KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, November 30, 2015

KILI STARS YATOLEWA KOMBE LA CHALENJI, YAFUNGWA KWA MATUTA NA WENYEJI ETHIOPIA


Na Mwandishi Wetu, ADDIS ABABA
TANZANIA Bara imetolewa katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 na wenyeji Ethiopia, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
Katika mchezo huo wa Robo Fainali uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa, Tanzania Bara walikuwa wa kwanza kupata kupata bao liliofungwa na Nahodha wake, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyemalizia krosi ya Deus Kaseke dakika ya 25.
Ethiopia walisawazisha kwa penalti ya utata iliyofungwa na Nahodha wake, Panom Gathouch baada ya Mohammed Naser kujiangusha wakati akidhibitiwa na Shomary Kapombe dakika ya 57.
Stars walionekana kutaka kupagawa baada ya wapinzani wao kusawazisha bao na kuanza kuwaletea ubabe marefa, lakini baadaye wakatulia na kuendelea kucheza mpira.
Hata hivyo, bado bahati haikuwa yao, kwani baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1, walitolewa kwa matuta.
Beki Shomary Kapombe na kiungo Jonas Mkude walikwenda kupoteza penalti zao, wakati waliofunga kwa upande wa Kilimanjaro Stars ni kiungo Himid Mao, mshambuliaji Bocco na beki Hassan Kessy.
Waliofunga penalti za Ethiopia ni Panon Gathouch, Mohammed Naser, Ashalew Tamene na Behaylu Girima. 
Katika Robo Fainali ya Kwanza, Uganda imeifunga 2-0 Malawi mabao ya Farouk Miya na Ceasar Okhuti na sasa itakutana na Ethiopia katika Nusu Fainali, wakati Kili Stars inarejea nyumbani Dar es Salaam.
Kikosi cha Tanzania Bara kilikuwa; Said Mohamed, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Kevin Yondan, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Simon Msuva, Himid Mao, John Bocco, Said Ndemla na Deus Kaseke.
Ethiopia; Abel Mamo, Yared Bayeh, Aschalew Tamane, Anteneh Tesfaye, Aschalew Girma, Eliyas Mamo, Zekariyas Tuji, Gothuoch Panom, Beneyam Belay, Mohammed Naser na Bereket Yisshak.
IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BINZUBEIRY

U-15 YAKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA


Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) leo hii imekabidhiwa bendera ya Taifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.

Akiongea wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo ya vijana, Ole Gabriel amewashukuru TFF kwa kuwekeza katika soka la vijana, na kusema mafaniko yote yanandaliwa chini, hivyo analipongeza Shirikisho kwa kuamua kuwalea na kuwaendeleza vijana hawa wenye vipaji kwa manufaa ya taifa ya baadae.

Ole Gabriel amewataka vijana waliochaguiwa katika kikosi hicho, kuitumia nafasi hiyo adimu ipasavyo kuwawakilisha watanzania, kujituma katika mafunzo wanayopewa na waalimu wao, nidhamu ndani na nje ya uwanja na kuonyesha uzalendo wao wanapoiperesuha bendera ya Taifa.

Kikosi hicho cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 kinatarajiwa kuondoka kesho alfajiri (Jumatatu) kuelekea jijini Mwanza kwa mchezo wa kirafiki na kombaini ya mkoa wa Mwanza (U17), kisha kuelekea mkoani Kigoma kwa michezo miwili ya kirafiki dhidi ya kombaini ya mkoa wa Kigoma (U17) na timu ya Taifa ya Burundi (U17).

Baada ya michezo ya mkoani Kigoma, U15 itaelekea Kigali Rwanda kwa michezo na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, kisha Jinja kucheza na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Uganda, Nairobi itacheza na timu ya taifa ya Kenya (U17) na kumalizia jijini Arusha kwa kucheza na kombaini ya mkoa wa huo (U17).

Timu inatarajiwa kurejea jijini Dar ess alaam Disemba 24 baada ya kuwa imecheza michezo kumi ya kirafiki, mechi hizo zitampataia nafasi kocha mkuu Sebastiani Mkomwa kuona maendeleo ya vijana wake, wakiajiandaa kucheza michezo ya kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika U17 mwaka 2017 nchini Madagascar.

PROFESA OLE GABRIEL AFUNGA PROGRAMU YA 'YOUNG GOAL'Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel leo amefunga program ya Live Your Goal iliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Ole Gabriel amewashukuru vijana waliojitokeza kushiriki katika program hiyo na kuwaomba wazazi kuwarushu watoto wa kike kujtokeza na kushiriki katika program hiyo ya kuhamasisha wanawake kucheza mpira wa miguu.

Live Your Goal ni program inayoendeshwa na TFF kwa msaada kutoka FIFA yenye lengo la kuwahamasisha watoto wa kike, na wasichana kujitokeza kuucheza na kuupenda mpira wa miguu.

Programu hii iliyomalizika leo imejumuisha vilabu sita vya wanawake, kutoka wilaya za Ilala, Kinodoni na Temeke, shule za msingi sita kutoka jijini Dar es salaam ambapo washiriki walikua wanafunzi wenye umri kaunzia miaka 8 na kuendelea, na ikifanyika kwa mara ya pili baada ya awalia mwezi Juni mwaka huu mkoani Geita.

Saturday, November 28, 2015

KILI STARS YATOKA SARE YA 1-1 NA WENYEJI ETHIOPIANa Mwandishi Wetu, ADDIS ABABA
TANZANIA Bara imefuzu kwa kishindo Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kufuatia kumaliza mechi za makundi bila kupoteza mchezo.
Bara imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Ethiopia katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi A leo Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa. Dakika 45 za kwanza zilimalizika bila ya timu hizo kufungana na kipindi cha pili, Kilimanjaro Stars ilianza kupata bao kupitia ka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simon Msuva.
Msuva alifunga bao hilo la pili kwake katika mashindano ya mwaka huu kwa kichwa dakika ya 51 akimalizia krosi maridadi ya beki wa kushoto, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
Hata hivyo, Wahabeshi walifanikiwa kupata bao la kusawazisha baada ya beki Salum Mbonde kujifunga katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Mohamed Naser dakika ya 90 na ushei.
Stars sasa inamaliza kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na Rwanda iliyomaliza na pointi sita, Ethiopia pointi nne, wakati Somalia inaondoka mikono mitupu.
Mchezo wa kwanza leo, bao la dakika ya 70 la Frank Kalanda limeipa Uganda ushindi wa 1-0 dhidi ya Burundi.
Uganda imemaliza kileleni mwa Kundi B kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Kenya pointi nne ambazo zote zinafuzu moja kwa moja Robo Fainali. 
Sasa Tanzania Bara itamenyana tena na Ethiopia katika Robo Fainali Jumatatu, wakati Uganda itacheza na Malawi katika mchezo wa kwanza keshokutwa.
Jumanne Sudan Kusini itacheza tena na Sudan, wakati Rwanda itamenyana na Kenya.
Kikosi cha Tanzania Bara kilikuwa; Aishi Manula, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Salum Mbonde, Kevin Yondan, Himid Mao, Said Ndemla, Jonas Mkude, John Bocco, Elias Maguri na Simon Msuva.
Ethiopia; Abel Mamo, Seyoum Tesfaye, Najib Sani, Anteneh Tesfaye, Yared Bayeh, Aschalew Tamene, Panom Gathuoch, Beneyam Tesfaye, Behaylu Girma, Yissack Bereket na Mohamed Naser.

IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BINZUBEIRY

ZANZIBAR YAFUFUA MATUMAINI KOMBE LA CHALENJI


ADDIS ABABA, ETHIOPITA

TIMU ya soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), jana ilifufua matumaini ya kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea mjini hapa.

Zanzibar jana iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kenya katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Addis Ababa.

Katika mchezo huo, timu zote zilianza kwa kushambuliana kwa zamu na katika dakika 29, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alifunga bao lakini mwamuzi alikataa kwa madai alikuwa ameotea.

Zanzibar Heroes walifanya shambulizi la kushitukiza dakika 45 ambapo Suleiman Kassim ‘Selembe’ aliipatia timu yake bao la kwanza baada ya kuachia shuti kali akiwa nje ya 18 na kujaa wavuni moja kwa moja.

Hadi mapumziko ya kipindi cha kwanza Zanzibar Heroes walitoka wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu ambapo dakika ya 49 Cannavaro alipata nafasi na kupiga shuti ambalo lilitoka nje.

Dakika ya 56 Zanzibar Heroes walipata bao la pili kupitia kwa Hamisi Mcha baada ya kuonganisha krosi safiiliyochongwa na Selembe na kujaa wavuni moja kwa moja.

Kenya walifanya mabadiliko dakika ya 65 ambapo walimtoa Jacob Keli na nafasi yake ilichukuliwa na Kelvin Kimani wakati Zanzibar walimtoa Awadh Juma na kuingia Anthon Mathew.

Wakitandaza kandanda safi, Zanzibar walipata bao la tatu dakika 73 kupitia kwa Selembe baada ya kuwapiga chenga mabeki na kuachia shuti kali lililojaa wavuni moja kwa moja.

Kenya nusura wapate bao dakika 83 ambapo mshambuliaji wake Michael Olunga aliachia shuti kali lililookolewa na kipa Abdulrahman Mohamed.

Kenya walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Jacob Keli baada ya kuachia shuti kali kutokana na mabeki wa Zanzibar Heroes kujichanganya.

Kutokana na matokeo hayo, Zanzibar Heroes inaweza kwenda katika hatua inayofuata ya robo fainali kwa nafasi ya ‘best looser’, lakini inategemea na matokeo ya mechi za leo.

Katika msimamo wa kundi B, Kenya inaongoza kwa kuwa na pointi nne, sawa na Burundi ambapo zimepishana kwa mabao ya kufunga na kufungwa. Uganda ina pointi tatu sawa na Zanzibar.

Friday, November 27, 2015

LIGI YA SDL KUENDELEA WIKIENDI HIILigi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu 24 za makundi A, B, C na D kucheza  katika viwanja 12 mbalimbali nchini, kusaka nafasi nne za kupanda Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao (StarTime First League).

Kesho Jumamosi Kundi A, Mvuvuma FC watakua wenyeji wa Abajalo FC ya Tabora  uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Transit Camp watacheza dhidi ya Mirambo FC uwanja wa Kamabarage Shinyanga, huku Singida United watawakaribisha Green Warriors katika uwanja wa Namfua mjini Singida.

Kundi B, Allicane FC watawakaribisha AFC ya Arusha uwanja wa CCM Kirumba, JKT Rwamkoma watacheza dhidi ya Madini FC uwanja wa Karume Musoma, Kundi C, Changanyikeni dhidi ya Karikoo ya Lindi watacheza katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Mechi hizo zitaendelea kwa Kundi D, ambapo African Wanderes watawakaribisha Sabasaba FC uwanja wa Wambi, Mafinga, Mkamba Rangers dhidi ya Mbeya Warriors uwanja wa CCM Mkamba, na Wenda FC watacheza dhidi ya Mighty Elephant uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa michezo mitatu kuchezwa katika kundi B, na C, Pamba FC watawakaribisha Bulyanhulu FC uwanja wa CCM Kirumba, Mshikamo dhidi ya Abajalo uwanja wa Mabatini, Mlandizi na Villa Squad kuchuana dhidi ya Comsopolitan uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

KIKOSI CHA U-15 CHAINGIA KAMBINI


Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) imeingia kambini jana jioni katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam, kujiandaa na ziara ya mafunzo katika ukanda wa Afrika Mashariki itakayoanza Disemba Mosi mwaka huu.

Kocha wa timu hiyo Sebastian Mkomwa amesema vijana wote wameshawasili jijini Dar es salaam na leo wameanza mazoezi asubuhi katika uwanja wa Karume watakapokua wanajifua kila asubuhi na jioni mpaka siku ya safari.

Kikosi cha wachezaji 24 kimeingia kambini kujifua na ziara ya Afrika Mashariki, ambapo timu hiyo inaandaliwa kwa ajili ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, zitakazofanyika mwaka 2017 nchini Madagascar.

Timu ya Taifa ya vijana imeakua na program ya kukutana kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya kufanya mazoezi na kucheza michezo ya kirafiki na timu za kombani za U15 katika mikoa mbalimbali nchini, ambapo kwe mwezi Disemba itakua pamoja kwa wiki tatu katika nchi za Afrika Mashariki ikicheza michezo ya kirafiki.

Disemba Mosi, U-15 itasasiri kuelekea jijini Mwanza ambapo itacheza mchezo mmoja wa kirafiki na kombani ya jijini Mwanza (U17), kasha kusafiri kueleka mkoani Kigoma itakapocheza michezo miwili dhidi ya kombaini ya mkoa wa Kigoma (U17) na timu ya Taifa ya Burundi (U17).

Ziara hiyo itaendelea katika jiji la Kigali kwa kucheza michezo miwili dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda (U17), Jinja dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda (U17), Nairobi dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya (U17) na kumalizia kwa mchezo dhidi ya kombaini ya mkoa wa Arusha (U17) na kurudi jijini Dar es salaam.

KAMATI YA TAIFA STARS YAWASHUKURU WATANZANIAMwenyekiti wa Kamati Taifa Stars, Farough Baghozah amewashukuru watanzania kwa michango yao waliyoitoa kuispaoti timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ katika michezo ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi dhidi ya Algeria.

Farough alianza kwa kuwashukuru watanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika mechi ya Taifa Stars na Algeria na kuwashukuru pia wale wote waliosafiri na timu hiyo ya Taifa, Taifa Stars kwenda Algeria katika mechi ya marudiano.

Pia Mwenyekiti amechukua fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Makamu wa Raisi Mama Samiha Suluhu, Raisi Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam na Pwani na viongozi wote wa chama na serikali kwa njia moja au nyingine katika kusapoti timu ya Taifa Taifa Stars kwenye Mchezo na Algeria

Naye Mkuu wa mkoa Dar es salaa, ambaye ni mlezi wa kamati hiyo, Mh Mecky Sadick aliwashukuru watu wote, kuanzia wanakamati kwa jinsi walivyojitoa kwa muda wao wote katika maandalizi na hasa kuhamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao ya taifa kwa kuomnyesha uzalendo.

Kwa namna ya kipekee Mecky Sadick amewashukuru watu wote na makampuni yaliyojitokeza katika kuchangia Timu ya taifa wakiwemo Jubilee Insurance, Equity Bank, PPF, Serena Hotel, GSM, bila kusahau vyombo vote vya habari ambavyo kwa namna moja au nyingine waliweza kujitoa na kuhamasisha watanzania wajitokeze kwa wingi uwanja wa taifa kuishangilia timu yao.

Katika mchakato mzima wa awali wa mechi ya kufuzu kombe la dunia 2018, Kamati kupitia kwa wadau mbalimbali iliweza kuchangisha pesa jumla ya milioni 122,640,000 za kitanzania, dola za kimarekani 19,800 na 177,000 kutoka tigo pesa na airtel money.

