KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, June 30, 2015

TAIFA STARS KUIFUATA UGANDA ALHAMISI


Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kuondoka nchini siku ya Alhamisi kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaofanyika siku ya jumamosi nchini humo.

Mchezo huo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN 2017 zitakazofanyika nchini Rwanda utachezwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Nakivubo jijini Kampala kuanzia majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa, amesema kikosi chake kinaendelea vizuri na maandalizi ya mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa juma nchini Uganda.

“Wachezaji wote waliopo kambini wanaendelea na mazoezi, vijana wanajituma mazoezin, morali ni ya hali ya juu naamini tutafanya vizuri katika mchezo wetu wa siku ya jumamosi” alisem Mkwasa.

Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamisi jioni kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda (Rwanda Air) ikiwa na kikosi cha wachezaji 20, benchi la ufundi pamoja na viongozi.

Aidha Mkwasa amesema ataongea na waandishi wa habari siku ya alhamis asubuhi saa 5 kamili - Karume juu ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea kwenye mchezo wa marudiano na kuweka wazi kikosi kitakachosafiri kuelekea nchini Uganda.

Stars imeweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo na inafanya mazoezi katika uwanja wa Boko Veterani kila siku jioni kuanzia majira ya saa 10 jioni.

FDL KUCHEZWA MAKUNDI MATATU 2015/2016
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2015/2016 itachezwa katika makundi matatu ya timu nane nane kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Mfuko huo wa makundi matatu umetokana na marekebisho ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) yaliyofanywa hivi karibuni na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao cake kilichofanyika mjini Zanzibar.

Timu ya kwanza katika kila kundi la ligi hiyo itakayoanza Septemba 12 mwaka huu itapanda kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa msimu wa 2016/2017 wakati timu itakayoshika nafasi ya mwisho katika kila kundi itashuka kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa msimu wa 2016/2017.

Kundi A linaundwa na timu za African Lyon FC (Dar es Salaam), Ashanti United SC (Dar es Salaam), Friends Rangers FC (Dar es Salaam), Kiluvya United FC (Pwani), Kinondoni Municipal Council FC (Dar es Salaam), Mji Mkuu FC (Dodoma), Polisi Dar es Salaam na Polisi Dodoma.

Timu zinazounda kundi B ni Burkina Faso FC (Morogoro), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mafinga FC (Iringa), Lipuli FC (Iringa), Njombe Mji FC (Njombe), Polisi Morogoro na Ruvu Shooting (Pwani).

Kundi C ni Geita Gold SC (Geita), JKT Kanembwa FC (Kigoma), JKT Oljoro (Arusha), Mbao FC (Mwanza), Panone FC (Kilimanjaro), Polisi Mara, Polisi Tabora na Rhino Rangers (Tabora).

U15 YAREJEA DAR
Kikosi cha timu ya Taifa cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) leo kinarejea jijini Dar es salaam kikitokea mkoani Mbeya ambapo jana kiliibuk ana ushindi wa ushindi wa mabao 4-1.

Monday, June 29, 2015

U-15 YAICHAPA KOMBAINI YA MBEYA 3-0



TIMU ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kombaini ya vijana chini ya umri wa 17 ya mkoa wa Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa.

Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi dakika 45 za kwanza zilimalizika U15 wakiwa mbele kwa bao 1-0.

Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji Timoth Maziku dakika ya 17 kwa guu la kulia akimalizia krosi ya Nahodha Issa Abdi.

Baada ya bao hilo, Mbeya Kombaini walitulia na kuanza kusukuma mashambulizi langoni mwa timu ya taifa, hali ambayo ilifanya timu hizo zishambuliane kwa zamu huku pia vijana wakionyesha uwezo wa kuridhisha.

Dakika ya 72, Albinius Haule almanusra aisawazishie bao Mbeya kama si shuti lake zuri la kitaalamu alilopiga kutoka umbali wa mita 25 kugonga mwamba wa juu na kutoka nje.

Nahodha Issa Abdi aliifungia timu ya taifa bao la pili dakika ya 82 kwa shuti la mpira wa adhabu baada ya Timoth Maziku kuangushwa nje kidogo ya boksi na Richard Paul.

Emmanuel Ntindi wa Mbeya alijifunga dakika ya 87 katika harakati za kuokoa krosi ya Asad Ally dhidi ya Maziku.

Mchezo ulikuwa mzuri, vijana walionyesha ufundi wa hali ya juu na Mbeya pamoja na kufungwa, walicheza vizuri na kilichowakwamisha kupata japo bao moja ni uhodari wa kipa Kelvin Deogratius wa U15 ya taifa.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana kesho jioni kwenye Uwanja Sokoine na mapema Jumanne U15 watarejea Dar es Salaam na vijana kuvunja kambi hadi watakapokusanyika tena mwishoni mwa mwezi ujao kwa safari ya Zanzibar kwa michezo mingine ya kujipima.

Vijana hao walio chini ya kocha Bakari Shime wanaandaliwa kwa ajili ya kucheza mechi za kufuzu Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2017 na kila wiki ya mwisho wa mwezi watakuwa wakikutana kwa mazoezi na michezo ya kujipima nguvu.

Kikosi cha Mbeya Kombaini kilikuwa; Edward Mwakyusa, Josephat Frank, Seif Gabriel, Emmanuel Ntindi, Richard Paul/Hassam Abdallah dk87, Goodluck Ezeria, Amiri Nyeo, Castro Issa, Albinius Haule, Biya Stephen na Daniel Samson/Castro Moses dk73.

Tanzania U15; Kelvin Deogratius, Kibwana Ally, Faraji John, Maulid Salum, Ally Hussein, Athumani Maulid/Rashid Kilomtola dk75, Robert Philipo/Morris Michael ‘Chuji’ dk86, Asad Ally, Timoth Joseph, Issa Abdi na Juma Zubeiry/Juma Juma dk61. 

Friday, June 26, 2015

KLABU ZATAKIWA KUWALIPIA KODI, WALIMU NA WACHEZAJI



Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeviagiza vilabu vinavyoshiriki Ligi kuu ya nchini (mpira wa kulipwa) Tanzania, kuhakikisha kuwa wanalipa kodi kutokana na kuajiri makocha na wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

Kamshina wa TRA ameliagiza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kupitia kwa katibu mkuu wake kuwa, vilabu vyote vya mpira wa miguu nchini vinavyoajiri walimu, wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi wahakikishe wanaweka kipengele cha kodi katika mikataba wanayoingia kuwaajiri.

Vilbu vya vinapaswa kuwasilisha mikataba yote ya ajira ya wachezaji na walimu wao ili kukokotoa kodi stahiki kwa kila mmoja wao na mikataba yao kugongwa muhuri na stempu.

Kwa mujibu wa sheria za Kodi ya Mapato ya mwaka 2004, kufungu namba 7, kila mtu anayepata mapato yatokanayo na ajira katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawajibika kulipa kodi ya mapato kulingana na kipato chake.

Aidha kwa mujibu wa Sheria ya Ushuru wa stempu ya mwaka 1973, kifungu namba 5 kikisomwa pamoja na jedwali la sheria hii, kila mkataba unatakiwa kugongwa muhuri na stempu na ofisa wa stempu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Kwa kuwa TFF ndio mlezi na msimamizi mkuu wa vilabu vya Mpira wa Miguu hapana nchini na hasa Ligi Kuu, tunaviomba vilabu vyote kuhakikisha vinawasilisha mikataba ya walimu na wachezaji yao ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya kugongwa mihuri na stempu.

U15 KWENDA MBEYA KESHO
Kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) kesho ijumaa kinatarajia kusafiri kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na timu kombani ya mbeya U15.

U15 ambayo inanolewa na kocha Bakari Shime, itaondoka na kikosi cha wachezaji wa thelathini (30) ambapo wanatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya kombani ya mkoa wa Mbeya ya vijana wenye umri chini ya miaka 15.

Timu itacheza michezo ya kirafiki siku ya jumapili na jumatatu ambapo kocha Shime atatumia nafasi hiyo kutambua uwezo wa wachezaji wake na kuongeza wachezaji wengine watakaonekana kutoka katika kombani ya mkoa wa Mbeya.

Mwezi ujao kikosi cha U-15 kitaelekea kisiwani Zanzibar kucheza michezo ya kirafiki na timu za kombaini ya Zanzibar kisha baadae kuendelea na ziara ya kucheza michezo ya kirafiki katika mikoa ya Iringa, Morogoro, Tanga, Arusha, Mwanza na Dodoma.

Lengo la TFF ni kuhakikisha Tanzania inakua na kikosi bora cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 kitachoshiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2017 nchini Madagascar.

TANZANITE YAINGIA KAMBINI
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 20 (U-20) Tanzanite Stars, imeingia kambini jana jioni Mbande jijini Dar es salaam na itakua ikifanya mazoezi katika uwanja wa Azam Complex.

Kikosi cha wacheaji 22 chini ya Kocha Mkuu Rogasian Kaijage kinafanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwnaja wa Azam uliopo Chamazi kujiandaa na mchezo dhidi ya U-20 ya Zambia utakaofanyika kati ya tarehe 10, 11 na 12 July jijini Dar es salaam.

Mchezo huo dhidi ya Zambia ni wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Wanawake za Dunia wenye umri chini ya miaka ya 20, zitakazofanyika nchini Papua New Guinea mwaka 2016.

Wachezaji waliopo kambini ni, Najiati Abbasi, Zuwena Aziz, Shelder Boniface, Stumai Abdallah, Donisia Daniel, Tatu Iddy (Evergreen Queens), Niwael  Khalfani, Maimuna Hamis (Mburahati Queens), Anastazia Anthony, Amisa Athumani, Amina Ramadhani, Neem Paulo (JKT Queens).

