KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, January 30, 2014

USAJILI WA WACHEZAJI DIRISHA DOGO ENGLAND


ARSENAL
WALIOSAJILIWA
Hakuna
WALIOONDOKA
Chuba Akpom (Brentford, mkopo), Anthony Jeffrey (Wycombe, mkopo)

ASTON VILLA
WALIOSAJILIWA
Grant Holt (Wigan, mkopo)
WALIOONDOKA
Stephen Ireland (Stoke, huru), Michael Drennen (Carlisle, mkopo)

CARDIFF
WALIOSAJILIWA
Magnus Wolff Eikrem (Heerenveen, £2m), Mats Moller Daehli (Mold,ada haikutajwa),
Jo Inge Berget (Molde, ada haikutajwa), Kenwyne Jones (Stoke, mabadilishano)
WALIOONDOKA
Rudy Gestede (Blackburn, ada haikutajwa), Filip Kiss (Ross County, mkopo), Nicky Maynard (Wigan, mkopo), John Brayford (Sheffield Utd,mkopo), Peter Odemwingie (Stoke, mabadilishano)

CHELSEA
WALIOSAJILIWA
Bertrand Traore (Association Jeunes Espoirs De Bobo-Dioulasso, ada haikutajwa), Nemanja Matic (Benfica, £21m), Mohamed Salah (Basel £11m)
WALIOONDOKA
Bertrand Traore (Vitesse Arnhem, mkopo), Kevin de Bruyne (Wolfsburg, £17m), Josh McEachran (Wigan, mkopo), Michael Essien (AC Milan, ada haikutajwa), Sam Walker (Colchester, mkopo), Nathaniel Chalobah (MIddlesbrough, mkopo)

CRYSTAL PALACE
WALIOSAJILIWA
Hakuna
WALIOONDOKA
Jason Banton (Plymouth, huru), Jimmy Kebe (Leeds, mkopo), Kwesi Appiah (Notts County, mkopo), Matt Parsons (Plymouth, ada haikutajwa)

EVERTON
WALIOSAJILIWA
Aiden McGeady (Spartak Moscow, ada haikutajwa), Lacina Traore (Monaco, mkopo)
WALIOONDOKA
Nikica Jelavic (Hull, ada haikutajwa)

FULHAM
WALIOSAJILIWA
Clint Dempsey (Seattle Sounders, mkopo)
WALIOONDOKA
Bryan Ruiz (PSV, mkopo)

HULL
WALIOSAJILIWA
Nikica Jelavic (Everton, ada haikutajwa), Elliott Kebbie (Atletico Madrid, mkopo), Shane Long (West Brom, £6m)
WALIOONDOKA
Tom Cairney (Blackburn, £500,000), Conor Townsend (Carlisle, mkopo), Eldin Jakupovic (Leyton Orient, mkopo), Cameron Stewart (Leeds, mkopo), Nick Proschwitz (Barnsley, mkopo).

LIVERPOOL
WALIOSAJILIWA
Hakuna
WALIOONDOKA
Adam Morgan (Yeovil, huru), Tiago Ilori (Granada, mkopo)

MANCHESTER CITY
WALIOSAJILIWA
Hakuna
WALIOONDOKA
John Guidetti (Stoke, mkopo), Albert Rusnak (Birmingham, mkopo)

MANCHESTER UNITED
WALIOSAJILIWA
Juan Mata (Chelsea, £37.1m)
WALIOONDOKA
Jack Barmby (Hartlepool, mkopo), Anderson (Fiorentina)

NEWCASTLE
WALIOSAJILIWA
Luuk de Jong (Borussia Monchengladbach, mkopo)
WALIOONDOKA
Yohan Cabaye (Paris-Saint Germain, £23m), Jonas Gutierrez (Norwich, mkopo)

NORWICH
WALIOSAJILIWA
Jonas Gutierrez (Newcastle, mkopo)
WALIOONDOKA
Daniel Ayala (Middlesbrough, £350k)

SOUTHAMPTON 
WALIOSAJILIWA
Hakuna
WALIOONDOKA
Lee Barnard (Southend, mkopo)

STOKE CITY
WALIOSAJILIWA
John Guidetti (Man City, mkopo), Stephen Ireland (Aston Villa, huru), Juan Agudelo (New England Revolution, huru)
WALIOONDOKA
Brek Shea (Barnsley, mkopo), Jamie Ness (Leyton Orient, mkopo), Juan Agudelo (FC Utrecht, mkopo)

SUNDERLAND
WALIOSAJILIWA
Marcos Alonso (Fiorentina, mkopo), Santiago Vergini (Estudiantes, mkopo), Oscar Ustari (Almeria, huru)
WALIOONDOKA
Mikael Mandron (Fleetwood, mkopo), Ji Dong-won (Ausburg, ada haikutajwa), Billy Knot (Port Vale, mkopo)

SWANSEA
WALIOSAJILIWA
Hakuna
WALIOONDOKA
Alan Tate (Aberdeen, mkopo)

TOTTENHAM
WALIOSAJILIWA
Hakuna
WALIOONDOKA
Jermain Defoe (Toronto, £6m), Simon Dawkins (Derby, ada haikutajwa), Shaquile Coulthirst (Leyton Orient, mkopo), Jon Obika (Brighton, mkopo), Ryan Fredericks (Millwall, mkopo)

WEST BROMWICH ALBION
WALIOSAJILIWA
Hakuna
WALIOONDOKA
Lee Camp (Bournemouth, huru)

WEST HAM
WALIOSAJILIWA
Roger Johnson (Wolves, mkopo), Antonio Nocerino (Milan, mkopo), Marco Borrielo (Roma, mkopo)
WALIOONDOKA
Blair Turgott (Rotherham, mkopo)

AZAM YAISHUSHA YANGA KILELENI, MBEYA CITY YABANWA


MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara, Yanga jana walishindwa kutamba mbele ya Coastal Union baada ya kulazimishwa kutoka nayo suluhu katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Sare hiyo imeifanya Yanga ienguliwe kutoka kileleni mwa ligi hiyo baada ya Azam kuishinda Rhino Rangers bao 1-0 na kuwa mbele ya mabingwa hao kwa tofauti ya pointi moja.

Azam inaongoza ligi hiyo kwa kuwa na pointi 33 baada ya kucheza mechi 15, ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 32 na Mbeya City yenye pointi 31.

Yanga ilizianza dakika tatu za kwanza kufanya mashambulizi kwenye lango la Coastal Union, lakini washambuliaji wake hawakuwa makini katika kulenga lango la wapinzani wao.
Coastal Union nayo ililishambulia mfululizo lango la Yanga dakika 30 za kwanza, na kama si uhodari wa kipa Deogratius Bonaventura 'Dida' kuzuia mashuti ya Haruna Moshi, Yaya Lutimba na Kenneth Masumbuko, huenda hadithi ingekuwa nyingine. Timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa suluhu.

Timu zote mbili zilifanya mabadiliko kadhaa ya wachezaji katika kipindi cha pili, lakini hayakuweza kuzisaidia kubadili sura ya mchezo.

Katika hatua nyingine, tiketi za elektroniki jana zilishindwa kufungua milango ya kwenye Uwanja wa Mkwakwani na kusababisha tafrani kubwa.

Kwa mujibu wa utaratibu mpya, mashabiki huzitumia tiketi hizo kufungua milango, lakini ilishindikana na kusababisha kutokea kwa vurugu.

Kutokana na kadhia hiyo, ilibidi utaratibu wa kawaida utumike kwa mashabiki kwenda na tiketi zao mlangoni na kuchanwa na walinzi wa milangoni.

YANGA: Degratius Bonaventura 'Dida', Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Cannavaro, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu, Mrisho Ngassa na David Luhende/Jerry Tegete.

COASTAL UNION: Shabani Kado, Shabani Hamisi, Abdi Banda, Mbwana Hamis, Juma Nyosso, Jerry Santo, Danny Lyanga, Crispine Odula, Yayo Lutimba, Haruna Moshi 'Boban' na Kenneth Masumbuko.

Wakati huo huo, Azam jana iliishusha Yanga kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuichapa Rhino Rangers bao 1-0 kwenye Uwanja wa Chamazi ulioko Mbagala, Dar es Salaam.

Bao pekee na la ushindi la Azam lilipachikwa wavuni na mshambuliaji Kipre Tchetche kipindi cha kwanza na kumfanya alingane na Hamisi Tambwe wa Simba kwa ufungaji mabao, wote wakiwa wamefunga mabao 10 kila mmoja.

Mbeya City  ilishindwa kutamba mbele ya Ruvu Shooting baada ya kulazimishwa kutoka nayo sare ya bao 1-1 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizo mkoani Pwani.

CHUJI YAMETIMIA YANGA


UONGOZI wa klabu ya Yanga, umeamua kumsamehe kiungo mkongwe wa timu hiyo, Athumani Iddi 'Chuji', aliyekuwa amesimamishwa kwa muda usiojulikana.

Uamuzi wa kumsamehe mchezaji huyo, ulifikiwa katika kikao cha kamati ya utendaji ya Yanga, kilichofanyika juzi mjini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, wajumbe wa kamati hiyo walivutana kwa muda mrefu, baadhi yao wakitaka mchezaji huyo asamehewe na wengine wakitaka aendelee na adhabu ya kusimamishwa.

Wajumbe waliotaka asamehewe, walisema Chuji ameonyesha uungwana kwa kuomba radhi na kuahidi kutorudia makosa, hivyo anastahili kupata msamaha kwa vile adhabu aliyotumikia inatosha.

Lakini baadhi ya wajumbe walipinga kwa madai kuwa, mchezaji huyo ameendelea kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kunukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa, Yanga haijamsaidia lolote kimaisha.

Baada ya mvutano huo, wajumbe walikubaliana kwa pamoja kumsamehe mchezaji huyo, kwa masharti kwamba apewe onyo kali.

Chuji alikabidhiwa barua hiyo jana na anatarajiwa kujiunga na wachezaji wenzake baada ya timu kurejea kutoka Tanga.

Kiungo huyo wa zamani wa Simba na Polisi Dodoma, alisimamishwa mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuondoka uwanjani baada ya kupumzishwa wakati Yanga ilipomenyana na Simba katika mechi ya Nani Mtani Jembe.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba iliichapa Yanga mabao 3-1. Chuji ni miongoni mwa wachezaji waliodaiwa kucheza chini ya kiwango.

Yanga ilitarajiwa kushuka dimbani jana kumenyana na Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kabla ya kushuka tena dimbani Jumapili kukipiga na Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mbali na kushiriki katika ligi, Yanga inajiandaa kwa michuano ya klabu bingwa Afrika, ambapo imepangwa kuanza raundi ya kwanza kwa kumenyana na Komoronize ya Comoro mwanzoni mwa mwezi ujao.
  

OWINO AIVIMBIA SIMBA


HATMA ya beki Joseph Owino katika klabu ya Simba, imeendelea kuwa shakani baada ya kugoma kwenda kufanya mazoezi na kikosi cha pili cha timu hiyo.

Owino alitakiwa kuanza mazoezi na kikosi hicho jana asubuhi kwenye uwanja wa Kinesi ulioko Urafiki, Dar es Salaam.

Hata hivyo, beki huyo kutoka Uganda, hakuweza kuhudhuria mazoezi hayo na hakutoa taarifa yoyote kwa Kocha wa timu hiyo, Selemani Matola.

Alipoulizwa jana iwapo Owino alihudhuria mazoezi ya kikosi cha pili, Matola alisema:
"Sijamwona Owino na sifahamu habari zake, waulize viongozi."

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic aliamua kumshusha beki huyo kwenye kikosi cha pili baada ya kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu wakati wa mazoezi yaliyofanyika wiki iliyopita.