Matumizi ni dola za kimarekani 70355, na milioni 47,904, 743 za kitanzania.

Mwisho kamati imewashukuru sana Watanzania na na kuwaomba wadumishe umoja wtue.. Nchi Yangu, Timu Yangu Taifa langu.

Wednesday, November 25, 2015

KILIMANJARO STARS YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CHALENJI, ZANZIBAR YAPIGWA 4-0


TANZANIA Bara imejihakikishia kwenda Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kushinda 2-1 dhidi ya Rwanda katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa, Ethiopia.
Ushindi huo, unaifanya Tanzania Bara iongoze Kundi A kwa kufikisha pointi sita na mabao sita, huku ikiwa imefungwa bao moja na sasa itamaliza na wenyeji Ethiopia ikiwa ‘haina presha’.
Kilimanjaro Stars leo ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa kiungo wa Simba SC, Said Ndemla kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 22 baada ya Nahodha John Bocco ‘Adebayor’ kuchezewa rafu na mchezaji mwenzake wa Azam FC, Jean Baptiste Mugiraneza.
Winga wa Yanga SC, Simon Msuva na mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara – akaifungia Stars inayofundishwa Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ bao la pili dakika ya 78.
Rwanda ilipata bao lake la kufutia machozi kupitia kwa Jacques Tuyisenge dakika ya 85. Sasa Amavubi iliyoifunga Ethiopia 1-0 katika mchezo wa kwanza, itamaliza na Somalia waliofungwa 4-0 na Kili Stars.     
Kikosi cha Tanzania Bara kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Kevin Yondan, Salum Mbonde, Himid Mao/Jonas Mkude, Simon Msuva, Said Ndemla, John Bocco, Elias Maguri na Deus Kaseke.
Wakati huo huo, Uganda imezinduka katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Zanzibar jioni ya leo mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Huo unakuwa mchezo wa pili mfululizo kwa Zanzibar Heroes kufungwa, baada ya awali kugungwa 1-0 na Burundi na sasa inajiweka katika mazingira magumu kwenda Robo Fainali.
Mabao ya Uganda katika mchezo huo wa Kundi B yamefungwa na Farouk Miya dakika ya 10 na 18, Erisa Ssekisambu dakika ya 48 na Ceasar Okhuti dakika ya 79.
Zanzibar ilipoteza wachezaji wawili kwa kadi nyekundu katika mchezo huo, kwanza kipa wake Mwadini Ally dakika ya 13 na baadaye kiungo Mudathir Yahya dakika ya 74, wote wa Azam FC ya Dar es Salaam. Zanzibar itamaliza na Kenya wakati Uganda itamaliza na Burundi.

CAF YAZIPA SEMINA KLABU ZA LIGI KUUMwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Yahya Hamad leo amefungua semina ya mafunzo ya leseni za vilabu katika ukumbi wa mikutano wa Dar es salaam International Conference Centre (DICC) uliopo jijini Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Yahya amesema imekua jambo jema kwa CAF kutupatia nafasi ya mafunzo ya leseni za vilabu hapa nyumbani, kwani viongozi wa vilabu wote wanapata nafasi ya kushiriki semina hii ya siku mbili kutoka kwa wakufunzui wa CAF.

“Uendeshaji wa mpira wa miguu duniani umebadilika, mabadiliko haya yapo katika nyanja zote za uongozi (utawala), miundombinu, kitu ambacho kwa sisi Tanania tumeshaanza kuendana na mabadiliko hayo, na sasa kupata kwetu semina hii kutawafanya viongozi wengi kufahamu umuhimu wa leseni za vilabu na kufanyia kazi mapungufu yaliyokuwepo” alisema Yahya.

Semina hiyo ya Leseni kwa Vilabu itakayofanyika kwa siku mbili inaedeshwa na wakufunzi watatu kutoka CAF ambao ni Dr. Bolaji Ojo Oba (Nigeria), Amanze Uchegbulanm (Nigeria) na Othman Mohamed kutoka nchini Sudan.

Agizo la CAF ni kuwa kila klabu inayoshiriki michuano ya kimataifa (Ligi ya Mabingwa, Kombe l Shirikisho) lazima iwe imepata leseni hiyo ambayo itaipa nafasi ya kushiriki michuano inayoandaliwa na CAF, na kwa klabu ambayo haitatimiza mahitaji ya kupata leseni hiyo haitaweza kushiriki michuano ya kimataifa.

Ili kupata leseni ya klabu, klabu inapaswa kutimiza vigezo vilvyowekwa ikiwemo masuala ya utawala, ripoti ya mapato na matumizi iliyokaguliwa, uwanja wa mazoezi nk.

Mmiliki mmoja wa klabu hatarusiwa kumiliki timu zaidi ya moja kwenye ligi moja, kila klabu lazima iwe na program za vijana na uwanja wa mazoezi.

Saturday, November 21, 2015

PICHA YA KIHISTORIA KWA WATANZANIA, HAIJAWAHI KUTOKEA NA HAITAKUJA KUTOKEA AFRIKA

RAIS John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na marais wastaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi; wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete

Friday, November 20, 2015

KILIMANJARO STARS YAWASILI ETHIOPIA


Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ tayari kimewasili Addis Ababa nchini Ethiopia leo alfajiri kikiwa na wachezaji 18 pamoja na vinogozi tayari kwa mashindano ya Kombe la Chalenji yatakayoanza kutimua vumbi kesho Jumamosi nchini humo.

Kilimanjaro Stars inayonolewa na kocha mkuu Abdallah Kibadeni, akisaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, imepangwa katika kundi A, ikiwa na wenyeji timu ya taifa ya Ethiopia, Rwanda, pamoja na Somalia.

Wachezaji waliosafiri na timu hiyo ni magolikipa Ally Mustafa na Aishi Manula, walinzi Shomari Kapombe, Kessy Radmahani, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Ishaka, Salim Mbonde na Kelvin Yondani.
Wengine ni viungo Himid Mao, Salum Abubakar, Jonas Mkude, Salum Telela na Said

Ndemla, huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Malimi Busungu, Elias Maguri, Saimon Msuva, Deus Kaseke na nahodha John Bocco.

Stars itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Somalia siku ya Jumapili katika uwanja wa Addis Ababa.

DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA DESEMBA 15

 
Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto

Kalenda ya dirisha la usajili kwa vilabu vya Ligi Kuu (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) lilofunguliwa Novemba 15, litafungwa Disemba 15 mwaka huu.

Vilabu vinavyoshiriki ligi hizo zilizopo chini ya Shirikisho Mpira wa Miguu (TFF) vinaombwa kufanya usajili katika muda uliopangwa ili kuepukana na kuchelewa, na kufungwa kwa dirisha hilo.

Usajili wa dirisha dogo ni kwa vilabu ambavyo havijajaza idadi ya wachezaji 30 katika usajili uliofanyika wakati wa dirisha kubwa la usajili (Juni – Agosti 2015), usajili huo wa wachezaji unafanyika katika tovuti ya TFF, www.tff.or.tz kisha kwenye link ya Club Registration.

Thursday, November 19, 2015

MALINZI ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA


MKWASA ATAKA STARS IPEWE MUDA ZAIDI


Kocha Mkuu wa timuya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa amewashukuru watanzania kwa kuwapa sapoti katika michezo miwili ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume, Mkwasa amesema pamoja na kupoteza nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya makundi kuwania kufuzu kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018, anawashukuru watanzania wote kwa ujumla kwa sapoti waliyowapatia.

