KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, February 28, 2013

TBL YANOGESHA SAFARI YA SIMBA ANGOLA



WATANZANIA wametakiwa kuweka tofauti zao mbali na kuishangilia timu ya Simba inapocheza mechi yake ya marudiano na Libolo ya Angola Jumapili hii kuwania kufuzu katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

Wito huo umetolewa na wadhamini wa Timu ya Simba, Kilimanjaro Premium Lager, kupitia Meneja Masoko, Fimbo Butallah wakati wa kutoa vifaa kwa timu ya Simba tayari kwa mechi hiyo kama sehemu ya udhamini.

“Wanapokwenda kwenye mechi hii hawaendi tu kama Simba bali wanakwenda kuiwakilisha Tanzania kwa hivyo ni muhimu kwa watanzania wote kuungana na Kilimanjaro Premium Lager kuleta hamasa ili timu yetu iibuke na ushindi na kusogea mbele katika mashindano haya,” alisema.

Alisema wao kama wadhamini wana imani kuwa Simba imejiandaa vizuri na watafanya maajabu na kuibuka na ushindi ugenini. “Mechi hii ni ngumu, lakini tuna imani watafanya vizuri na kuwafurahisha watanzania,” alisema Butallah.

Akipokea vifaa hivyo, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga aliishukuru Kilimanjaro Premium Lager kwa udhamini wake mnono, ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa klabu yao.

“Zawadi ambayo tunaweza kuwapa wadhamini wetu ni kushinda Jumapili,” alisema Kamwaga.

Alisema watanzania wasiwe na wasiwasi kwani Simba ina uwezo wa kufanya ilichofanya kwa Zamalek miaka kumi iliyopia kwani Zamalek ilishinda Tanzania lakini katika mechi ya marudiano Simba ikashinda.

“Kuna wakati pia Mufurira Wanderers ya Zambia ilitufunga mabao manne nyumbani lakini tulivyoenda kwa tukawafunga matano,” alisema Kamwaga.

Simba inatarajiwa kuondoka kesho alfajiri kwenda Angola  kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Jumapili.
Kilimanjaro Premium Lager ni mdhamini wa timu za Simba na Yanga na Timu ya Taifa (Taifa Stars).

POULSEN KUSHIRIKI KILI MARATHON



Na Michael Mukunza

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amethibitisha kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathon mwaka huu. Mbio hizo zimepangwa kufanyika mjini Moshi Jumapili ya Machi na atakimbia umbali wa kilomita 21.

Hii ni historia mpya kwa Tanzania kwa kocha wa timu ya taifa kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathon ambazo zilianza rasmi zaidi ya miaka 10 iliyopita kwa udhamini wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

“Nataka kujaribu mbio hizo kwa sababu napenda changamoto na hii itanipa fursa nzuri ya kukimbia huku nikiuzunguka Mlima Kilimanjaro ambao ni maarufu,” alisema.

Poulsen aliongeza kuwa yupo tayari kwa mashindano baada ya kufanya mazoezi kwa miezi kadhaa. “Kwa kawaida kila siku nafanya mazoezi ya kukimbia, na sasa naweza kusema kuwa nipo tayari kwa ajili yam bio hizo,” alisema.

Aliongeza: “Nikiwa kocha timu ya taifa, nimeona umuhimu wa kuungana na watu wengine katika medani nyingine za michezo…sijawahi kushiriki Kilimanjaro marathon lakini nimesikia mengi mazuri kuhusu mbio hizo na ndiyo maana nikaamua kushiriki.”

Kwa ushiriki huo, kocha huyo atakutana na magwiji wa mbio hizo Tanzania na maelfu ya wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 40.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe amesifu uamuzi wa wa kocha na kusema kuwa hatua ya Poulsen itachangia kwa kiasi kikubwa kuhamasisha zaidi mbio hizo. “Kocha ameamua kwa dhati kushiriki na hali hiyo inaonyesha wazi kuwa hata katika timu ya taifa anatimiza vema majukumu yake,” alisema Kavishe.

Kampuni ya Executive Solutions ndio waratibu rasmi wa mashindano hayo hapa nchini huku wadhamini wengine wakiwa ni Vodacom Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (Mbio fupi kwa wenye ulemavu), Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, Hoteli ya New Arusha, Maji ya Kilimanjaro , FastJet, Clouds FM na Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA).

UTAMU WA LIGI KUU HATA KWA WATASHA

Raia hawa wa kigeni wakiwa kwenye Uwanja wa soka wa Mkwakwani mjini Tanga juzi wakishuhudia pambano la ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Coastal Union na Ruvu Shooting. Katika pambano hilo, timu hizo zilishindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu. (Picha na Sophia Wakati)

MASHINDANO YA KOMBE LA MPINGA YAANZA




Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akidaka mpira ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup inayowahusisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi leo kwa muda wa wiki moja. Mpinga cup imedhaminiwa na Airtel , Rotary Club, Mr price na Shoprite ikiwa na lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki na kupunguza ajali barabarani . akishuhudia. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga  
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga akikagua timu kabla ya mechi kati ya Kawe Tiptop na Manzese leo wakati wa uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup, anayefata pichani ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando

SIMBA YATANGAZA NYOTA 18 WANAOKWENDA ANGOLA KESHO




WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya soka ya klabu bingwa Afrika, Simba wanaondoka nchini leo kwenda Angola kwa ajili ya mechi yao ya marudiano ya raundi ya kwanza dhidi ya Recreativo Libolo.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, timu hiyo itakwenda Angola ikiwa na msafara wa wachezaji 18 na viongozi saba.

Kamwaga alisema Simba inatarajiwa kuondoka saa 11.10 alfajiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways) na inatarajiwa kuwasili Luanda saa nne asubuhi.

Aliwataja wachezaji watakaokuwemo kwenye msafara wa timu hiyo kuwa ni Juma Kaseja, Abel Dhaira, Nassor Masoud, Amir Maftah, Koman Bili Keita, Juma Nyoso, Shomari Kapombe, Salim Kinje, Ramadhani Chomboh, Amri Kiemba, Haruna Moshi, Kiggi Makasi, Abdallah Seseme, Amri Kiemba, Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa, Felix Sunzu na Abdallah Juma. Viongozi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia

Hanspope, mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Muhsin Balhabou, Kocha Mkuu, Patrick Liewig, msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo, Daktari wa timu, Cosmas Kapinga, kocha wa makipa, James Kisaka na mtunza vifaa Kessy Rajab.

Kwa mujibu wa Kamwaga, timu hiyo ilitarajiwa kufanya mazoezi ya mwisho jana jioni kabla ya kwenda kambini, ambako watapumzika kwa muda kwa ajili ya kusubiri muda wa safari.

Pambano kati ya Simba na Libolo limepangwa kufanyika keshokutwa katika uwanja wa Calulo uliopo katika mji mdogo wa Calulo kwenye Jimbo la Kwanza Kusini.

Katika mechi ya awali iliyochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Libolo iliichapa Simba bao 1-0. Ili isonge mbele katika michuano hiyo, Simba italazimika kuishinda Libolo mabao 2-0.

Kamwaga alisema licha ya kufungwa katika mechi ya awali, matumaini ya Simba kusonga mbele ni makubwa kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

ANNA ABWAGA MANYANGA CHANETA



Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Anna Bayi ametangaza rasmi kuwa hatagombea tena ili kutetea nafasi yake wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika Machi 23 mjini Dodoma.

Bayi amesema kuwa ameamua kung’atuka ili kutoa nafasi kwa Watanzania wengine wenye sifa kujitokeza na kuongoza chama hicho kwa matarajio ya kuleta mawazo mapya na kuendeleza mchezo huo nchini.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa muda aliotumia kukaa madarakani unatosha kwake na kwamba, anaamini kuwa akishirikiana na wenzake, amesaidia kuipa Chaneta mafanikio makubwa, yakiwamo ya kuipeleka timu ya taifa kushiriki michuano kadhaa ya kimataifa.

"Nimeamua kutogombea tena ili kutoa nafasi kwa wadau wengine kuendeleza gurudumu la netiboli nchini," Bayi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chaneta, Rose Mkisi, aliwasihi watu wenye sifa kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania uongozi katika chama chao.

Mkisi amesema kuwa tangu watangaze tarehe ya kutoa fomu hizo, hakuna mgombea yeyote aliyejitokeza kuchukua fomu hadi sasa, isipokuwa wamepokea taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa baadhi ya wanamichezo kutoka mikoani kuwa wanahitaji fomu za kuwania ujumbe.

"Tunaomba wanamichezo wenye sifa wachangamkie fursa hii ya kuchukua fomu za kuwania uongozi," Mkisi, akiongeza kuwa tarehe ya mwisho ya kurejesha fomu hizo ni Machi 15 na usaili utafanyika Dodoma Machi 21.

Nafasi zitakazowaniwa katika uchaguzi huo ni pamoja na za mwenyekiti, katibu mkuu, mweka hazina na wajumbe.

Katika hatua nyingine, Chaneta imetaka mikoa kulipa ada ya uanachama kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu kufika

Mkisi amesema mikoa itakayoshindwa kulipia ada ya uanachama haitaruhusiwa kutoa wawakilishi wa kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu.

Awali, uchaguzi wa Chaneta ulikuwa ukipigwa kalenda mara kadhaa kutokana na baadhi ya mikoa kusuasua kuitisha chaguzi zake na pia, baadhi yao kushindwa kulipia ada za uanachama

RONALDO: KUIFUNGA BARCELONA RAHAAA



MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo wa Real Madrid amesema huwa anajisikia raha timu yake inapoifunga Barcelona katika michuano mbalimbali.

Ronaldo alisema hayo juzi baada ya Real Madrid kuichapa Barcelona mabao 3-1 na kufuzu kucheza fainali ya michuano ya Kombe la Del Rey kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nou Camp, Ronaldo aliifungia Real Madrid mabao mawili kati ya matatu. Bao lingine lingine lilifungwa na Raphael Varane.

"Inafurahisha, nitakuwemo kwenye vitabu vya kumbukumbu ya soka ya Hispania,"alisema mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ureno.

Ronaldo alisema wamekuwa wakipata matokeo mazuri kila wanapocheza na Barcelona kwenye uwanja wa Nou Camp kuliko wanavyocheza nao Santiago Bernabeu.

"Ulikuwa mchezo nzuri. Tulicheza vizuri sana. Kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho, tulicheza kwa ari kubwa. Tulicheza vizuri kuliko Barcelona. Kufunga mabao matatu kwenye uwanja wa Nou Camp ni kazi ngumu,"alisema.

Ronaldo alisema kwa sasa, michuano ya ligi ya Hispania haina umuhimu kwao kutokana na kuwa nyuma kwa tofauti na pointi nyingi kati yao na Barcelona.

Alisema wameamua kuelekeza akili zao katika michuano ya Del Rey na ligi ya mabingwa wa Ulaya kwa vile wana uwezo wa kufanya vizuri.

SIMBA KUIFUATA LIBOLO KESHO



WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa Afrika, Simba wanatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Angola kwa ajili ya mechi yao ya marudiano dhidi ya Recreativo Libolo.

Simba imepanga kwenda Angola ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 na viongozi saba.
Pambano kati ya Simba na Libolo limepangwa kuchezwa Jumapili katika mji mdogo wa Calulo.

Katika mechi ya awali kati ya timu hizo, iliyochezwa wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ilichapwa bao 1-0. Ili isonge mbele katika michuano hiyo, Simba italazimika kuishinda Libolo mabao 2-1.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, kikosi kitakachokwenda Angola kinatarajiwa kutangazwa kesho.

Kamwaga alisema wameamua kutokitangaza mapema kikosi hicho kwa kuhofia kujitokeza kwa wachezaji majeruhi katika mazoezi yaliyotarajiwa kufanyika jana na yatakayofanyika leo.