Wengine ni Asha Shaban, Rebeka Daniel, Brandina Wincelaus (Tanga), Happines Hezroni, Jane Cloudy (JKT Queens), Wema Richard, Gerwa Lugomba, Sadda Ramadhani (Uzuri Queens), Anna Hebron (Evergreen Queens) na Shehati Mohamed (Mburahati Queens)

Aidha wachezaji Monica Henry, Tumaini Michael (Uzuri Queens), Diana Msewa (Mbeya), na Vailet Nicolaus (Evergreen) bado hawajaripoti kambini wanaombwa kuripoti  na kuungana na wenzao katika maandalizi ya mchezo huo dhidi ya Zambia.

MKWASA AITA 26 TAIFA STARS


Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine leo amemtambuisha kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Charles Boniface Mkwasa mbele ya waandishi wa habari.

Akiongea na waandishi wa habari, Mwesigwa amewaomba wadau wa mpira wa miguu nchini kuwapa sapoti makocha hao wazawa wanaoanza kazi kesho kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda julai 4, 2015 jijini Kampala.

Mara baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari, Mkwasa amesema anashukuru kwa TFF kumpatia nafasi hiyo ya kuingoza Taifa Stars na msaidizi wake Hemed Morocco, na kuomba watanzania kuwapa sapoti.

Mkwasa amesema cha kwanza atakachokifanya na msaidizi wake Morocco ni kurudisha imani ya watanzania juu ya timu yao ya Taifa, kisha watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri katika michezo inayowakabili.

Aidha Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kesho alhamisi katika hoteli ya Tansoma tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.

Wachezaji walioitwa ni makipa: Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ally (Azam), Ally Mustafa “Barthez” (Yanga).

Walinzi: Shomari Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohamed Hussein “Tshabalala” (Simba), Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub “Cannavaro” (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey Morris (Azam).
Viungo: Jonas Mkude (Simba), Abdi Banda (Simba), Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam).

Viungo wa pembeni: Saimon Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba), Deus Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano “Messi” (Simba).

Washambuliaji: John Bocco (Azam), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ally (Mtibwa Sugar).

Wachezaji Juma Abdul (Yanga), Mudathir Yahya (Azam) na Samwel Kamuntu (JKT Ruvu) wameitwa kama wachezaji wa akiba katika kikosi cha timu ya Taifa kinachoingia kambini kesho.

Katika hatua nyingine Mkwasa ametangaza benchi la ufundi la Taifa Stars, kocha msaidizi Hemed Morocco, kocha wa magolikipa Peter Manyika, Mshauri wa timu Abdallah Kibadeni, mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku mratibu wa timu akiwa ni Alhaj Ahemd Mgoyi.

Kamati ya tiba ya TFF itapendekeza majina ya daktari wa timu na mchua misuli watakaoungana na kambi ya Taifa Stars.

MAYANJA KOCHA MPYA COASTAL UNION


MABINGWA wa Ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 1988,Coastal Union,Wagosi wa Kaya imeingia mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja ambaye ni raia wa Uganda kuifundisha timu ya Coastal Union katika msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania Bara itakayoanza Mwezi Agosti mwaka huu .

Utiliaji wa saini wa Kocha huyo ulifanyika (leo)jana mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa timu ya Coastal Union akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Albert Peter na Katibu Mkuu wa timu hiyo,Kassim El Siagi.

Akizungumza baada ya kumalizika zoezi hilo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa kutokana na umahiri aliokuwa nao kocha huyo wanaimani kubwa ataipa mafanikio timu hiyo hasa katika harakati za kuhakikisha inafanya vizuri ligi kuu msimu ujao.

Amesema kuwa uwezo wa Kocha huyo utaleta matumaini makubwa ya mafanikio hasa ukizingatia ni kocha mwenye uwezo mzuri wa kufundisha na kuzipa mafanikio timu hivyo tunaamini kuja wake kwetu itakuwa chachu katika maendeleo.

Mayanja ambaye aliwahi kuzifundisha timu za soka Kiyuvu FC ya Rwanda,Timu ya Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA),Vipers  FC ya Bunamwaya  na KCC ya Uganda amesema kutua kwenye timu hiyo kumpa faraja kubwa hivyo atahakikisha anatoa mchango wake kwenye kuipa mafanikio.

Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha timu hiyo inang’ara katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao ikiwemo kubadili aina ya mchezo wa timu hiyo ili iweze kupata mafanikio kwa kuweka umoja baina ya wachezaji mashabiki, wanachama na wapenzi.

Amesistiza pia umuhimu wa mshikamano baina ya wapenzi,wanachama na viongozi ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao kwani dhamira yake ni kutaka kuona timu hiyo inang’ara kwenye medani za kitaifa na kimataifa.

NOOIJ AWAAGA WATANZANIA, MKWASA KUINOA STARS


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania - TFF, Jamal Malinzi leo ameagana rasmi na aliyekua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, mholanzi Mart Nooij.

Akiongea na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Tansoma, Malinzi amesema wameamua kuagana nae mbele ya vyombo ya habari kama iliyofanyika pia wakati wa utambulisho wake wakati wa kuanza kazi.

“Mpira wa miguu unachangamoto nyingi, watanzania tunasafari ndefu katika mafanikio ndio maana  TFF imeanza kuwekeza katika soka la vijana, sababu ndio msingi wa kuwa na timu bora ya Taifa” alisema Malinzi.

Duniani kote chimbuko la timu bora ni soka la vijana na watoto, tukiwa na vijana wengi walioanza kucheza mpira katika umri mdogo wanapofikia umri wa kuchezea timu ya Taifa tutakua na kikosi bora.

Nchi za wenzetu inapofikia kocha kuita wachezaji wa timu ya Taifa anakuwa na wigo mpana, kwetu sisi wachezaji wanocheza soka nje ya nchi wanahesabika, hivyo ni lazima tuanze kuwekeza kwenye soka la vijana

TFF ilishaanza mkakati huo ndio maana kuna timu za U13, U15 ambazo zitakua zikiingia kambini na kucheza michezo ya kirafiki ndani ya nje kwa lengo la kupata uzoefu kabla ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana mwaka 2016.

Kikosi cha U15 kinatarajiwa kufanya ziara mwezi Disemba mwaka huu katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini, kisha mwakani mwezi April 2016 kitaenda Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya kucheza michezo ya kirafiki.

Naye Mart Nooij aliyekua kocha wa Taifa Stars, akiongea na waaandishi wa habari alisema anawashukuru watanzania wote, serikali, wadau wa mpira wa miguu nchini na TFF kwa sapoti waliyompatia wakati akiwa kocha mkuu wa timu ya Taifa.

Nooij alisema alifurahia maisha yake akiwa Tanzania kwa kipindi chote alichokua akifundisha timu ya Taifa, lakini kwa sababu imefikia mwisho wa ajira yake hana jinsi anaondoka, lakini ataendelea kuikumbuka Tanzania na watanzania wote kila siku kwa ukarimu wao.

Wakati huo huo Rais wa TFF. Jamal Malinzi amemtangaza Charles Mkwasa kuwa kocha mpya wa Taifa Stars akisaidiwa na kocha Hemed Morocco, Mkwasa  ambaye ni kocha wa Yanga na Morocco kocha wa Mafunzo watafanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya kuwania kufuzu kwa CHAN na AFCON.

Malinzi amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa timu ya Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana kutoka mashiriksho mengine duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo makocha  hao wazawa wamekizi.

Kocha Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi  (zikiwemo posho) alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao wazawa” aliongeza Malinzi”

Aidha Kamati ya utendaji ya TFF Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa timu ya Taifa, lengo la uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya kamati ya Utendaji na timu ya Taifa.

U15 YAINGIA KAMBINI
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ya Tanzania, imeingia kambini jana na kuanza mazoezi leo katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini U15 ya mkoa wa Mbeya siku ya jumapili.

Kikosi hicho kilicho chini ya makocha Bakari Shime na Peter Manyika kitacheza mchezo huo kwa lengo la waalimu kupatawa fursa ya kuwaona vijana hao na kuwaongeza wengine watakaoneka katika kikosi hicho.

U15 ni mpango wa TFF kuandaa kikosi kizuri chenye ubora kuelekea kuwania kufuzu ka fainali za vijana Afrika mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Madagascar, ambapo vijana hao watakua na umri wa miaka 16 kufikia mwakani wakati michezo ya kuwania kufuzu itakaponza mwezi Julai, 2016.

NB: Kesho siku ya jumatano kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Mkwasa na msaidizi wake Hemed Moroco wataongea na waandishi wa habari saa 5:30 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume.

Sunday, June 21, 2015

NOOIJ ATIMULIWA TAIFA STARS



KAMATI YA UTENDAJI YASITISHA AJIRA YA NOOIJ

Kamati ya utendaji ya Shirikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Katika kikao chake cha leo pamoja na mambo mengine ilipitia mwenendo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmin ya mwenendo wa timu.

Kamati ya utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo:

1.Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia  tarehe 21/June/2015.

2.Benchi lote la ufundi la Taifa stars limevunjwa kuanzia tarehe 21/06/2015.

3.Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.

Wakati huo huo, timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars jana ilipigwa mweleka wa mabao 3-0 na Uganda katika mechi ya michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani AFCON.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, Taifa Stars ilicheza chini ya kiwango, hali iliyowafedhehesha mashabiki wachache waliofika uwanjani kushuhudia mechi hiyo na kuamua kuwazomea wachezaji.

Kamati ya Utendaji ya TFF ililazimika kufanya kikao cha dharula baada ya Stars kufungwa mabao 3-0 na Uganda na kufikia uamuzi wa kumtimua Nooij.

Hata hivyo, baada ya mchezo huo, Nooij alisema hawezi kuondoka kwa matokeo ya uwanjani, kwa sababu ana mkataba hadi mwaka 2016.

TFF italazimika kumlipa Nooij dola za Kimarekani zisizopungua 125, 000 (sh. milioni 250,000) kwa kumvunjia mkataba, ambao ni mishahara yake ya miezi 10, kwa sababu kwa mwezi alikuwa analipwa dola 12,500 (sh. milioni 25).