Logarusic aliwaeleza viongozi wa klabu hiyo kwamba, amechoshwa na tabia za mchezaji huyo kwa madai kuwa, hana nidhamu na amekuwa akijisikia kwa kujiona yuko juu ya kocha na wachezaji wenzake.

Alipoulizwa jana kuhusu sakata la mchezaji huyo, Ofisa Habari wa Yanga, Asha Muhaji alisema kwa sasa lipo mikononi mwa benchi la ufundi.

"Suala la Owino kwa sasa lipo mikononi mwa benchi la ufundi, halipo kwa uongozi.
Tunachofahamu kwa sasa ni kwamba kocha ameamua kumshusha kikosi cha pili na ni lazima atekeleze adhabu hiyo,"alisema Asha.

Kwa mujibu wa Asha, Owino alipaswa kuanza mazoezi na kikosi cha pili jana chini ya Kocha Msaidizi, Matola, ambaye pia amepewa jukumu la kukinoa kikosi hicho.

Alisema Kocha Logarusic ameamua kumshusha Owino kikosi cha pili kutokana na kushindwa kufikia vigezo anavyovihitaji na huo ni uamuzi wa kawaida kwa kocha yoyote.

"Jambo la msingi ni kwa Owino kutii adhabu hiyo. Anaweza kufanya mazoezi na kikosi cha pili kwa siku tatu au wiki moja, na iwapo ataonekana amejirekebisha, atarudishwa kikosi cha kwanza," alisisitiza Asha.

TIKETI ZA ELEKTRONIKI BADO TATIZO-MWESIGWA



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limekiri kutokea kwa baadhi ya matatizo kwenye viwanja, ambavyo vimeanza kutumia mfumo wa uuzaji wa tiketi kwa njia ya elektroniki.

Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa alisema mjini Dar es Salaam, wiki hii kuwa, matatizo hayo yametokana na ugeni wa teknolojia hiyo kwa mashabiki.

"Unajua kitu kinapoanza kwa mara ya kwanza, hasa inapotumika teknolojia mpya, lazima yajitokeze matatizo. Na hivyo ndivyo ilivyotokea katika baadhi ya viwanja na tumeshaanza kuyafanyia kazi matatizo hayo ili kuiboresha huduma hiyo,"alisema Mwesigwa.

Aliongeza kuwa, hadi sasa hakuna taarifa yoyote ya mapato iliyopatikana katika viwanja vilivyoanza kuuza tiketi kwa kutumia mfumo huo, lakini aliahidi watazipata baada ya siku chache zijazo.

Mwesigwa alisema uuzaji wa tiketi za elektroniki umeshindwa kutumika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kutokana na idadi kubwa ya mashabiki wanaofika uwanjani, hasa katika mechi za Simba na Yanga.

Alisema waliamua utaratibu huo uanze kwanza kwenye viwanja vya mikoani ili kuona faida na hasara zake kabla ya kuuhusisha Uwanja wa Taifa, ambao unachukua idadi kubwa ya mashabiki.

Katibu Mkuu huyo wa TFF alisema ana hakika baada ya siku chache zijazo, tiketi za elektroniki zitaanza kutumika kwenye uwanja huo baada ya kufanyika tathmini kwenye viwanja vingine.

Alisema utaratibu huo ni mzuri kwa vile unasaidia kupunguza msongamano wa watu wakati wa kuingia uwanjani na vilevile unaepusha wizi wa tiketi na mapato ya milangoni.

Mwesigwa alisema TFF inaamini kuwa, uuzaji wa tiketi kwa njia hiyo utazisaidia klabu kupata mapato mengi, tofauti na ilivyo sasa, ambapo baadhi ya wajanja wachache wamekuwa wakitengeneza na kuuza tiketi feki.

Aliongeza kuwa TFF imeshaanza kutoa elimu kwa mashabiki kuhusu utaratibu wa kununua tiketi hizo ili kuepusha usumbufu kwa wale, ambao hawaujui. Alisema wamekuwa wakitoa elimu hiyo kupitia matangazo ya kwenye redio na televisheni.

MOYES KUTEMBEZA CHEKECHE MAN UTD


LONDON, England

KOCHA Mkuu wa Manchester United, David Moyes amewaonya wachezaji wake nyota wanaocheza chini ya kiwango kwa kuwaambia, atawapiga chekeche iwapo watashindwa kujirekebisha.

Moyes amesema amepanga kusajili nyota wapya kadhaa kutoka klabu mbalimbali za Ulaya kwa ajili ya kuziba nafasi za wale atakaowatema.

Kocha huyo aliyerithi mikoba ya Sir Alex Fergsuon amesema, lengo lake ni kuwa na kikosi cha wachezaji wanaojituma na kutimiza wajibu wao ipasavyo uwanjani.

Tayari Moyes ameshamsajili nyota wa zamani wa Chelsea, Juan Mata kwa kitita cha pauni milioni 37 na alitarajiwa kuanza kuichezea Manchester United mwanzoni mwa wiki hii katika mechi dhidi ya Cardiff.

Kocha huyo amesema ujio wa Mata ni salamu kwa wachezaji watakaoshindwa kujirekebisha kwa vile anatarajia kusajili nyota wengine wapya hivi karibuni.

Uamuzi wa Moyes kuwapiga chekecheke wachezaji wazembe, umetokana na mwenendo usioridhisha wa Manchester United katika michuano ya ligi kuu ya England.

Kuvurunda kwa timu hiyo katika ligi na michuano mingine, kumemfanya Moyes aseme sasa basi na kuanza kuchukua hatua.

"Siwezi kuruhusu hali hii iendelee,"alisema kocha huyo, ambaye kama Ferguson, ni raia wa Scotland.

"Nimekatishwa tamaa kuona hatuko kwenye nafasi nzuri. Nimekatishwa tamaa na uchezaji wetu,"alisema kocha huyo.

"Ninapaswa kuchukua hatua. Nitasajili wachezaji wazuri zaidi. Sidhani kama nitasajili zaidi Januari, lakini timu itabadilika,"alisisitiza.

Kuondoka kwa Anderson, aliyesajiliwa kwa mkopo na Fiorentina ya Italia na pia kuondolewa kwa Wilfried Zaha na Fabio kwenye kikosi cha kwanza, kunathibitisha lengo la Moyes kukisuka upya kikosi cha timu hiyo.

Beki mkongwe Rio Ferdinand naye anatarajiwa kufungasha viraga msimu ujao wakati hatma ya mabeki wengine, Nemanja Vidic na Patrice Evra ipo shakani.

Wachezaji wengine, ambao huenda wakafungashiwa virago ni pamoja na Alexander Buttner, Nani, Ashley Young na Javier Hernandez 'Chicharito'.

Moyes ameamua kufanya marekebisho makubwa kwenye kikosi chake kwa lengo la kurejesha imani kwa mashabiki wa klabu hiyo maarufu duniani, ambao kwa sasa wamekata tamaa.

"Nimetoa nafasi kwa kila mchezaji kucheza na kuonyesha uwezo wake. Tulipata nafasi ya kuona uwezo wa kila mmoja. Kinachofuata sasa ni kuchukua hatua,"alisema kocha huyo.

"Wachezaji wanapaswa kuonyesha uwezo wao. Kama wanataka kubaki hapa na kupata namba, wanapaswa kuthibitisha hilo katika mechi wanazocheza,"alisisitiza.

Moyes alisema Manchester United ni klabu kubwa na inapaswa kuwepo kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi na kuonyesha ushindani.

"Kwa wakati huu, tumeshindwa kufanya hivyo. Tunapaswa kulishughulikia tatizo hili,"aliongeza.

NANI KASEMA BONGO FLEVA HAILIPI?


MWAKA 2014 umeanza kwa wasanii kadhaa wa muziki wa kizazi kipya nchini, maarufu kwa jina la bongo fleva kuonyesha mali wanazozimiliki au nyumba walizojenga na kununua.

Lengo la wasanii hao kuonyesha mali zao hizo ni kuithibitishia jamii kwamba, muziki wa kizazi kipya unalipa, tofauti na mawazo yaliyotawala vichwani mwa watu wengi.

Alianza Naseeb Abdul 'Diamond', ambaye kupitia mitandao mbalimbali, alionyesha gari lake aina ya Land Cruiser lenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 60. Ni bonge la 'mkoko', si mchezo.

Akafuata Judith Wambura, maarufu kwa jina la Lady Jaydee. Naye pia alionyesha gari lake jipya aina ya Jaguar, lenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 20.

Hivi karibuni, mshindi wa shindano la Bongo Star Search (BSS), Emmanuel Msuya, ambaye alizawadiwa kitita cha sh. milioni 50, naye ameonyesha jinsi alivyozitumia pesa hizo.


Kabla ya kubahatika kupata kitita hicho cha pesa, Msuya hakuwahi kushika au kumiliki zaidi ya sh. 500,000. Aliwahi kupata kiasi hicho cha pesa mara moja, alipolipwa posho ya miezi mitatu iliyotokana na kuifundisha na kuisimamia kwaya ya KKKT kucheza ili ikafanye onyesho.

Mambo matatu makubwa, yaliyofanywa na Msuya baada ya kupata kitita hicho cha BSS ni kununua nyumba yenye thamani ya sh. milioni 17 iliyoko nyumbani kwao Musoma Mjini.

Msuya pia amenunua gari lenye thamani ya sh. milioni tisa na pia amejenga studio ya kurekodi muziki, ambayo imemgharimu sh. milioni 12 na tayari amepata nyumba ya kufanyia biashara ya vifaa vya shule katika moja ya mitaa ya Musoma Mjini.

Msanii mwingine aliyeamua kuweka mali zake hadharani ni Jux, ambaye hivi karibuni, video yake ya Uzuri wako, aliyeirekodi China, ilifungiwa kuonyeshwa kwenye luninga.



Jux aliamua kuonyesha gari lake jipya aina ya Nissan Fuga, lakini hakuwa tayari kutaja thamani yake. Lakini kwa kawaida, magari ya aina hii yanauzwa kati ya dola 2,000 na dola 4,000, ambazo ni zaidi ya sh. milioni sita za Kitanzania. Hapo bado gharama za kulisafirisha, kulipa ushuru na mambo mengine muhimu.

Kwa mujibu wa Jux, amenunua gari hilo kwa pesa, ambazo zimetokana na biashara anazozifanya. Hakuziweka wazi biashara hizo.

Naye David Geez, maarufu kwa jina la Young D, ameonyesha picha za nyumba aliyonunua maeneo ya Kimara Suka, Dar es Salaam.


Nyumba hiyo iliwahi kutumika ikiwa haijamaliziwa. Msanii huyo amesema ataifanyia ukarabati mkubwa ili iweze kufikia kiwango anachokitaka yeye kabla ya kuhamia na kuishi huko.

Msanii mwingine aliyeamua kuonyesha mali zake ni Barnaba Elias. Huyu alionyesha nyumba yake anayoijenga maeneo ya Tabata na gari lake jipya aina ya Toyota Mark X.


Barnaba ni msanii mwenye kipaji cha aina yake katika kuimba na kutunga nyimbo zenye mvuto. Amekuwa akialikwa kufanya maonyesho katika sehemu mbalimbali, ndani na nje ya nchi.

Msanii huyo wa kundi la THT pia amekuwa akipata dili kutoka kwenye mashirika, taasisi na kufanya nazo kazi mbalimbali, ikiwemo kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsui na benki ya Barclays.

Hii yote imedhihirisha kwamba, wasanii wa bongo fleva wanaweza kufaidika iwapo watakuwa na mpangilio mzuri wa matumizi kutokana na fedha wanazolipwa katika maonyesho na mauzo ya nyimbo na albamu zao.