“Tumepotezea mchezo wa mwisho dhidi ya Algeria, wenzetu walituzidi kiufundi, uwezo wa wachezaji binafsi ulikua chachu ya kuweza kuibuka na ushindi nyumbani kwao, lakini bado watanzania waishio Algeria na washabiki waliokuja uwanjani walitusapoti katika mchezo huo” alisema Mkwasa.

“Tupo katika kipindi cha kujenga timu, tuna vijana wengi wanaochipukia, hivyo wanahitaji muda wa kucheza zaidi na kupata uzoefu, tuendelee kuwapa sapoti vijana hawa kwa ajili ya kujenga kikosi bora cha baadae” ameongeza Mkwasa.

Mkwasa amewaomba watanzania kuendelea kuwasapoti vijana, pamoja na matokeo mabaya dhidi ya Algeria, bado kuna nafasi ya kufanya vizuri katika michezo inayofuata ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2017.

Naye nahodha msaidizi wa Taifa Stars, John Bocco ameishukuru TFF kwa kuwapatia huduma bora za maandalizi na wakati wa michezo yao yote, amewashukru watanzania na vyombo vya habari kwa kuwapa sapoti na kuwaomba kuendelea kuwaunga mkono pindi wanapokua na majukumu ya kuiwakilisha nchi katika michuano mbalimbali.

“Matokeo ya juzi (dhidi ya Algeria) sisi wachezaji yametusikitisha, tulikua na malengo na mtazamo tofauti wa kupata ushindi, lakini katika mpira kuna matokeo matatu, tumepoteza mchezo huo kikubwa ni kujipanga kwa ajili ya michezo ijayo na watanzania muendelea kutusapoti timu ya Taifa kama ambavyo mmekua mkifanya kwa sasa” alisema Bocco.

Stars imerejea leo alfajiri ikitokea nchini Algeria ilipokua na mchezo wa marudiano dhidi ya Algeria, Jumanne katika uwanja wa Mustapher Tchaker mjin Bilda ambapo ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 7 -0.

Wednesday, November 18, 2015

TAIFA STARS YAPIGWA 7-0 NA ALGERIA UGENINI


Na Mahmoud Zubeiry, BLIDA
TANZANIA imetolewa katika mbio za kugombania tiketi ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 zitakazofanyika nchini Urusi, baada ya kufungwa mabao 7-0 usiku huu na wenyeji Algeria katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida.
Matokeo hayo, yanaifanya Taifa Stars itolewe kwa jumla ya mabao 9-2, baada ya awali kulazimishwa sare ya 2-2 na Mbweha hao wa Jangwani katika mechi ya kwanza iliyochezwa Jumamosi mjini Dar es Salaam.
Katika mchezo wa leo usiku wa saa moja kwa majira ya huku sawa na saa tatu kwa majira ya  Afrika ya Mashariki , Algeria walipata bao lao la kwanza mapema tu sekunde ya 43 dakika ya kwanza, mfungaji Yacine Brahimi, aliyemalizia krosi ya Mesloub Walid aliyempita beki wa kushoto Mwinyi Hajji Mngwali, baada ya Himid Mao kupokonywa mpira
Algeria walipata bao la pili dakika ya 23 kupitia kwa Ghoulam Faouzi aliyepiga shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa zaidi ya 20, baada ya kiungo Mudathir Yahya kumchezea rafu Mesloub Walid na kuonyeshwa kadi ya njano.
Mshambuliaji Elias Maguri aliifungia Taifa Stars bao dakika ya 27 kwa shuti la mbali nje ya boki, lakini pamoja na refa Alioum Alioum kuelekea kukubali, akaghairi baada ya ushauri wa msaidizi wake namba mbili, Noupue Nguegoue.
Mudathir Yahya alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 40 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 40 kwa kumkwatua Yacine Brahimi
Na Mahrez Ryad akaifungia Algeria bao la tatu dakika ya 41 kwa shuti kali, akimalizia krosi ya Islam Slimani.
Kipindi cha pili, kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa alianza na mabadiliko akiwatoa kipa Ally Mustafa Barthez na winga Farid Mussa na kuwiangiza kipa Aishi Manula na kiungo Salum Telela.
Mabadiliko hayo hayakuwa na msaada wowote kwa Taifa Stars, kwani Algeria ilinufaika zaidi kipindi cha pili kwa kupata mabao manne zaidi.  
Islam Slimani alifunga bao la nne dakika ya 48 kwa penalti baada ya Mahrez kugongana na beki wa Taifa Stars, Kevin Yondan.
Ghezzal Faouzi akafunga bao la tano dakika ya 58 kwa penalti baada ya Slimani kugongana na Aishi Manula kwenye boksi wakigombea mpira.
Nahodha wa Mbweha wa Jangwani, Carl Medjani akafunga bao la sita kwa kichwa akimalizia kona ya Mahrez.
Ghezzal Rachid aliyetokea benchi akafunga bao la saba dakika ya 74 akimalizia kwa kichwa mpira wa adhabu wa Mahrez.
Taifa Stars ikazinduka baada ya bao hilo na kukaribia kufunga mara mbili, kupitia kwa washambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu. 
Dakika ya 85 Ulimwengu alimpa pasi nzuri Samatta baada ya wawili hao kugongeana vizuri, lakini Mbwana akapiga nje.
Na dakika ya 89, Maguri alimpa pasi nzuri Ulimwengu akafanikiwa kumtoka beki Carl Medjani, lakini kipa M’bolhi Rais akaugusa mpira kidogo na kutoka nje, ikawa kona ambayo haikuzaa matunda.
Kikosi cha Taifa Stars kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’/Aishi Manula dk46, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Himid Mao, Mudathir Yahya, Elias Maguri, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Farid Mussa/Salum Telela dk46.
Algeria; M’bolhi Rais, Medjani Carl, Mandi Issa, Ghoulam Faouzi, Belkarou Hichem, Bentaleb Nabil/Guedioura Aldane d36, Riyad Mahrez, Yacine Brahimi/Ghezzal Rachis dk66, Slimani Islam, Mesloub Walid/Ryad Boudebouz dk81 na Zeffanie Mehdi.

IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BINZUBEIRY

Monday, November 16, 2015

TAIFA STARS YATUA SALAMA ALGERIA


Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimewasili salama nchini Algeria leo jioni majira yaa 10 jioni, kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika mji wa Bilda.

Msafara wa Taifa Stars unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Athumani Kambi, ambapo jumla ya watu 40 wapo katika mji wa Bilda wakiwemo wachezaji 21 wanaojiandaa kwa mchezo wa marudiano.

Mara baada ya kufika katika uwanja wa ndege Algiers, Stars ilipokelewa na watanzania na wanafunzi wanaoshi nchini Algeria, na kuongozana na timu mpaka katika mji wa Bilda ilipofiki timu.

Stars inatarajiwa kufanya mazoezi kesho saa 1 jioni katika uwanja wa Mustapha Tchaker utakaotumika kwa mchezo wa marudiano siku ya Jumanne.

Katika mchezo wa awali uliochezwa jana jioni jijini Dar es salaam, Tanzania ilitoka sare ya mabao 2 – 2 dhidi ya Algeria, hivyo kuifanya Stars kusaka ushindi katika mchezo wa marudiano ili kuweza kusonga mbele.

Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vjana wake wote wapo katik ahali, hakuna majeruhi na wapo tayari kwa ajili ya kusaka ushindi siku ya Jumanne, na kusema makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa jana wanayafanyia kazi yasijitokeze tena katika mchezo unaofuata.