Mabao mawili ya mshambuliaji Erisa Sekisambu na lingine la Farouk Miya yanahitimisha historia ya kocha huyo Mholanzi Tanzania.

Kipigo hicho kiliwakosesha wachezaji wa Taifa Stars donge nono la sh. milioni 1 kila mmoja ahadi iliyotolewa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi juzi.

Mchezo huo ni tano mfululizo Taifa Stars kufungwa chini ya Nooij, aliyerithi mikoba ya Mdenmark Kim Poulsen, Aprili, mwaka jana na kwa ujumla timu hiyo imecheza mechi tisa bila ya ushindi chini ya Mholanzi huyo.

TFF YARUHUSU TIMU KUSAJILI NYOTA SABA WA KIGENI, WATALIPIA DOLA 2,000 KILA MSIMU


MAAMUZI YA KAMATI YA UTENDAJI

Kamati ya Utendaji ya TFF imefanya kikao chake cha kawaida leo tarehe 20/06/2015 katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo kisiwani Zanzibar,

Baadhi ya maamuzi yake ni haya yafuatayo:

TUNZO ZA VODACOM.
Baada ya kuzingatia  mapungufu yaliyojitokeza katika uteuzi wa tuzo za ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2014/15, Kamati ya utendaji imeagiza Rais wa TFF aunde kamati maalum ya kusimamia mchakato wa utoaji wa tuzo za Vodacom. Kamati hii itazingatia umuhimu wa kuhusisha idara za ufundi za TFF katika zoezi hilo na wadhamini na ligi watahusishwa kwa ukaribu katika zoezi hili.

KANUNI ZA LIGI 2015/16.
Kamati ya utendaji ilipitia rasimu ya kanuni za ligi kuu, FDL na SDL za msimu ujao wa 2015/16.

Mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni kwenye maeneo yafuatayo:

LESENI ZA VILABU.
Kamati ya utendaji imesisitiza kuwa hakuna klabu itakayopitishiwa usajili wake kama kupewa leseni ya klabu ya msimu.( Club Licencing).

WAAMUZI.
Kamati ya utendaji imeridhia wazo la kamati ya maamuzi kuwa kuanzia msimu 2015/16 kutakuwa na jopo maalum ya waamuzi ( Elite referees) litakalochezeshwa mechi zote za ligi kuu.

Waamuzi hawa watakuwa ni 16 wa kati, 32 wa pembeni na 4 wa akiba. Hii itasaidia kuongoza ufanisi katika uamuzi. (refereeing).

MGAWANYO WA MAPATO YA MILANGONI.
Vilabu vimeongezwa mgawanyo wa mapato  ya milangoni na sasa vitakuwa vinachukua asilimia 60% ya mapato ya mlangoni, makato mengine ni 18% VAT na 15% gharama za uwanja.

UDHIBITI WA WACHEZAJI.
Kanuni ilikuwa inatoa fursa timu ya kuamua mechi ipi mchezaji asicheze baada ya kuwa na kadi tatu za njano imefutwa.

KUSAJILI MIKATABA YA WACHEZAJI.
Kuanzia sasa mikataba kati ya wachezaji na klabu itakayotambuliwa na TFF itakuwa ni ile ambayo ni nakala halisi zilizopigwa muhuri na lakiri ya TFF  na kusajiliwa kwenye kumbukumbu ya TFF. Vilabu na mwachezaji watapewa nakala hizi baada ya  kusajiliwa na TFF.

WACHEZAJI WA KIGENI.
Kamati ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu 2015/16 idadi ya wachezaji wa kigeni watakaosajiliwa na klabu ya ligi kuu itakuwa 7 (saba) wachezaji wote hawa, wote wataruhusiwa kucheza kwa wakati wote.

Mikakati ya kusajiliwa wachezaji hawa ni haya yafuatayo:

Mchezaji awe ni mchezaji wa timu za Taifa za nchi yake ( Senior, U23, U20, U19, U17 nk) au
Mchezaji awe anacheza katika ligi kuu ya nchi yake au nchi nyingine wakati anasajiliwa.

Kila mchezaji wa kigeni atakayesajiliwa atalipia ada ya maendeleo. Mpira wa vijana ya dola 2,000 kwa kila msimu atakaocheza hapa nchini. Fedha hizi zitapelekwa katika mfuko wa maendeleo ya mpira (Football Development Fund).

Pia imeamriwa kuwa mikataba ya vilabu na wachezaji iliyo hai itaendelea kutambuliwa na TFF. Na kwa wale ambao tayari wapo nchini wataruhusiwa  kuuhisha (to renew) mikataba yao iwapo watakubaliana na vilabu vyao.

4. LESENI ZA MAKOCHA
Kamati ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu huu, Kocha wa timu ya ligi kuu sharti awe na leseni B ya CAF au itakayolingana nayo kutoka katika mashirikisho mengine duniani na kocha msaidizi awe na leseni C ya CAF, hii ni kwa misimu mitatu.

Kuanzia msimu wa 2018/2019 kocha wa Ligi Kuu atatakiwa kuwa na leseni A ya CAF au inayolingana na hiyo kutoka katika mashirikisho mengine duniani.

Aidha Kamati ya Utendajji ya TFF imemteua Meshack Bandawe kuwa mjumbe wa bodi ya mfuko wa  maendeleo ya mpira wa miguu - TFF (FDF), Bandawe ni meneja wa PPF kanda ya ziwa.

Friday, June 19, 2015

STARS KUWAKABILI UGANDA KESHO ZANZIBAR



Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kesho inatarajiwa kushuka dimbani kucheza na timu ya Taifa ya Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainaili za wachezaji wa ndani CHAN 2016.

Kikosi cha Taifa Stars kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa kuanzia majira a saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Stars inahitaji ushindi katika mchezo huo wa awali ili kujiweka katika mzingira mazuri ya kusonga mbele, kabla ya mchezo wa marudaino utakaofanyika baada ya wiki mbili jijini Kampala.

Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema vijana wake wako katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo wa kesho, na kuwaomba watanzania kuwapa sapoti katika mchezo huo.

Endapo Stars itaitoa Uganda katika hatua ya awali, itafuzu katika hatua ya pili ambapo itacheza dhidi ya timu ya Taifa ya Sudan, na mshindi wa mchezo huo moja kwa moja atafuzu kwa fainali za CHAN 2016 nchini Rwanda.

Wakati huo huo, timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili leo mchana jijini Dar es salaam kisha kuelekea kisiwani Zanzibar tayari kwa mchezo huo wa kesho dhidi ya Taifa Stars.

TWFA KUFANYA UCHAGUZI AGOSTI 15

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA), George Mushumba ametangaza uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika agosti 15, 2015 kujaza nafasi mbalimbali.

Kwa mamlaka aliyonayo anapenda kutangaza uchaguzi mkuu wa TWFA leo kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi, uchaguzi huo utafanyika tarehe 15, Agosti 2015 katika nafasi zifuatazo:

Mwenyekiti
Katibu Msaidizi
Mweka Hazina
Wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji.       

Fomu za kuomba nafasi hizo zitaanza kutolewa tarehe 19-23 Juni 2015 katika ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.


Kalenda ya Uchaguzi wa TWFA imeambatanishwa:
JEDWALI NAMBA MOJA (1)
KALENDA YA MATUKIO YA UCHAGUZI YA TWFA
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

DAR ES SALAAM YAWA MABINGWA MICHUANO YA UMISETA TAIFA

.
Michuano ya UMISETA ngazi ya taifa imemalizika leo asubuhi huko jijini Mwanza kwa mchezo wa fainali kati ya Dar es salaam dhidi ya Nyanda za juu Kusini wavulana, huku fainali nyingine kwa upande wa wasichana ikipigwa jana kati ya Dar es salaam dhidi ya Kanda ya Mashariki.
Katika fainali ya jana wasichana, Dar es salaam wametawazwa kuwa mabingwa  baada ya kuwatandika bila huruma Kanda ya Mashariki kwa mabao 7-1,kwenye mchezo uliokuwa na msisimko mkubwa kwa Dar es salaam kuonesha uwezo mkubwa wa kusakata kandanda.
Dar es salaama ilifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuisukumiza nje Kanda ya Ziwa mabao 4-1,huku Kanda ya Mashariki ikifanikiwa kutinga katika hatua ya fainali baada ya kuifunga Kanda ya Kaskazini kwa mabao 3-1.
Kwa upande wa fainali ya wavulana leo asubuhi,Nyanda za Juu Kusini wametawazwa mabingwa baada ya kuifunga Dar es salaam bao 1-0,bao ambalo ni la kujifungwa baada ya mabeki wa Dar kujichanganya katika harakati za kuokoa hatari langoni mwao.
Nyanda za Juu Kusini walifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuifunga Kanda ya Ziwa kwa mabao 3-0,huku Dar es salaam wakitinga hatua hiyo baada ya kuifunga Zanzibar ambao ndio walikuwa mabingwa wa tetezi kwa mabao 4-3.
Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA chini ya mwenyekiti wake Almas Kasongo,kimeelezwa kufurahishwa kwake na mafanikio yaliyooneshwa na vikosi hivyo vilivyo katika himaya yake (Dar es salaam),na kuviomba vilabu vya ligi mbalimbali kujitokeza kuangalia mashindano ya vijana ili kupata wachezaji wa baadaye kwenye vilabu vyao.

 LIGI YA WANAWAKE DAR YASUBIRI RATIBA YA TWIGA STARZ.
Ligi ya wanawake mkoa wa Dar es salaam iliyomaliza mzunguko wake wa kwanza,ipo katika maandalizi ya kuanza mzunguko wa pili na wa mwisho kumpata bingwa wa ligi hiyo.
Kamati ya mashindano ya DRFA,imesema kinachosubiriwa kwa sasa ni ratiba ya benchi la ufundi la timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars,ambao wapo kambini kujiandaa na michuano ya afrika (All African Games) huko Congo Brazavile,mwezi Septemba mwaka huu.
Mpaka sasa kikosi cha Mburahati Queens ndicho kinachoshikilia usukuni wa ligi kwa kuwa na pointi 18,nafasi ya pili inashikiliwa na Evergreen Queens wenye pointi 12,sawa na JKT Queens wenye pointi 12 katika nafasi ya tatu wakitofautiana magoli.
Mwisho.