Wapo baadhi ya wasanii waliobahatika kupata pesa nyingi miaka ya nyuma kutokana na muziki huo, lakini hawakuweza kufika popote kwa sababu ya kutokuwa na nidhamu katika matumizi ya pesa zao. Waliendekeza zaidi starehe.

Wednesday, January 29, 2014

KUMEKUCHA SIKINDE, YAIPUA VIBAO VIPYA SABA

Waimbaji wa bendi ya muziki wa dansi ya Mlimani Park, Hassan Bitchuka na Abdalla Hemba wakiwajibika jukwaani katika moja ya maonyesho yao.

BENDI ya muziki wa dansi ya Mlimani Park Orchestra 'Sikinde', imeanza kurekodi vibao vyake vipya saba, ikiwa ni maandalizi ya kuitambulisha albamu mpya.

Katibu wa bendi hiyo, Hamisi Milambo alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, kwanza kuanzia, wamesharekodi vibao vinne kati ya saba.

Milambo alisema wamerekodi vibao hivyo kwenye studio za Sound Crafters, zilizoko Temeke, Dar es Salaam.

Alivitaja vibao hivyo kuwa ni Tabasamu kilichotungwa na mwimbaji, Hassan Bitchuka, Mkwezi kilichotungwa na Abdalla Hemba, Nitalipa deni kilichotungwa na mpiga solo, Ramadhani Mapesa na Jinamizi la Talaka kilichotungwa na wanamuziki wote.

Milambo alisema vibao vingine vitatu, vinatarajiwa kurekodiwa mwishoni mwa wiki hii kwenye studio hizo. Alivitaja vibao hivyo kuwa ni Dole gumba, kilichotungwa na Bitchuka, Nundule kilichotungwa na Mapesa na Kibogoyo, kilichotungwa na wanamuziki wote.

Katibu huyo wa Sikinde alisema albamu mpya ya bendi hiyo itakuwa na vibao saba na itatambulishwa wakati wa tamasha la kusherehekea miaka 36 ya bendi hiyo.

"Tunachopenda kuwaeleza mashabiki wetu ni kwamba, Sikinde kwa sasa imekamilika katika kila idara. Kwa sasa tupo katika maandalizi ya kuzindua albamu yetu mpya na tayari tumesharekodi nyimbo mpya nne kati ya saba,"alisema.

Wakati huo huo, kwa mara ya kwanza, bendi ya Mlimani Park inatarajiwa kufanya onyesho kesho kwenye ukumbi wa Meeda ulioko Sinza, Dar es Salaam.

Milambo alisema jana kuwa, wameamua kufanya onyesho kwenye ukumbi huo kutokana na maombi mengi ya mashabiki.

Kwa mujibu wa Milambo, keshokutwa bendi hiyo itafanya onyesho kwenye ukumbi wa Pentagon, ulioko Kurasini wakati Jumapili itaendelea kuwapa maraha mashabiki wake kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo, Dar es Salaam.

Tuesday, January 28, 2014

MCD HATUNAYE



MPIGA tumba namba moja katika muziki wa dansi hapa nchini, Soud Mohamed 'MCD' wa Twanga Pepeta, amefariki dunia usiku huu mjini Moshi.

MCD alikuwa huko kwa zaidi ya miezi miwili akiugua na hali yake ilikuwa inaendelea vizuri lakini hali ikabadilika usiku huu na kuaga dunia.

Msemaji wa Twanga Pepeta, Hassan Rehani ameithibitishia Saluti5 kuwa MCD amefariki dunia.

Wiki iliyopita MCD aliongeana Saluti5 na kusema anaendelea vizuri na kwamba ile hatua ngumu ya dozi kali ya kifua kikuu alikuwa ameshaivuka na sasa amebadilishiwa dawa.

MCD aliongea kwa matumaini makubwa kuwa atarejea jukwaani muda si mrefu.

Majuzi MCD aliomba nauli ya kurejea Dar kwa uongozi wa Aset, jambo ambalo lilitekelezwa haraka na pengine kama siku zake za kuishi duniani zilikuwa bado zipo japo kwa wiki moja  mbele, MCD angeaga dunia akiwa Dar es Salaam.

Katika uhai wake bendi zingine alizozitumikia MCD ni  na Diamond Sound, Mashujaa Band.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Aset, Asha Baraka, mpiga tumba wa Twanga Pepeta, Soud Mohamed “MCD” aliyefariki Jumatatu (jana) usiku, mauti yalimfika mara tu baada ya kufika kwenye mlangowa hospitali ya KCMC Moshi.

Akiongea na Saluti5 muda mfupi baada ya taarifa za msiba, Asha Baraka alisema hadi mchana wa leo (Jumatatu) MCD alikuwa kwenye hali nzuri, lakini baadaye hali ikaanza kubadilika.

Asha Baraka anasema dada wa marehemu amemjulisha kuwa ilipofika usiku MCD aliendelea kujiskia ovyo na wakaamua kumkimbiza hospitali ya KCMC.

Lakini kwa mujibu wa maelezo ya dada huyo kupitia kwa Asha Baraka, MCD alifariki mara tu walipofika kwenye mlango wa hospitali hiyo.

Mwili wa MCD umehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti hospitalini hapo.
MCD alikuwa Moshi ambako ndiko nyumbani kwao alikozaliwa kwa ajili ya kujiuguza maradhi ya kifua kikuu.
IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA SALUTE 5.

BREAKING NEWSSSSS, MZEE DUDE WA FUTUHI AFARIKI



MUIGIZAJI WA KUNDI LA VICHEKESHO LA FUTUHI LA JIJINI MWANZA, LINALORUSHA MCHEZO WAKE KUPITIA RUNINGA YA STAR, MZEE DUDE, AMEFARIKI DUNIA, JANA SAA 12 JIONI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO, BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MFUPI. TAARIFA ZAIDI JUU YA KIFO CHAKE NA MAZISHI UTAENDELEA KUKUJUZUA!

HABARI HIZI NI KWA MUJIBU WA BLOGU YA STRAIKA.

YANGA YATUA TANGA, KUKIPIGA NA COASTAL UNION KESHO


Na Baraka Kaziguto, Tanga

Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans, imewasili
salama katika jiji la Tanga majira ya saa 6 kasorobo ikitokea jijini Dar es salaam
tayari kwa kuwakabili wenyeji timu ya Coastal Union siku ya Jumatano katika Uwanja
wa Mkwakwani.

Msafara wa watu 30 ukiwa na wachezaji 20, umewasili jijini Tanga na kufikia katika
hotel ya Central City, ambayo ndio huwa wanafikia siku zote na kikosi cha kocha
mholanzi Hans Van Der Pluijm jioni kimefanya mazoezi katika viwanja vya Gymkana
eneo la Raskazone kujiandaa na mchezo huo.

Kocha Mkuu Hans sambamba na wasaidizi wake Charles Mkwasa na Juma Pondamali
wamesema wamekuja na kikosi kilichokamilika na kushirikiana kwa pamoja na benchi
la ufundi wanaamini kitaibuka na ushindi hiyo siku ya jumatano.

Kocha msaidizi wa Young Africans Charles Mkwasa amesema vijana wake wote fit
kwa sasa baada ya kupata muda mzuri wa kupumzika kufuatia safari ndefu kutoka
nchini Uturuki mwishoni mwa wiki kisha kubadirisha hali ya hewa, na kwa sasa
anasema vijana wako vizuri.

Akiongelea mchezo wa kesho Mkwasa amesema anaua Coastal Union wana timu
nzuri ambayo imekua ikitoa upinzani mkali kwa timu nyingi za Ligi Kuu lakini anaamini
katika mchezo wa kesho jinsi walivyowaandaa vijana wake watafanya vizuri na
kuwapa furaha washabiki, wapenzi na wanachama wake.

Hali ya kikosi ni nzuri hata mara baada ya mazoezi ya leo hakuna mchezaji majeruhi
hata mmoja, hivyo wachezaji wote 20 waliokuja jijini Tanga wapo tayari kwa mchezo
huo wa kesho na kazi inabakia kwa benchi la ufundi kuchagua wamtumie nani katika
mchezo huo.

Mechi itaaanza majira ya 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki .
Viingilio vya mchezo:
Jukwaa Kuu Tshs 10,000/=
Mzunguko Tshs 5,000/=

Kikosi kilichopo jijini Tanga ni
Makipa: Juma Kaseja, Deogratias Munish "Dida" na Ally Mustafa "Barthez"
Walinzi: Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende, Mbuyu Twite, Kelvin Yondani,
Rajab Zahir na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Haruna Niyonzima, Hamis Thabit, Nizar Khalfan na Haruna Niyonzima
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Jerson Tegete, Mrisho Ngasa, Saimon Msuva,
Hussein Javu na Said Bahanuzi

TIKETI ZA ELEKTRONIKI ZIPO SOKONI



Mauzo ya tiketi za elektroniki kwa mechi tatu kati ya nne za Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) zitakazochezwa keshokutwa (Januari 27 mwaka huu) tayari yameanza, hivyo
wanatakiwa kununua mapema.

Mechi hizo ni kati ya Coastal Union na Yanga itakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar itakayochezwa Uwanja wa Kaitaba mjini
Bukoba na ile ya Azam dhidi ya Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Kwa washabiki wa Dar es Salaam watakaokwenda Tanga kushuhudia mechi kati ya
Coastal Union na Yanga wanashauriwa kuanza safari wakiwa na tiketi zao mikononi,
hasa kwa wale watakaonunua kupitia maduka ya Fahari Huduma.

Tiketi pia zinaweza kununuliwa kupitia mtandao wa M-Pesa kwa kupiga namba
*150*03*02#. Kwa wanaotumia CRDB simbanking wanaingia kawaida kwa *150*03.

Vilevile tunawakumbusha washabiki kuwa kwa viwanja ambavyo tayari vina mfumo
wa tiketi za elektroniki hakuna tiketi zitakazouzwa uwanjani, hivyo wanaokwenda
kwenye mechi wanatakiwa kuwa na tiketi zao mikononi.

YANGA YAINGIZA MIL 86/- SIMBA YAINGIZA MIL 53/-



Mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zilizohusisha timu za Simba na Yanga na kuchezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wikiendi zimeingiza jumla ya sh. 139,850,000.

Yanga iliyoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ashanti United pambano lake
liliingiza sh. 86,035,000 kutokana na watazamaji 14,261. Mechi ya Simba ambayo
ilishinda bao 1-0 dhidi ya Rhino Rangers kutoka Tabora iliingiza sh. 53,815,00 kwa
watazamaji 9,629.

Mgawanyo kwa mechi ya Yanga ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
13,123,983.05, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,910,300 wakati kila klabu ilipata sh.
20,650,211.50.

Uwanja sh. 10,500,107.54, gharama za mechi sh. 6,300,064.53, Bodi ya Ligi sh.
6,300,064.53, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,150,032.26 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,450,025.09.

Mechi ya Simba mgawo ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
8,209,067.80, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,910,300 wakati kila klabu ilipata sh.
12,595,211.50.

Uwanja sh. 6,404,344.83, gharama za mechi sh. 3,842,606.90, Bodi ya Ligi sh.
3,842,606.90, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,921,303.45 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,494,347.13.

Vilevile tiketi zinapatikana kupitia maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo
katika maeneo mbalimbali nchini. Watakaonunua kupitia maduka hayo watapata tiketi
na kwenda moja kwa moja uwanjani.