Taifa Stars imefikia katika hoteli ya Ville Des Roses imetumia takriabn muda wa saa 1 kutoka katika uwanja wa Ndege wa Algiers mpaka katika hoteli hiyo iliyopo eneo la Bilda.

Namba ya simu ya Afisa Habari wa TFF aliyeambatana na timu nchini Algeria +213 558 465069

Sunday, November 15, 2015

MAKAMU WA RAIS AWAFARIJI WACHEZAJI WA TAIFA STARS

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan, akimfariji nahodha wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Nadir Haroub 'Cannavaro' baada ya timu hiyo kulazimishwa kutoka sare ya mabao 2-2 na Algeria, katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan, akimfariji mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu. Kulia ni Mbwana Samatta akibubujikwa na machozi.
SAMIA akimfariji Samatta, baada ya Taifa Stars kulazimishwa kutoka sare ya mabao 2-2 na Algeria.
SAMIA akinyoosha mkono kushangilia wakati Taifa Stars ilipopata bao la kuongoza dhidi ya Algeria. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.
SAMIA akiteta jambo na Malinzi wakati wa mchezo huo.
VIKOSI vya Taifa Stars na Algeria kabla ya kuanza kwa mchezo wao jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka wachezaji wa timu ya Taifa, Taifa Stars, wasikatishwe na tamaa na matokeo ya sare waliyoyapata jana dhidi ya Algeria.

Katika mechi hiyo ya raundi ya kwanza ya michuano ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Taifa Stars ilitoka sare ya mabao 2-2 na Algeria.

Akizungumza na wachezaji hao baada ya mchezo huo, Samia aliwataka wachezaji hao kuongeza juhudi na kujituma zaidi ili waweze kushinda mechi ya marudiano.

"Japokuwa mmetoka sare na wapinzani wenu, lakini tumewaona mlivyocheza na kujituma. Msivunjike moyo, hayo ni matokeo ya kawaida katika mchezo. Ongezeni juhudi na kujituma, mna uwezo wa kushinda ugenini,"alisema.

Makamu wa Rais amewataka wachezaji wa Taifa Stars kumuweka mbele Mungu kwa kila jambo kwa vile kwa uwezo wake, wanaweza kushinda mechi ya marudiano.

Taifa Stars na Algeria zinatarajiwa kurudiana keshokutwa mjini Algiers. Ili isonge mbele, Taifa Stars italazimika kushinda mchezo huo au kupata sare ya zaidi ya mabao matatu.

Kikosi cha Taifa Stars kilitarajiwa kuondoka nchini jana usiku kwa ndege ya Fastjet kwenda Algiers kwa ajili ya maandalizi ya mechi hiyo.

Samia aliwaeleza wachezaji wa Taifa Stars kuwa, dua za Watanzania zitaelekezwa kwao hivyo wasiwe na hofu ya mchezo huo.

TAIFA STARS YAPOKONYWA TONGE MDOMONI NA ALGERIA, ZATOKA SARE YA MABAO 2-2


TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars jana ilipokonywa tonge mdomoni na Algeria baada ya kulazimishwa kutoka nayo sare ya mabao 2-2 katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia.

Stars itabidi ijilaumu kwa kushindwa kutoka uwanjani na ushindi kwani ilikuwa mbele kwa mabao 1-0 hadi wakati wa mapumziko na kuwazidi Waalgeria kwa kila hali uwanjani.

Mbali na kuongoza kipindi hicho, Stars pia ilipata nafasi nzuri zaidi ya tano za kufunga mabao, lakini zilipotezwa na washambuliaji wake, Elias Maguri, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Farid Mussa.

Maguri alianza kuwainua vitini mashabiki wa Taifa Stars dakika ya 42 alipofunga bao la kwanza kwa kuunganisha kwa kichwa krosi kutoka kwa Mwinyi Haji, aliyepanda na mpira pembeni ya uwanja.

Bao la pili la Stars lilifungwa na Samatta dakika ya 54 baada ya kuunganisha wavuni pande maridhawa kutoka kwa Mudathir Yahya.

Mabadiliko yaliyofanywa na Kocha Charles Boniface kipindi cha pili, kwa kuwapumzisha Mudathir na Maguri na kuwaingiza Saidi Ndemla na Mrisho Ngasa, yalionekana kupunguza kasi ya timu hiyo na kutoa mwanya kwa Algeria kutawala.

Mabao yote ya Algeria yalifungwa na mshambuliaji wake, Slimani Islam dakika ya 71 na 74.

Friday, November 13, 2015

SAMATTA AITOSA TP MAZEMBE, ATAKA KUCHEZA ULAYA


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars, Mbwana Samatta, amesema anatarajia kuihama klabu yake ya TP Mazembe Englebert ya Congo kwenda kucheza soka ya kulipwa Ulaya.

Samatta, anaondoka TP Mazembe akiwa ameipa ubingwa wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika na kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo Afrika.

Akizungumza Dar es Salaam jana,  Samatta alisema amechukua uamuzi huo, baada ya kupewa ushauri na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, akimtaka kucheza soka Ulaya.

Samatta, alisema amekuwa akizungumza na Rais huyo mstaafu mara kwa mara na anapowatembelea katika TP Mazembe, aliwasisitizia yeye na Thomas Ulimwengu wasiishie kucheza soka Afrika.

“Ushauri na wosia wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete naufanyia kazi  haraka, siku sio nyingi mtafahamu wapi nitakwenda, ndoto zangu ni kucheza soka Ulaya,”alisema Samatta.

Pia nyota huyo amewataka wachezaji chipukizi wa Tanzania kuongeza kasi ili kuchukua nafasi zao TP Mazembe.

“Naamini TP Mazembe itataka tena wachezaji kutoka Tanzania, baada ya sisi kuondoka, huu ni wakati wa wachezaji chipukizi kuchukua nafasi,”alisema Samatta.

Mchezaji huyo aliwasili Dar es Salaam jana asubuhi na Ulimwengu  na walijiunga na Taifa Stars kujiandaa na mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Algeria.

Taifa Stars na Algeria zitavaana Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 

RAIS MAGUFULI KUZISHUHUDIA TAIFA STARS NA ALGERIA KESHO


RAIS Dk. John Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia, ambao timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ itavaana na Algeria.

Taifa Stars na Algeria zitapepetana kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki, alisema Rais Dk. Magufuli, ataongoza Watanzania kuishangilia Taifa Stars katika mchezo huo.

“Tunategemea Rais wetu Dk. John Magufuli atakuwa mstari wa mbele kuwaongoza Watanzania Uwanja wa Taifa kuishangilia Taifa Stars. Ulinzi utaimarishwa,”alisema Sadiki.

Sadiki, ambaye ni mlezi wa Kamati ya Saidia Taifa Stars alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika.

Alisema kamati hiyo imefanya kazi nzuri kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya kuiwezesha Taifa Stars kushinda mchezo huo.

Mkuu huyo wa mkoa alisema Tanzania ina kila sababu ya kushinda kwa kuwa imepata maandalizi ya kutosha na ina kocha makini Charles Mkwasa, ambaye ni rafiki wa wachezaji wote.

Alisema hivi karibuni Watanzania walikosa imani na Taifa Stars, baada ya kufanya vibaya, lakini tangu Mkwasa apewe jukumu hilo hamasa imerejea.

Pia Sadiki, amewataka washambuliaji wa kimataifa wanaocheza soka ya kulipwa  timu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, kuipa ushindi Taifa Stars.

