KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, February 3, 2013

YANGA, MTIBWA ZAINGIZA MIL 125/-


PAMBANO la ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara kati ya Yanga na Mtibwa Sugar, lililochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. milioni 125.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, kila timu ilipata mgawo wa sh. milioni 30.

Wambura alisema jumla ya watazamaji 22,030 walikata tiketi kwa ajili ya kushuhudia pambano hilo kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Ofisa huyo wa TFF alisema, kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi zaidi, ambapo watu 19,583 walikata tiketi hizo na kuingiza sh. 97,915,000.

Alisema katika makato, kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 19,095,406.78.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 15,435,255.48, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 9,261,153.29, Kamati ya Ligi sh. 9,261,153.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,630,576.64 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,601,559.61.

No comments:

Post a Comment