TAIFA STARS YATUA ZANZIBAR


Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, imewasili leo asubuhi Visiwani Zanzibar tayari kwa maandalizi ya mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya timu ya Uganda kuwania kufuzu kwa CHAN 2016.

Msafara wa Taifa Stars unajumuisha wachezaji 21 na benchi la ufundi 7 ambao wamefikia katika hoteli ya Nungwi Inn, mchezo dhid ya Uganda utachezwa katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar jumamosi kuanzia majira ya saa 2 usiku.

Stars inakutana na Uganda katika mchezo huo wa awali wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Rwanda, kabla ya kurudiana wiki mbili baadae katika uwanja wa Namboole jijini Kampala.

Mara baada ya kurejea kutoka nchini Misri kikosi cha Stars kiliendelea na kambi katika hoteli ya Tansoma na kufanya mazoezi katika uwanja wa Karume kabla ya kuondoka leo asubuhi kuelekea visiwani Zanzibar.

Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij amewaongeza wachezaji watano ambao hawakua katika kikosi kilichocheza dhidi ya Misri, kufuatia wachezaji wa kimataifa wa Tanzania kutoruhusiwa kucheza mchezo huo wa CHAN wikiendi hii.

Wachezaji waliongezwa ni Atupele Green, Hassan Isihaka, Hassan Dilunga, Rashid Mandawa na Kelvin Friday, wanaungana na wachezaji Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Salum Mbonde, Aggrey Morris na Nadir Haroub.

Wengine ni Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Mwinyi Haji, Abdi Banda, Frank Domayo, Amri Kiemba, Said Ndemla, Saimon Msuva, na John Bocco.

Aidha Shirikisho la Mpirani wa Miguu barani Afrika (CAF) limetoa mwongozo kuwa mchezaji Mrisho Halfan Ngasa haruhusiwi kucheza CHAN kwa sababu sio mchezaji tena wa ndani, hivyo Ngasa ameondolewa kikosini

Waaamuzi wa mchezo huo wanatarajiwa kuwasili kesho kutoka nchini ambao ni Hudu Munyemana (Rwanda), akisaidiwa na Hakizimana Ambroise (Rwanda), Justin Karangwa (Rwanda), mwamuzi wa akiba ni Issa Kagabo (Rwanda), na kamishina wa mchezo Nicholaus Musonye kutoka Kenya.

U15 KUINGIA KAMBINI JUMATATU

Kikosi cha timu ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 15 (U-15) kitaingia kambini siku ya jumatatu tarehe 22/06/2015 ili kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini ya mkoa wa Mbeya, mchezo utakaofanyika mjini Mbeya jumatatu ya tarehe 28/06/2015.

Kikosi hiki kinaandaliwa kwa ajili ya kujiandaa na na michuano ya mtoano kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyia nchini Madagascar mwaka 2017. Hatua ya mtoano wa awali itaanza mwakani 2016 mwezi Juni.

Timu itakua chini ya kocha Bakari Shime kwa muda akisaidiwa na Peter Manyika. Kocha aliyekua ameteuliwa awali kufundisha timu hiyo Adolf Rishard ameomba udhuru baada ya kupata fursa ya kwenda masomoni.

Wachezaji watakaoingia kambini na mikoa wanayotokea kwenye mabano ni Mwijuma Yahya (Tanga), David Mpakazi, Shilole Anthony (Geita),  Kibwana Shomari , Ibrahim Koba, (Morogoro), Faraji John, Kelvin Deogratius, Davison Meddy , Maulid Lembe (Dodoma), Ally Msengi (Mwanza).

Wengine ni Timoth Timothy, Juma Juma, Pius Raphael, Mohamed Ally (Dodoma), Athumani Rajabu, Juma Zubeir, Jonathan Rafael (Kigoma), Robert Philip, Jaffari Juma (Arusha), Michael Kanuti, Alex Peter, Rashid Kilongola (Kinondoni), Morris Michael (Ilala), Karim Mfaume (Lindi), Assad Juma (Unguja Magharibi), Francis Mrope, Kelvin Pius (Mara)

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MNIGERIA WA STAND UNITED ATUA COASTAL UNION


MSHAMBULIAJI wa timu ya Stand United ya Shinyanga, Abasalim Chidiebele amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu ya Coastal Union ya Tanga  msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Chidiebele alitua mkoani Tanga jana kwa ajili ya kuingia makubaliana na uongozi wa timu ya Coastal Union ambapo utiliaji saini huo ulishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa Coastal Union, Kassim El Siagi, Meneja wa Coastal Union, Akida Machai na viongozi wengine.
Akizungumza mara baada ya kusaini, Chidiebele amesema kuwa amefurahi kusajiliwa na Coastal Union na kuhaidi kutumia uwezo wake aliokuwa nao kwa ajili ya kuipa mafanikio timu hiyo msimu ujao

“Nashukuru kusajiliwa Coastal Union kikubwa niwahaidi tu wapenzi, wanachama na mashabiki kutumia uwezo wangu katika kuipa mafanikio timu yetu, “amesema Mshambuliaji huyo ambaye ni tishio hapa nchini.
Kwa upande wake, Ofisa Habari wa Klabu ya Coastal Union, Oscar Assenga alisema kuwa msimu huu timu hiyo imedhamiria kufanya usajili wa nguvu utakaowawezesha kuhakikisha wanachukua ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
“Unajua usajili wetu sio wa kukurupuka hivyo lazima tuwe makini kwani hiyo ndio itakuwa njia pekee ya kuhakikisha tunatimiza mipango yetu ya kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao “Alisema.
Hata hivyo aliwataka wapenzi mashabiki kuweka mshikamano wa pamoja ambao utatuwezesha kufanikisha malengo yao ya mwakani kushiriki kombe la shirikisho kwa kuanza kufanya vizuri katika michuano ya Ligi Kuu.

Monday, June 15, 2015

USAJILI WA WACHEZAJI KUANZA RASMI LEO

Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2015/2016) unaanza Juni 15 hadi Agosti 6 mwaka huu wakati kipindi cha kutangaza wachezaji walioachwa au kusitishiwa mikataba ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu.

Kipindi cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi Julai 30 mwaka huu. Kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya Agosti 7 na 14 mwaka huu. Kuthibitisha usajili hatua ya awali ni Agosti 15 hadi 19 mwaka huu.

Usajili hatua ya pili utakuwa kati ya Agosti 17 na Septemba 8 mwaka huu. Kupitia na kutangaza majina ya pingamizi hatua ya pili ya usajili ni kuanzia Septemba 8 hadi 14 mwaka huu. Uthibitisho wa usajili hatua ya pili ni Septemba 15 na 17 mwaka huu.

Wachezaji wanaotoka nje ya Tanzania, usajili wa mtandao wa FIFA wa TMS utakuwa wazi kuanzia kesho (Juni 15) hadi Septemba 6 mwaka huu. Klabu zinazosajili wachezaji kutoka nje zinatakiwa kufanya hivyo kupitia akaunti zao za mtandao wa TMS.

Kwa klabu ambazo hazina akaunti ya TMS zinatakiwa kuwasiliana na TFF ili mameneja wao wa usajili wapatiwe mafunzo ya TMS, na baadaye kuombewa akaunti hizo FIFA.

Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza Agosti 22 mwaka huu, na ratiba inatarajiwa kutoka mwezi mmoja kabla (Julai 22 mwaka huu).

Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inatarajiwa kuanza Septemba 12 mwaka huu, wakati Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajia kuanza Oktoba 17 mwaka huu.

TAIFA STARS YAFUNGWA 3-0 NA MISRI

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, leo imepoteza mchezo wake wa kwanza kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017 baada ya kufungwa kwa mabao 3 - 0 na wenyeji Misri.

Taifa Stars ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na hasa sehemu ya ulinzi ilifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya washambuliaji wa timu ya Misri, na kupelekea kwenda mapumziko -0 - 0.

Kipindi cha pili Misri walifanya mabadiliko yaliyowapelekea kupata mabao hayo 3 ndani ya dakika 10, kupitia kwa Ramy Rabia(60), Basem Morsy(64) na Mohamed Salah (69).

Stars ilifanya mabadiliko ya kuwaingiza Frank Domayo, Saimon Msuva na Salim Mbonde na kufanya shambulizi kadhaa langoni kwa Misri lakini mashambulzi hayo yaliokolewa na walinzi wa timu ya Misri.

Mara baada ya mchezo huo, Taifa Stars inaondoka leo Alexandria kuelekea Cairo ambapo itaondoka na shirika la ndege la Ethiopia saa 8 usiku na kufika jijini Dar es salaam jumanne saa 7 mchana.

Tanzania: Deogratias Munish, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Aggrey Morris/Salim Mbonde, Nadir Haroub, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/Saimon Msuva, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, Amri Kiemba/Frank Domayo.

Misri: Ahmed El Shenawy, Ahmed Hegazy, Ramy Rabea, Mohamed Abd Elshafy, Hazem Emam, Mohamed Elneny, Ibrahim Salah, Mahmoud Abd Elmonem/Ramadan Soffiy, Mohamed Salah/Mostafa Ftahy, Doly Elgabay/Basem Morsy, Ahmed Hassan Meky.

DRFA YASIKITISHWA NA MATOKEO MABAYA YA TAIFA STARS.

Chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimesikitishwa na
matokeo mabaya iliyoyapata timu ya taifa (Taifa Stars) kwa kufungwa mabao
3-0 dhidi ya Mafarao wa Misri,katika mchezo wake wa kwanza uliopigwa jana usiku ugenini wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya kuwania kombe la mataifa ya afrika (AFCON).

Mwenyekiti wachama hicho,Almas Kasongo, amesema matokeo hayo
yamewafadhaisha mno watanzania wenye uchu wa kuona timu hiyo inapata matokeo mazuri yaliyokosekana kwa kipindi kirefu.