Sunday, January 26, 2014

SIMBA, YANGA, AZAM ZAANZA VYEMA MZUNGUKO WA PILI WA LIGI KUU



TIMU kongwe ya Simba jana iliuanza vyema mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka ya
Tanzania Bara baada ya kuichapa Rhino Rangers bao 1-0 katika mechi iliyopigwa
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao pekee na la ushindi la Simba lilifungwa na mshambuliaji machachari, Ramadhani
Singano 'Messi katika dakika ya 14.
Simba ilifanikiwa kupata mabao mengine mawili, moja katika kila kipindi, lakini
yalikataliwa na mwamuzi Andrew Shamba kwa madai kuwa yalitendeka madhambi
kabla ya mpira kujaa wavuni.
Simba ilipata nafasi nyingine nzuri ya kufunga bao kipindi cha pili baada ya
kuzawadiwa penalti, kufuatia beki mmoja wa Rhino kuunawa mpira ndani ya eneo la
hatari, lakini shuti la Messi lilimlenga kipa Charles Mpinuki wa maafande hao wa
jeshi.


Katika mechi zingine za ligi hiyo zilizochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita, mabingwa
watetezi Yanga waliichapa Ashanti mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Nayo Azam iliendelea kujichimbia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo baada ya
kuichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 kwenye uwanja wa Chamazi wakati Mbeya City
iliitambia Kagera Sugar ugenini baada ya kuichapa bao 1-0 kwenye Uwanja wa
Kaitaba.
Katika mechi zingine za ligi hiyo zilizochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita, Coastal
Union ilitoka sare ya bao 1-1 na JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Saturday, January 25, 2014

ILICHOSEMA YANGA BAADA YA OKWI KUFUNGIWA



Uongozi wa klabu ya Young Africans umeamua kuweka hadharani ukweli kuhusiana na usajili wa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi ambaye kamati ya maadili na hadhi za wachezaji imemzuia kuichezea Young Africana mpaka watakapopata uthibitisho kutoka FIFA.

Young Africans ilikamlisha usajili wa mshambuliaji huyo tangu Disemba 15 mwaka 2013, na kupata hati ya uhamisho wake wa kimataifa (ITC) ambayo iliwasilishwa TFF pamoja na fomu mama za usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Baada ya kukamilisha zoezi hilo TFF ilipitisha jina lake kwa kutupatia leseni no: 921225001 ambayo inamruhusu mchezaji kuichezea Young Africans na kisha kulituma CAF Disemba 31, 2013 kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika  ambapo CAF nao walimuidhinisha kuwa mchezaji halali wa Young Africans kwa mashindano hayo.

Cha kustaajabisha siku mbili kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Kamati ya Maadili na hadhi za wachezaji wakamzuia mchezaji huyo kuichezea Young Africans ilihali akiwa ameshaidhinishwa na TFF na CAF kuwa mchezaji halali wa Young Africans.

Swali?? walikuwa wapi Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji kujiridhisha juu ya usajili ambao ulishakamilika tangu Disemba 15 2013?

Wanakuja kutoa maamuzi hayo mwezi mmoja na nusu baada ya dirisha la usajili kufungwa, ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom??

Friday, January 24, 2014

LIGI KUU KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO,TIKETI ZA ELEKTRONIKI DAR BADO, MAKOCHA WAONYWA


Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza kesho (Januari 25 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa katika miji ya Bukoba, Dar es Salaam na Tanga.

Mabingwa watetezi Yanga watakuwa wageni wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati kwenye jiji hilo hilo Uwanja wa Azam Complex kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Azam FC na Mtibwa Sugar kutoka Morogoro.

Coastal Union na Oljoro JKT zitaumana kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Kagera Sugar ikiikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Raundi ya 14 ya ligi hiyo itaendelea Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi mbili. Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa shuhuda wa mechi kati ya Simba na Rhino Rangers kutoka Tabora wakati maafande wa JKT Ruvu na Mgambo Shooting watapambana Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Viingilio kwenye mechi ya Ashanti United na Yanga vitakuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Viingilio mechi ya Mkwakwani vitakuwa sh. 10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa Azam Complex sh. 10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa Kaitaba ni sh. 5,000 kwa sh. 3,000.

MECHI ZOTE TIKETI ELEKTRONIKI ISIPOKUWA TAIFA
Viwanja vyote ambavyo tayari vimefungwa mfumo wa elektroniki vitatumia tiketi za elektroniki isipokuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambao wenyewe utachelewa kidogo ili kuangalia kwanza mfumo huo unavyofanya kazi katika viwanja vingine.

Kwa viwanja vinavyotumia mfumo huo tiketi zinanunuliwa kupitia mtandao wa Vodacom ambapo mteja ni lazima awe amesajiliwa katika MPESA. Ataanza kwa kupiga *150*03*02# ambapo atapewa namba ya kumbukumbu anayotakiwa kuihifadhi kwani ataulizwa wakati anafanya malipo kwa kupitia MPESA ambapo ataingia kama kawaida kwa kutumia *150*00#.

Baada ya kulipa atapewa namba ya tiketi ambapo atakwenda kwenye mashine maalumu za kuchapa (printer) ambazo ziko katika vituo mbalimbali na kuchapa tiketi hiyo ambayo ndiyo atakayokwenda nayo uwanjani.

Njia nyingine ya kununua ni kwa wateja wa benki ya CRDB ambayo wamejisajili kwenye simbanking. Wao wataingia kwa kutumia *150*03# na kufanya malipo ya tiketi. Nao baada ya kupata namba watakwenda ku-print tiketi kwenye mashine hizo maalumu.

Vilevile tiketi zinapatikana kupitia maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo katika maeneo mbalimbali nchini. Watakaonunua kupitia maduka hayo watapata tiketi na kwenda moja kwa moja uwanjani.

DAR ES SALAAM
Kwa mechi za Dar es Salaam (Uwanja wa Azam) ambao ndiyo unaanza kutumia tiketi za elektroniki maduka ya CRDB Fahari Huduma yanayouza tiketi hizo ni; 1 Shs Distributors Limited (Mtoni Kwa Aziz Ally), ABC Computer (Mtaa wa Samora), Abdi Ally Abdi (Kariakoo), Aika- El Traders (Africana), Amaly Investment (Mtaa wa Sikukuu, Kariakoo), Athuman Fakhi Adam (Kongowe, Mbagala) na Bemuda Supplies Agency (Tegeta- Kibo Complex).

Benedict Traders (Barabara ya Uhuru/Lumumba), Ellytex Investment (Mtaa wa Indira Gandhi), Fedha Investment Limited (Pamba Road), Fuya Godwin Kimbita (Tegeta Block E), Hakika Limited (Mtaa wa Swahili, Kariakoo), Irice Stationary (Tegea Kwa Ndevu), Joshua Andrew Kisamo (Mtaa wa Kongo, Kariakoo), LB Pharmacy (Mtoni Kijichi) na Lista Phares Barnabas (Tabata Segerea).

L.M.S. Agro Chemical (Sokoni Kariakoo), Matei Laurent Kiria (Mbuyuni, Kinyerezi), Michael Elisante Mchomvu (Mtaa wa Sikukuu, Kariakoo), Palmall General Supplies (Barabara ya Shekilango), Rafabi Communications (Mtaa wa Livingstone, Kariakoo), Therry Inestment Limited (Tegeta Kibaoni) na Wemerick Independent Vehicle Diagnostic Company Limited (Mtaa wa Boko).

Mashine za kuchapia tiketi zipo matawi ya CRDB Azikiwe, Holland House (mashine mbili), Kariakoo, Tabata, Tegeta, Mbezi beach, Vijana na Quality Center. Mashine nyingine maeneo ya ATM ya Mtaa wa Shaurimoyo (mbili), Kawe Oilcom, Tabata Camel, Manzese, Ubungo Oilcom, Sabasaba na Mbagala Oilcom.


BUKOBA
Maduka ya CRDB Fahari Huduma ni Tak-Biir Investment Company (Mtaa wa Jamhuri, Bilele), Mary Mother of Peace Buhembe School (Sido Block, Rwamishenye), Muleba Secretarial Bureau (Nyerere Road), Akimu Abdallah Tirutoijwa (Mtaa wa Forodhani), Jamila Rajabu Songoro (Mtaa wa Jamhuri, Bilele), Rukia Kassim Mohamed (Mtaa wa Kashai, Kashenye) na Novath Michael Kibira (Uganda Road, Majengo).

Mashine tatu za kuchapia tiketi (printers) zipo Benki ya CRDB Tawi la Bukoba.

TANGA
Maduka ya CRDB Fahari Huduma ni Fax Auction Mart (Sabasaba Ground, Korogwe Road) na Rozalia Aloyce Masanja (Usagara, Block K). Mashine tatu za kuchapia tiketi (printers) zipo Benki ya CRDB Tawi la Tanga.

MBEYA
Maduka ya CRDB Fahari Huduma ni Blue Bird Bureau de Change (Lupa way), Meenda Pharmacy Limited (Maendeleo), Access Computer Limited (Lupa way, Sisimba) na Japhes James Mwanjisi (Mtaa wa Njisi). Mashine za kuchapia tiketi (printers) zipo Benki ya CRDB Tawi la Mbeya (mbili), Tawi la Mwanjelwa na Uyole.

MOROGORO
Duka la CRDB Fahari Huduma ni Shambani Graduates Enterprises Limited (Kihonda) na pia kutakuwa na gari za CRDB (Mobile bank). Mashine za kuchapia tiketi (printers) zipo Benki ya CRDB Tawi la Morogoro, Msamvu na Morogoro Agency.

ARUSHA
Maduka ya CRDB Fahari Huduma ni Fanuel John Andrew (Arumeru, Maji ya Chai), Robert William Maeda (Arumeru, Usa River), Wakwetu General Supplies (Mtaa wa Ngongongare, Arumeru), Wallace Ndawonga Mtawa (Kimandolu Suye), Side Corner Multi Business (Levolosi, Makao Mapya Street) na Albertha Ibrahimu General (Usa River Bus Stand).

Mashine za kuchapia tiketi (printers) zipo Benki ya CRDB Tawi la Arusha (mbili), Tawi la Meru, TFA, TRA Mapato na Ngaramtoni.

MWANZA
Maduka ya CRDB Fahari Huduma ni Majura General Supplies (Mecco Street), Prisca Joachim Kitani (Gilishi Street), Niche Consult (Nyerere Road), Deogratias Just Silayo (Malimbe, Mkolani), Yohana Ndili Mahago (Igoma Mashariki), Emily Elias Sambo (Sweya Street), Y Financing Limited (Kilimahewa) na Mangare Office Solutions (Station Road).

Makoye E. Serikali (Ilemela, Kiseke Street), Elizabeth George Kiwia (Uhuru Road), Mwalimu General Services (Kitangiri Road), George Edward Mulambo (Pasiansi), Nginila Office Solutions (Rufiji Street), Elvando IT Solutions (Nkrumah, Nyamagana), Sarimosa Company Limited (Kaluta Street) na Sahara Trasport and Scrappers Dealers (Mission, Pamba Road).

Mashine za kuchapia tiketi (printers) zipo CRDB matawi ya Mwanza, Nyerere na Mwaloni wakati nyingine zipo Nyanza, Buzuruga na Ilemela.

ONYO KWA MAKOCHA, MAOFISA HABARI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawakumbusha makocha na maofisa habari wa klabu za Ligi Kuu kujiepusha na kauli za chuki, uchochezi na uongo kwa shirikisho na waamuzi kila timu zao zinapofanya vibaya kwenye mechi.

Ni wajibu wa makocha kuzungumzia matokeo ya timu zao kiufundi badala ya kushambulia waamuzi na TFF kwa maneno makali. Pia maofisa habari nao wanatakiwa kuwa makini katika kauli zao kuhusiana na matokeo na masuala mengine.