Licha ya kufungwa katika mechi ya kwanza, Kamwaga alisema matumaini ya timu hiyo kusonga mbele ni makubwa kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

"Kufungwa nyumbani haina maana kwamba tumeshatolewa. Mara nyingi hutokea timu kufungwa nyumbani, lakini ikafanya vizuri ugenini,"alisema.

Kamwaga alisema wamepata wasiwasi baada ya kusikia wenyeji wao wamepanga mechi hiyo ichezwe katika mji wa Calulo kwa vile watalazimika kuwasafirisha kwa ndege.

"Hatutakuwa tayari kusafiri kwa basi umbali wa saa nne kwa vile kanuni za CAF (Shirikisho la Soka Afrika) zipo wazi kuhusu hilo,"alisema.

NIYONZIMA AITAKATISHA YANGA


BAO lililofungwa na Haruna Niyonzima jana liliiwezesha Yanga kujikita zaidi kileleni mwa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Kagera Sugar bao 1-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Niyonzima alifunga bao hilo dakika ya 65 kwa shuti kali la mbali, ambalo kipa Hannington Kalyesubula wa Kagera Sugar alishindwa kuliona na kujikuta akidaka hewa.

Hii ni mara ya pili kwa Niyonzima kuifungia Yanga bao muhimu katika mechi za ligi kuu ndani ya muda wa siku tano. Wiki iliyopita, Niyonzima aliifungia Yanga bao pekee na la ushindi katika mechi dhidi ya Azam iliyochezwa kwenye uwanja huo.

Ushindi huo uliifanya Yanga iwe na pointi 42 baada ya kucheza mechi 18, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 36 na Simba yenye pointi 31.

Pamoja na kupata ushindi, Yanga jana iliweka rekodi baada ya wachezaji wake watano kuonyeshwa kadi za njano. Wachezaji hao ni Saidi Bahanuzi, Athumani Iddi, Nadir Haroub, David Luhende na Nizar Khalfan.

Kutokana na kupata idadi hiyo ya kadi, Yanga inakabiliwa na adhabu ya kutozwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni za ligi.

Timu zote mbili ziliuanza mchezo huo kwa kasi ndogo, lakini Kagera Sugar walionekana kuchangamka zaidi na kufika kwenye lango la Yanga mara tatu katika dakika za mwanzo.

Yanga ingeweza kufunga bao dakika ya tatu wakati Didier Kavumbagu alipounganisha kwa kichwa krosi ya Simon Msuva, lakini kipa Hannington Kalyesubula alikuwa makini kudaka mpira huo.

Msuva alipata nafasi nzuri ya kuifungia Yanga bao dakika ya 13 baada ya kuunasa mpira uliompita beki Muganyizi Martin ndani ya eneo la hatari, lakini shuti lake liliokolewa na kipa Hannigton.

Lango la Yanga lilipata msukosuko dakika ya 34 wakati Juma Nade alipofumua shuti kali akiwa umbali wa mita 20, lakini lilipaa juu ya lango.

Dakika nne baadaye, Shija Mkina alipenya na mpira ndani ya eneo la hatari la Yanga baada ya kupewa pasi ndefu kutoka katikati ya uwanja, lakini kiki yake ilitoka pembeni ya uwanja.

Yanga ilifanikiwa kupata adhabu ya penalti dakika ya 45 baada ya kipa Hannington wa Kagera kumwangusha Kavumbagu ndani ya eneo la hatari. Hata hivyo, shuti la adhabu hiyo la Kavumbagu lilipaa juu ya lango.

Awali, wachezaji wa Kagera waligomea adhabu hiyo kwa madai kuwa, haikuwa halali. lakini waliruhusu ipigwe baada ya kushauriana kwa dakika kadhaa na kushangilia baada ya shuti la Kavumbagu kutoka nje. Timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa suluhu.

Yanga ikilianza kipindi cha pili kwa kasi na nusura ipate bao dakika ya 49 wakati Domayo alipofumua shuti kali, lakini liligonga mwamba na mpira kurudi uwanjani, ambako uliokolewa na mabeki wa Kagera.

Yanga: Ally Mustapha, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Kelvin Yondan, Athumani Iddi, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu/Jerry Tegete, Saidi Bahanuzi/Hamisi Kiiza, Haruna Niyonzima.

Kagera: Hannington Kalyesubula, Benjamin Asukile, Muganyizi Martin, Malegesi Mwangwa, Amandus Nesta, George Kavilla, Julius Mrope/ Paul Ngwai, Juma Nade, Darlington Enyinna, Shija Mkina, Daudi Jumanne.

DEFOE APATA MTOTO



LONDON, England
MWANASOKA Jermain Defoe wa klabu ya Tottenham ya England, amepata mtoto wa kwanza baada ya rafiki yake wa zamani wa kike, Anne-Marie Moore kujifungua.

Anne-Marie alijifungua mtoto huyo wa kike wiki iliyopita na kubatizwa jina la Joshua-James Defoe.

Defoe (30) aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mfupi na Anne-Marie mwaka jana baada ya kutengana na mpenzi wake wa zamani, Alexandra Burke

Beki huyo alikuwepo hospitali wakati mpenzi wake huyo wa zamani akijifungua na tangu wakati huo amekuwa akimtembelea mwanaye kila siku.

"Defoe amepatwa na furaha ya ajabu kutokana na kuwa baba. Ni tukio linalomfanya mtu apevuke kimaisha na sasa anajiandaa kwa majukumu ya kifamilia,"alisema mtu mmoja wa karibu wa mwanasoka huyo.

Wapenzi hao wawili walifichua kuwa, walitarajia kupata mtoto wa kiume miezi kadhaa iliyopita baada ya penzi lao kuvunjika 2012.

Defoe alipigwa chini na Alexandra, ambaye ni mwanamuziki Mei mwaka jana baada ya kugundulika alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Anne-Marie.

Baada ya fumanizi hilo, Defoe aliamua kuanzisha rasmi uhusiano wa kimapenzi na Anne-Marie.

Licha ya wapenzi hao wawili kutoishi pamoja kwa sasa, Defoe alikuwepo karibu ya Anne-Marie wakati wa kujifungua.

Anne-Marie (32) alifichua kuwa ana uja uzito wakati alipotuma picha ya x-ray ikionyesha tumbo lake kwenye mtandao wa Facebook.

Rafiki mmoja wa Anne-Marie alidokeza kuwa, wapenzi hao wawili walikuwa pamoja kwa muda mwingi kabla ya kila mmoja wao kuamua kuishi kivyakevyake.

Defoe amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na nyota kadhaa wa muziki na filamu, wakiwemo Imogen Thomas, Chantelle Houghton na Danielle Lloyd.

Lakini baada ya kupata mtoto, watu wake wa karibu wamesema, maisha ya ujana aliyokuwa nayo Defoe kwa sasa yamefikia ukingoni.

TOURE: MAN CITY HAIWEZI KUFANANA NA BARCELONA



LONDON, England
KIUNGO Yaya Toure wa klabu ya Manchester City ameonya kuwa, itakuwa vigumu kwa timu hiyo kupata mafanikio katika ligi kuu ya England kwa kuiga staili ya Barcelona.

Toure (29) amesema hayo kufuatia mpango ulioandaliwa na Manchester City wa kuanzisha timu za vijana na pia kuiga staili ya uchezaji ya miamba hiyo ya soka duniani.

Katika kutimiza azma hiyo, tayari Manchester City imeshawaajiri Mtendaji Mkuu, Ferran Soriano na Mkurugenzi wa Soka, Txiki Begiristain kutoka Barcelona.

Toure, ambaye kwa sasa ndiye mchezaji ghali kuliko wote katika klabu ya Manchester City, aliichezea Barcelona kwa miaka mitatu akiwa na kina Xavi, Andres Iniesta na Lionel Messi na kuiwezesha kutwaa taji la ligi ya mabingwa wa Ulaya 2009 kabla ya kuhamia England mwaka juzi.

Manchester City imepanga kusajili wachezaji nyota wenye umri mdogo kutoka sehemu mbalimbali duniani na kuwapeleka katika kituo chake maalumu cha kukuza soka.

Hata hivyo, Toure ameukosoa mpango huo kwa kusema, itakuwa vigumu kwa Manchester City kumudu kucheza soka ya pasi nyingi inayochezwa na Barcelona katika ligi kuu ya England.

"Sifikirii iwapo itakuwa sahihi kucheza kama Barcelona kwa sababu ligi kuu ya England ni tofauti na soka ya Hispania,"alisema Toure alipohojiwa na gazeti la Daily Mail la Uingereza wiki hii.

"Kiwango cha soka cha Hispania kipo juu na soka yake inachezwa kwa ufundi mkubwa. Ukiwa England, unahitajika kuwa na kila kitu, nguvu, stamina na mbio,"aliongeza.

Toure alisema pia kuwa, katika ligi ya England, wachezaji wanatumia ngumu zaidi kuliko Hispania na kwamba si rahisi kwa mchezaji kumiliki mpira na wakati huo huo kumtazama mwenzake yupo wapi.

"Unapaswa kuwa mwepesi katika maamuzi, vinginevyo mchezaji kama Kyle Walker (wa Tottenham) atakuangusha. Hapa England, wachezaji wanacheza kwa kutumua nguvu zaidi. Unapaswa kupigania kila mpira na kuwa wa kwanza katika kila tukio, tofauti na Hispania na Italia,"alisema kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast.

Toure ameibuka kuwa shujaa wa Manchester City tangu alipojiunga na klabu hiyo 2010 kwa malipo ya pauni 240,000 kwa wiki na kuifungia bao la ushindi katika mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Stoke City mwaka uliofuata, lililofuta ukame wa mataji uliodumu kwenye klabu hiyo kwa miaka 35.

Kocha Mkuu wa Manchester City, Roberto Mancini amemwelezea kiungo huyo kuwa ni mchezaji muhimu na wa aina yake na aliyesababisha kiwango cha timu hiyo kubadilika Januari mwaka huu alipokwenda kushiriki katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Makocha kadhaa wanaofundisha klabu za ligi ya Hispania wamekuwa wakihusishwa na mipango ya kurithi kibarua cha Mancini, akiwemo Manuel Pellegrini wa Malaga.

Manchester City mwishoni mwa wiki iliyopita ilifufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa England baada ya kuichapa Chelsea mabao 2-0.

Kabla ya ushindi huo, matumaini ya Manchester City kutwaa taji hilo yaliingia doa baada ya kupigwa mweleka wa mabao 3-1 na Southampton.

Akizungumzia mchezo huo, Toure alisema kucheza na timu ngumu kama Chelsea ilikuwa rahisi kwa Manchester City, inayoundwa na nyota wengi kuliko kucheza na timu kama Southampton.

"Napenda kucheza mechi ngumu. Baadhi ya wakati ni kwa sababu ya mashabiki na wakati mwingine kwa sababu ya kiwango cha soka,"alisema nyota huyo.

"Mechi ngumu ni zile dhidi ya klabu kama Chelsea, Manchester United, Tottenham, Liverpool. Tunapaswa kuonyesha uwezo wetu katika mechi za aina hii. Lakini Chelsea sio timu nyepesi kuifunga,"aliongeza.

Toure alisema siku zote wapinzani wao wamekuwa wakicheza kwa kukamia kutokana na timu yake kuwa mabingwa wa ligi hiyo. Alisema unapokuwa mwanamichezo, unapaswa kushinda mechi zote.

Mwanasoka huyo amecheza soka katika nchi tano tofauti. Alianzia Ubelgiji, Ukraine, Ugiriki, Hispania na sasa England. Aliondoka Afrika tangu akiwa mdogo.