Amesema anaamini kuwa kikosi hicho kina wachezaji wazuri na wenye uwezo
lakini wamekuwa wakikosa mbinu za kufanya vizuri kwenye timu ya taifa hasa kwenye safu ya ushambuliaji,ikilinganishwa na uwezo wanaouonesha kwenye michuano ya ligi wakiwa na klabuzao.

Hata hivyo Kasongo amesema licha ya Stars kuanza vibaya katika harakati zake za
kuwania tiketi yamichuano hiyo ya afrika,bado nafasi ipo ya kujipanga upya
kwa kuanza kuangalia uwezo wa benchi la ufundi.

Aidha amesema DRFA inaamini kuwa Tff  inauwezo wa kutafuta mwarobaini wa
kutibu tatizo la matokeo mabaya kwa Starz,bila kumuonea mtu aibu.

Thursday, June 11, 2015

VODACOM KUTOA ZAWADI ZA VPL LEO



Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kushirikiana na wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, leo Alhamisi, Juni 11,  wanatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa Vodacom Premier League msimu wa 2014/2015.

Hafla ya utoaji wa zawadi hizo itafanyika katika ukumbi wa JB Belmonte (Kilimanjaro) uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower (PSPF), mtaa wa Ohio eneo la Posta Mpya jijini Dar es salaam kuanzia saa 12 jioni.

Mgeni rasmi katika halfa hiyo ya utoaji zawadi kwa wachezaji, makocha, na timu washindi atakua ni Juma Nkamia, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Vodacom watatoa zawadi kwa Bingwa wa Ligi Kuu msimu 2014/2015, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na mshindi wa nne, baadhi ya vipengele vitakavyotolewa zawadi pia na wadhamini hao wa Ligi Kuu ni :

1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mohamed Hussein (Simba SC)
Mrisho Ngasa (Young Africans)
Saimon Msuva (Young Africans)

2. Mlinda mlango bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons)
Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
Shaban Hassan (Coastal union)

3. Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Goran Kopunovic (Simba SC)
Hans Van Der Pluijm (Young Africans)
Mbwana Makata - (Tanzania Prisons)

4. Mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Israel Mjuni Nkongo
Jonesia Rukyaa
Samwel Mpenzu

5. Timu yenye nidhamu Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
Mgambo JKT
Mtibwa Sugar
Simba SC

MAHUNDI MCHEZAJI BORA MWEZI MEI
Wakati huo huo mchezaji John Mahundi wa timu ya Coastal Union amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Mei, 2015 na jopo la makocha kufuatia kuwazidi wachezaji wengine 14 aliokuwa anananiwa nao nafasi hiyo.

Kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi mei, Mahundi atazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom. 


STARS KUWAFUATA MISRI KESHO


Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premier Lager, kesho siku ya ijumaa jioni inatarajiwa kuondoka Addis Ababa Ethiopia kuelekea nchini Misri tayari kwa mchezo wa siku ya jumapili.

Stars ambayo imeweka kambi ya mazoezi takribani kwa wiki moja sasa jijini Addis Ababa leo imeendelea na raiba yake ya mazoezi katika uwanja wa Taifa, amabpo leo imefanya mazoezi yake asububuhi tu.

Kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema, anashukuru maendeleo ya kambi ni mazuri timu yake inafanya mazoezi katika viwanja viwili vizuri vilivyopo Addis Ababa, uwanja wa Taifa na  uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia.

Nooij amesema amekuwa akiwafundisha wachezaji wake kucheza mpira wa kasi na pasi za haraka haraka, jambo ambalo wachezaji wameonyesha kufuata vizuri maelekezo yake na kusema wanamuelewa vizuri.

Akiongelea mchezo dhidi ya Misri siku ya jumapili, Nooij amesema timu inakwenda kupambana kusaka matokeo mazuri katika mchezo, nafahamu tunaenda cheza ugenini, nimewaelekeza vijana wangu wanaocheza nafasi ya ushambuliaji kutumia vizuri nafasi tutakazozipata katika mchezo huo.

Aidha, Kocha Nooij amesema katika mpira hakuna kinachoshindikana, kambi ya wiki moja Addis Ababa imewasaidia wachezaji kukaa pamoja na kushika maelekezo yake vizuri, hivyo anaamini timu yake itafanya vizuri katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON.

Katika kikosi cha wachezaji wa 22 waliopo kambini jijini Addis Ababa hakuna mchezaji majeruhi, wachezaji wote wako vizuri kiafya, kifikra na morali ni ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo dhidi ya Mapharao.

Taifa Stars inatarajia kuondoka kesho jioni ijumaa kuelekea nchini Misri kwa shirika la ndege la Ethiopia majira ya saa 5 usiku na kufika Cairo majira ya saa 8 usiku, kisha kuunganisha safari ya kuelekea jijini Alexandria ambapo timu mchezo huo utakapofanyika.

Mchezo kati ya Misri dhidi ya Tanzania utachezwa katika uwanja wa Borg El Arab kuanzia majira ya saa 1 jioni kwa saaa za huku, sawa na saa 2 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Waamuzi wa mchezo huo wanatokea nchini Ethiopia ambapo ni Bamlak Tessema Weyesa (mwamuzi wa kati), Kinfe Yilma (mwamuzi msaidizi wa kwanza), na Wolday Hailerague (mwamuzi msaidizi wa pili).

Wakati huo huo, kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro kimeendelea kujifua katika uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia eneo la CMC asubuhi na jioni katika uwanja wa Taifa wa Addis Ababa.

Stars ambayo imeweka kambi jijini Addis Ababa imekua ikijifua mara mbili kwa siku, kuhakikisha wachezaji wanakua vizuri kuelekea katika mchezo dhidi ya timu ya Taifa  Misri mwishoni mwa wiki hii jijini Alexandria.

Hali ya kambi kiujumla ni nzuri, wachezaji wote ni wazima, wakiwa wenye ari, na morali ya hali ya juu katika maandalizi ya mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017.

Kocha mkuu wa Taifa Stars mholanzi, Mart Nooij amekuwa akiwafundisha vijana wake mbinu mbali mbali kuelekea kwenye mechi dhidi ya Misri,  kuanzia sehemu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji kuhakikisha wanakua fit katika mchezo unaowakabili.

Ikiwa ni siku ya nne tangu Taifa Stars kuanza mazoezi yake jijini Addis Ababa, kocha Nooij amesema anashukuru vijana wake wanamuelewa vizuri anachowaelekeza, sasa timu inacheza mpira wa kasi na pasi za haraka haraka, vijana wamechangamka na morali ni ya hali ya juu kambini kuelekea kwenye mchezo unaowakabili.

Hali ya nidhamu kambini ni ya hali ya juu, wachezaji waanatambua umuhimu wa mchezo huo, na kikubwa wameahidi kupambana kusaka matokeo mazuri katika mchezo dhidi ya Misri.

“Katika mpira hakuna kinachoshindikana, sie tumejiandaa vizuri, naamini tutakapofika Misri tutafanya vizuri na kuwapa furaha watanzania, kikubwa watuombee kwa mwenyezi mungu, tuwe wazima mpaka siku ya mchezo, naamini tutafanya vizuri” alisema Nadri.

Stars inatarajiwa kuelekea jijini Cairo siku ya ijumaa, kisha kuunganisha katika jiji la Alexandria tayari kwa mchezo dhidi ya Misri utakaochezwa katika uwanja wa Boeg El Arab siku ya jumapili Juni 14, 2015.

MULONGO AZINDUA MASHINDANO YA U13 TAIFA



Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh Magessa Mulongo leo hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba amefungua mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13.

Akifungua mashindano haya Mh Mulongo amewataka vijana hao kujituma katika michezo na masomo kwa kuwa vyote vinakwenda sambamba.

Amelisisitizia Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kuongeza juhudi katika kuimarisha soka la vijana.

Katika salam zake za utangulizi Rais wa TFF Jamal Malinzi ameeleza kuwa lengo la mashindano haya ni kuibua timu ya vijana wa umri wa miaka 13 ambao watahamishiwa kwenye shule ya Alliance, watakua pamoja hapo kusoma na kufundishwa mpira.

Mpango wa TFF ni kuwa hadi kufikia mwaka 2019 timu hii itakuwa imara kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya fainali za Afrika umri chini ya miaka 17,fainali ambazo zitafanyika Tanzania.

Mikoa yote 25 ya Tanzania bara inashiriki mashindano haya na mkoa wa Dar es salaam umewakilishwa na timu tatu Kinondoni Ilala na Temeke.

