KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, February 14, 2013

DR. LEADER: Maprodyuza wengi wanyanyasaji, hawawajali wasanii



BAADA ya ukimya wa muda mrefu, msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya wa mkoani Tanga, Lucas Silas
'Dr.Leader' ameibuka na kusema wamiliki wa studio za kurekodi muziki ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya wasanii.

Dr. Leader amesema baadhi ya wamiliki hao wa studio wamekuwa wakichukua muda mrefu kukamilisha kurekodi nyimbo za wasanii na baadhi ya wakati huchukua kati ya miezi sita hadi mwaka mmoja kukamilisha wimbo mmoja.

Akitoa mfano, Dr. Leader alisema alirekodi nyimbo zake mbili za Mtoto Suzy na Pwani raha mwaka jana katika studio moja ya mjini Dar es Salaam, lakini ilimchukua miezi saba kuzipata.

Alisema hali hiyo imekuwa ikisababisha wasanii wakate tamaa mapema na wakati mwingine nyimbo zao zinapotoka, zinakuwa zimeshapitwa na wakati kimaudhui.

Msanii huyo aliyeanza kung'ara kwa kibao chake cha Msambaa, alichokirekodi kwenye studio ya Motika Records, iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu Abel Motika 'Mr. Ebbo', alisema hayo hivi karibuni alipozungumza na Burudani mjini Tanga.

"Unajua watu wengi hawajui jinsi wasanii wanavyotaabika kutokana na tabia za maprodyuza na wamiliki wa studio. Binafsi nimesota na kutaabika sana hadi kufika hapa nilipo. Kurekodi nyimbo kwenye studio za Dar es Salaam ni mateso matupu. Maprodyuza wengi ni wanyanyasaji na hawawajali wasanii,"alisema msanii huyo.

Alisema kuna wakati yeye na wasanii wenzake waliwahi kusoteshwa studio usiku kucha wakisubiri kurekodi nyimbo zao na kulazimika kulala uani bila kula chochote. Aliita tabia hiyo kuwa ni ya kinyama.

Dr. Leader alisema ni vyema wamiliki wa studio wajifunze kuwa wakweli kwa wasanii na wanapolipwa kwa ajili ya kazi wanazozifanya, wazikamilishe mapema ili nyimbo zisipitwe na wakati.

Alisema baadhi ya maprodyuza na wamiliki wa studio wanasahau kwamba, nyimbo inapofanya vizuri sokoni, sifa zinakwenda kwao kutokana na kazi ya kuisuka.

"Nimeacha nyimbo nyingi kwenye studio za Dar es Salaam kwa sababu ya tabia hiyo ya maprodyuza. Kule kwa Alan Mapigo zipo nyimbo zangu nyingi tu,"alisema msanii huyo.

"Mimi napenda ninapokwenda studio kurekodi nyimbo zangu, tuwe na makubaliano maalumu na prodyuza na ikiwezekana nizipate mapema kwa sababu tunatunga nyimbo kulingana na wakati. Vivyo hivyo kwa watangazaji, ninapompelekea nyimbo zangu, kama hawezi kuzipiga hadi nimpe pesa, aniambie mapema ili nifanye hivyo," alisema msanii huyo mwenye mke na watoto wawili.

Dr. Leader alisema binafsi amekuwa akirekodi nyimbo zake kwa fedha zake mwenyewe kwa vile yeye ni mwajiriwa na amekuwa akibana matumizi kwa ajili ya kazi hiyo, hivyo inapotokea kazi zake kucheleweshwa, roho inamuuma.

Msanii huyo alisema kutokana na adha hizo, ameamua kuendelea kurekodi nyimbo zake katika studio za mjini Tanga na kwa sasa anajiandaa kuipua nyimbo mbili zinazokwenda kwa jina la Mganga na Nasaka mbule.

Alisema ameamua kutunga na kurekodi nyimbo zake nyingi kwa lugha ya kisambaa kwa vile anataka kulitangaza kabila hilo kimataifa.

Dr. Leader alikiri kuwa, marehemu Mr. Ebbo ndiye aliyeibua kipaji chake na kumuendeleza kimuziki, lakini aliamua kuachana naye baada ya kujitokeza hali ya kutokuelewana.