Kwa wale watakaokwenda kinyume TFF itawafikisha kwenye vyombo vya kinidhamu na maadili kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki.

Thursday, January 23, 2014

VIONGOZI WAMALIZA TOFAUTI ZAO, RAGE AIONYA YANGA KUHUSU KAPOMBE



NA AMINA ATHUMANI

KAMATI ya utendaji ya Simba pamoja na Mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Rage wamemaliza tofauti zao .

Rage na Kamati ya Utendaji ya Simba walikuwa na mgogoro uliosababisha kutoweka kwa amani ndani ya klabu hiyo kongwe nchini.

Katika kikao cha makubaliano hayo kilichofanyika juzi usiku wamekubaliana kushirikiana na kuacha yale yote yaliyojitokeza katika kipindi cha nyuma na kusababisha kuwepo kwa mgogoro ndani ya klabu hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Rage alisema anashukuru kumaliza tofauti zao na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo na sasa amani imetawala.

"Kikao cha jana (juzi) tumekubaliana tuwe kitu kimoja na kufanya kazi kwa ushirikiano na hakuna tena mgogoro ndani ya klabu yetu,"alisema Rage.

Rage alitoa wito kwa wanachama wa klabu hiyo wasijaribu tena kuigawa klabu hiyo kwa kuwa inaathiri mfumo mzima wa maendeleo ya soka katika klabu hiyo.

Mgogoro wa Simba na Rage ulizuka baada ya Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kufanya mapinduzi ya kumsimamisha Mwenyekiti huyo kwa madai kuwa amekuwa akijiamulia mambo kinyume na matakwa ya kamati hiyo.

Hata hivyo, mapinduzi hayo yalipingwa na Shirikisho la Soka Tanzania  TFF, ambalo lilisema Rage ndiye Mwenyekiti halali wa klabu hiyo.

Wakati huo huo, Rage alizionya klabu za soka nchini zinazomtumbulia macho beki wao, Shomari Kapombe kwa vile ni mali ya Simba kwani mkataba wake unamalizika 2016.

Alisema pia kuwa, suala la Kapombe na klabu ya Cannes ya Ufaransa, aliyokuwa akiichezea,
limemalizika na sasa mchezaji huyo atarejea nchini kuendelea na kabumbu.

Alisema Kapombe alikuwa akiidai klabu hiyo mshahara wake wa Novemba ambapo tayari amezungumza na mkurugenzi wa timu hiyo na ameahidi kuilipa fedha hiyo ndani ya wiki hii.

Alisema kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, wanamuhitaji Kapombe kwani ni mchezaji aliyeonekana na uwezo mkubwa wa kisoka.

Pia Rage alisema Kapombe alikaa nje ya uwanja siku 72 kutokana na kuwa majeruhi katika kidole gumba cha mguu hivyo hali hiyo pia ilichangia kucheleweshwa kwa mshahara huo.

MKUTANO MKUU SIMBA MACHI 23, MZEE KINESI AVULIWA UMAKAMU MWENYEKITI, KAMWAGA KATIBU MKUU MPYA, ASHA MUHAJI AWA OFISA HABARI



NA AMINA ATHUMANI

MWENYEKITI wa Klabu ya Simba Ismail Rage amesema ataitisha mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo utakaofanyika Machi 23 mwaka huu.

Mkutano huo utakuwa na ajenda moja tu ya marekebisho ya katika ya klabu hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Rage alisema atauendesha mkutano huo kwa ajenda moja kwani tayari mkutano wa kikatiba wa klabu hiyo wa kila mwaka ulishafanyika Agosti mwaka jana.

"Mkutano huu utakuwa na ajenda  moja tu na yoyote atakayeleta mambo ambayo hayamo ndani ya ajenda hiyo nitamkalisha chini ama kumtoa nje  ya ukumbi, mimi ndiye nitakayeendesha mkutano huo kama vile Spika wa bunge anavyolimiliki bunge lake na sitaruhusu mtu akurupuke kama vile anatoka chooni,"alisema Rage.

Rage alisema amepata barua mbili kutoka Shirikisho la soka Tanzania (TFF) moja  ikitumwa Desemba 2 na nyingine Desemba 30 ambazo zimetaka vyama kufanya marekebisho ya katiba zao huku nyingine ikimtaka aitishe uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya makamu Mwenyekiti.

Rage alisema katika marekebisho ya Katiba amegundua kuna upungufu katika katiba ya Simba  ambayo haina kamati ya maadili na katika mkutano huo wataiweka kamati hiyo baada ya marekebisho hayo.

Alisema pia ndani ya Katiba ya Simba amegundua vipo vipengele vya Simba ambavyo vimepitwa na wakati hivyo vinahitaji kuondolewa.

Alisema pia kuanzia sasa klabu ya Simba haina makamu Mwenyekiti nafasi ambayo ilikuwa ikiongozwa na Joseph Itang'are 'kinesi' na kwamba ataiomba TFF kama itawezekana kuufanya uchaguzi mkuu mapema kwa kuwa mchakato wa kufanya uchaguzi mdogo utatatakiwa kufanyika ndani ya siku 90.

"Kwa maana hiyo ukifanya mchakato ndani ya siku 90 na sisi kikatiba tunatakiwa kufanya uchaguzi Juni, huyo atakayechaguliwa atakaa madarakani kwa mwezi mmoja tu itakuwa haina maana yoyote,"alisema Rage.

Alisema kwa maana hiyo nafasi hiyo ni bora ibaki wazi hadi hapo uchaguzi mkuu utakapofanyika kwani katiba ya Simba ipo wazi na atakapokuwa hayupo nchini atamteuwa mtu yoyote ndani ya Sekretarieti ya Simba kukaimu nafasi yake.

Wakati huo huo, Rage amemteuwa Ezekiel Kamwaka kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo akisaidiana na Stanley Philipo na nafasi ya Ofisa Habari akimpa Asha Muhaji.

KUMEKUCHA LIGI KUU BARA


MZUNGUKO wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara, unatarajiwa kuanza kutimua vumbi keshokutwa katika mechi tano zitakazochezwa kwenye viwanja vitano tofauti.

Katika mechi hizo, mabingwa watetezi Yanga watamenyana na Ashanti kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na maandalizi yaliyofanywa na kila timu. Katika mechi ya mzunguko wa kwanza, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-1.

Yanga iliweka kambi Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko huo na inatarajiwa kurejea nchini kesho. Ashanti ilitumia mashindano ya Kombe la Mapinduzi kujiandaa na mzunguko huo.

Katika mechi zingine zitakazochezwa keshokutwa, Azam wataikaribisha Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Chamazi, ulioko Mbagala, Dar es Salaam, Coastal Union itakipiga na JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Mkwakwa, Tanga, Kagera Sugar itavaana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba wakati Prisons itamenyana na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.

Awali, mechi kati ya Prisons na Ruvu ilipangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Sokoine wa Mbeya, lakini imehamishiwa Samora kutokana na eneo la kuchezea mpira kutokuwa  na nyasi.

Uwanja wa Sokoine ni miongoni mwa viwanja sita vilivyofungiwa na Bodi ya Ligi Kuu kutumika katika ligi kutokana na kuwa na kasoro mbalimbali.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho wakati timu kongwe ya Simba itakapomenyana na Rhino Rangers ya Tabora wakati JKT Ruvu itamenyana na ndugu zao wa Mgambo JKT kwenye uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema jana kuwa, maandalizi yote muhimu kwa ajili ya mechi hizo yamekamilika.

Wambura alisema pia kuwa, matumizi ya tiketi za elektroniki yanaanza katika mzunguko huu kwa vile tayari viwanja vinane vimeshafungwa vifaa vya tiketi hizo.

Ofisa huyo wa TFF alitoa onyo kwa mashabiki kuepuka kununua tiketi kupitia mikononi mwa watu binafsi kwa vile tiketi za elektroniki haziuzwi viwanjani.

YANGA UTAIPENDA, INAREJEA NCHINI KESHO





Na Baraka Kaziguto, Uturuki

KOCHA Mkuu mpya wa Yanga,  Hans Van Der Plyum, amesema amefurahishwa na nidhamu iliyoonyeshwa na wachezaji wa timu hiyo katika muda wote aliokaa nayo kambini Uturuki.

Hans amesema wachezaji wote waliosajiliwa na Yanga wana uwezo mzuri wa kucheza soka, wanajituma, wana nidhamu na upendo wa hali ya juu miongoni mwao.

Kocha huyo kutoka Uholanzi, alisema hayo jana baada ya mazoezi yaliyofanyika asubuhi kwenye hoteli ya Sueno iliyoko katika mji wa Antalya.

"Nina uzoefu na soka ya Afrika kwa takribani miaka 15. Wachezaji niliowakuta hapa
wana uwezo mzuri wote, wanajituma, wana nidhamu na upendo wa hali ya juu kitu ambacho kwa mwalimu yoyote lazima atafurahia mazingira hayo kwani hata ufanyaji wake kazi unakuwa mzuri, "alisema Hans.

Kocha huyo aliyerithi mikoba ya Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts, alisema kwa muda wa siku tisa alizokaa na timu hiyo Uturuki, anaamini kikosi chake kipo tayari kutetea ubingwa wa ligi kuu na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Hans alisema kwa siku 14, ambazo Yanga imeweka kambi nchini humo, wachezaji na benchi la ufundi wameweza kutimiza wajibu wao vizuri kwa kufanya mazoezi kwa bidii na kucheza mechi za kirafiki za kujipima nguvu

Yanga imecheza mechi nne za kirafiki dhidi ya Ankara Sekerspor na Altay SK zinazoshiriki ligi daraja la pili Uturuki kabla ya kuivaa KS Flumartari ya Albania na
Simurq PIK ya Azerbajain. Ilishinda mechi mbili na kutoka sare mbili.
  
   KUREJEA NCHINI KESHO
Wakati huo huo, kikosi cha Yanga kilichokuwa kambini Uturuki, kinatarajiwa kuondoka hapa leo mchana kurejea nchini.

Yanga ilifanya mazoezi yake ya mwisho jana asubuhi na jioni, chini ya Kocha Hans kwa ajili ya kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika mechi nne za kirafiki ilizocheza.

Kocha Hans alisema jana kuwa, hadi sasa hakuna mchezaji aliye majeruhi na kwamba wachezaji wote wapo fiti tayari kwa mechi yao ya kwanza ya mzunguko wa pili wa ligi kuu dhidi ya Ashanti.

Yanga na Ashanti zinatarajiwa kushuka dimbani keshokutwa katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mechi ya mzunguko wa kwanza, Yanga iliibugiza Ashanti mabao 5-1.

   SEIF ATAMBA
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa wa Yanga, Seif  Ahmed 'Magari' amesema watahakikisha kikosi chao  hakifungwi katika mechi za mzunguko wa pili wa ligi kuu.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Zanzibar jana, Seif alisema kamati yake itatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa wachezaji na benchi la ufundi ili kuwaongezea ari ya kufanya vizuri na kutetea ubingwa wa ligi.

Seif alisema mara baada ya timu hiyo kutua nchini kesho alfajiri ikitokea Uturuki, itakwenda kambini moja kwa moja kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao ya ligi dhidi ya Ashanti.

Yanga na Ashanti zinatarajiwa kushuka dimbani keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mechi ya mzunguko wa kwanza, Yanga iliibugiza Ashanti mabao 5-1.

"Tumepanga kukutana na wachezaji na kocha baada ya timu kurejea nchini Ijumaa kutoka Uturuki ili kupanga mikakati. Safari hii nawahakikishia wanachama na wapenzi wa Yanga kwamba hatutafungwa mechi yoyote,"alitamba.

