KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, April 2, 2015

DIAMOND APEWA MIL. 14/- NA CRDB



MWANAMUZIKI nyota nchini, Naseeb Abdul, maarufu kwa jina la Diamond, amepewa shilingi milioni 14 na benki ya CRDB kama fidia kwa ajili ya kujenga sehemu ya ukuta wa nyumba yake uliobomoka.

Ukuta wa nyumba ya Diamond, iliyoko Tegeta, Dar es Salaam, ulianguka wiki mbili zilizopita kutokana na kunyesha kwa mvua kubwa.

Akikabidhi fedha hizo kwa Diamond jana, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bima ya UAP, ambayo ni wakala wa CRDB, Raymond Komanga, alisema Diamond amekatia bima mali zake zote, ikiwemo nyumba yake.

Alisema kutokana na sababu hiyo, wameamua kumlipa bima ya nyumba yake yenye thamani ya sh. milioni 14 kwa ajili ya kutengeneza ukuta uliobomoka.

Diamond aliishukuru CRDB kupitia wakala wake wa UAP, kwa kumpatia fedha hizo kwa kuwa yuko kwenye kipindi kigumu kifedha.

"Nipo kwenye kipindi kigumu mno, mama yangu ni mgonjwa, halafu nipo kwenye maandalizi ya kutengeneza na kutoa video zangu mpya na vyote hivyo vinahitaji fedha,"alisema.

2 comments:

  1. CORRECTION PEOPLE.
    CRDB ni wakala UAP INSURANCE TANZANIA LTD.

    Over.

    ReplyDelete
  2. CORRECTION PEOPLE.
    CRDB ni wakala UAP INSURANCE TANZANIA LTD.

    Over.

    ReplyDelete