Toure alisema anapenda kuendelea kubaki Manchester City baada ya mkataba wake wa sasa kumalizika mwaka 2015, licha ya kaka yake, Kolo Toure kusema kuwa, ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

Alisema hajawahi kuichezea klabu yoyote kwa zaidi ya miaka mitatu, lakini hali ni tofauti England kwa vile anataka kubaki Manchester City kwa miaka mingi zaidi.

"Unaweza kubadilika pale unapokosa furaha na kitu fulani. Manchester City inaundwa na wachezaji wenye mvuto kama David Silva na Sergio Aguero na mashabiki wanafanya vitu vya kuvutia.

"Kila wiki wanaimba nyimbo na kutaja jina lako na wapo karibu na klabu. Siku zote mashabiki wamekuwa wakijaribu kutusaidia na hiki ni kitu cha aina yake,"alisisitiza.

GIGGS AWEKA REKODI YA KUCHEZA MECHI 999



LONDON, England
WAKATI Ryan Giggs alipoifungia Manchester United bao la ushindi katika mechi ya ligi kuu ya England dhidi ya QPR na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, alikuwa ameweka rekodi ya kucheza mechi 999.

Mwanasoka huyo mkongwe anaweza kuweka rekodi ya kucheza mechi 1,000 keshokutwa wakati Manchester United itakapomenyana na Norwich City katika mechi ya ligi hiyo.

Giggs ni jina kubwa katika kikosi cha sasa cha Manchester United. Ni mchezaji aliyeanza kuichezea klabu hiyo tangu Machi 2, 1991, wakati ambao baadhi ya wachezaji alionao sasa aidha walikuwa na umri mdogo au hawajazaliwa.

Mbali na rekodi hiyo, wiki chache zijazo, Giggs anaweza kuongeza mataji na medali akiwa na kikosi cha Manchester United, ambacho kinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England msimu huu.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Wales aliichezea Manchester United kwa mara ya kwanza katika mechi ya ligi dhidi ya Everton. Mechi hiyo ilipigwa Machi 2, 1999.

Wakati Giggs akiteremka dimbani kucheza mechi hiyo, mkongwe mwenzake, Paul Scholes alikuwa na umri wa miaka 16 na miezi minne wakati Rio Ferdinand alikuwa na umri wa miaka 12 na miezi minne na huenda walikuwa sekondari.

Katika kipindi hicho, wachezaji kama David de Gea na Danny Welbeck walikuwa bado hawajaanza hata kutembea wakati Phil Jones na Nick Powell walikuwa hawajazaliwa.

Nahodha wa zamani wa Manchester United, Roy Keane, David Beckham na Gary Neville walicheza pamoja na Giggs kwenye kikosi cha timu hiyo na kuondoka wakimwacha bado tegemeo kubwa.

Manchester United ilitumia pauni milioni 50 msimu huu kuwasajili Ashley Young, Nani na Shinji Kagawa, ambao wanacheza nafasi moja na Giggs wakati Tom Cleverley na Anderson pia wanapigania namba kwenye nafasi hiyo na nahodha huyo wa zamani wa Wales.

Kocha Mkuu wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amekuwa na utamaduni wa kuwaamini wachezaji wake wakongwe na hivyo ndivyo anavyofanya kwa Giggs.

Iwapo Giggs atafanikiwa kuweka rekodi ya kucheza mechi 1,000 msimu huu, atakuwa mchezaji wa saba nchini England kufanya hivyo. Wachezaji waliowahi kuweka rekodi hiyo ni Peter Shilton, Ray Clemence, Pat Jennings, David Seaman, Tony Ford na Graham Alexander.

Wachezaji wengine walioweka rekodi ya kucheza mechi nyingi katika ligi kuu ya England ni Alan Shearer (797) na Eric Cantona (453).

UMRI WA WACHEZAJI WA MAN UTD ULIVYOKUWA WAKATI
GIGGS ALIPOANZA KUICHEZEA TIMU HIYO MACHI 2, 1999

Paul Scholes, miaka 16 na miezi minne
Anderson, miaka miwili na miezi 11
Rio Ferdinand, miaka 12 na miezi minne
Javier Hernandez, miaka miwili na miezi minane
Michael Carrick, miaka tisa na miezi minane
Alexander Buttner, miaka miwili na mwezi mmoja
Nemanja Vidic, miaka tisa na miezi mitano
Shinji Kagawa, mwaka mmoja na miezi 11
Patrice Evra, miaka tisa na miezi miwili
Tom Cleverley, mwaka mmoja na miezi saba
Robin van Persie, miaka saba na miezi saba
Chris Smalling, mwaka mmoja na miezi minne
Darren Fletcher, miaka saba na mwezi mmoja
Ben Amos, miezi 11
Anders Lindegaard, miaka sita na miezi 11
Rafael, miezi tisa
Ashley Young, miaka mitano na miezi minane
David de Gea, miezi mitatu
Antonio Valencia, miaka mitano na miezi saba
Danny Welbeck, miezi mitatu
Wayne Rooney, miaka mitano na miezi mitano
Phil Jones, alikuwa hajazaliwa (Alizaliwa Feb 21, 1992)
Nani, miaka minne na miezi minne
Nick Powell, alikuwa hajazaliwa (Alizaliwa Machi 23,1994)
Jonny Evans, miaka minne na miezi miwili

IDADI YA MECHI NA TIMU ALIZOCHEZEA GIGGS
Manchester United: Mechi 931
Wales: Mechi 64
Timu ya GB: Mechi 4
Jumla: Mechi 999

WACHEZAJI WALIOWEKA REKODI YA KUCHEZA MECHI 1,000 ENGLAND
Peter Shilton
Ray Clemence
Pat Jennings
David Seaman
Tony Ford
Graham Alexander

SIKIA HII KALI YA GUARDIOLA


MADRID, Hispania
KOCHA Mkuu wa zamani wa Barcelona ya Hispania, Pep Guardiola alikuwa akikodi wapelelezi wa kujitegemea kwa ajili ya kufuatilia maisha ya wanasoka wake nyota.

Uamuzi huo wa Guardiola ulilenga kuwaepusha nyota hao wasijihusishe na vitendo vinavyoweza kushusha viwango vyao.

Miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakifuatiliwa na kocha huyo ni Ronaldinho Gaucho, Deco Souza, Samuel Eto’o na Gerard Pique.

Imeelezwa kuwa, Guardiola alianza kufanya hivyo tangu 2008 alipoanza kuinoa timu hiyo hadi alipomaliza mkataba wake mwaka jana.

Chanzo cha habari kimeeleza kuwa, hiyo ndiyo siri kubwa ya mafanikio iliyoyapata Barcelona katika kipindi cha miaka minne ilichokuwa ikinolewa na kocha huyo.

Guardiola (42) aliiwezesha Barcelona kushinda mataji 12 katika miaka minne ya utawala wake, yakiwemo mataji mawili ya ligi ya mabingwa wa Ulaya.

Kwa sasa, Guardiona anajiandaa kuifundisha Bayern Munich ya Ujerumani, akichukua nafasi ya kocha wa sasa wa timu hiyo, Jupp Heynckes. Anatarajia kuanza kazi hiyo mwishoni mwa msimu huu.

CHRIS: RIHANA ANANIPENDA, AMENISAMEHE



LOS ANGELES, Marekani
MWANAMUZIKI Chris Brown amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu kitendo chake cha kumpiga na kumjeruhi mpenzi wake, Rihanna na kusema kwamba anakijutia.

Brown alisema mjini hapa wiki hii kuwa, kitendo hicho ni cha kwanza kikubwa kukijutia katika maisha yake.

Japokuwa mwanamuziki huyo wa Marekani amekielezea kitendo hicho kuwa ni makosa, pia amekiri kwamba wameamua kuendelea na uhusiano wao baada ya Rihanna kuamua kumsamehe.

Brown, ambaye anajaribu kubadili mwonekano wake kwa jamii, alisema kwa sasa ameamua kuufanyiakazi uamuzi wa Rihanna kumsamehe.

"Niliujutia usiku ule katika maisha yangu. Lilikuwa kosa kubwa,"alisema mwanamuziki huyo nyota wa miondoko ya R&B.

"Lakini ananipenda, nisemeje? Nimesamehewa, ndio, naufanyiakazi uamuzi wake huo,"aliongeza mwanamuziki huyo.

Brown alisema wameamua kulisahau tukio hilo hata kama watu wengine hawataki kufanya hivyo.

Mwanamuziki huyo alikiri kuwa, baadhi ya wakati hutokea mtu kugombana na mpenzi wake na baadaye kusameheana.

Brown alidaiwa kumpiga na kumjeruhi Rihanna 2009 baada ya kutokea mabishano kati yao.

Kutokana na kukiri kufanya kitendo hicho, mahakama ilimweka mwanamuziki huyo chini ya uangalizi kwa miaka mitano na kutakiwa kufanyakazi za kijamii kwa miezi sita.

Licha ya kuamua kusameheana na kuendeleza uhusiano wao, Brown na Rihanna wamekuwa wakikumbana na upinzani mkali kutoka kwa wanaharakati.

Wapenzi hao wawili wiki iliyopita walisherehekea Rihanna kutimiza miaka 25 katika ufukwe wa Hawaii.

JANET JACKSON AFUNGA NDOA KWA SIRI


LOS ANGELES, Marekani
MWANAMUZIKI nyota wa Marekani, Janet Jackson ameibuka na kusema kuwa, alifunga ndoa na rafiki yake, mfanyabiashara wa Qatar tangu mwaka jana.

Janet (46), ambaye ni ndugu wa mwanamuziki nyota wa zamani wa miondoko ya pop duniani, marehemu Michael Jackson, alifunga ndoa na mfanyabiashara huyo, Wissa Al Mana (37) kwa siri.

Mwanadada huyo ameamua kuanika ukweli huo hadharani ili kukanusha taarifa zilizokuwa zikiripotiwa na vyombo vya habari kuhusu ndoa hiyo.

Kwa mujibu wa Janet, waliamua kuifanya ndoa hiyo iwe siri ili kuepuka taarifa potofu zinazoweza kutolewa na vyombo vya habari.

"Uvumi uliozagaa kuhusu ndoa yetu sio wa kweli. Tulifunga ndoa mwaka jana katika harusi ndogo, nzuri na iliyofanyika kwa siri," ilisema taarifa iliyotolewa kwa pamoja na Janet na Al Mana wiki hii.

Janet amekuwa akifahamika kutokana na kuyafanya maisha yake kuwa siri ili kuepuka kupakaziwa na vyombo vya habari.

Mwanamama huyo amewahi kufunga ndoa mara mbili, lakini ndoa ya kwanza ilivunjika baada ya mwaka mmoja na ya pili ilivunjika baada ya miaka tisa.

Alifunga ndoa kwa mara ya kwanza 1984 na James DeBarge kabla ya kuolewa kwa mara ya pili na Rene Elizondoa 1991.

DAUDI SALUM 'BRUCE LEE': VIONGOZI WA SOKA BONGO WABABAISHAJI



Asema wanawania uongozi ili kufanya biashara
Ajivunia rekodi zake tatu za kimataifa

KWA mashabiki wa soka wanaolikumbuka jina la Daudi Salum, bila shaka wataikumbuka vyema staili yake ya uchezaji, iliyomfanya apachikwe jina la Bruce Lee.

Alikuwa beki kisiki, mwenye kasi na asiyepitika kirahisi. Na kila alipokuwa akiondosha mpira kwenye eneo lake la hatari, alipenda kuruka kwa staili ya kungfu. Hiyo ndiyo sababu iliyowafanya mashabiki wampachike jina la Bruce Lee.

Sababu nyingine iliyowafanya mashabiki wampachike jina hilo ni rangi yake. Alikuwa na weupe uliong'ara na kufanya iwe rahisi kumtambua mara moja awapo uwanjani. Ilikuwa rangi adimu kwa wachezaji wakati huo.