Seif alisema pia kuwa, wameshaanza kufanya upelelezi dhidi ya timu ya Komorozine Sports ya Comoro, watakayopambana nayo katika michuano ya klabu bingwa Afrika mwezi ujao.

OKWI APIGWA STOP YANGA


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana mjini Dar es Salaam jana, kupitia masuala mbalimbali, imesimamisha usajili huo baada ya kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.

Okwi, ambaye aliingia mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia, aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya Etoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.

Katika FIFA, kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo, ambayo
ni dola za Marekani 300,000.

"Hivyo, TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake,"alisema Wambura.

WANAMUZIKI WA MLIMANI PARK WAPO KAZINI

WANAMUZIKI wa bendi ya Mlimani Park Orchestra wakiwajibika jukwaani wakati ilipofanya onyesho mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo, Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni mpiga gita la solo, Adolph Mbinga, waimbaji Hassan Bitchuka, Abdalla Hemba na Musemba wa Minyigu.(Picha na Emmanuel Ndege).

ROSE MUHANDO: SIJAWAHI KUTAFUNA PESA ZA PROMOTA NA KUINGIA MITINI


MWIMBAJI nyota wa nyimbo za muziki wa Injili nchini, Rose Muhando amesema kamwe hajawahi kutafuna pesa za mapromota na kukwepa kufanya maonyesho.

Rose amesema kwa kipindi cha miezi sita iliyopita, ameshindwa kushiriki kwenye matamasha mbalimbali ya muziki huo kutokana na binti yake kuwa mgonjwa.

Mwimbaji huyo anayeongoza kwa mauzo ya nyimbo za muziki wa Injili, ametoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya mapromota kwamba, amekuwa akilipwa pesa na kukwepa kushiriki kwenye maonyesho yao.

Malalamiko mengine yaliyokuwa yakimuhusisha msanii huyo ni baadhi ya mapromota kuonekana waongo kwa kutumia jina la Rose wanapoandaa matamasha kwa lengo la kuvuta idadi kubwa ya mashabiki.

Hii ilifanya baadhi ya watu kukwazika, baadhi ya mapromota kuonekana waongo na kuonekana kama walitaka kujikusanyia kiingilio au kupata idadi kubwa ya watu kwa kutumia tu jina la Rose lakini hakuna kitu.

"Kwa kipindi cha miezi sita sikuweza kwenda kwenye tamasha lolote lile kwa sababu binti yangu ni mgonjwa mpaka sasa,"amesema Rose alipokuwa akihojiwa na kituo cha redio cha Clouds FM juzi.

"Sina tabia hiyo na wala siwezi kufanya hicho kitu. Kila ambaye amenilipa pesa yake, nimeanza kuzirudisha tangu muda mrefu uliopita. Nawaomba wawe na amani na mimi niwe na amani," amesema mwanamama huyo mwenye watoto wanne.

"Mimi ni mama na ni binadamu kama wengine na ninapata matatizo ndio maana siwezi kumuacha binti yangu hoi kitandani wakati ananitegemea mama yake mzazi.Hata roho mtakatifu ataniona ni mwanamke mjinga kuliko wote, ni heri niwe sina kitu manake kama sina, Bwana Yesu atanipa tu, atanipa mara mia zaidi," amesisitiza mwimbaji huyo.

Katika hatua nyingine, Rose amesema tangu alipoingia mkataba na Kampuni ya Sony ya Afrika Kusini, amefanikiwa kurekodi wimbo mmoja unaokwenda kwa jina la Yesu kung'uta.

Rose amesema alirekodi video ya wimbo huo, ambao pia unajulikana kwa jina la Wololo, nchini Afrika Kusini. Alirekodi wimbo huo Julai mwaka jana.

Mwimbaji huyo machachari, aliingia mkataba na Sony miaka miwili iliyopita kwa lengo la kuongeza mapato na kujitangaza kimataifa.

Kwa mujibu wa Rose, wimbo huo ulichelewa kutoka kwa sababu ilibidi amalizie kurekodi video kwa vile isingekuwa rahisi kutoa audio kabla ya video.

"Hii ni kwa mujibu wa taratibu za ofisi, huwezi kutoa audio kabla ya video,"amesema Rose.
Mwanadada huyo amesema, tangu alipoanza kufanyakazi na Sony, ameona tofauti kubwa, ikiwa ni pamoja na kutoachiwa kufanya vitu vyote peke yake.

"Vitu vingi sifanyi mwenyewe, ninachofanya ni kuandaa nyimbo zangu ila vingine sijui nitavaa nguo gani, nitapanda gari au ndege gani, kila kitu ni wao," amesema.

Rose amesema tangu alipoanza kufanyakazi na Sony, wapo wanaoufurahia uamuzi wake huo, lakini wengine wamechukia, lakini kamwe hawezi kuwajali.

"Mungu akisema imeandikwa, nitafanya kama ilivyoandikwa. Mungu akiniambia fanya, ninafanya, haijalishi kuna mtu anataka au kuna mtu hataki," amesema Rose.

SIKU ZOTE NILIKUWA WA MWISHO KULIPA ADA YA SHULE-RITHA


LAGOS, Nigeria
MCHEZA filamu Ruth Kadiri wa Nigeria amethibitisha taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni kwamba, siku zote alikuwa mwanafunzi wa mwisho kulipa ada ya shule katika darasa lake wakati alipokuwa anasoka sekondari.

Binti huyo, ambaye anatoka katika familia maskini, kwa sasa ana shahada ya kwanza ya mawasiliano ya umma, aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Nigeria.

"Ni kweli siku zote nilikuwa wa mwisho kulipa ada ya shule. Nakumbuka nilipokuwa kidato cha tatu, wanafunzi wenzangu wawili waliacha shule kwa sababu ya kushindwa kulipa ada," amesema mwanadada huyo msomi.

Ruth amesema kwa sasa anaye mpenzi, lakini hakuwa tayari kutaja jina lake kwa hofu ya kuandamwa na vyombo vya habari.

"Nafikiri kumpenda mtu hakuwezi kuamua furaha yako, lakini unapojipenda wewe mwenyewe kuliko unavyompenda mtu mwingine, kunakupa furaha kubwa,"amesema.

Ruth amesema kujipenda kwake binafsi ndiyo siri kubwa ya furaha yake.

"Unataka kusema kwamba kama sipo kwenye uhusiano, furaha itakuwa mbali na mimi? Hapana. Mapenzi ni kitu kizuri na chakula katika mioyo yetu, lakini nimeshafikia hatua ya kujitambua mimi ni nani,"amesema.

Alipoulizwa ni lini anatarajia kufunga ndoa, Ruth alisema: "Naomba kwa Mungu iwe hivyo kwa sababu mpenzi wangu ni mtu anayeheshimu hisia zangu, ananiunga mkono katika kazi yangu na amenionyesha mapenzi mwanana."

ALICHI: SIWEZI KUCHEZA FILAMU ZA NGONO


LAGOS, Nigeria
CHIZZY Alichi ni mwigizaji mpya wa filamu nchini Nigeria, lakini ameweza kujipatia sifa na umaarufu kutokana na staili yake ya uigizaji.

Ni mwigizaji mwenye umbo lenye mvuto, akiwa na macho ya kuvutia. Sifa zake katika kucheza filamu, hazina tofauti na zile za Genevieve Nnaji, Ini Edo au Mercy Johnson.

Akihojiwa na mtandao wa naijerules hivi karibuni, Alichi alisema ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi yoyote atakayopangiwa na mtayarishaji wa filamu.

Alichi anasema mwanaume wa kwanza kupigana naye mabusu kwenye filamu, alikuwa Kenneth Okonkwo. Anasema alijisikia raha kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba, siku zote amekuwa akivutiwa na uigizaji wa Okonkwo.

"Nimepigana mabusu mara nyingi na waigizaji tofauti. Mara ya kwanza ilikuwa kwa Okonkwo,"amesema Alichi. 

"Ni mwigizaji ninayevutiwa naye, hivyo kupigana naye mabusu kilikuwa kitendo chenye maana kubwa kwangu. Aliyapokea vizuri mabusu yangu," aliongeza binti huyo mantashau.

Alichi amesema si kweli kwamba, msanii wa filamu anaweza kupata umaarufu kwa kucheza filamu ya ngono. Amesema binafsi anaweza kucheza nafasi yoyote katika filamu, lakini siyo ile itakayomwonyesha akiwa uchi.

"Nataka niwe mfano mzuri wa kuigwa na wasanii wengine, na pia natarajia kuolewa na kupata watoto. Watajisikiaje kumuona mama yao akicheza filamu ya aina hiyo?" Amehoji.

"Wazazi wangu wananiunga mkono, lakini hawawezi kufanya hivyo iwapo nitacheza filamu za ngono. Naweza kuvaa mavazi yenye mvuto wakati wa kucheza filamu, lakini sio kuwa uchi ama kucheza filamu ya ngono," amesisitiza.

Alichi amesema kwa sasa haoni aibu anapokuwa mbele ya kamera kama ilivyokuwa zamani kwa vile ameshaizoea kazi hiyo. Anasema anapenda uigizaji na amekuwa akiifanyakazi hiyo kwa umakini mkubwa.

Hata hivyo, Alichi amesema linapokuja suala la maisha yake binafsi, bado yeye ni msichana mwenye aibu.

Wednesday, January 22, 2014

RATIBA YA MZUNGUKO WA PILI WA LIGI KUU TZ BARA


Januari 25, 2014
Ashanti Utd   vs   Yanga SC 
Azam FC    vs Mtibwa S 
Coastal U    vs JKT Oljoro 
Kagera S    vs Mbeya City 
Prisons  vs R.Shooting 
Januari 26, 2014
JKTRuvu    vs Mgambo 
Simba SC    vs Rhino
***********
 
Januari 29, 2014  
Kagera S    vs Mtibwa  Azam FC    vs Rhino 
Prisons    vs JKTRuvu 
Ruvu Shooting   vs Mbeya City 
Coastal U    vs Yanga SC 
Februari 1, 2014
Ashanti Utd   vs Mgambo 
Simba SC    vs JKT Oljoro 
**********
Februari 2, 2014
Yanga SC  vs Mbeya City 
Prisons    vs Coastal 
Mgambo   vs  Ruvu Shooting
Azam FC    vs Kagera Sugar
Februari 5, 2014
Mtibwa S    vs Simba SC 
Rhino     vs  JKT Oljoro 
JKTRuvu    vs Ashanti Utd 
************
Februari 9, 2014
Mgambo     vs  Simba SC 
JKT Oljoro   vs Kagera S 
Rhino     vs  Coastal U 
Mbeya City   vs Mtibwa 
JKTRuvu    vs R.Shooting
Februari 15, 2014
Rhino     vs  Mgambo 
Ashanti Utd   vs Kagera
***********
Februari 15, 2014
Mtibwa S    vs Prisons 
JKT Oljoro   vs JKTRuvu 
Mbeya City   vs Simba SC 
Ruvu Shooting   vs Coastal U 
Februari 22, 2014