TFF inaishukuru Symbion Power kwa ushirikiano wa kuendeleza mpira wa vijana

SIMBA YAKAIDI AGIZO LA TFF, YAMNG'ANG'ANIA MESSI


SIMBA SC imesema haitafanya kikao chochote na mchezaji wake, Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ kama ilivyoshauriwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari mchana huu kwamba, Kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu kilichofanyika jana, pamoja na mambo mengine kilijadili suala la Singano.
“Kwa kuwa mchezaji Ramadhan Yahya Singano alivunja makubaliano yaliyoamriwa katika kikao cha pamoja kati ya klabu ya Simba, mchezaji mwenyewe, SPUTANZA na Sekretarieti ya TFF, kutozungumzia yaliyojadiliwa na kupendekezwa kwenye kikao, kwa kuyazungumza kwenye vyombo vya habari kwa kusema yeye ni mchezaji huru, klabu ya Simba imeamua kutokufanya mazungumzo na mchezaji huyo kwa sasa, kwa kuwa bado ina mkataba naye ambao utaisha Julai 1 mwaka 2016,”imesema taarifa ya Aveva
Hata hivyo, Aveva amesema klabu itakuwa tayari kufanya naye mazungumzo muda muafaka utakapofika, kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mikataba.
“Ni matarajio yetu mchezaji Singano ataheshimu maamuzi hayo na mkataba ambao pia upo TFF na kwenye mtandao TMS,”amesema.
Juzi, TFF iliitaka Simba SC kuketi na Singano ‘Messi’ kujadili namna ya kuingia Mkataba mpya, baada ya pande zote kuafiki Mkataba wa sasa una hitilafu.
Katika kikao hicho kilichofanyika, makao makuu ya TFF, Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam, Simba SC iliwakilishwa na Mjumbe wa Kamati yake ya Utendaji, Collins Frisch wakati Messi aliandamana na Mussa Kisoky wa Chama cha Wanasoka Tanzania  (SPUTANZA). 
TFF ilisema kaatika kikao hicho pande zote zilitambua utata ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa Simba SC.
TFF ikasema, pande hizo mbili zimekubaliana kuanza mazungumzo ya makubaliano mapya kwa ajili ya Mkataba utakaoanza msimu mpya wa 2015/2016
Messi aliyeibukia timu ya vijana ya Simba SC miaka minne iliyopita, hivi karibuni ameibua shutuma dhidi ya klabu yake hiyo kwamba imeghushi Mkataba wake.
Messi anadai Mkataba wake halali ulikuwa unamalizika mwaka huu, na si huu wa sasa ambao inaelezwa utamalizika mwakani.
Lakini baada ya kikao pamoja na taarifa rasmi ya TFF, Messi alizungumza na vyombo vya Habari akisema yeye ni mchezaji huru ana hiari ya kuzungumza na Simba au klabu yoyote kwa ajili ya Mkataba mpya.
Na Kisoky wa SPUTANZA akasema wanalihamishia suala hilo kwenye Kamati ya Sheria Maadili na Hadhi za Wachezaji kutafuta haki zaidi.
IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BIN ZUBEIRY

Wednesday, June 10, 2015

TFF YAVUNJA MKATABA WA SIMBA NA MESSI


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limevunja mkataba kati ya klabu ya Simba na mshambuliaji, Ramadhani Singano (Messi).

Kutokana na kuvunjwa kwa mkataba huo, Simba imetakiwa kuanza upya mazungumzo na mchezaji huyo, kama ina lengo la kutaka kumsajili msimu ujao kwa vile mkataba wa miaka mitatu walionao Simba, hautambuliki tena TFF.

Hatua hiyo imekuja baada ya TFF kubaini kuwa, kuna mkanganyiko katika mkataba alionao Messi na ule uliokuwa ukishikiliwa na viongozi wa Simba.

Mgogoro kati ya Messi na Simba, ulianza baada ya Messi kudai mkataba wake wa miaka miwili, umemalizika msimu uliopita huku Simba ikidai kuwa mchezaji huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja, utakaomalizika mwakani.

Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa, alisema mkataba wa mchezaji huyo na Simba, umegundulika una matatizo ndio maana wamefikia uamuzi wa kuuvunja.

"Kama Simba inataka kumsajili tena Messi, inachotakiwa kufanya ni kuzungumza naye upya,"alisema.

"Tumegundua kuna matatizo makubwa, siwezi kusema nani ameghushi mkataba kwa kuwa haya tayari ni makubaliano tuliyoafikiana kwa sasa. Mkataba wa miaka mitatu walionao Simba hatuutambui hivyo tunauvunja rasmi na tunaiagiza Simba ianze upya mazungumzo na Messi,"alisisitiza.

Mwesigwa alizitaka klabu za soka nchini, kuhakikisha zinatekeleza haki za wachezaji katika mikataba wanaoingia nao ili kuepusha migogoro.

Aidha, alitoa mwito kwa wachezaji wa Tanzania kuhakikisha wanatambua haki zao katika mikataba kwa kuisoma na kuielewa kabla ya kutia saini ili kujua nini wanachotakiwa kufanyiwa na klabu zinazowasajili.

Kwa upande wake, Messi alisema hana mpango wa kuichezea Simba msimu ujao kwa vile ameshahakikishiwa na TFF kwamba hawautambui mkataba wa miaka mitatu wa klabu hiyo.

Sunday, June 7, 2015

STARS YATUA ETHIOPIA, YAJIFUA MARA MBILI



Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, leo kimeendelea na mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.

Jana kikosi cha Stars kilifanya mazoezi majira ya saa 9 mchana katika uwanja wa Taifa wa Ethiopia (Addis Ababa) ambao pia unatumiwa na timu yao ya Taifa kwa mazoezi.

Taifa Stars ambayo imeweka kambi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia inajiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017 dhidi ya timu ya taifa ya Misri.

Daktari wa Taifa Stars, Billy Haonga amesema hali ya hewa ya Addis Ababa ni nzuri kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri, kutokana na timu kufanya mazoezi katika ukanda wa juu (mwinuko kutoka usawa wa bahari) hali itakayopelekea wachezaji kuwa fit kwa ajili ya mchezo.

"Hali ya hewa ya Alexandria ni ya kawaida, hakuna baridi sana kutokana na kuzungukwa na bahari ya  Mediterania, hivyo kipindi cha wiki moja tutakachokuwa kambini hapa Addis Ababa tunatarajiwa vijana watakua vizuri kabisa kw aajili ya mchezo” Alisema Haonga”.

Wachezaji wote wa Taifa Stars waliopo kambini Addis Ababa wapo katika hali nzuri, kiafya, kifikra na morali ya juu kujiandaa na mchezo dhidi ya Mapaharao.

Wenyeji Chama cha Soka cha Ethiopia (EFF) wanaangalia uwezekano wa Taifa Stars kupata mchezo mmoja wa kirafiki wa kujipima nguvu kabla ya kuelekea nchini Misri.

Mchezo kati ya Misri na Tanzania unatarajiwa kuchezwa Juni 14, katika uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria, ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka  2017.

Wachezaji walioko kwenye kikosi cha Stars ni  Deogratias Munish, Aishi Manula, Mwadini Ali, walinzi Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Aggrey Morris, Mwinyi Haji, Salum Mbonde na Juma Abdul.

Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, Salum Telela, Frank Domayo, Jonas Mkude, Said Ndemla, washambuliaji Saimon Msuva, John Bocco, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta,Mrisho Ngasa na Juma Liuzio.

Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Vedastus Lufano na Geofrey Irick Nyange “Kaburu”.

Naye mjumbe wa kamati ya Utendaji  ya TFF Vedastus Lufano amesema timu inakwenda kuweka kambi Ethiopia kwa ajili ya kupambana katika mchezo dhidi ya Misri.

Kikosi kingine cha timu ya Taifa kitaondoka nchini siku ya jumamosi kuelekea nchini Rwanda kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Rwanda katika kumbukumbu ya mauaji ya Kimbali.

Kocha Salum Mayanga ataondoka na kikosi cha wachezaji 18 kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki, akisaidiwa na kocha Bakari Shime.

Wachezaji watakaondoka kwenda Rwanda ni Peter Manyika, Said Mohamed, Emmanuel Semwanda, Joram Mgeveke, Hassan Isihaka, Gadiel Michael, Hassan Dilunga, Rashid Mandawa, Atupele Green, Kelvin Friday, Hassan Kessy, Ibrahim Hajibu, Malimi Busungu, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Andre Vicent, Amri Kiemba na Mohamed Hussein.

WATANZANIA SABA WATEULIWA KAMATI ZA CAF


Shirikisho la mpira barani Afrika CAF limewateua watanzania saba kuwa wajumbe wa kamati zake mbali mbali kwa kwa kipindi cha miaka miwili 2015-2017.

Walioteuliwa pamoja na kamati zao katika mabano ni:
1. Leodeger Tenga- (Makami Mwenyekiti Kamati ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa Kamati ya Vyama Wanachama).
2. Jamal Malinzi - (Mjumbe kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20)
3. Mwesigwa Selestine - (Mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya Miaka 17).
4. Richard Sinamtwa -(Mjumbe Kamati ya Rufaa)
5.Dr Paul Marealle -(Mjumbe Kamati ya Tiba)
6. Lina Kessy -(Mjumbe ya Soka la Wanawake)
7. Crescentius Magori-(Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la Ndani)
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania - TFF linawapongeza wajumbe wote walioteuliwa kuingia katika kamati mbali mbali na linawatakia kila la kheri wanapoiwakilisha nchi yetu.TFF.

TFF YAZINDUA JEZI MPYA, TOVUTI

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF leo limezindua jezi mpya za timu za Taifa, zitakazokuwa zikitumika na timu za Taifa katika michuano mbali mbali itakayokua inazikabili.

Uzinduzi huo wa jezi mpya uliofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la Golden Jubilee uliambatana na uziduzi wa tovuti mpya ya shirikisho, uliongozwa na mgeni rasmi Mh. Said Mtanda, mbunge wa jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii.

Katika uzinduzi huo, kulizunduliwa jezi aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini, jezi za nyumbani na jezi zitakazokuwa zikitumika kwa ajili ya mazoezi.

Ifuatayo ni hotuba ya Rais wa TFF , Jamal Malinzi aliyoisoma wakati wa uzinduzi wa jezi mpya za timu za Taifa, uzinduzi wa tovuti mpya ya TFF na kutunuku vyeti kwa viongozi mbalimbali, makocha, wachezaji na wadhamini.

Mh Said Mtanda Mbunge wa Jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii

Mzee Said el Maamry Mwenyekiti Msataafu wa FAT

Ndugu Leodeger Tenga Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya CAF na Rais mstaafu wa TFF

Ndugu wageni waalikwa

Ndugu waandishi wa habari

Mabibi na mabwana

Salam aleikum.

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutufikisha hapa leo na kwa mafanikio mbali mbali ambayo tumekuwa tukiyapata.Ninakushukuru sana ndugu mgeni rasmi kwa kuacha shughuli zako kuja kujiunga nasi asubuhi hii katika shughuli hii.

Ndugu mgeni rasmi,tarehe 08 oktoba 1964 Tanzania ilipata uanachama rasmi wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA. TFF tuliona jambo zito kama hili hatuwezi kuliacha lipite hivi hivi.Hivyo mwaka jana tuliamua kuenzi  maadhimisho ya miaka 50 ya kujiunga na FIFA kwa kufanya mambo mambo matatu makubwa.