Pamoja na umri mkubwa alionao sasa, rangi ya Daudi bado ni ile ile. Tofauti ipo kidogo kwenye umbo na hii ni kutokana na umri. Lakini bado ana ukakamavu. Pengine kutokana na majukumu ya kazi yake.

Daudi alikuwa mmoja wa wanasoka wa timu ya Taifa, Taifa Stars iliyofuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za 1980 zilizofanyika nchini Nigeria na kutolewa hatua ya makundi baada ya kufungwa mechi mbili na kutoka sare moja.

Beki huyo mkongwe pia alikuwemo kwenye kikosi cha Simba kilichotolewa na Mehala El-Kubra ya Misri katika nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika 1974.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, Simba iliichapa Mehala El-Kubra bao 1-0 na ziliporudiana mjini Cairo, ilichapwa idadi hiyo ya bao. Mshindi ilibidi apatikane kwa njia ya penalti tano tano.

Daudi pia alikuwemo kwenye kikosi cha Simba kilichoonyesha maajabu katika michuano hiyo mwaka 1975, ambapo baadaya kuchapwa mabao 4-0 na Mufurira Wanderers ya Zambia mjini Dar es Salaam, kikashinda mabao 5-0 katika mechi ya marudiano iliyochezwa mjini Lusaka, Zambia.

Hizo ndizo rekodi za kujivunia alizonazo sasa mwanasoka huyo mkongwe na ambazo anasema ni nadra kwa wachezaji wa sasa kuweza kuzifikia.

"Tatizo la wachezaji wa sasa ni kwamba wanakosa ari ya kufikia mafanikio ya aina hii,"alisema Daudi alipozungumza na mwandishi wa makala hii kwa njia ya simu baada ya juhudi za kukutana naye ana kwa ana kushindwa kufanikiwa.

Nililazimika kuzungumza na Daudi kwa njia ya simu kwa sababu kumpata na kuzungumza naye ana kwa ana ni kazi ngumu. Hii ni kutokana na majukumu yake kikazi. Muda mwingi yupo bize.

Tofauti na wanasoka wengine wa zamani, kwa sasa Daudi havutiwi sana na mchezo huo. Inawezekana ni kwa sababu ya majukumu yake kikazi, lakini pia kutofurahishwa na mwenendo wa mchezo huo hivi sasa.

"Mchezo wa soka hivi sasa umegeuzwa kuwa biashara. Viongozi wa sasa wameshindwa kuweka mbele zaidi. Wameugeuza mchezo huo kuwa biashara,"alisema Daudi.

"Watu wameamua kuingia kwenye soka kwa sababu ya kufanya biashara. Hawana malengo ya dhati ya kuendeleza mchezo huo kama ilivyokuwa kwa viongozi wa zamani,"aliongeza.

Kwa mujibu wa Daudi, hali hii ndiyo iliyosababisha viongozi wengi wa soka nchini kuonekana kuwa wababaishaji kwa vile wamelenga kujinufaisha zaidi wao binafsi.

Daudi alisema enzi zao, wanasoka wengi walikuwa wakicheza mchezo huo kutokana na mapenzi waliyokuwa nayo kwa klabu zao na kwamba waliweza mbele zaidi uzalendo kwa nchi yao.

Alisema pia kuwa, nidhamu kwa wachezaji wa zamani ilikuwa juu na kwamba haikuwa rahisi kwa mchezaji kuonyesha utovu wa nidhamu kwa viongozi au ndani na nje ya uwanja.

Mkongwe huyo alisema enzi zao hakukuwa na malipo makubwa ya pesa kwa wachezaji kama ilivyo sasa, lakini walicheza kwa ari kubwa na kujituma kwa sababu ya mapenzi waliyokuwa nayo kwa mchezo huo.

"Enzi zetu, timu ya taifa ilikuwa ikipata huduma nzuri. Tuliwekwa kambini kwenye hoteli kubwa kama vile Bahari Beach au Kunduchi Beach na tulipata huduma zote muhimu. Ilikuwa vigumu kwa mchezaji kwenda nje ya misingi ya kambi,"alisema beki huyo mkongwe.

"Lakini wachezaji wa sasa wana matatizo na wengi hawana nidhamu ndio sababu wanashindwa kucheza soka kwa muda mrefu na kuziletea timu zao mafanikio," aliongeza.

Mwanasoka huyo mkongwe alisema ni makosa kuilaumu serikali kwa kushindwa kuendeleza michezo nchini wakati vyama vya michezo havionyeshi juhudi zozote katika kuiendeleza .

Alisema viongozi wa vyama vya michezo wanapaswa kuonyesha juhudi binafsi katika kuendeleza michezo wanayoiongoza ndipo serikali inapoweza kuingiza mkono wake.

"Hakuna mtu anayeweza kuwekeza kwenye tope. Unawekeza mahali penye neema. Panapokuwepo viashiria vizuri ndipo mwekezaji anaposhawishika kuwekeza,"alisisitiza mwanasoka huyo.

"Kwa hiyo hatuwezi kuilaumu serikali wakati ambapo viongozi wenyewe ni wabinafsi na wameweka mbele zaidi maslahi yao binafsi,"alisisitiza.

Daudi pia ameuponda utaratibu unaotumiwa sasa na baadhi ya klabu kubwa za soka nchini kupapatikia kusajili wanasoka wengi wa kigeni wakati uwezo wao ni mdogo. Alisema kufanya hivyo ni kuwakatisha tamaa wanasoka wazawa.

Alisema klabu inaposajili wachezaji wengi wa kigeni, inawavunja nguvu wazawa, ambao baadhi yao kiwango cha ni cha juu, lakini hawathaminiwi.

"Huwezi kuleta mchezaji wa kigeni, ambaye kiwango chake ni kibovu ukategemea kupata maendeleo. Hayo ni matumizi mabaya ya fedha za klabu na yanaonyesha ni mbinu za kuhalalisha ulaji,"alisema.

Daudi ametoa mwito kwa serikali kuendeleza mashindano ya shule za msingi na sekondari, ambayo alisema miaka ya nyuma ilikuwa chimbuko la wanasoka wengi waliochezea klabu za Simba, Yanga na Taifa Stars.

WAGOSI WA KAYA HAIJAFA-DK. JOHN




JOHN EVANS 'DK. JOHN'


Asema walipigwa vita baridi ili kupunguzwa makali
Adai soko la bongo fleva limeoza na ni wizi mtupu

WAKATI wasanii John Evans 'Dk. John' na Fredy Maliki 'Mkoloni' walipounda kundi la Wagosi wa Kaya na kuibuka na albamu ya Ukweli mtupu, kila shabiki wa muziki wa kizazi kipya nchini alikiri kwamba kundi hilo lilikuwa moto wa kuotea mbali.

Hiyo ilitokana na baadhi ya vibao vyao vilivyomo kwenye albamu hiyo waliyoirekodi 2002 kama vile Tanga Kunani, Wauguzi, Trafiki, Kero na Soka ya Bongo, kutikisa anga ya muziki nchini.

Vibao hivyo vilitamba kutokana na sababu nyingi, lakini kubwa ni mpangilio wa ala za muziki na ujumbe uliomo kwenye nyimbo hizo, ambao uligusa maisha ya kila siku ya jamii.

Kundi hilo liliendelea kutamba 2003 baada ya kuibuka na albamu yao ya pili, inayojulikana kwa jina la Ripoti kamili kabla ya kuipua albamu ya tatu 2005, inayokwenda kwa jina la Nyeti. Albamu hizo zilirekodiwa kwenye studio za Master J zilizopo Dar es Salaam.

Kwa sasa, kundi hilo lililokuwa na maskani yake katika Jiji la Tanga, linaonekana kufa kimya kimya baada ya kushindwa kutoa albamu tangu 2006. Wasanii wa kundi hilo kila mmoja ameamua kufanyakazi kivyake.

Je, ni kipi kilichowasibu Wagosi wa Kaya? Ni kweli kundi hilo limesambaratika au bado lipo? Na ni kwa nini limesambaratika?

"Hili kundi bado lipo, halijasambaratika, isipokuwa limesimamisha shughuli zake kwa muda, lakini kurudi kwake itachukua muda mrefu,"alisema Dk. John alipozungumza na Burudani mjini Tanga hivi karibuni.

Dk. John alisema wameamua kusimamisha shughuli za kundi hilo kwa muda kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutingwa na shughuli binafsi na za kimaisha.

Aliitaja sababu nyingine iliyowafanya wasimamishe shughuli za kundi hilo kuwa ni mbinu chafu zilizokuwa zikifanywa na wapinzani wao kwa lengo la kuwamaliza.

"Zilifanywa mbinu nyingi kutushusha na kutumaliza kiusanii. Kulikuwa na vita baridi dhidi yetu bila sisi kujua,"alisema msanii huyo, ambaye katika nyimbo za kundi hilo alikuwa akiimba kwa sauti ya kisambaa.

"Ulifika wakati hata vyombo vya habari vilishiriki kutumaliza. Kila tulipokuwa tukipeleka nyimbo zetu kwenye vituo vya redio na televisheni, tulibaniwa,"aliongeza.

Kwa mujibu wa Dk. John, baadhi ya watangazaji wa redio na waandaaji wa vipindi vya muziki vya televisheni waliwalazimisha wawapatie pesa ndipo wapige nyimbo zao, lakini hawakukubaliana na jambo hilo.

Dk. John alisema walijaribu kutaka kulirejesha upya kundi hilo 2007, lakini walishindwa kutokana na kuendelea kwa vita hiyo baridi dhidi yao.

"Ni kuanzia wakati huo tukaamua kusimamisha shughuli zetu za muziki, mimi nikarejea Tanga, mwenzangu akabaki Dar es Salaam,"alisema.

Tangu wakati huo, Dk. John amekuwa akiendelea kujihusisha na muziki kwa kurekodi nyimbo zake binafsi wakati Mkoloni ameamua kujitosa kwenye ulingo wa siasa kwa kujiunga na CHADEMA.

Kibao chake cha kwanza kinajulikana kwa jina la Mashamsham ngoma ya Tanga, alichokirekodi 2008 kabla ya kuipua Mauzauza 2011. Kwa sasa, tayari Dk. John ameshakamilisha albamu inayojulikana kwa jina la Mashamsham, lakini alishindwa kuizindua kutokana na kukosa pesa.

Akizungumzia maendeleo ya muziki huo nchini, msanii huyo alikiri kuwa ni mazuri na makubwa ikilinganishwa na ilivyokuwa miaka ya nyuma, lakini nyimbo hazidumu kwa muda mrefu.

"Muziki hivi sasa ni biashara na una pesa nyingi kuliko ilivyokuwa enzi zetu. Tatizo pekee lililopo ni kwamba, nyimbo za siku hizi hazidumu kwa muda mrefu. Ikitoka leo, baada ya miezi minne inasahaulika,"alisema.

"Na hii ni kwa sababu wasanii tumekuwa wengi sana na kila mmoja anataka atoke. Na mwelekeo wa nyimbo zetu sote ni mmoja tu, mapenzi. Haiwezekani watu wote wauze nyanya," aliongeza.

Dk. John alisema wakati kundi lao lilipokuwa kwenye chati, walitegemea zaidi mauzo ya albamu kupata pesa kwa sababu idadi ya wasanii wa muziki huo ilikuwa ndogo ikilinganishwa na hivi sasa.

Alisema kwa sasa mauzo ya albamu yamekuwa mabaya kutokana na kukithiri kwa wizi wa kazi za wasanii, hasa kupitia kwenye mitandao.