Ruvu Shooting   vs Yanga SC 
Kagera S    vs Rhino 
Mtibwa S    vs Ashanti Utd 
************
Februari 22, 2014
Coastal U  vs Mbeya City 
JKT Oljoro   vs Mgambo 
Azam FC    vs Prisons
Februari 23, 2014
Simba SC    vs JKTRuvu 
Februari 26, 2014
Yanga SC    vs Prisons 
Ashanti Utd   vs Azam FC 
Machi 2, 2014
Simba SC    vs R.Shooting 
*************
Machi 2, 2014
Kagera S    vs JKTRuvu 
Mbeya City   vs JKT Oljoro 
Ashanti Utd   vs Rhino 
Prisons    vs Mgambo 
Machi 8, 2014
Mbeya City   vs Rhino 
R.Shooting   vs JKT Oljoro 
Prisons    vs Simba SC 
*************
Machi 8, 2014
Coastal U    vs Ashanti Utd 
Machi 9, 2014
JKTRuvu    vs Mtibwa S 
Machi 12, 2014
Simba SC    vs Coastal 
Mgambo     vs  Mtibwa 
Machi 15, 2014
Azam FC    vs Coastal 
Mtibwa S    vs Yanga SC 
Kagera S    vs Prisons 
*************
Machi 15, 2014
R.Shooting   vs Ashanti Utd 
Machi 16, 2014
JKTRuvu    vs Mbeya City 
Machi 19, 2014
Yanga SC    vs Azam FC 
Mbeya City   vs Prisons 
Machi 23,2014
Ashanti Utd   vs JKT Oljoro 
Kagera S    vs R.Shooting 
Mtibwa S    vs Coastal U 
**************
Machi 23, 2014
JKTRuvu    vs Rhino 
Kagera S    vs R.Shooting 
March 26, 2014
Azam FC    vs Simba SC 
March 26, 2014
Mgambo     vs  Yanga SC 
March 30, 2014
Coastal U    vs Mgambo
JKT Oljoro   vs Prisons 
Rhino     vs  Mtibwa S 
***************
Machi 30, 2014
Ashanti Utd   vs Mbeya City 
Aprili 2, 2014
R.Shooting   vs Azam FC 
Yanga SC    vs JKTRuvu 
Aprili 6, 2014
Mgambo     vs  Azam FC 
Rhino     vs  Yanga SC 
Mtibwa S    vs R.Shooting 
Aprili 9, 2014
Yanga SC    vs Kagera S 

***************
Aprili 9, 2014
Azam FC    vs JKT Oljoro
Coastal U    vs JKTRuvu 
Aprili 12, 2014
Mgambo     vs  Kagera 
Prisons    vs Rhino 
Aprili 13, 2014
Simba SC    vs Ashanti Utd 
Aprili 23, 2014
Mbeya City   vs Azam FC 
JKT Oljoro   vs Yanga SC 
***************
Aprili 27, 2014
Rhino     vs  R.Shooting 
Mbeya City   vs Mgambo 
Prisons    vs Ashanti Utd 
JKTRuvu    vs Azam FC 
JKT Oljoro   vs Mtibwa 
Coastal U    vs Kagera 
Yanga SC    vs Simba SC 
***************

KILI MARATHONI MAMBO YAIVA, VIINGILIO VYATAJWA


Na Ibrahim Kyaruzi, Dar es Salaam
MAANDALIZI ya mbio za 12 za Kilimanjaro Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi 2, 2014 huko Moshi yanaendelea kushika kasi baada ya waandaaji wa mbio hizo kutangaza ada za ushiriki pamoja na ratiba ya mbio hizo.

John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kwamba mbio ndefu za 42km Kilimanjaro Premium Lager Marathon zitaanza saa 12:30 asubuhi huku mbio za 10km Gapco Disabled Marathon zikianza saa 12:45 asubuhi, Nusu Marathon km 21 saa 1 kamili asubuhi na mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run zitaanza saa moja na robo asubuhi. 
Alisema ratiba hii imepangwa kwa mtiririko huu ili kuwapa fursa washiriki wa kila mbio kuona mandhari ya mji wa Moshi na Mlima Kilimanjaro.
Alisema kuwa viingilio vya mbio ndefu za Full Marathon km 42 viingilio itakuwa ni dola 60 kwa washiriki wa kimataifa, Tsh 6,000 kwa raia wa Afrika Mashariki na dola 30 kwa raia wa kigeni wanaoishi au kufanya kazi Afrika Mashariki wakati huku Nusu Marathon viingilio ikiwa ni dola 60 kwa washiriki wa kimataifa, shilingi 4,000 kwa raia wa Afrika Mashariki na dola 30 raia wa kigeni wanaoishi Afrika Mashariki
Aidha, washiriki wa kimataifa kwenye mbio za walemavu za GAPCO watalipia dola 10, shilingi 3,000 kwa raia wa Afrika Mashariki na dola tano kwa raia wa kigeni wanaoishi Afrika Mashariki.

Mbio hizo za walemavu zitahusisha shindano la mbio za kutumia baiskeli za mikono (Handcycle) na viti vyenye magurudumu (Wheelchair) tu. Washiriki wa kimataifa na raia wa kigeni waishio Afrika Mashariki watalipa dola mbili na raia wa Afrika Mashariki watalipa shilingi 3,000 mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run.
Kwa mujibu wa Addison, umri wa kushiriki mbio za kilomita 42 ni miaka 21, miaka 18 kwa nusu marathon na mbio za walemavu huku kwenye mbio za kujifurahisha ikiwa ni miaka kumi. "Tutasajili washiriki kwa muda wa siku mbili kabla ya mbio ambapo kwenye hoteli ya Keys Hotel mjini Moshi tarehe 28 Februari na tarehe 1 Machi kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 11 jioni kila siku na pia uandikishwaji utafanyika Arusha tarehe 27 Februari katika eneo ambalo litatangazwa badae," alisema.
Mbio hizo zinadhaniwa kuwa kati ya mbio kubwa zaidi duniani za kitalii na ndio tukio kubwa zaidi la kimichezo Tanzania. Kilimanjaro Marathon ya mwaka huu inatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 6,000 wakiwemo takribani wageni 600 kutoka nchi zaidi ya 40.
Kilimanjaro Marathon 2014 inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager (wadhamini wakuu), Vodacom Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (10km Disabled Run), FNB Tanzania, TPC Sugar, Simba Cement, KK Security, Kilimanjaro Water, Keys Hotel, TanzaniteOne na UNFPA.

Tuesday, January 21, 2014

BAWAZIR AIPIGA JEKI UHURU SC


Mwenyekiti wa CCM kata ya Jangwani, Mohamed Bawazir akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mwenyekiti wa CCM kata ya Jangwani, Mohamed Bawazir (kulia) akikabidhi mpira kwa Katibu wa klabu ya michezo ya Uhuru, Rashid Zahor (kushoto), ikiwa ni sehemu ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. 450,000 alivyotoa msaada kwa timu hiyo juzi katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Uhuru Publications Ltd, inayochapisha magazeti ya Uhuru, Mzalendo la Burudani, zilizoko barabara ya Lumumba, Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM tawi la Uhuru, Chamwingi Mpondachuma. (Picha na Yassin Kayombo).

Mwenyekiti wa CCM kata ya Jangwani, Mohamed Bawazir (kulia) akikabidhi jezi kwa Katibu wa klabu ya michezo ya Uhuru, Rashid Zahor (kushoto), ikiwa ni sehemu ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. 450,000 alivyotoa msaada kwa timu hiyo juzi katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Uhuru Publications Ltd, inayochapisha magazeti ya Uhuru, Mzalendo la Burudani, zilizoko barabara ya Lumumba, Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM tawi la Uhuru, Chamwingi Mpondachuma
 
Mwenyekiti wa CCM kata ya Jangwani, Mohamed Bawazir (kulia) akikabidhi jezi kwa Katibu wa klabu ya michezo ya Uhuru, Rashid Zahor (kushoto), ikiwa ni sehemu ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. 450,000 alivyotoa msaada kwa timu hiyo juzi katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Uhuru Publications Ltd, inayochapisha magazeti ya Uhuru, Mzalendo la Burudani, zilizoko barabara ya Lumumba, Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM tawi la Uhuru, Chamwingi Mpondachuma
Bawazir akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Uhuru SC na wajumbe wa kamati ya siasa na halmashauri kuu ya tawi la CCM la UPL


MWENYEKITI wa CCM kata ya Jangwani, Ilala, Dar es Salaam, Mohamed Bawazir, ametoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu ya soka ya Uhuru.

Bawazir alikabidhi vifaa hivyo vya michezo kwa Katibu wa Uhuru SC, Rashid Zahor, katika hafla iliyofanyika juzi kwenye ofisi za CCM za tawi la Uhuru, zilizopo barabara ya Lumumba, Dar es Salaam.

Uhuru SC, inaundwa na wafanyakazi wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, inayochapisha magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani pamoja na kituo cha Redio cha Uhuru FM.

Vifaa vilivyotolewa na Bawazir kwa Uhuru SC ni seti moja ya jezi na mpira mmoja, vyote vikiwa na thamani ya sh. 450,000.

Akizungumza katika hafla hiyo, Bawazir alisema jezi hizo na mpira ni sehemu ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni tano, anavyotarajia kuvitoa kwa timu mbalimbali za soka za kata ya Jangwani.

Alisema ameamua kutoa vifaa hivyo kwa lengo la kutekeleza kwa vitendo ilani ya CCM na pia kuendeleza soka katika kata hiyo kwa kuzisaidia timu zinazoshiriki katika ligi za madaraja mbalimbali ili ziweze kupata mafanikio.

"Nimeamua kuanzia na timu ya Uhuru kwa sababu hapa ndiko nilikolelewa. Uhuru ni nyumbani kwangu. Nitaendelea kuisaidia timu yenu kila nitakapopata nafasi na uwezo wa kufanya hivyo,"alisema.

Mwenyekiti huyo wa CCM kata ya Jangwani pia aliahidi kutoa vifaa vya michezo kwa timu ya netiboli ya Uhuru, ambayo pamoja na ya soka, zinatarajiwa kushiriki kwenye mashindano ya kuwania Kombe la Shirika la  Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa Machi mwaka huu.

Naye Mwenyekiti wa CCM tawi la Uhuru, Chamwingi Mpondachuma, alimshukuru Bawazir kwa msaada huo wa vifaa vya michezo na kuahidi kuutumia vyema kuwashirikisha wafanyakazi wa UPL katika michezo.

Mpondachuma alisema msaada huo umeonyesha wazi dhamira ya Bawazir katika kuendeleza michezo katika kata yake na pia kutekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM.

Katibu wa Uhuru SC, Zahor alimuomba Bawazir, azitafutie wadhamini timu za soka na netiboli za UPL ili ziweze kucheza mechi mbalimbali za kirafiki.

Monday, January 20, 2014

YANGA 2 SIMURG PIK 2



Kapteni wa Young Africans Mbuyu Twite (kushoto) na kapteni wa Simurq PIK Ruslan Poladov wakibadilishna beji za timu kabla ya mchezo kuanza.



Young Africans imekamlisha ziara ya kambi yake nchini Uturuki bila ya kupoteza mchezo hata mmoja baada ya leo kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya timu ya Simurq PIK inayoshiriki Ligi Kuu nchini Azerbajain katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya Side Star Hotel Complex Manavgat jijini Antalya Uturuki.

Mchezo wa leo dhidi ya Simurq PIK ulikuwa ni mchezo wa nne kwa Young Africans tangu kuwasili nchini Uturuki ambapo imeweza kushinda michezo mwili dhidi ya Ankara Sekerspor 3-0, na Altay SK 2-0 zote za Ligi Daraja la pili nchini Uturuki kabla ya kutoka sare na timu ya KS Flamurtari ya Ligi Kuu nchini Albania.

Dakika ya 13 ya mchezo mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Burundi, Didier Kavumbagu aliipatia Young Africans bao la kwanza kufuatia pasi nzuri ya mshambulaji Emmanuel Okwi na Didier kuukwamisha mpira wavuni na kumuacha mlinda mlango wa Simurq PIK Pawel Kapsa akiduwaa.