La kwanza ni kutoa vyeti maalum kwa watu binafsi na taasisi mbali mbali kwa kutambua mchango wao uliotukuka katika kuendeleza mpira wa miguu Tanzania.

Leo hii ndugu mgeni rasmi tutakuomba ukabidhi vyeti hivi kwa wawakilishi wa makundi kadhaa kwa niaba ya wenzao.Makundi haya ni pamoja na viongozi wa kitaifa wastaafu,mawaziri wa michezo wastaafu,viongozi waliopita wa TFF?

FAT,wakurugenzi wa idara ya michezo,wenyeviti na makatibu wa baraza la michezo la taifa,Timuya Taifa iliyocheza fainali za Afrika mwaka 1980,waamuzi,makocha,wachezaji wa timu ya Taifa na watangazaji mahiri wa michezo.Jumla tumetunuku vyeti 194.

Kiuhalisia idadi hii ni ndogo sana ukilinganisha na wingi na uzito wa michango ya wadau mbali mbali wa mpira katika miaka 50 iliyopita.

Tunaomba Watanzania wenzetu watuelewe katika hili kuwa hawa tutakaowatunuku vyeti hivi ni wawakalilisha wa wadau wote wa mpira Tanzania.

Ninaomba tusimame kwa muda mfupi tuwaombe ewadau wenzetu na viongozi wa mpira wa miguu ambao wako katika orodha hii na wametangulia mbele ya haki.

Ndugu mgeni rasmi katika kuenzi miaka 50 ya Tanzania kujiunga na FIFA leo hii pia tutatoa mchango wa fedha kwa makundi yenye mahitaji katika jamii.

Pesa hizi zinatokana na makusanyo mbali mbali ikiwemo makusanyo ya mechi ya ngao ya hisani ifanyikayo kila mwaka. Makundi haya ni pamoja na walemavu wa viuongo,walemavu wa ngozi na wasioona.

Kitendo hii ni moja ya juhudi za TFF kurudisha katika jamii kile tunachokusanya. Kila kundi litapewa shilingi milioni tano na tunaendelea kupokea maombi toka makundi mbali ya kijamii na tukiyapitisha tutaendelea kugawa fedha hizi.

Jambo la tatu tutakalolifanya leo litakuwa ni kuzindua rasmi tovuti mpya ya TFF (www.tff.or.tz). Tumeamua kufanya jamabo hili katika kuenzi miaka hamsini ya kujiunga na FIFA ili kutoa msisitizo kuwa sasa TFF na sisi tunajiunga Na kuendeleza mpira kisasa kulingana na teknolojia iliyopo.

Kupitia tovuti hii wadau wa mpira watapata fursa ya kuhabarishwana kuelimishwa nkuhusu masuala mbali mbali yahusuyo mpira wa miguu.

Tovuti hii itakuwa pia na sehemu ya kumbu kumbu (archive) zihusuzo historia ya mpira wa miguu na matukio mbali mbali katika historia ya mpira wetu.

Tunaomba wadau wenye kumbu kumbu mbali za mpira kama picha,takwimu,vipande vya magazeti ya zamani na kadhalika mtuletee ili viingizwe katika tovuti yetu.

Tunaamini tovuti hii itakuwa ndio chanzo kikuu cha taarifa na rekodi mbali mbali za sasa na za zamani  zihusuzo mpira wa miguu.

Ndugu mgeni rasmi shughuli ya leo tutaihitimisha kwa kuzindua jezi mpya ya timu ya Taifa. Jezi hizi zitakuwa ni mbili moja ya ugenini na nyingine ya nyumbani.Tunawapongeza watanzania wote walioshiriki katika kubuni jezi na mwisho tuliunganisha ubunifu tofauti na kupata jezi itakayozinduliwa leo.

Ubunifu huu tayari umetafutiwa hati miliki Brela hivyo TFF tutalinda hakii hii kwa kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wale wote watakaodiriki kuchapisha na kuuza kwa magendo jezi hizi.Utaratibu unafanyika kumpata msambaji mmoja halali atakayesambaza jezi hizi nchini kwa ajili ya wapenzi wa mpira wa miguu.Ukinunua jezi hii utakuwa umechangia maendeleo ya mpira wa miguu.

 TFF inawashukuru na kuwapongeza sana Tanzania Breweries ltd ambao ndio wazalishaji wa bia ya Kilimanjaro Lager kwa sapoti wanayoitia kwa timu ya Taifa na kutuwezesha kubuni na kuzalisha jezi hizi.Tunawashukuru sana.

Ndugu mgeni rasmi ninaomba nimalizie kwa kuzungumzia kwa kifupi program yetu ya mpira wa vijana.kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza soka la vijana TFF tumejipanga vilivyo kwa mpambano wa hatua za awali za kucheza fainali za vijana za Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2017.

Mechi za ufaulu zitafanyika kati kati ya mwaka 2016.TFF tayari tumeunda kikosi cha awali cha vijana chini ya umri wa miaka 15 kujiandaa na michuano hii.Kikosi hiki kimetokana na michuano ya copa coca cola ya mwaka jana.

Tunapenda tuchukue fursa hii kumshukuru Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha nchi yetu ya Tanzania,kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii,kupata uenyeji wa fainali za Afrika. Shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF limeipatia Tanzania uenyeji wa fainali za Afrika za vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.

Tunaomba Serikali itushike mkono katika hili ili tuweze kuandaa mashindano mazuri.Lakini haitakuwa vyema Tanzania kuandaa mashindano mazuri lakini tukatolewa hatua ya makundi.Siku ya jumapili tarehe 07/juni TFF tutazindua mashindano ya taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 mjini mwanza.

 Wachezaji bora wa mashindano haya ndio wataunda kikosi cha awali cha Taifa kwa ajili ya kushiriki fainali za Afrika watoto umri chini ya miaka 17 mwaka 2109.

Tunaomba Serikali pamoja na wadau wote tushirikiane katika kukilea kikosi hiki ili mwaka 2019 tuwe na timu nzuri.

Tunamshukuru Mh Dr Fennela Mukangara na wizara nzima ya habari vijana utamaduni na michezo kwa ushirikiano wanaotupatia katika hatua hizi na katika shughuli nyingine za kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu.

Ndugu mgeni rasmi ninaomba sasa nikukaribishe uhutubie hafla  hii na pia utuongoze katika shughuli zitakazofuata.

Ahsate sana

Jamal Malinzi

Dar es salaam

03/juni/2015

Tuesday, June 2, 2015

15 WAJITOKEZA KUWANIA UONGOZI COASTAL UNION

KUELEKEA Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Coastal Union tayari maandalizi
yameanza kukamilika kwa asilimia kubwa ambapo jumla ya wagombea kumi
na tano wamejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi.

Akizungumza leo ,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema
katika uchaguzi mkuu nafasi ambazo wagombea wamejitokeza ni Mwenyekiti
ambapo nafasi hiyo amejitokeza Dokta Ahmed Twaha akiwa hapa mpinzani.

Nafasi ya makamu Mwenyekiti wamejitokeza wagombea wawili ambao ni
Salim Amiri na Hussein Abdull Ally ambao watachuana ili kuweza
kupatikana mshindi ambayo atachukua nafasi hiyo.

Aidha amesema kuwa katika nafasi ya Kamati ya utendaji wamejitokeza
wagombea kumi na mbili ambao watachuana na kubaki wajumbe watano
watakaounda kamati ya utendaji.

Amewataja waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni Albert Clement
Peter,Omari Mwambasha,Waziri Mohamed,Mohamed Ally “Dondo”,Mohamed
Maulid Rajabu,Abubakari Ahmed Machai,Aggrey Ally Mbapu,Hassani Omari
Bwana.

Wengine ambao wamejitokeza kuwania nafasi hiyo kuwa ni Abdallah Zuberi
Ally “Unenge”,Hassani Ramadhani Muhsin,Albert Clement Peter,Hussein
Ally Mwinyi Hamis na Salim Abasi Perembo.

STARS YAINGIA KAMBINI


Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambayo inadhaminiwa na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, imeingia kambini jana katika hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON).

Kikosi kitakachoingia kambini kinawajumuisha wachezaji waliocheza michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi Mei, wachezaji 20 walioanza kambi tangu wiki iliyopita na wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Congo DR.

Taifa Stars inatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Gymkana na Uwanja wa Taifa kwa muda siku mbili kabla ya siku ya alhamis kusafiiri kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.

Wachezaji wanaotarajiwa kuingia kambini leo ni Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Aggrey Morris, Salum Mbonde, Erasto Nyoni, Saimon Msuva, Hassan Dilunga, Joram Mgeveke, Juma Liuzio, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, John Bocco, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Ibrahim Hajibu, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.

Wachezaji waliopo kambini tangu wiki iliyopita ni Nadir Haroub, Juma Abdul, Salum Telela, Peter Manyika jr, Jonas Mkude, Hassan Isihaka, Mohamed Hussein, Aishi Manula, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Kelvin Friday, Malimi Busungu, Bennedict Tinoco, Rashid Mandawa, Atupele Green, Haroun Chanongo, Emmanuel Simwanda, Said Mohamed, Andrew Vicent, Gadiel Michael, Deus Kaseke.

Msafara wa Taifa Stars unatarajiwa kuondoka nchini Alhamis Juni 4, 2015 kuelekea Ethiopia ukiwa na wachezaji 23,benchi la ufundi pamoja na viongozi .

Mechi kati ya Misri dhidi ya Tanzania inatarajiwa  kuchezwa Juni 14, 2015 katika uwanja wa Borg El Arab pembeni kidogo ya jiji la Alexandria.

Wakati huo huo, Tanzania imepata mwaliko wa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda kati ya Juni 6, 7 mwaka huu jijini Kigali, kwenye kumbukumbu ya mauaji ya kimbali, Tanzania itapeleka kikosi cha vijana U23 katika mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa wiki.