Alisema msanii anaweza kurekodi albamu, lakini kabla hajaizindua, anakuta nyimbo zake zimeshavuja, watu wanazo kwenye simu na wengine wanaziuza kwenye CD. "Kwa jumla, mauzo ya albamu kwa sasa hayalipi,"alisema.

Dk. John alisema kinachowatoa wasanii hivi sasa ni maonyesho ya kwenye kumbi za burudani na matangazo ya biashara. Alisema hali hiyo ndiyo iliyowafanya wasanii wengi waamue kurekodi nyimbo moja moja kwa lengo la kujitangaza.

Alikiri kwamba ushindani katika muziki huo kwa sasa umekuwa mkubwa kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wasanii. Alisema msanii asiyekuwa makini katika kutunga na kurekodi nyimbo zenye ujumbe mzuri kwa jamii, hawezi kudumu muda mrefu.

"Hali hii ndiyo imesababisha baadhi ya wasanii waanze kushikana uchawi kwa sababu wengi hawajiamini. Wanakwenda kwa waganga wa kienyeji ili wapate dawa za kuwaletea mafanikio,"alisema.

Dk. John ameilaumu serikali kwa kushindwa kusimamia vyema biashara ya muziki na kusababisha ikose malipo ya kodi. Alisema kutokana na kukua kwa biashara hiyo, wakati umefika kwa serikali kudhibiti wizi wa kazi za sanaa.

Akitoa mfano, alisema baadhi ya watu wamekuwa wakianzisha studio za kurekodi muziki katika nyumba zao binafsi bila kufuata taratibu na hivyo kuikosesha serikali mapato.

Alisema pia kuwa, mauzo ya albamu yamekuwa yakifanyika holela na kuwanufaisha wafanyabiashara wachache huku wasanii wakiendelea kunyonywa.
"Muziki ni uchumi kama ilivyo kwa madini na maliasili. Ukiwepo usimamizi mzuri, serikali itaingiza fedha nyingi,"alisema.

Dk. John alisema biashara ya muziki wa kizazi kipya kwa sasa ni wizi mtupu na soko lake limeoza ndio sababu wasanii wakongwe wamejikita zaidi katika kurekodi nyimbo moja moja na kufanya maonyesho kwenye kumbi za burudani badala ya kurekodi albamu.
"Hebu jiulize, AY na Mwana FA wamerekodi albamu kwa mara ya mwisho lini? Pengine utakuta 2005. Hawafanyi tena hivyo. Wameamua kurekodi nyimbo moja moja kwa lengo la kujitangaza ili wapate shoo,"alisisita.
Dk. John alisema iwapo maonyesho ya muziki wa kizazi kipya nayo yatakosa soko, utakuwa ndio mwisho wa wasanii na kwamba hali hiyo inaweza pia kuikuta fani ya filamu, ambayo ameielezea kuwa, utafika wakati nayo itakuwa hailipi.

Tuesday, February 26, 2013

RONALDO AIPELEKA REAL MADRID FAINALI COPA DEL REY



Barcelona 1 Real Madrid 3 (Agg 2-4): Ronaldo sends Jose's men into Copa del Rey final on miserable night for Messi


Real Madrid star Cristiano Ronaldo made the perfect response to those who say Leo Messi is the world’s best player by scoring two goals and inspiring his side to a shock Copa Del Rey semi-final win over Barcelona.

And Manchester United manager Sir Alex Ferguson was at the Nou Camp to see Jose Mourinho’s side win a two-leg cup-tie after drawing the home leg 1-1 — much as Real hope to do in the Champions League at Old Trafford next Tuesday.

This was Mourinho’s greatest night at Barcelona since his Inter Milan reached the Champions League final with 10 men.

And in the match when the absence of ex-Barca boss Pep Guardiola and his successor Tito Vilanova really started to show, Ronaldo was imperious.

He raced away on 15 minutes to draw a foul from Gerard Pique inside the area, then picked himself up and put the penalty past Manuel Pinto to become the first player ever to score in six consecutive away Clasicos.

In the second half, with stunned Barcelona chasing the game, Angel Di Maria sped past Carles Puyol in another lightning counter attack and when he squared to Ronaldo, the former Manchester United striker scored again — the first player to score doubles in consecutive Clasicos away from home.

In contrast, Messi, who went into the game looking for his 50th goal of the season, cut a forlorn figure as Barcelona repeated the same starting 10 outfield players as they had against AC Milan and delivered a similar lacklustre performance.

Messi was frustrated by the brilliant young French defender Raphael Varane, and it was the 19-year-old who headed in the third. Varane’s goal — a carbon copy of his first-leg equaliser — brought the most emotional of responses from Mourinho, who embraced the centre-back on the touchline and was in turn mobbed by most of his players as Madrid celebrated a home humiliation for Barcelona.

Jordi Alba scored a late consolation goal, running on to an excellent pass from Andres Iniesta, but it did little to take the shine off Madrid’s win

Mourinho sent Iker Casillas out to face the media on the final whistle and he urged Real Madrid to ensure Ronaldo stayed.

Speculation is linking the player with a return to England, as neither he nor the club seem to be interested in a contract extension on his deal which runs out in 2015, and Casillas said: ‘He is our most important player in these big games.

‘He was not just superb tonight, but he has been in the other clasicos. He is vital for us.

SIMBA YAITISHA MKUTANO MKUU WA DHARULA



KAMATI ya utendaji ya klabu ya Simba imeazimia kuitisha mkutanio mkuu wa dharura wa klabu hiyo ambao utakuwa na ajenda moja tu ya kujadili mwenendo mbaya wa klabu hiyo kwenye ligi kuu ya Vodacom.

Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema leo kwamba kamati ya utendaji ya Simba iliyokutana jana usiku imepitisha uamuzi wa kuitishwa kwa mkutano huo ili kujadili hali hiyo.

Alisema wanatarajiwa kutangaza tarehe na mahala utakapofanyika mkutano huo wakati wowote kuanzia sasa na kwamba uongozi umewataka wanachama wa klabu hiyo kusuusubiria mkutano huo.

“Uongozi pia umesikitishwa na sintofahamu inayoendelea ndani ya klabu yetu na hasa katika michezo yake ya ligi kuu hivyo basi uongozi umekubaliana kuitisha mkutano mkuu wa dharula ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa hali hii,”alisema.

SIMBA, MTIBWA ZAINGIZA MIL 62/-




Mechi namba 121 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Februari 24 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Mtibwa Sugar kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba imeingiza sh. 62,686,000.

Watazamaji 10,669 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,577,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,467,694.92.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 9,491 na kuingiza sh. 47,455,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 105 na kuingiza sh. 2,100,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,412,162.26, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,447,297.36, Kamati ya Ligi sh. 4,447,297.36, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,223,648.68 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,729,504.53.

Wakati huo huo, michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Februari 27 mwaka huu) kwa mechi tano zitakazochezwa katika viwanja tofauti.


Vinara wa ligi hiyo Yanga wataikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa viingilio vya sh. 5,000 (viti vya bluu na kijani), sh. 8,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh. 15,000 (VIP C na B) na sh. 20,000 (VIP A).

Mechi nyingine za ligi hiyo ni Coastal Union vs Ruvu Shooting (Mkwakwani, Tanga), Polisi Morogoro vs Mgambo Shooting (Jamhuri, Morogoro), JKT Ruvu vs Toto Africans (Azam Complex, Dar es Salaam) na Mtibwa Sugar vs Tanzania Prisons (Manungu, Morogoro).

TFF YAFUNGIA WAAMUZI NA KAMAMISHNA WA LIGI KUU




Mwamuzi Msaidizi wa FIFA, Ferdinand Chacha ameondolewa kuchezesha mechi za VPL baada ya kupata alama za chini kwenye mechi kati ya African Lyon na Simba iliyochezwa mwezi uliopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Waamuzi wanaopata alama 6.5 au chini ya hapo kati ya 10 zinazohitajika pia wanaondolewa kwenye mechi za VPL na FDL.


Waamuzi wengine walioondolewa kwa kutomudu mechi walizochezesha za VPL ni Mathew Akrama (Yanga vs Simba), Ephrony Ndissa (Yanga vs Simba), Ronald Swai (Yanga vs Mtibwa Sugar).

Walioondolewa kwa kupata alama za chini ni Alex Mahagi (Simba vs JKT Ruvu), Methusela Musebula (Toto Africans vs Coastal Union), Lingstone Lwiza (Toto Africans vs Coastal Union), Idd Mikongoti (Toto Africans vs Mtibwa Sugar) na Samson Kobe (Toto Africans vs Mtibwa Sugar).

Masoud Mkelemi aliyekuwa mwamuzi wa mezani katika mechi ya FDL kati ya Moro United na Villa Squad ameondolewa kwa kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting) na alichelewa kwa dakika tano kufika uwanjani.

Wakati huo huo, baadhi ya makamishna wa VPL na FDL wameondolewa na wengine kusimamishwa kusimamia mechi za ligi hizo kutokana na upungufu kwenye ripoti zao au kutowasilisha kabisa ripoti hizo TFF baada ya mechi.

Kamishna Mohamed Jumbe aliyesimamia mechi kati ya Mgambo Shooting na Simba ameondolewa kwenye orodha ya makamishna kutokana na ripoti yake kuwa na upungufu.

Makamishna wa mechi kati ya JKT Oljoro vs Yanga (Hakim Byemba), JKT Oljoro vs Kagera Sugar (Salum Kikwamba), Toto Africans vs African Lyon (Charles Komba), Coastal Union vs JKT Oljoro (Mohamed Nyange) wamesimamishwa hadi watakapowasilisha ripoti zao TFF.

Kwa upande wa FDL makamishna waliosimamishwa hadi watakapowasilisha ripoti zao TFF ni wa mechi kati ya Kurugenzi vs Polisi Iringa, Morani vs Mwadui, Polisi Mara vs Pamba, Polisi Mara vs Mwadui, Morani vs JKT Kanembwa na Pamba vs Polisi Dodoma.

Wengine ni Mwadui vs JKT Kanembwa, Polisi Tabora vs Morani, Polisi Dodoma vs Polisi Mara, Polisi Tabora vs Mwadui, Polisi Mara vs Morani, JKT Kanembwa vs Polisi Mara, Morani vs Rhino Rangers na Small Kids vs Mkamba Rangers.

Kamati ya Ligi imewakumbusha makamishna wote kuwa ni jukumu lao kuhakikisha ripoti zao zimefika TFF na kurekebisha upungufu wa jinsi ya kuripoti matukio yanayotokea uwanjani. Licha ya kutuma nakala kwa njia ya email, wanatakiwa pia kuwasilisha ripoti halisi (original) TFF.

KOCHA AZAM AFUNGIWA, ATOZWA FAINI


Kocha Mkuu wa Azam, Stewart John Hall amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushusha bukta yake na kumlalamikia mwamuzi msaidizi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Kagera Sugar iliyochezwa Januari 26 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana mwishoni mwa wiki kupitia ripoti za michuano ya VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 inayoendelea hivi sasa na kufanya uamuzi mbalimbali.

Naye Kocha Msaidizi wa timu ya Mgambo Shooting, Denis Mwingira ametozwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Oktoba mwaka jana katika Uwanja wa Manungu.

Ally Jangalu ambaye ni Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro naye ameangukiwa na rungu la Kamati ya Ligi kwa kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kupinga uamuzi wa refa kwa sauti ya juu. Alitenda kosa hilo kwenye mechi kati yao na Kagera Sugar iliyochezwa Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Matukio ya aina hiyo kwa kocha Jangalu yamekuwa ya kujirudiarudia ambapo Oktoba 13 mwaka jana katika mechi dhidi ya Azam iliyochezwa mjini Morogoro aliondolewa na mwamuzi kwenye benchi kwa kuchochea wachezaji wa timu yake wacheze rafu.