Simuriq PIK walifanya shambulizi kupitia kwa kwa kiungo wao Stephan Polyak lakini golikipa wa Young Africans Juma Kaseja alikoa hatari hiyo, huku Tagim Novruzov akishindwa kumalizia mpira uliotoka sentimeta chache langoni.

Dakika ya 30 ya mchezo Young Africans ilijipatia bao lake la pili kupitia kwa kiungo Mrisho Ngasa ambaye aliwatoka walinzi wa Simurq kufuatia migongeo mizuri katika Niyonzima, Okwi , Kavumbagu na kumkuta Ngasa ambaye aliukwamsiha mpira katika nyavu ndogo.

Mpira wa krosi uliopigwa na nahodha wa Simurq Ruslan Poladov uliwapita walinzi wa Young Africans wakishindwa kuucheza na kumkuta mlinzi wa kati Anderson Oliveira aliyepanda kusaidia mashambulizi aliyeipatia timu yake bao la kusawazisha.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwaza, Young Africans 2 - 1 Simurq PIK.

 Kipindi cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo Nadir Haroub "Cannavaro" aliingia kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani huku kiungo Hamis Thabit akichukua nafasi ya kiungo mkabaji Frank Domayo "Chumvi".

Dakika ya 56 ya mchezo Simuriq PIK walipata bao la pili na la kusawazisha kupitia kwa mshambulaji wao Murad Sattarli baada ya kazi nzuri iiyofanywa na kiungo wao Stephan Polyak na mpira huo kuwapita walinzi wa Young Africans na kumkuta mfungaji.

Mara baada ya bao hilo, timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 2 - 2 Simurq PIK.

Mara baada ya mchezo wa leo kocha mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van Der Plyum amesema vijana wake wamecheza vizuri kwa kufuata maelekezo, ana muda wa wiki moja lakini tayari anaona mabadiliko kiuchezaji na kutegemea kufanya vizuri katika mashidano yatakayotukabili.

"Timu imecheza vizuri nawapongeza vijana kwa kujituma, hakuna lisilowezekana katika mpira, wachezaji wangu sasa hivi wanajiamini na wanajua wanatakiwa wafanye nini kwa wakati muafaka, ilikua mechi nzuri sana hata kocha wa Simurq PIK amefurahi uwezo wetu" alisema Hans.

Mara baada ya mechi ya leo timu itaendelea na mazoezi kesho asubuhi kuendelea kujiweka fit kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini katikati ya wiki hii tayari kwa ajili ya mzunguko wa Pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa.

Young Africans: 1.Juma Kaseja, 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Mbuyu Twite, 5.Kelvin Yondani/Nadir Haroub, 6.Frank Domayo/Hamis Thabit, 7.Mrisho Ngasa/Saimon Msuva, 8.Haruna Niyonzima, 9.Didier Kavumbagu, 10.Emmanuel Okwi, 11.David Luhende/Said Bahanuzi

Simurq PIK: 1.Pawel Kapasa, 2. Ruslan Poladov , 3.Dilaver Zrnanovich, 4.Tural Axundov, 5.Anderson De Oliveira, 6.Tagim Novruzov, 7.Nichat Kurbanov/Bashir Jamilu, 8.Patrick Osiako, 9.Salif Ballo, 10.Rashad Ayyubov, 11.Stepahn Polyak

MALINZI AELEZA MIKAKATI YAKE KWA LOWASSA



Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambapo alimwelezea mikakati ya shirikisho lake katika kuinua kiwango cha mpira wa miguu Tanzania. Mkutano huo umefanyika leo (Januari 20 mwaka huu) ofisini kwa Lowassa jijini Dar es Salaam.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema shirikisho lake limepanga malengo ya muda mfupi na mrefu ikiwa na sehemu ya mkakati wa kuendeleza na kuinua kiwango cha mchezo huo nchini.

Malinzi ameeleza mikakati hiyo ya uongozi wake leo (Januari 20 mwaka huu) wakati alipomtembelea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Amesema uongozi wake umepanga malengo hayo ikiwemo kuandaa mashindano maalumu ya kutafuta vipaji mikoani ili kuondokana na mtindo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) kuundwa na wachezaji kutoka katika klabu chache tu.

Kwa upande wake Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli ameelezea matumaini yake kwa uongozi mpya wa TFF katika kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika kuimarisha na kuinyayua Tanzania katika ramani ya mpira wa miguu duniani.

Sunday, January 19, 2014

MANJI AMSHUKIA AKILIMALI



MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji amemtaja Katibu wa Baraza la Wazee, Ibrahim Akilimali kuwa ni adui namba moja wa klabu hiyo.

Manji alisema hayo jana wakati wa mkutano mkuu wa wanachama wa Yanga uliofanyika kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam.

Alisema Akilimali ni chanzo cha migogoro ya mara kwa mara ndani ya klabu hiyo kongwe nchini na amekuwa akimpa wakati mgumu katika kutekeleza majukumu yake.

"Huyu mzee wakati naingia Yanga, alinipokea na alinifanyia kampeni nishinde, cha ajabu ananitukanisha katika vyombo vya habari, ananivua nguo, ananifanya nishindwe kutekeleza wajibu wangu ipasavyo,"alisema Manji.

Aliongeza kuwa, Akilimali amekuwa akiingilia mambo ya  Yanga kama kwamba ni msemaji mkuu na mwenye mamlaka katika klabu hiyo, hali ambayo imeleta mgawanyiko.

Manji alisema Akilimali anavunja katiba ya Yanga kwa kuwa, haitambui kuwepo kwa Baraza la Wazee, isipokuwa viongozi wamekubali uwepo wake kutokana na busara zao katika ustawi wa klabu.

Hata hivyo,baada ya kumpasulia Akilimali ukweli huo, Manji aliamua kumfuata, akazungumza naye kwa sekunde kadhaa na kisha kumkumbatia.

Katika hatua nyingine, Manji amewaeleza wanachama wa Yanga kwamba hana mpango wa kuwania tena uongozi wa klabu hiyo katika uchaguzi mkuu, unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Alisema uamuzi wake wa kuwania uenyekiti wa Yanga ulilenga kuwatuliza wanachama wa klabu hiyo baada ya kuchapwa mabao 5-0 na Simba katika mechi ya mwisho ya ligi kuu.

"Tayari amani imerejea, sitaki kugombea tena uongozi na sitaki suala hili lijadiliwe tena,"alisema Manji.

COASTAL YACHANUA OMAN



Na Mahmoud Zubeity, Muscat

COASTAL Union imelazimishwa sare ya bila kufungana na Seeb Club ya Oman
kwenye Uwanja wa Seeb, mjini Muscat jioni hii katika mchezo mzuri wa kirafiki.
Ikimtumia mshambuliaji aliye majaribioni kutoka Ruvu Shooting ya Tanzania, Elias
Maguri, Seeb ilionyesha upinzani mkali kwa Coastal tangu mwanzo hadi mwisho wa
mchezo.
Seeb walikuwa wakicheza kwa kupiga pasi nyingi za haraka uwanjani, wakati Coastal
ilitumia mipira mirefu na mashambulizi ya kutokea pembeni.

Mshambuliaji wa Coastal Union, Atupele Green akiwania mpira dhidi ya mabeki wa
Seeb leo

Haruna Moshi ‘Boban’ aliyeanza pamoja na Mganda Yayo Lutimba mbele waliisumbua
ngome ya Seeb na Danny Lyanga na Atuepele Green waliwasumbua mabeki wa
pembeni wa timu hiyo ya katikati ya jiji a Muscat.
Baada ya mchezo wa leo, Coastal itacheza mechi moja zaidi na timu ambayo itatajwa
baadaye, kufuatia Al Thuwaiq kugoma kucheza nao kwa madai hawakuwa na taarifa
za uhakika.
Katika mechi zake tatu za awali, Coastal ilizifunga 2-0 kila timu Nadi Oman na
Musannaa kabla ya kufungwa 1-0 na Fanja.

SIMBA YAPIGISHWA KWATA NA MTIBWA SUGAR



BAO pekee la Masoud Ally ‘Chile’, jioni hii limeipa ushindi wa 1-0 Mtibwa Sugar ya
Morogoro dhidi ya Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa
kirafiki.
Masoud alifunga bao hilo akimalizia pasi nzuri ya kiungo wa pembeni Jamal Mnyate
dakika ya 64 ya mchezo huo mkali na wa kusisimua.
Huo ni mchezo wa pili mfululizo Simba SC kufungwa chini ya kocha mpya, Mcroatia,
Zdravko Logarusic baada ya awali kufungwa na KCC ya Uganda katika ya Kombe kla
Mapinduzi.
Awali, Logarusic aliiongoza Simba SC kushinda mechi saba mfululizo, ikiwemo ya
Nani Mtani Jembe dhidi ya wapinzani, Yanga SC mabao 3-1.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Yaw Berko, William Lucian ‘Gallas’/Nassor Masoud
‘Chollo’, Omar Salum/Adeyoum Saleh, Gilbert Kaze, Donald Mosoti, Awadh Juma,
Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Edward Christopher, Betra Mombeki/Zahor Pazi, Ali
Badru na Said Ndemla.
Mtibwa Sugar; Hussein Sharrif ‘Casillas’, Said Mkopi ‘Mpiluka’, Paul Ngalema,
Salvatory Ntebe, Salum Mbonde, Shaaban Nditi, Ally Shomary, Masoud Ally ‘Chile’,
Juma Luizio, Jamal Mnyate, Ally Mohammed ‘Gaucho’/Vincent Barnabas

YANGA KUCHEZA MECHI YA MWISHO UTURUKI LEO



Young Africans leo jumatatu saa 8 mchana kwa saa za nchini Uturuki sawa na saa
9 kamili kwa saa za Afrika Mashariki itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa
mwisho wa kirafiki dhidi ya timu ya Simurq PIK inayoshiriki Ligi Kuu nchini Azerbajain
katika viwanja vya Side Manavgat.

Kocha mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van Der Plyum amesema watautumia
mchezo huo kama sehemu ya mwisho ya maandalizi ya kujianda na Ligi Kuu ambayo
inatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki ijayo ambapo watoto wa jangwani watafugua
dimba dhidi ya Ashanti United uwanja wa Taifa.

Mchezo wa kesho utakua mgumu pia, kwani timu ya Simurq PIK ina wachezaji wazuri
ambao wanatoka sehemu mbali mbali dunianina ipo katika nafasi ya tano katika
msimamo wa Ligi Kuu nchini kwao, hivyo nadhani kitakua kipimo kizuri cha mwisho
kabla ya kurejea nchini Tanzania

Akiongelea kikosi chake mara baada ya mazoezi ya asubuhi, Hans amesema
anashukuru mungu maendeleo ya timu ni mazuri, mabadiliko yapo na wachezaji
wanaonekana kumuelewa hivyo anaamini kadri siku zinavyokwenda timu itakua katika
kiwango kizuri zaidi.

"Nimeshashuhudia michezo miwili mmoja tukishinda 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK Lidi
Daraja la pili Uturuki na jana tukitoka sare ya 0-0 dhidi ya timu ya KS Flumartari ya
Ligi Kuu Albania, kwa kweli nawapongeza vijana wanaonyesha kweli wanajua wajibu
wao na kucheza kwa kufuata maelekezo ya walimu" alisema Hans.

Aidha Hans amesema ni jambo njema timu imecheza jumla ya michezo mitatu,
ikishinda miwili na kutoka sare mchezo mmoja, huku ikifunga mabao 5 na
kutokuruhusu nyavu zake kutikisika hii yote inayonyesha timu imeiva tayari kwa
mashindano yanayotukabili.

Mpaka sasa hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja kufuatia kiungo Hassan Dilunga
kupona malaria na kuungana na wenzake katika mazoezi.