FORA KWA MUZIKI WA KIASILI UJERUMANI


Muziki wa dansi wa Tanzania umezidi kufungua ukurusa mpya katka tufe la dunia,
baada ya wasanii na wanamuziki wa Tanzania kutumbuiza katika onyesho la TFF Rudolstadt 2014,yaliofanyika kuanzia tarehe 3 adi 6 Julai 2014 mjini Rudolstadt,Ujerumani,ambako vikundi mbali mbali vya sanaa na bendi za muziki kutoka Tanzania zilishiriki,zikiwemo bendi ya Black Warriors ikiwashirikisha jukwaani na wakongwe wa muziki akina Mafumu Bilal,Hassan Bichuka,Cosmas Chidumule na wengine,pia Mchiriku ulikuwapo,bila kukosa Kikundi cha ngoma ya Kaya Baikoko
kutoka mkoani Tanga, kikundi cha Qwasida " Tarbiyya Islamiyya" kutoka Zanzibar, Kikundi cha kinamama cha Ngoma za Wagogo kutoka Dodoma, Mambo moto moto band na Segere lao walikuwapo hayo yote yalikuwa mjini Rudolstad, nchini Ujerumani nchi ambayo ndipo makao makuu ya "FFU-Ughaibuni"

WASANII wa kundi la muziki la Segere Orijino wakifanya vitu vyao 
MWIMBAJI wa muziki wa Baikoko kutoka Tanga akiwajibika

MPULIZA saxaphone maarufu nchini, Mafumu Bilali 'Bombenga' akionyesha umahiri wake
HILI ni kundi zima la Black Warriors likiongozwa na Cosmas Chidumule na Hassan Bitchuka

 HASSAN Bitchuka na Cosmas Chidumule wakifanya vitu vyao
SEHEMU ya umati wa watu waliohudhuria onyesho hilo