Naye Kocha wa timu ya Moro United inayoshiriki FDL, Yusuf Macho amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumtolea lugha chafu refa baada ya mechi dhidi ya Transit Camp iliyofanyika Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.

Pia Kocha wa Burkina Faso, Hasheem Mkingie amepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kutoa lugha chafu katika mechi ya FDL dhidi ya Mkamba Rangers.

Kiongozi wa Majimaji, Joseph Nswila ambaye aliingia uwanjani baada ya mechi dhidi ya Mlale JKT kumalizika na kuvamia waamuzi amefungiwa miezi sita.

Vilevile timu ya Azam imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi kati yao na JKT Oljoro iliyochezwa Novemba 7 mwaka jana katika Uwanja wao wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Pia Coastal Union imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Simba iliyochezwa Oktoba mwaka jana Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Nayo klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa timu yake kugoma kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Oktoba 24 mwaka jana.

Timu ya Burkina Faso ya Morogoro imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na kuonesha vitendo vya ushirikina kabla ya mechi yao dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Oktoba 24 mwaka jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Faini ya ushirikina ya sh. 200,000 pia imepigwa timu ya Pamba baada ya kuonesha vitendo hivyo kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui iliyochezwa Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Nayo Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya washabiki wake kumtolea lugha chafu Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka na kumrushia chupa za maji mwamuzi wa mezani katika mechi dhidi ya Mbeya City iliyochezwa mjini Morogoro.

Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kuvamia uwanjani na kutaka kuwapiga waamuzi katika mechi yao dhidi ya JKT Kanembwa na kusababisha mipira miwili ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kupotea.

Pia klabu kadhaa zimeandikiwa barua za onyo kwa timu zao kuchelewa kufika uwanjani au kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting). Klabu hizo ni Coastal Union, JKT Ruvu, Toto Africans, Simba, Green Warriors, Majimaji, Mkamba Rangers, Polisi Dodoma, JKT Kanembwa, Moro United.

Mchezaji Stanley Nkomola wa JKT Ruvu baada ya mechi dhidi ya Coastal Union alikwenda jukwaani na kuanza kupigana na washabiki. Pia kipa wa timu ya Transit Camp, Baltazar Makene baada ya mechi dhidi ya Tessema aliruka uzio na kwenda kupigana na washabiki.

Kwa vile masuala ya wachezaji hao ni ya kinidhamu yamepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

Monday, February 25, 2013

SERIKALI YAITUNISHIA MISULI FIFA, TANZANIA HATARINI KUFUNGIWA



SERIKALI imeamuru mchakato wa uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uanze upya kwa kufuata katiba ya 2006.

Uamuzi huo ulitangazwa jana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam.

Waziri Fenella alisema serikali imefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa, katiba ya sasa ina mapungufu mengi na ilipitishwa bila kufuata katiba ya TFF.

Mbali na kutoa agizo hilo, Waziri Fenella alitangaza kumfuta kazi Msajili wa Vyama na Klabu za Michezo nchini, aliyepitisha katiba hiyo kwa madai kuwa alifanya hivyo kimakosa.

Uamuzi huo wa Waziri Fenella huenda ukasababisha Tanzania ifungiwe na Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) kwa vile katiba ya TFF inazuia serikali kuingilia kati masuala ya soka.

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, hawajapata barua yenye agizo hilo kutoka kwa Waziri Fenella, lakini uamuzi huo unamaanisha kwamba, Tanzania ipo hatarini kufungiwa.

"FIFA imeshaelekeza wazi kwa wanachama wake kuwa, serikali haziruhisiwi kuingilia kati masuala ya soka kwa sababu vipo vyombo maalum vilivyopewa jukumu hilo kikatiba, sasa kama waziri ametoa agizo hilo, tusubiri tuone,"alisema.

Uchaguzi mkuu wa TFF ulisimamishwa baada ya kutokea mgogoro, kufuatia Kamati ya Rufani kumwengua Jamal Malinzi kugombea nafasi ya urais kwa madai kuwa hana uzoefu wa uongozi wa miaka mitano.

FIFA ilitangaza wiki iliyopita kuwa, itatuma wajumbe wake kuja nchini mwezi ujao kuchunguza mgogoro huo ikiwa ni pamoja na kuzihoji pande husika kabla ya kutoa uamuzi.

Hii ni mara ya pili kwa serikali kuingilia kati mgogoro ndani ya TFF, wakati huo kikijulikana Chama cha Soka nchini (FAT) na kusababisha Tanzania kabla ya serikali kusalimu amri.

Sunday, February 24, 2013

SIMBA YAANGUKIA PUA KWA MTIBWA


MATUMAINI ya Simba kutetea ubingwa wa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara leo yameendelea kuyeyuka baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar.


Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wachezaji wa Simba tangu mwanzo hawakuonekana kucheza kwa kujituma na hivyo kutoa mwanya kwa Mtibwa kutawala.

Bao pekee na la ushindi la Simba lilipachikwa wavuni na beki Salvatory Ntebe, aliyepanda mbele kusaidia mashambulizi. Alifunga bao hilo baada ya kuunganisha wavuni krosi kutoka kwa Vicent Barnabas.

YANGA, AZAM ZAINGIZA MIL 239/-



MECHI namba 120 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam imeingiza sh. 239,686,000.


Watazamaji 39,315 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 58,794,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 36,562,271.19.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 33,315 na kuingiza sh. 165,655,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 485 na kuingiza sh. 9,700,000.   Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 29,895,725.82, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 17,937,435.49, Kamati ya Ligi sh. 17,937,435.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 8,968,717.75 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 6,975,669.36.

YANGA NUSU BINGWA

YANGA jana iliendelea kujiimarisha kileleni mwa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Azam bao 1-0 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salam.

Ushindi huo uliiwezesha Yanga kuwa na pointi 39 baada ya kucheza mechi 16 huku ikiwa na mechi moja mkononi wakati Azam ni ya pili ikiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 17. Simba ni ya tatu ikiwa na pointi 31.

Kiungo Haruna Niyonzima ndiye aliyepeleka majonzi kwa mashabiki wa Azam baada ya kuifungia Yanga bao pekee na la ushindi dakika ya 31. Alifunga bao hilo baada ya gonga safi kati yake na Hamisi Kiiza.

Pambano hilo lilikuwa na burudani ya aina yake kutokana na timu zote mbili kuonyesha soka ya ufundi, hasa katika safu ya kiungo na ulinzi. Katika safu ya ushambuliaji, ukosefu wa umakini ndio uliokuwa kikwazo kuzikosesha kupata mabao.

Mshambuliaji Jerry Tegete aliikosesha Yanga mabao mengi wakati alipobaki yeye na kipa Mwadini Ally wa Azam mara tatu. Kipa huyo ndiye aliyekuwa nyota ya mchezo kutokana na kuokoa mipira mingi ya hatari.

Mwamuzi Abdalla Hashim wa Dar es Salaam alijikuta akiingia kwenye matatizo na wachezaji wa Azam kutokana na maamuzi yake kuwa ya kutatanisha. Baada ya pambano hilo kumalizika, mwamuzi huyo alilazimika kuokolewa na askari wa kutuliza ghasia (FFU) baada ya wachezaji wa Azam kumvamia.

Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa jana, Prisons ilishindwa kutambiana na Polisi Moro baada ya kutoka suluhu katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

JKT Mgambo iliutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kuichapa JKT Ruvu bao 1-0 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Bao pekee na la ushindi la Mgambo JKT lilifungwa na Fully Maganga dakika ya 25.

Friday, February 22, 2013

FIFA KUILIPUA YANGA


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limesema linapeleka rasmi madai ya mchezaji wa zamani wa Yanga, Kenneth Asamoah kwenye chombo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber) baada ya klabu hiyo kutojibu chochote.

Awali FIFA ilipokea malalamiko ya Asamoah kuwa anaidai Yanga dola 5,000 za Marekani ambapo ilikuwa ni sehemu ya malipo yake (signing fee) baada ya kujiunga na klabu hiyo.

Desemba mwaka jana FIFA iliiandikia barua Yanga kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikitaka maelezo yake kuhusu madai hayo ya Asamoah, lakini hadi sasa haijajibu madai hayo.

Kwa mujibu wa FIFA, hatua ya uchunguzi wa suala hilo umekamilika, na sasa linapelekwa rasmi katika chombo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber) kwa ajili ya kufanya uamuzi.

HASHIM ABDALLA KUZIHUKUMU YANGA NA AZAM




LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Februari 23 mwaka huu) kwa mechi tatu, lakini macho na masikio ya washabiki wa mpira wa miguu yatakuwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Uwanja huo wa kisasa utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Yanga na makamu bingwa Azam. Ingawa Azam imecheza mechi moja zaidi, lakini timu hizo zinatofautishwa kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa kwenye msimamo wa ligi huku kila moja ikiwa na pointi 36.

Pia vinara wa ufungaji kwenye ligi kwa sasa wanatoka katika timu hizo mbili. Kipre Tchetche aliyepachika mabao tisa hadi sasa ndiye anayeongoza akifuatiwa na Didier Kavumbagu wa Yanga mwenye mabao manane.

Iwapo timu yoyote itafanikiwa kuondoka na pointi tatu katika mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam, kasi ya mbio za kuwania ubingwa itaongezeka. Waamuzi wasaidizi watakuwa Hamis Chang’walu wa Dar es Salaam na John Kanyenye kutoka Mbeya wakati mezani atakuwepo Oden Mbaga.

Mechi nyingine za kesho ni Mgambo Shooting dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Jumapili (Februari 24 mwaka huu), Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa katika hekaheka nyingine kwa Simba chini ya Mfaransa Patrick Liewig kuikabili Mtibwa Sugar inayonolewa na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Maxime.

FDL YAENDELEA KUSHIKA KASI

Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi kumi na moja katika viwanja tofauti. Timu hizo zinapambana kutafuta hadhi ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao 2013/2014.

Kesho (Februari 23 mwaka huu) kundi A litakuwa na mechi moja itakayozikutanisha timu za Mkamba Rangers na JKT Mlale itakayochezwa Uwanja wa Ruaha mkoani Morogoro.

Kundi B lenyewe litakuwa na mechi mbili; Tessema itacheza na Ashanti United katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam wakati Ndanda itaikaribisha Polisi Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara.

Raundi ya 12 ya ligi hiyo kundi A itashuhudia timu zote nane zikiwa viwanjani; Pamba vs Mwadui (CCM Kirumba), Polisi Tabora vs Polisi Mara (Ali Hassan Mwinyi), Polisi Dodoma vs Morani (Jamhuri) na JKT Kanembwa vs Rhino Rangers (Lake Tanganyika).

Jumapili (Februari 24 mwaka huu) kundi A litakuwa na mechi kati ya Burkina Faso dhidi ya Kurugenzi (Jamhuri), Majimaji vs Polisi Iringa (Majimaji) wakati kundi B ni Transit Camp vs Villa Squad (Karume), na Green Warriors vs Moro United (Mlandizi).

Wednesday, February 20, 2013

MALKIA WA NYUKI AWAPONDA VIONGOZI SIMBA NA MAKOCHA WA KIGENI




MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya klabu ya Simba, Rahma Al-Kharoos ameponda utaratibu wa klabu za Tanzania kuajiri makocha wa kigeni na kuwadharau wazalendo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam jana, Rahma alisema Simba haina hadhi ya kufundishwa na kocha wa kigeni kutokana na viwango walivyonavyo wachezaji.

Rahma alisema viwango vya wachezaji wa Simba ni vya kawaida na amependekeza iwe chini ya Kocha Msaidizi, Jamhuri Kihwelu.

Mwanamama huyo, ambaye ni maarufu zaidi kwa jina la Malkia wa Nyuki alisema, kama Simba wanataka kufundishwa na kocha wa kigeni, ni vyema watafute wachezaji wenye viwango vya juu.