Kufuatia kupata mwaliko huo kikosi cha U23 kitaondoka nchini ijumaa tarehe 5, Juni 2015 kuelekea nchini Rwanda kikiwa na wachezaji 18 chini ya kocha Salum Mayanga.

Kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime ameongezwa kwenye benchi la ufundi litakalokwenda Ethiopia kisha nchini  Misri kufuatia kocha Salum Mayanga kuwa na timu ya U23 nchini Rwanda.

TFF KUZINDUA JEZI MPYA ZA TIMU ZA TAIFA


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, kesho jumatano linatarajia kuzindua jezi mpya za timu za Taifa Tanzania, zitakazokuwa zikitumika katika michuano mbalimbali, uzinduzi huo utakafanyika katika hoteli ya JB Belmonte (PSPF) iliyopo eneo la Posta jijini Dar es salaam.

Katika hafla hiyo, TFF itawatunukia vyeti viongozi mbalimbali waliotoa mchango katika mpira wa miguu, wadhamini, wahamashisashaji pamoja na wachezaji waliochezea Taifa Stars ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu Tanzania kujiunga na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).

WATUNUKIWA WA VYETI VYA KUMBUKUMBU YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50, TANZANIA KUJIUNGA NA FIFA.

VIONGOZI WA KITAIFA:
1. Rais Msataafu Mwl. Julius K Nyerere
2. Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi
3. Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa
4. Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
5. Rais Mstaafu Abeid Amani Karume
6. Rais Mstaafu Amani Abeid Karume
7.Rais Mstaafu Abdul Wakili
8. Rais Mstaafu Abdu Jumbe
9. Rais Dk. Salmin Amour
10. Rais Dk. Mohamed Shein

WENYEVITI/MARAIS FAT/TFF
11.Balozi Maggid
12. Mzee Ali Chambuso
13. Said Hamad El Maamry
14. Alhaj Muhidin Ahmad Ndolanga
15. Leodgar Chilla Tenga

MAKATIBU WAKUU
16. Said Hassan
17. Abdallah Mpolaki
18. Kitwana Ibrahim
19. Martin Maude
20. Meshack Maganga
21. Col. Yunus Abdallah
22. Patrick Songora
23. Ali Mwanakatwe
24. Ismail Aden Rage
25. Angetile Osiah
26. Michael Wambura
27. Fredrick Mwakalebela

MAKOCHA
28. Mansour Magram
29. Paul West Gwivaha
30. Joel Nkaya Bendera
31. Don Korosso
32. Mohamed Msomali
33. Shaban Marijani
34. Hamis Kilomoni
35. Syllersaid Mziray

WAAMUZI
36. Gratian Matovu
37. Kassim Chona
38. Zuberi Bundala
39. Mohamed Nyama
40. Mussa Lyaunga
41. Ramadhani Mwinyikonda
42. Ramadhani Kaabuka
43. Joseph Mapunda
44. Dunstan Daffa
45. Said Almasi
46. Abdul Rasul Ismail

WACHEZAJI
47. Mohamed Chuma
48. Kitwana Manara
49. Miraji Juma
50. Dracula
51. Mathias Kissa
52. Hamis Fikirini
53. Emily Kondo
54. Abdulrahman Lukongo
55. Hemedi Seif
56. Abdul Aziz
57. Mbwana Abushir
58. Sembwana
59. Mweri Simba
60. Omar Zimbwe
61. Arthur Mwambeta
62. Ayoub Mohamed
63. John Lyimo
64. Mohamed Mwabuda

TIMU YA TAIFA 1979-1980 ILIYOENDA NIGERIA
65. Leodgar Tenga (Nahodha)
66. Athuman Mambosasa
67. Idd Pazi
68. Juma Pondamali
69. Leopold Mukebezi
70. Ahmed Amasha
71. Ramadhani Nyamwela
72. Mohamed Kajole
73. Salim Amir
74. Jella Mtegwa
75. Mtemi Ramadhani
76. Adolf Rishard
77. Hussein Ngulungu
78. Juma Mkambi
79. Omari Hussein
80. Thuweni Ally
81. Mohamed Salim
82. Peter Tino
83. Rashid Chama
84. Slomir Wolk (Kocha Mkuu)
85. Joel Bendera (Kocha Msaidizi)
86. Dk. Katala (Daktari wa timu)
87. Mzee Mwinyi (Meneja)
88. Willy Kiango
89. Daud Salum
90. Stanford Nkondora (Mkuu wa Msafara)

MAWAZIRI WA MICHEZO
91. Mrisho Sarakikya
92. Chadiel Mgonja
93. Fatma Said Ally
94. Prof. Phillemon Sarungi
95. Prof. Juma Kapuya
96. Mohamed Seif Khatib
97. Dk. Emmanue Nchimbi

VIONGOZI WA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA (BMT)
98. Said Hamad El Maamry
99. Balozi Maggid
100. Moses Mnauye
101. Makame Rashid

MAKATIBU BMT
102. Salum Dossi
103. Mohamed Lutta
104. Ernest Mlinda
105. Leonard Thadeo

WAKURUGENZI WA MICHEZO SERIKALINI
106. Khalifa Abdallah
107. Chabanga Hassan Dyamwale
108. Joas Nkongo
109. Flavian Kipanga
110. Henry Ramadhani
111. Leonard Thadeo
112. Jenerali Ulimwengu

WADHAMINI
113. TBL
114. VODACOM
115. SERENGETI BREWERIES
116. NMB
117. AZAM
118. BAHATI NASIBU YA TAIFA
119. AIRTEL
120. BANK ABC
121. COCA COLA
122. NSSF
123. AZAM MEDIA
124. BARRICK GOLD MINE
125. AIR TANZANIA
126. TANZANIA RAILWAY CORPORATION
127. SYMBION
128. TANZANIA TOBACCO BOARD
129. TANZANIA COFFEE BOARD
130. TANZANIA SISAL BOARD
131. TANZANIA HARBOU AUTHORITY
132. BIMA
133. UHAMIAJI
134. BORA
135. URAFIKI
136. TACOSHILL

WATANGAZAJI WA MPIRA
137. Omar Masoud Jarawa
138. Salim Seif Mkamba
139. Ahmed Jongo
140. Nadhir Mayoka
141. Halima Mchuka
142. Idd Rashid Mchatta
143. Charles Hilary
144. Dominic Chilambo
145. Tido Mhando
146. Abdul Ngalawa
147. Mikidad Mohamoud
148. Abdallah Majura

WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO
149. Tommy Shitole
150. Willie Chiwango
151. Steven Rweikiza
152. Muhidin Issa Michuzi
153. John Ngahyoma
154. Mwalimu Omar
155. James Nhende

WAHAMASISHAJI WA TIMU YA TAIFA
156. JKT Mafinga Kimulimuli
157. Mbaraka Mwinshehe

MABINGWA WA LIGI
158. Cosmopolitan
159. Simba Sports Club
160. Young Africans Sports Club
161. Mseto
162. Pan African
163. Tukuyu Stars
164. Coastal Union
165. Mtibwa Sugar Football Club
166. Azam Football Club

WAWAKILISHI WA MUUNGANO
167. Malindi FC
168. Tanzania Stars
169. Pamba FC
170. Reli Morogoro
171. African Sports
172. Tanzania Prisons
173. Simba Sports Club
174. Young Africans Sports Club

VIONGOZI WA VILABU
175. Shaban Mwakayungwa
176. Tabu Mangara
177. Kondo Kipwata
178. Jabir Katundu
179. Amiri Ali Bamchawi
180. Juma Salud
181. David Ngonya
182. Priva Mtema
183. Mama Fatma Karume
184. Ramnik Patel Kaka
185. Aboubakar Mgumia
186. Kitwana Kondo
187. Kitwana Athuman
188. Abdulwahab Abbas Maziwa
189. Ally Sykes (Kleist Sykes)

VIONGOZI WALIOJENGA VIWANJA
190. Richard Wambura
191. Lawrence Gama
192. Abdulnur Suleiman
193. Sheikh Amri Abeid
194. Mohamed Kissoky

U13 KUTIMUA VUMBI MWANZA JUNI 7

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Julai 7 mwaka huu litafungua mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 jijini Mwanza kwa mikoa yote ya Tanzania kwa lengo la kung’amua vipaji kwa ajili ya kuunda timu ya Taifa  ya vijana wenye umri huo.

Mashindano hayo yatakayofanyika kwa kipindi cha wiki moja, yatafanyika katika viwanja vya CCM Kirumba na Alliance vyote vilivyopo jijini Mwanza, na maandalizi ya michuano hiyo yamekamilika na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa Mwanza.

Jopo la makocha litakua katika viwanja hivyo kusaka vipaji kwa lengo la kuanza kuiandaa timu ya Taifa ya vijana wenye umri wa miaka 13, ili ifikapo mwaka 2019 waweze kuiwakilisha Tanzania katika fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyika hapa nchini.

Mapema wiki iliyopita Shirikisho la Soka barani Afrika - CAF liliipa Tanzania uenyeji wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019.

TFF katika kuhakikisha inafanya vizuri katika soka la vijana, mapema mwezi Aprili iliendesha kozi ya waamuzi vijana jijiji Dar es salaam, ambapo vijana 36 walishiriki kozi hiyo na kutunukiwa vyeti.

Aidha TFF ina programu ya vijana chini ya miaka 15 ambayo ilianza kambi mwezi Aprili mwaka huu, na inatarajiwa kucheza michezo ya kirafiki katika mikoa saba nchini kati ya mwezi Juni na Agosti, kabla ya mwezi Disemba kusafiri katika nchi Malawi, Zambia, Zimbabwe, Bostwana na Afrika Kusini.

Kikosi hicho cha umri chini ya miaka 15 kinajiandaa na kuwania kufuzu kwa fainali za Vijana Afrika mwaka 2017 ambapo katika ziara hizo za mikoani, walimu watatumia nafasi hiyo kungamua na kuongeza vijana wengine katika kikosi.