KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, July 1, 2014

NYOTA KUTOKA HUNGARY, SWEDEN WATUA AZAM




WACHEZAJI watatu akiwemo winga kutoka akademi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Gery Epeso wametua klabu bingwa ya Tanzania Bara, Azam FC kwa ajili ya majaribo.

Kocha Mcameroon Joseph Marius Omog amewapokea wachezaji hao mazoezini na amesema atahitaji kuwaangalia kabla ya kuamua.

“Wakati mwingine unaweza kupata mchezaji mzuri kati ya hawa ambao wanakuja majaribio, acha tuwaangalie kwa muda,”alisema.

Epeso alisema wiki hii kwamba alikuwa anachezea akademi ya Orlando, lakini kwa sasa ni mchezaji wa klabu ya Don Bosco ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambako ndiko nyumbani kwao.

Mbali na winga huyo wa kushoto, wachezaji wengine waliotua kujaribu bahati yao Azam FC ni mshambuliaji Hisham Abdallah aliyekuwa anacheza soka ya kulipwa Hungary na kiungo mkabaji, Athumani Ali Sheikh kutoka IFK Amal ya Daraja la Pili Sweden.

Hisham anayecheza zaidi kama mshambuliaji wa pili, asili yake ni Zanzibar wakati Sheikh ni mwenyeji wa Dar es Salaam.

Tayari Azam FC ina wachezaji watano wa kigeni ambao ni kiungo Kipre Michael Balou, washambuliaji Kipre Herman Tchetche wote kutoka Ivory Coast, Didier Kavubangu kutoka Burundi, Ismaila Diara kutoka Mali na Brian Umony kutoka Uganda.

Hata hivyo, kuna uwezekano Umony akatemwa na nafasi yake akapewa mchezaji mwingine- maana yake Epeso kama atamvutia kocha Omog anaweza kuziba nafasi ya Mganda huy

Wakati huo huo, mshambuliaji mpya wa Azam FC kutoka Mali, Ismaila Diara amesema kwamba atajihitaji muda kuzoea mazingira ya soka ya Tanzania kabla ya kuanza kuwika.

Akizungumza wiki hii Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam mchezaji huyo mwenye mwili mkubwa amesema kwamba hajui lolote kuhusu soka ya Tanzania na yote atajifunza hapa.

“Sijui, sijui kabisa, mimi ni mchezaji na naweza kucheza popote. Nitahitaji muda kidogo nizoee, ila nina amini nitafanya vizuri,”amesema.

No comments:

Post a Comment