KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, April 2, 2015

TFF YAIOMBEA DUA YANGA



RAIS  wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF), Jamal Malinzi, amewatakia kila la kheri wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Young Africans, katika mchezo wa marudiano dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe, utakochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Mandava ulioko mjini Bulawayo.

Malinzi amesema Young Africans hawapaswi kubweteka kwa ushindi walioupata awali wa mabao 5-1 na kwamba kikubwa wanapaswa kwenda kupambana kusaka ushindi ugenini ili kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.

Endapo Young Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum, itaingia katika hatua ya 16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.

No comments:

Post a Comment