Akitoa mfano, alisema ilivyo Simba sasa ni sawa na mtoto wa shule ya awali kufundishwa na mwalimu wa chuo kikuu.

"Kwani sisi hatuna makocha wazalendo, si wapo wengi tu?" Alihoji mwanamama huyo.

Rahma alisema haiingii akilini kuona kuwa, klabu ya Simba inatumia dola 8,000 za Marekani kila mwezi kumlipa mshahara kocha wa kigeni wakati fedha hizo zingeweza kutumika kwa mambo mengine muhimu.

Mfanyabiashara huyo alisema haoni tatizo kwa timu za Tanzania kufundishwa na makocha wazawa kwa sababu katika nchi ya Oman, makocha wa kitanzania wana thamani kubwa.

"Kwa nini tutafute makocha wa nje wakati uwezo wa kuwalipa hatuna. Tunatafuta sifa? Lazima tubadilike,"alisisitiza.

Simba inafundishwa na Kocha Patrick Liewig kutoka Ufaransa, anayesaidiwa na Moses Basena kutoka Uganda na Jamhuri Kihwelu.

SIMBA YAUNGURUMA, AZAM YAFANYA MAUAJI


BAO lililofungwa na Amri Kiemba jana liliiwezesha Simba kutoka uwanjani na pointi zote tatu baada ya kuichapa Prisons bao 1-0 katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa.

Kiemba alifunga bao hilo dakika ya 36 kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Haruna Moshi 'Boban' aliyepiga krosi kutoka pembeni ya uwanja.

Ushindi huo umeiwezesha Simba kuendelea kujichimbia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo, ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 17 wakati Prisons ni ya 10 ikiwa na pointi 18.

Iliwachukua Simba dakika tano kufanya shambulizi kali kwenye lango la Prisons baada ya Mrisho Ngasa kupewa pasi ndani ya eneo la hatari na kubaki ana kwa ana na kipa David Abdalla, lakini shuti lake lilikuwa mboga kwa kipa huyo. Timu hizo zilikwenda mapumziko Simba ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Prisons ilikianza kipindi cha pili kwa kasi na nusura ipate bao dakika ya 59 wakati Fred Chudu alipoingia na mpira ndani ya 18, lakini shuti lake liliokolewa na kipa Juma Kaseja.

Maafande hao waliendelea kulitia misukosuko lango la Simba dakika ya 61 na kulazimisha kona, lakini mabeki Juma Nyoso, Komabil Keita, Nassoro Cholo na Amir Maftah walikaa imara kuondosha hatari.

Simba: Juma Kaseja, Nassoro Cholo, Amir Maftah/Kigi Makasi, Komabil Keita, Juma Nyoso,Abdalla Seseme, Mrisho Ngasa/Haruna Chanongo, Amri Kiemba/Felix Sunzu, Mwinyi Kazimoto, Haruna Moshi, Ramadhani Chombo.

Prisons: David Abdalla, Azizi Sibo, Laurian Mrale, Jumanne Elfadhil, Lugano Mwangama, Nurdin Issa, Sino Augustine, Fred Chudu, Emmanuel Gabriel, Elias Maguli na John Matei.

Wakati huo huo, Azam jana iliifanyia mauaji JKT Ruvu baada ya kuitandika mabao 4-0 katika mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.

Matokeo hayo yameiwezesha Azam kuzidi kukabana koo na Yanga katika uongozi wa ligi hiyo, baada ya kila moja kuwa na pointi 36, lakini zikiwa zinatofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Yanga, ambayo ina mchezo mmoja mkononi, imefunga mabao 33 wakati Azam, iliyocheza mechi 17, imefunga mabao 31. Timu hizo mbili zinatarajiwa kukutana keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabao ya Azam yalifungwa na Khamis Mcha, aliyepachika wavuni mawili, Abdi Kassim 'Babi' na John Bocco.

MALKIA WA NYUKI KUMLIPA MILOVAN MIL 40/-


MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya klabu ya Simba, Rahma Al-Kharoos amejitolea kumlipa kocha wa zamani wa timu hiyo, Milovan Circkovic.

Milovan, ambaye aliinoa Simba msimu uliopita kabla ya kutemeshwa kibarua baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania Bara, alikuwa akiidai Simba dola 24,000 za Marekani (sawa na sh. milioni 40).

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye hoteli ya Movenpick, Dar es Salaam, Rahma alisema amejitolea kumlipa kocha huyo kutokana na mapenzi yake kwa Simba.

Rahma, ambaye ni maarufu zaidi kwa jina la Malkia wa Nyuki alisema, malipo hayo ni haki kwa kocha huyo kwa vile aliitumikia Simba.

“Sasa hivi kuna matatizo mengi, kwa hiyo timu haifanyi vizuri, wanachama hawajui waangalie nini, matatizo ya kocha wa zamani, ambaye hajalipwa pesa zake an waaangalie timu kwa nini haifanyi vizuri,”alisema.

Rahma alisema Simba lazima iondokane na hali hiyo na hakuna haja ya kuoneana haya wala kuogopana.

"Kuna watu wanaodhani mimi naburuzwa, ninachoweza kusema mimi siburuziki, nasema ukweli, kama tatizo lipo, litatuliwe,"alisema Rahma.

Makamu mwenyekiti huyo wa kamati ya fedha ya Simba alisema, tatizo lililopo sasa kwa klabu hiyo ni uongozi na amewashauri kukaa chini ya kumaliza tofauti zao.

Alisema madai ya kocha huyo yalikuwa ya msingi na lilikuwa ni suala la viongozi kukutana naye na kuyamaliza, lakini alishangaa kuona wakimkwepa.

"Nitampa kocha fedha zake kwa sababu ni haki yake, mtu katoka kwao amewafanyieni kazi, mpeni haki yake, kwa nini mnamzungusha," alisema mwanamama huyo.

Rahma alimtaka kocha huyo kucheki akaunti yake wiki ijayo na atakuta malipo hayo yakiwa yamefanyika kupitia benki.

NGULI WA FILAMU NIGERIA AFARIKI DUNIA


LAGOS, Nigeria

MCHEZA filamu mkongwe wa Nigeria, Justus Esiri amefariki dunia.

Esiri, ambaye ni baba wa mwanamuziki nyota wa Nigeria, Dr. Sid alifariki dunia Jumanne iliyopita akiwa na umri wa miaka 70.

Katibu wa Chama cha Wacheza Filamu wa Nigeria (AGN), Abubakar Yakub alisema jana kuwa, Esiri alifariki kutokana na ugonjwa wa kisukari.

Kwa mujibu wa Yakub, mkongwe huyo wa filamu alifariki akiwa katika hospitali ya Lagos, ambako alikuwa amelazwa akitibiwa ugonjwa huo.

"Ni pigo na simanzi kubwa. Sielewi kwa nini kifo kimekuwa kikiwanyemelea wacheza filamu wa Nigeria kwa muda mrefu sasa. Tayari tumewapoteza wacheza filamu wanne mwaka huu. Mjomba Justus aikuwa kama baba kwetu sote, tutamkumbuka,"alisema.

Taarifa za kifo cha Esiri zimekuja wakati mashabiki wa fani ya filamu na muziki nchini Nigeria wakiwa wanaomboleza kifo cha Goldie Harvey kilichotokea Februari 14 mwaka huu na mkongwe mwingine wa fani hiyo, Enebeli Elebuwa, aliyefariki dunia mwaka jana.

Marehemu Esiri alizaliwa Novemba 20, 1942 katika Jimbo la Delta. Alisoma na kujitosa kwenye fani ya uigizaji nchini Ujerumani kabla ya kurejea Nigeria mwanzoni mwa 1970.

Esiri alianza kupata umaarufu baada ya kucheza tamthilia ya Village Headmaster iliyokuwa ikirushwa kwenye kituo cha televisheni nchini Nigeria.

Tangu wakati huo, mkongwe huyo alicheza filamu zaidi ya 100, zikiwemo Home in Exile, Kingdom of Men, Most Wanted Bachelor.

KASEJA MBAYAAAA!



KIPA namba moja wa klabu ya Simba na timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, Juma Kaseja ameelezwa kuwa kikwazo kikubwa kwa makipa wenzake kupata namba kwenye timu hizo.

Uchunguzi uliofanywa na Burudani umebaini kuwa, makipa wote waliowahi kusajiliwa na Kaseja katika kikosi cha Simba ilikuwa nadra kwao kupata namba kwenye kikosi cha kwanza.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, kuna baadhi ya misimu, Kaseja aliidakia Simba mechi zote za ligi kuu ya Tanzania Bara na kuwaacha makipa wenzake wakisugua benchi.

Uchunguzi huo umabaini kuwa, sababu kubwa inayomfanya Kaseja apate namba ya kudumu Simba ni uwezo wake wa kulinda lango, kuwapanga mabeki na kucheza kwa kujituma.

Baadhi ya wadau wa soka wamekuwa wakimuhusi Kaseja kwamba anatumia ndumba kuwamaliza makipa wenzake, lakini imebainika kuwa tuhuma hizo hazina msingi.

Kaseja ndiye kipa mkongwe kuliko wote waliopo nchini hivi sasa na amekuwa akitunza kiwango chake kutokana na kufanya mazoezi kwa bidii na kutojihusisha na mambo ya anasa.

Baadhi ya makipa waliowahi kusugua benchi Simba wakiwa na Kaseja ni pamoja na Ally Mustapga 'Barthez', Kevin Mhagama, Shaaban Kado, Hamad Waziri, Wilbert Mweta na Deogratius Munishi.

Kati ya makipa hao, Bathez ndiye pekee aliyebahatika kucheza katika baadhi ya mechi muhimu na pia kuwa kipa namba moja wa Simba wakati Kaseja alipojiunga na Yanga msimu wa 2008/2009.

Waziri, ambaye alisajiliwa na Simba kwa mbwembwe msimu huu akitokea JKT Oljoro ya Arusha aliamua kufungasha virago baada ya kuonyesha kiwango cha chini kama ilivyokuwa kwa Mweta.

Hali hiyo pia imekuwa ikijitokeza kwenye kikosi cha Taifa Stars, ambapo Kaseja amekuwa akiwafunika makipa wenzake na kuwa chaguo la kwanza kwa makocha wa timu hiyo.

Kipa pekee, aliyekuwa akimpoka namba Kaseja kwenye kikosi hicho alikuwa Ivo Mapunda, ambaye alikuwa chaguo namba moja la kocha wa zamani wa timu hiyo, Marcio Maximo.

Kwa sasa, Simba imemsajili kipa wa kimataifa wa Uganda, Abbel Dhaira, ambaye alikuwa akicheza soka ya kulipwa Iceland, lakini upo uwezekano mkubwa naye akasugua benchi.

Tangu aliposajiliwa na Simba wakati wa usajili wa dirisha dogo, Dhaira hajapata nafasi ya kuichezea timu hiyo katika mechi za ligi kuu.

Mganda huyo alikuwa kipa wa akiba wakati Simba ilipocheza na Libolo ya Angola katika mechi ya awali ya raundi ya kwanza iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa umbo na urefu, Dhaira anaweza kuonekana kipa bora kuliko Kaseja, hasa kwa makocha wa Ulaya, lakini kutokana na umahiri wa Mtanzania huyo, anaweza kujikuta akisugua benchi msimu mzima na kulipwa mshahara wa bure.

WAERITREA WAPEWA UKIMBIZA UGANDA



KAMPALA, Uganda

SERIKALI ya Uganda imekubali kuwapa hifadhi ya ukimbizi wachezaji 15 wa timu ya soka ya taifa ya Eritrea waliozamia nchini humo.