Alisema nguvu kubwa waliotumia kuipa ubingwa wa Afrika klabu yao ya TP Mazembe Englebert ya Congo waitumie kuifunga Algeria.

“Kuna timu moja ya Ulaya siwezi kuitaja jina, wachezaji wa hiyo timu wakiwa kwenye klabu yao wanajituma mno, lakini wanapochezea timu ya taifa wamekuwa wakionesha uwezo wa chini hali inayosababisha kuzomewa

“Nawasihi Samata na Ulimwengu wasifike huko, tunataka juhudi zao kwenye timu ya Taifa zionekane na sisi tunawaamini,”alisema Sadiki.

Alisema anaamini wachezaji wa Taifa Stars watajituma na kuweka uzalendo wa taifa lao mbele kuichapa Algeria.

Taifa Stars itacheza na Algeria, baada ya kuitupa nje Malawi kwa jumla ya mabao 2-1 ikiwa chini ya Mkwasa.

Mkwasa, ameingoza timu hiyo katika michezo mitatu ya kimataifa ilipotoka sare ya bao 1-1 na Uganda katika mchezo wa kufuzu Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).

Aliiongoza Taifa Stars kutoka sare ya bao 1-1 na Nigeria katika mchezo wa kufuzu Fainali za Afrika kabla ya kuvaana na Malawi.

Thursday, November 12, 2015

STARS YAREJEA DAR, KUFANYA MAZOEZI LEO JIONI TAIFA


Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager imerejea jana jioni ikitokea chini Afrika Kusini ilipokuwa imeweka kambi ya siku kumi, ambapo leo jioni itafanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na kocha mzalendo Charles Boniface Mkwasa, kimefikia katika hoteli ya Serena iliyopo eneo la Posta, na leo jioni watafanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya Congo DR wameungana kambini na wachezaji wenzao jana na kufanya kikosi cha Stars kukamilika kwa maandalizi ya mwisho.

Wapinzani wa Taifa Stars, timu ya Taifa ya Algeria wanatarajiwa kuwasili leo saa 12 jioni nchini kwa usafiri wa ndege binafsi, na kufikia katika hoteli ya Kilimanjaro Kempsink (Hyatt) ambapo kesho jioni Ijumaa watafanya mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es slaam.

Wakati huo huo waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Mali, mwamuzi wa kati Keita Mahamadou, Diarra Bala, Niare Drissa Kamory na mwamuzi wa akiba Coulibaly Harouna tayari wameshawasili nchini leo asubuhi, huku mtathimini wa waamuzi Attama Ibrahim Boureima kutoka nchini Niger alishawasili nchini tangu juzi usiku.

Kamisaa wa mchezo huo Mukuna Wilfred kutoka nchini Zimbambwe anawasili nchini leo mchana kwa shirika la ndege la Afrika Kusini (South Africa Airways

TIKETI PAMBANO LA STARS, ALGERIA KUANZA KUUZWA KESHOTiketi za mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia chini Urusi mwaka 2018 kati ya Tanzania dhidi ya Algeria ziataanza kuuzwa kesho Ijumaa katika vituo 10 viliyopo jijini Dar es salaam.

Magari maalumu yenye stika yataanza kuuza tiketi hizo za mchezo kesho saa 2 kamili asubuhi mpaka saa 12 jioni, ambapo tiketi zinauzwa kwa shilingi elfu tano (5,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani na rangi ya machungwa, na elfu kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C.

Vituo vitakavyotumika kuuza tiketi hizo ni ofisi za TFF – Karume, Buguruni – Oilcom, Mbagala – Darlive, Mnazi Mmoja, Luther House – Posta, Big Bone – Msimbazi, Ubungo – Oilcom, Makumbusho – Stand ya Daladala, Uwanja wa Uhuru.

TFF inawaomba wadau, washabiki na watanzania kujitokeza kwa wingi kununua tiketi za mchezo huo katika magari maalumu yatakayokuwepo kwenye vituo vilivyotajwa, ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizokuwa halali.

Wakati huo huo Ubalozi wa Algeria nchini Tanzania, umewataka waandishi wa habari wanaotrajia kwenda kuripoti mchezo wa marudiano jijini Algiers siku ya jumanne, kuwasilisha maelezo ya chombo wanachofanyia kazi pamoja na vifaa watakavyovitumia kwenye mchezo huo (camera, vinasa sauti) kuwasilisha maelezo hayo leo Alhamsi kabla ya saa 9 mchana katika ofisi za Ubalozi huo kwa ajili ya kupatiwa Accreditation za kufanyia kazi.

Matokeo ya mchezo wa jana  Azam Sports Federtaion Cup (ASFC), ni Mshikamano 0 - 1 Cosmopolitan.

Wednesday, November 11, 2015

KIBADENI KOCHA MKUU KILIMANJARO STARS


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemteua Abdallah Kibadeni kuwa kocha mkuu wa timu wa Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Star’ akisaidiwa na Juma Mgunda kuelekea katika michuano ya CECAFA Chelenji itakayoanza kutimua vumbi Novemba 21 mjii Addis Ababa, Ethiopia.

Kilimanjaro Stars inashiriki michuano hiyo mikongwe kabisa barani Afrika, ambapo jumla ya nchi 12 wanachama wamedhibitisha kushiriki michuano hiyo itakayomalizika Disemba 6 mwaka huu.

Nchi zingine zinazoshiriki michuano hiyo ni tofati na Tanzania bara ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudani, Sudani Kusini, Uganda na Zanzibar.

Kibadeni mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, na timu ya Taifa Tanzania, ni kocha mwenye leseni B, ambapo ameshafundisha klabu nyingi nchini kwa mafanikio ikiwemo kuifikisha Simba katika hatua ya fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993.

Kocha Kibadeni ni mkurugenzi wa ufundi wa kituo cha mchezo cha KISA kilichopo Chanika, amewahi pia kuzifundisha timu za Kagera Sugar, JKT Ruvu.

Kocha msaidizi wa Kilimanjaro Stars, Juma Mgunda ana leseni B ya CAF, zamani alikuwa mshambuliaji wa timu ya Coastal Union na timu ya Taifa Tanzania, pia aliweza cheza soka la kulipwa katika klabu ya Nahd nchini Oman.

Mgunda amewahi kuifundisha timu ya Coastal Union ya jijini Tanga, timu ya mkoa wa Tanga, kocha wa kituo cha vijana cha mkoa wa Tanga.

Aidha Mgunda ni mkufunzi wa msaidizi wa mafunzo ya makocha ngazi pevu.

TAIFA STARS KUREJEA DAR LEOTimu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inarejea leo nyumbani kwa shirika la ndege la Fastjet, ambapo inatarajiwa kuwasili uwanja wa JK Nyerere majira ya saa 12 kamili jioni.

Stars iliyokuwa imeweka kambi nchini Afrika Kusini kwa takribani siku 10, inarejea nyumbani ikiwa imefanya mazoezi vizuri kujiandaa na kuwakabili Mbweha wa Jangwani Algeria siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akiongelea kuhusu kambi kocha wa Stars, Charles Mkwasa amesema anashukru kwa kambi waliyoipata Afrika Kusini, wachezaji wote wameweza kufanya mazoezi katika kiwango cha juu, hapakua na majeruhi hivyo ana imani vijana wake watafanya vizuri siku ya Jumamosi.

Mkwasa amewaomba watanzania na wapenzi wa mpira wa miguu nchini, kujitokeza kwa wingi uwanjani kuja kuwasapoti katika mchezo dhidi ya Algeria, uwepo wa watanzania wengi uwanjani kuwashangilia utaongeza morali zaidi kwa wachezaji watakaokuwa wanapeperusha bendera ya Tanzania.