"Sikuwa nimegombana naye. Tatizo lililojitokeza kati yetu ni kwamba alitaka nifanye vile anavyotaka yeye. Mimi nilikuwa nataka kubadilika,"alisema.

Dr. Leader alisema kuna wakati aliwahi kuwa chini ya lebo ya TMC, lakini kutokana na mgogoro wa uongozi, kampuni hiyo ilishindwa kutimiza malengo yake.

Alisema kufa kwa kampuni hiyo kulitokana na kiongozi wake mkuu kutaka kuwa mwamuzi wa mwisho wa kila kitu bila kuwashirikisha wenzake. Alisema tabia hiyo haikuwafurahisha wenzake.

Msanii huyo alisema licha ya yeye kuwa kiongozi wa mradi huo, kuna wakati wasanii wenzake walikuwa wakirekodi nyimbo zao na kuzipeleka vituo vya redio bila kumpa taarifa, hali iliyosababisha aamue kujiweka kando.

"Tulikuwa na malengo mazuri, lakini utekelezaji ulikuwa mbovu,"alisema msanii huyo.

Licha ya matatizo yanayojitokeza kwa wasanii wa muziki huo, Dr. Leader amewataka wasikate tamaa, badala yake waongeze bidii ya kufanya vizuri zaidi ili waweze kupata mafranikio.

Alisema baadhi ya changamoto, ambazo zimekuwa wasanii wa mikoani wamekuwa wakikumbana nazo ni pamoja na kutokuwa na watu wa kuziunga mkono kazi zao.

2 comments:

  1. I have been casting spells for many years and I have helped many people, I might be able to help you too. I am honest, and I genuinely care for all the clients who choose me to cast a spell for them.


    If you have any questions about Love, Money, curse, protection, bad luck, divorce, court cases, or about me please call or email me. I really want you to feel comfortable before moving forward with any spells, or other services. I will take the time to explain things to you and provide you with honest advice, to what is best for your situation. I will not pressure you into having a spell cast, I will leave that decision up to you, and when or if you decide to move forward, I might be able to help you.
    I will respect your Privacy. I will not seek to obtain any of your personal information beyond what you might voluntarily offer and all information you might give me including emails, phone numbers and photos will remain private and confidential.
    I perform my Rituals only at night between the hours of 0.00 - 0.59 (South African time) lasting 1 hour but of course, this depends on the nature of the ritual, some rituals might take hours and can also become necessary to be performed at specials places like; flowing streams, cemeteries and other places dictated by the gods.
    I do not want anyone to be under any illusions about my spells and its numerous rituals. Real and effective Voodoo is no child's play, it is expensive because, after the rituals, I will have to destroy all the materials involved by fire and the ashes scattered over a flowing stream or river.
    You will get what you seek.But please understand this might take a lot of time and that individual results may vary. contact +27663492930, greatogudugu@gmail.com

    Herbal cure for Following DISEASES,this is not scam is 100% Real.

    -HPV
    -DIABETES
    -PENIS ENLARGEMENT AND WEAK ERECTION
    -VIRGINA PROBLEM
    -WHOOPING COUGH
    - HEPATITIS B
    -FORDYCE SPOT
    -COLD SORE
    -ALS
    -LOWER RESPIRATORY INFECTION
    -LOW SPERM COUNT
    -MRSA(METHICILLIN-RESISTANT STAPHYLOCOCCUS AUREUS
    -ZIKA VIRUS
    -HIV
    -STROKE
    -IMPOTENCE
    -PILE
    -HYPERTENSION
    -LOW SPERM COUNT
    -MENOPAUSE DISEASE
    -ASTHMA
    -CANCER
    -BARENESS/INFERTILITY
    -PCOS
    -SHINGLES
    -VIRAL HEPATITIS/HEPATITIS B
    -FIBROID
    -ASTHMA
    -SICKLE CELL
    -TINNITUS
    -BARENESS/INFERTILITY
    -DIARRHEA and so on...

    ReplyDelete
  2. Ndugu yngu naomba unitumie iyo mtoto suz ya dr leader nisaidie kaka ata kwa whtsapp number +255679005799

    ReplyDelete