Wachezaji hao pamoja na daktari wa timu hiyo, walitoroka kwenye kambi ya Eritrea wakati wa michuano ya Kombe la Chalenji iliyofanyika Desemba mwaka jana mjini Kampala.

Kamishna wa Wakimbizi katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uganda, Apollo Kazungu aliieleza BBC juzi kuwa, wameamua kuwapa hifadhi ya ukimbizi wachezaji hao kutokana na madai yao kukidhi maombi yao.

Eritrea ilitolewa katika hatua ya awali ya michuano hiyo baada ya kutoka suluhu na Zanzibar, kuchapwa 3-2 na Malawi na kufungwa 2-0 na Rwanda.

Baada ya kutolewa katika michuano hiyo, wachezaji 17 wa Eritrea waliondoka kwenye hoteli ya Sky ya mjini Kampala, ambako walipangiwa kukaa na kuaga kwamba wanakwenda kutembea mjini.

Hata hivyo, wachezaji hao walitokomea kusikojulikana wakati wengine watatu waliokuwa wamebaki hotelini, walirejea kwao.

Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA), Patrick Ogwel alisema wamefurahishwa na uamuzi huo wa serikali wa kuwapa hifadhi ya ukimbizi wachezaji hao.

"Hizi ni habari nzuri kama mamlaka zinazohusika zimeweza kulitatua tatizo hilo. Lakini siku zijazo, timu zinapaswa kuja kucheza soka na kurejea katika nchi zao,"alisema.

Kazungu alisema wachezaji wengine wawili waliokuwa wameomba hifadhi ya ukimbizi, waliamua kurejea kwao wakati wengine waliobaki waligoma kuondoka kwa hofu ya kupewa adhabu za kijeshi.

Kwa mujibu wa sheria za Uganda, raia wa kigeni wanaopewa hifadhi ya ukimbizi, hawalazimishwi kuishi kwenye kambi maalumu, badala yake wanaruhusiwa kuishi mahali popote iwapo watakuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Hii ni mara ya pili kwa wachezaji wa Eritrea kuzamia katika nchi zinazounda Baraza la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) wakati wa michuano ya Chalenji na Kombe la Kagame.

Katika michuano ya 2010 iliyofanyika Tanzania, wachezaji 13 wa Eritrea walitoroka kambini na kuomba hifadhi ya ukimbizi. Baadhi ya wachezaji hao kwa sasa wako Marekani ambako wamepatiwa hifadhi.

SUNZU AKWAMA READING, MATAPELI WALIMPIGA CHANGA LA MACHO



LUSAKA, Zambia

BEKI wa kimataifa wa Zambia, Stoppila Sunzu ameshindwa kupata mkataba katika klabu ya Reading ya England.

Sunzu amekwama kujiunga na Reading baada ya klabu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kusema kuwa, bado ana mkataba wa kuichezea timu hiyo.

Beki huyo wa kimataifa wa Zambia alimaliza majaribio yake Reading na kufuzu, lakini TP Mazembe ilimzuia kuhama hadi atakapomaliza mkataba wake.

Awali, wakala wa mchezaji huyo alidai kuwa, Sunzu alishamaliza mkataba wake na TP Mazembe na kwamba alikuwa mchezaji huru.

Hata hivyo, klabu hiyo yenye makao makuu yake Lubumbashi imesema, mkataba wa Sunzu unatarajiwa kumalizika 2015.

Reading iliamua kuachana na Sunzu baada ya kuzuka kwa mgogoro wa mkataba kati yake na TP Mazembe.

Uongozi wa TP Mazembe mwishoni mwa wiki iliyopita ulikutana na Sunzu na kujadili suala la mkataba wake.

"Tatizo hilo limeshapatiwa ufumbuzi baada ya kila upande kupitia mkataba wake na mchezaji amekiri kuwa, bado ana mkataba na TP Mazembe hadi 2015," Rais wa TP Mazembe, Moise Katumbi aliieleza BBC juzi.

"Tatizo ni kwamba, washauri wake wamekuwa wakimdanganya ndio sababu alikuwa akituona sisi kama kikwazo kwake. Tunahisi walitaka kuchukua pesa zake zote za ada ya uhamisho kwa kudai kwamba ni mchezaji huru,"aliongeza.

Katumbi alisema TP Mazembe ni klabu ya kulipwa na kamwe haiwezi kuwazuia wachezaji wake kwenda kucheza soka ya kulipwa Ulaya. Alisema jambo la msingi ni kwa wachezaji hao kufuata taratibu.

Rais huyo wa TP Mazembe alisema, siku zote wamekuwa wakitaka Sunzu akacheze Ulaya kutokana na ukweli kwamba, hawakumsajili kwa michuano ya klabu bingwa Afrika mwaka huu.

"Kama kuna klabu yoyote inayomuhitaji, hatuwezi kumzuia kuondoka, lakini klabu hiyo inapaswa kuzungumza na sisi,"alisisitiza Katumbi.

Kwa upande wake, Sunzu aliieleza BBC kuwa, anafurahi kuona suala hilo limepatiwa ufumbuzi.

Sunzu alisema ataendelea kuheshimu mkataba wake na TP Mazembe wakati akiwa anasubiri kupata ofa kutoka klabu za Ulaya.

SALIM AMIR, MKOBA WA TAIFA STARS ILIYOCHEZA FAINALI ZA AFCON 1980 (2)


WIKI iliyopita tulisoma wasifu wa mwanasoka mkongwe, Salim Amir, ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars kilichofuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za 1980 zilizofanyika nchini Nigeria pamoja na mtazamo wake kuhusu mwenendo na maendeleo ya mchezo huo kwa sasa. Endelea na sehemu hii ya mwisho ya mahojiano yetu na mchezaji huyo.

Salim alisema wakati alipokuwa kwenye kiwango cha juu kisoka, hakuwahi kufikiria kujiunga na mojawapo kati ya klabu kongwe nchini za Simba na Yanga kwa vile hakuona tofauti ya maisha ya wachezaji wake.

Alisema baadhi ya wachezaji aliokuwa nao Coastal Union kama vile Elisha John na Yanga Bwanga, waliwahi kujiunga na Yanga, lakini kutokana na kutopata mafanikio, waliamua kuondoka na kwenda Arabuni.

Licha ya kucheza soka kwa zaidi ya miaka 10, Salim alisema hakuna manufaa yoyote makubwa aliyoweza kuyapata kimaisha zaidi ya kujulikana na watu wengi na kutembelea nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya.

"Enzi zetu hakukuwa na manufaa yoyote tuliyoyapata zaidi ya kutembelea nchi nyingi. Hali haikuwa kama ilivyo sasa kwa wachezaji wetu,"alisema mkongwe huyo.

Alisema kufuzu kwa Taifa Stars kucheza fainali za Afrika za 1980 ni tukio pekee kubwa na ambalo hawezi kulisahau katika maisha yake kisoka. Anasema inasikitisha kuona kuwa, rekodi hiyo haijaweza kufikiwa na timu hiyo hadi sasa.

"Tulionyesha ushujaa mkubwa na kufanya kitu cha kihistoria, lakini hatukupata hadhi yoyote. Inawezekana ni kwa sababu ya uongozi wa wakati ule,"alisema.

Salim ameponda utaratibu unaotumiwa sasa na viongozi wa baadhi ya klabu za soka nchini kusajili wachezaji wengi wa kigeni wakati uwezo wao hauna tofauti kubwa na ule wa wazawa.

Alisema mchezaji bora wa kigeni ni yule mwenye uwezo wa kubadili sura ya mchezo wakati wowote atakapoingizwa uwanjani na si kama walivyo waliopo sasa.

Salim alisema ni vyema makocha wa timu za soka nchini wawe na utaratibu wa kufuatilia na kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi na kuwaendelea badala ya kupapatikia wachezaji wa kigeni.

"Sipingi kuwepo kwa wachezaji wa kigeni hapa nchini kwa sababu uwepo wao unaweza kuleta changamoto kwa wachezaji wetu, lakini idadi yao inapaswa kupunguzwa,"alisema.

Salim alisema Tanzania inayo hazina kubwa ya vijana wenye vipaji vya kucheza soka, lakini bado hawajapata nafasi ya kuonyesha uwezo wao kwa vile hakuna utaratibu wa kuwafuatilia.

Mkongwe huyo alisema mchezo wa soka kwa sasa ni kazi na iwapo utatumiwa vizuri, unaweza kuwapa manufaa mkubwa kimaisha wanasoka wa Tanzania na pia kuinua uchumi wa nchi.

"Lakini ili hayo yote yaweze kutimia, wanapaswa kuwa na malengo. Enzi zetu hakukuwa na huduma nzuri zinazotolewa kwa wachezaji kama ilivyo sasa, hii ni bahati kubwa kwao, hivyo wanapaswa kuitumia vizuri,"alisema.

Amezitaja mechi zilizo kwenye kumbukumbu ya maisha yake hadi sasa kuwa ni kati ya Taifa Stars na Zambia ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika za 1980. Mechi hiyo ilichezwa 1979 mjini Dar es Salaam na katika mji wa Ndola.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Taifa Stars iliichapa Zambia bao 1-0 na ziliporudiana mjini Ndola, zilitoka sare ya bao 1-1.

"Ilikuwa mechi ngumu na ya kihistoria na iliyotuwezesha kuweka rekodi ya kufuzu kucheza fainali za Afrika kwa mara ya kwanza,'alisema Salim, ambaye katika mechi hizo alicheza nafasi ya beki wa kati akiwa na Jella Mtagwa.

Salim pia anaikumbuka mechi ya nusu fainali ya Kombe la Chalenji kati ya Taifa Stars na Malawi iliyochezwa 1979 nchini Uganda. Timu hizo zilitoka sare mara mbili kabla ya Taifa Stars kutolewa kwa mikwaju ya penalti.

Akizungumzia uchaguzi mkuu ujao wa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salim alisema wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho hilo wanapaswa kuwa makini kwa kuchagua viongozi wenye sifa na uwezo.

Alisema viongozi wapya wa TFF wanapaswa kuweka mbele utaifa kwa kuwa na mipango madhubuti ya kuendeleza soka badala ya kuweka mbele maslahi yao binafsi.

"Ni miaka mingi sasa timu zetu hazijaweza kufika mbali kisoka katika michuano ya kimataifa. Lazima mkazo kwa viongozi wapya uwe ni kuinua soka ya Tanzania,"alisisitiza.

Salim ametoa mwito kwa wanasoka wa zamani nchini kujitokeza kuwania nafasi mbali mbali za uongozi katika uchaguzi wa klabu za soka, vyama vya soka vya wilaya, mikoa na taifa.

Alisema wakati umefika kwa TFF kuweka kanuni zinazotaka viongozi wa soka katika ngazi hizo, lazima wawe wamecheza soka na kuwa na uzoefu wa uongozi.

Ametoa mwito kwa TFF kuanzisha utaratibu wa kuwaendeleza na kuwapa mafunzo ya ukocha na uongozi, wanasoka wa zamani badala ya kuwaacha bila kuwatumia kuendeleza mchezo huo.

"Wapo baadhi ya wanasoka wa zamani, ambao walifika mbali kielimu. Hawa wanapaswa kutumika katika kuendeleza mchezo huo na ni watu muhimu,"alisema.

Salim alisema ni vyema pia kwa wanasoka hao wa zamani kupewa nafasi ya kuwa makamishna wa mechi za ligi kuu ya Tanzania Bara na zinginezo kwa vile tayari wana uzoefu wa sheria za mchezo huo.

Mkongwe huyo wa soka alizaliwa 1953 katika mji wa Tanga. Alisoma shule ya msingi ya Jumuia na baadaye sekondari ya Usagara. Ana mke na watoto wanne, watatu wa kike na mmoja wa kiume.