Mara baada ya kuwasili jijini Dar es salaam, kikosi cha Mkwasa kitafanya mazoezi kesho Alhamis jioni katika uwanja wa Taifa, na Ijumaa yakiwa ni mazoezi ya mwisho kabisa ya mchezo wenyewe unaosubiriwa kwa hamu.

Wakati huo huo wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wamewasili jijini Dar es salaam leo asubuhi , na moja moja kuingia kambini huku wakiwasubiri wachezaji wenzao wanaowasili leo na kujumuika pamoja kambini.A

KOMBE LA AZAM KUENDELEA TENA LEOMichuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuendelea leo katika viwanja vinne tofauti nchini, ambapo kila timu inahitaji kupata ushindi ili kusonga mbele katika mzunguko wa pili utakaochezwa mwezi Disemba mwaka huu.

Jijini Mbeya wenyeji Mbeya Warriors watakuwa wenyeji wa Wenda FC mchezo utakaochezwa uwanja wa Sokoine jijini humo, huku katika uwanja wa Majimaji mjini Songera timu ya Mighty Elephant watakua wenyeji wa African Wanderes.

Kariakoo ya Lindi watawakaribisha Changanyikeni FC katika uwanja wa Ilulu, huku timu ya Sabasaba ya mjini Morogoro wakiwakaribisha jirani zao Mkamba Rangers katika uwanja wa Jamhuri.

Michuano hiyo itaendelea kesho Jumatano kwa michezo miwili, Polisi Morogoro watawakaribisha Green Warriors uwanja wa Jamhuri mjini humo, huku timu ya Mshikamano FC wakiwa wenyeji wa Cosmopolitan katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Katika michezo iliyochezwa jana, Abajalo ilibuka na ushindi wa mabao 5 – 1 dhidi ya Transit Camp, huku Pamba FC ya jijini Mwanza ikiibuka na ushindi wa bao 1- 10 dhidi ya Bulyankulu FC ya mkoani Shinyanga.

KILIMANJARO STARS YAPANGWA KUNDI MOJA NA ETHIOPIA KOMBE LA CHALENJI
Ratiba ya michuano ya Kombe la Challenji kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Senior Challenger Cup) imetoka jana ambapo timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Star’ imepangwa kundi moja na wenyeji Ethiopia.

Katika taarifa ya CECAFA iliyotolewa jana, Kilimanjaro Star imepangwa kundi A pamoja na wenyeji Ethiopia, Somalia na waalikwa wa michuano hiyo timu ya Taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’.

Kundi B lina  Bingwa mtetezi timu ya Kenya, Uganda, Burundi na Djibouti, huku kundi C likiwa na timu za Rwanda, Sudan, Sudan Kusini na Zanzibar.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21 nchini Ethiopia katika mji wa Addis Ababa na kumalizika Disemba 6 mwaka huu.

WAALGERIA KUTUA DAR KESHO


Msafara wa timu ya Taifa ya Algeria (The Desert Warriors) unatarajiwa kuwasili nchini siku ya Alhamis kwa ndege binafsi ya kukodi, ukiwa na jumla ya watu 65 wakiwamo wachezaji 24 tayari kwa mchezo wa Jumamosi Novemba 14 dhidi ya wenyeji Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kocha mkuu wa timu hiyo Iitakayofikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Kempsinki, Christian Gourcuff raia wa Ufaransa ametaja kikosi cha wachezaji 24, wakiwemo wachezaji 18 wanaocheza katika klabu za Ulaya kwa ajili ya kuikabili Tanzania.

Wachezaji wanaotarajiwa kuwasili Alhamisi ni walinda mlango, Doukha Izeddine (JS Kabliye), M’bolhi Rais (Antalyaspor), Asselah Malik (CR Belouizdad), walinzi Zeffane Mehdi (Rennes), Medjani Carl (Trabzonspor), Ziti Mohamed (JS Kabliye), Mesbah Eddine (Sampordia), Bensebaini Ramy (Montpeller), Belkarou Hichem (Club African), Ghoulam Faouzi (Namples), Mandi Aissa (Reims).

Viungo ni Guedioura Adlane (Watford), Boudebouz Ryad (Montpeller), Taider Saphir (Bologna), Abeid Mehdi (Panathinacos), Bentaleb Nabil (Tottenham), Ghezzal Rachid (Lyon), Melsoub Walid (Lorient), Marhez Ryad (Leicester).

Washambuliaji  Benrhama Said (Nice), Sliman Islam (Sporting Lisbon), Belfodil Ishak (Beni Yas), Brahimi Yassine (FC Porto) na Bounedjah Baghdad (Etoile du Saleh).

KUZIONA STARS, ALGERIA BUKU TANO


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Jumamosi kati ya Tanzania dhidi ya Algeria utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam bei ya chini kuwa ni shilingi elfu tano (5,000) tu.

Tiketi za mchezo huo zitaanzwa kuuzwa siku ya ijumaa katika vituo mbalimbali vinavyotumiwa na TFF kuuzia tiketi, ambapo kiingilio kingine kitakua ni elfu kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C, huku kiingilio cha elfu tano kikiwa ni kwa viti vya rangi ya Bluu, Kijani na rangi ya Machungwa.

Wakati huo huo kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhamininiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kurejea nyumbani kesho Jumatano mchana kwa shirika la ndege la Fastjet tayari kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi ya Algeria siku ya Jumamosi.

Stars iliyoweka kambi nchini Afrika Kusini imekua ikifanya mazoezi kila siku katika uwanja wa Edenvale, ambapo mpaka sasa wachezaji wote wapo katika hali nzuri hakuna majeruhi na kila mmoja yupo tayari kwa mchezo wa Jumamosi.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vijana wake wapo vizuri kifaya, kifikra na morali ni ya hali juu “wachezaji wamekua wakifanya mazoezi kwa nguvu na kuonyesha umakini mkubwa” alisema Mkwasa.

Aidha, Mkwasa amewaomba watanzania na wadau wote wa mpira wa miguu nchini kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti ya kuwashangilia vijana katika mchezo dhidi ya Algeria Jumamosi, kwani kutawafanya wachezaji kujisikia wapo nyumbani na kucheza kwa nguvu zaidi.

Wachezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu walioshinda kombe la Ligi ya Mabingwa mwishoni mwa wiki na klabu yao ya TP Mazembe wanatarajiwa kuungana na wenzao kambini kesho jijini Dar es Salaam.

MALINZI AWAFAGILIA SAMATTA NA ULIMWENGU
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amewatumia salamu za pongezi wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya Congo DR kufuatia kutwaa Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) jana kwa kuifunga timu ya USM Algiers kwa jumla ya mabao 4-1.

Katika salamu zake kwenda kwa wachezaji hao, Malinzi amewapa hongera kwa mafanikio waliyofikia ya kutwaa ubingwa huo wa vilabu Afrika, na kuwataka waongeze bidii ili waweze kufanya vizuri pia katika michuano ya Kombe la Dunia la Mabara litakalofanyika mwezi Disemba nchini Japan.

Malinzi amesema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu na Watanzania wote wanawashukuru kwa kuiwakilisha vizuri Tanzania kimataifa, na sasa moyo huyo wa kujituma kwao waundeleleze katika mchezo dhidi ya Algeria wikiendi hii kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Sunday, November 8, 2015

TWIGA STARS YAIPIGA MALAWI 2-0TIMU ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars imewapa raha Watanzania jioni ya leo baada ya kuifunga Malawi mabao 2-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Katika mchezo huo maalum wa kumuaga mchezaji mwenzao mkongwe, aliyeitumikia timu hiyo kwa zaidi ya muongo mmoja, Esther Chaburuma ‘Lunyamila’, Twiga ilipata bao moja kila kipindi.


Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Asha Rashid Mwalala na Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’.


Mwalala ndiye aliyeanza kufunga dakika ya 43 kwa shuti kali akiwa mbele ya mabeki wa Malawi baada ya kupasiwa na Gaucho aliyefunga la pili dakika ya 82 kwa pasi ya Amina Ally.


Esther Lunyamila alicheza kwa dakika 28 kabla ya kumpisha mrithi wake wingi ya kushoto, Stumai Abdallah na alizunguka Uwanja mzima kuwaaga mashabiki kabla ya kutoka.


Twiga inayofundishwa na Rogasian Kaijage leo ilicheza vizuri na kuwapa burudani nzuri mamia ya Watanzania waliolipa kiingilio cha Sh. 1,000 kuushuhudia mchezo huo. 


Kikosi cha Twiga Stars kilikuwa; Fatma Omar/Belina Julius dk58, Anastazia Anthony, Donizia Daniel, Fatuma Issa, Fatuma Bushiri, Happyness Hezron, Amina Ally, Sofia Mwasikili/Shelder Boniphace dk58, Asha Rashid ‘Mwalala’, Esther Chaburuma ‘Lunyamila’/Stumai Abdallah dk28 na Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ . 


Malawi; Chimwembe Madise, Ruth Nyirongo, Ania Alizi, Emilly Jossam, Madina Nguluwe, Wezzie Mvula/Funny Mwale dk50, Pilirani Malola/Limbikani Chikupira dk76, Sungeni Msiska/Nkuzirile Bridget dk76, Linda Kasenda na Temwa Chawinga.


HABARI, PICHA KWA HISANI YA BLOGU YA BINZUBEIRY

KOMBE LA AZAM KUANZA LEO
Michuano ya Kombe la Shirikisho ya (Azam Sports Federation Cup) itafunguliwa rasmi leo Jumapili (Novemba 8, 2015) kwa mechi tatu zitakazochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti, ambao jumla ya timu 64 zitashirki kuwania nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.

Mechi rasmi ya ufunguzi itakuwa kati ya wenyeji JKT Rwamkoma ya Mara na Villa Squad ya Dar es Salaam itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Azam Sports HD ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.

LIGI Y SDL KUANZA NOVEMBA 15


Ligi Daraja la Pili nchini (SDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi wikiendi ijayo Novemba 15 katika viwanja mbalimbali nchini, huku timu 24 zinazoshiriki ligi hiyo zikisaka nafasi nne za kupanda ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.

Makundi ya FDL ni kama ifuatvyo; Kundi A ni Abajalo FC (Tabora), Singida United (Singida), Mvuvuma FC (Kigoma), Milambo FC (Tabora), Green Warriors (Dar es Salaam) na Transit Camp (Dar es Salaam) wakati kundi B ni Bulyanhulu FC (Shinyanga), JKT Rwamkoma (Mara), Pamba FC (Mwanza), AFC Arusha, Madini FC (Arusha) na Alliance Schools (Mwanza).

Kundi C ni Kariakoo (Lindi), Mshikamano FC (Dar es Salaam), Cosmopolitan (Dar es Salaam), Abajalo FC (Dar es Salaam), Changanyikeni Rangers (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam). Kundi D ni African Wanderers (Iringa), Mkamba Rangers (Morogoro), Town Small Boys (Ruvuma), Wenda FC (Mbeya), Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya) na Sabasaba United (Morogoro).

TAIFA STARS SASA KUKIPIGA NA TIMU YA TAIFA YA U23 YA AFRIKA KUSINI


Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa ya Afrika Kusini ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 (Amaglug-glug) Jumanne jioni kwenye dimba la Eldorado jijini Johannesburg.

Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya kuwakabili Algeria Novemba 14 jijini Dar es salaa katika uwanja wa Taifa na marudiano yake kufanyika Novemba 17 jiji Algiers kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Taifa Stars iliyokweka kambi nchini Afrika Kusini imekua ikifanya mazoezi kila siku katika uwanja wa Edenvale, baada ya kuwa na mazoezi ya stamina na pumzi kuweka uwiano sawa wa mazoezi (fitness level), Kocha wa Stars Charles Mkwasa sasa anaendelea na mazoezi ya kutengeza mfumo kwa wachezaji wake.

Awali Stars ilikuwa icheze mechi mazoezi kesho Jumapili na timu ya University of Pretoria inayoshriki ligi kuu ya Afrika Kusni (PSL), lakini baada ya Chama cha Soka Afrika Kusini (SAFA) kuandaa mchezo  dhidi ya U23, sasa mchezo dhidi ya Tucks hautakuwepo.

Friday, November 6, 2015

TAIFA STARS YAENDELEA KUJIFUA SAUZIKocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa ameendelea na mazoezi ya kukinoa kikosi chake kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria Novemba 14 jijini Dar es salaam kuwania kufuzu kwa kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Baada ya kufanya mazoezi kutwa mara mbili (asubuhi na jioni) kwa siku tatu, leo Ijumaa kocha Mkwasa amekiongoza kikosi chake kufanya mazoezi mara moja wakati wa jioni katika uwanja wa Edenvale.

Mkwasa amesema baada ya kufanya mazoezi ya kujenga mwili, stamina, na pumzi sasa kazi anayoifanya ni kutengeneza mfumo wa kikosi chake kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Mbweha wa Jangwani.


“Tulipofika tulianza na mazoezi ya utimamu wa mwili, stamina na pumzi ili kuhakikisha wachezaji wote waliopo kambini wanakuwa katika kiwango kimoja kutokana na kuwa wachezaji wanatoka katika timu tofauti na zenye walimu na mifumo tofauti” Alisema Mkwasa.

“Sasa baada ya wachezaji kufanya mazoezi kwa siku nne kuweka uwiano sawa kiwango cha kimazoezi (fitness level) kwa sasa tunafanya kazi kutengeneza mfumo na jinsi ya uchezaji” aliongeza Mkwasa.

Stars inaendelea na mazoezi leo jioni na kesho Jumamosi itafanya mazoezi asubuhi katika uwanja wa Edenvale

NB: Namba ya Afisa Habari wa TFF aliyepo nchini Afrika Kusini +27 78 641 1595

KUZIONA TWIGA STARS, MALAWI BUKU
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza kiingilio cha shilingi Elfu moja (1,000)  ndio kitakachotumika kuingia kushuhudia mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya Timu ya Taifa Wanawake ‘Twiga Stars’ dhidi ya timu ya Taifa ya Wanawake Malawi utakaochezwa leo Jumamosi, Novemba 7 katika uwanja wa Azam Chamazi.

Twiga Stars inayonelewa na kocha mzawa Rogasian Kaijage iliingia kambini wiki iliyopita ambapo imekua ikifaya mazoezi kila siku katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa.

Katika mchezo huo, Twiga Stars itautumia nafasi hiyo kumuaga mshambuliaji wake wa siku nyingi Estha Chaburuma ambaye ni miongoni mwa waanzilishi wa Twiga Stars na sasa anastaafu rasmi kucheza mpira wa miguu.

Upande wa timu ya Taifa ya Malawi tayari imewasili jana jioni jijini Dar e salaam ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 pamoja na viongozi nane ambapo leo jioni kikosi chake kitafanya mazoezi katika uwanja wa Karume saa 10 jioni.