KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, February 28, 2015

JOHN DAMIANI KOMBA AMEDFARIKI DUNIA

Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, ambaye pia ni kiongozi wa Kundi la TOT,Capt.John Damian Komba amefatiki dunia hii leo katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam alikolazwa kwa matibabu.

Hakika kifo cha Komba ni pigo kubwa kwa wana Mbinga, CCMna watanzania kwa ujumla.

Komba atakumbukwa na maelfu ya watanzania kwa nyimbo zake za hamasa ndani ya Cjhama cha mapinduzi na taifa kwa ujumla.

Atakunbukwa kwa nyimbo kipindi cha uchaguzi tangu enzi ya chama kimoja na hata kipindi cha msiba wa Baba wa Taifa akivyoimba nyimbo za maombolezo.

Friday, February 27, 2015

TAIFA STARS KUSHIRIKI COSAFA CUP


Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imethibitisha kushiriki michuano ya kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini kufuatia mwaliko wa Baraza la vyama vya soka Kusini mwa Afrika (COSAFA).

Michuano ya kombe la COSAFA inatrajiwa kuanza kutimua vumbi katikati ya mwezi Mei mwaka huu nchini Afrika Kusini, na ratiba ya hatua ya awali ya makundi inatarajiwa kutangazwa leo jioni saa 1:00 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki moja kwa moja na kituo cha Luninga cha Supersport 4.

Taifa Stars itakuwa juu (seeded) katika hatua ya makundi, ambapo nchi nane zitagawanya katika makundi mawili na washindi wa kila kundi wataingia hatua ya robo fainali, nchi  nyingine zitakazoanzia kwenye makundi ni Lesotho, Madagascar, Marutius, Namibia, Seychelles, Swaziland.

Katika kila kundi, timu zote zitacheza michezo mitatu na mshindi wa kila kundi ataingia katika hatua inayofuata ya robo fainali itakayozijumuisha nchi za  Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia ambazo zimeingia katika hatua ya pili kutokana na nafasi zao kwenye msimamo wa viwango vya FIFA.

Kombe la COSAFA lilianza mwaka 1997 linajumuishaa nchi 16 wanchama kutoka Kusini mwa Bara la Afrika, limekua likifanyika kwa kushirikisha nchi wanachama waliopo Kusini mwa bara la Afrika.
Nchi wanachama wa COSAFA ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Comoros, Lesotho, Madagascar, Malawi, Maurtius, Mayotte, Msumbuji,Namibia, Reunion, Sychelles, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.

NGASA AIPAISHA YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO
BAO lililofungwa na mshambuliaji Mrisho Ngasa jana liliiwezesha Yanga kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika baada ya kuitoa BDF ya Sudan.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Lobatse, BDF iliichapa Yanga mabao 2-1.

Pamoja na kupata kipigo hicho, Yanga imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 kufuatia kushinda mechi ya awali wiki mbili zilizopita kwa mabao 2-0.

Timu hizo zilikwenda mapumziko Yanga ikiwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Ngasa dakika ya 30, akiunganisha wavuni kwa kichwa pasi kutoka kwa Amis Tambwe.

BDF ilikianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 49 kupitia kwa Mosimanyana, aliyemalizia pasi kutoka kwa Lerore.

Yanga ilipata pigo dakika ya 72 baada ya mshambuliaji wake Danny Mrwanda kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumchezea rafu mbaya Madziba.

Bao la pili la BDF lilifungwa na Kumbulani Madziba dakika ya 85, aliyewatoka mabeki wa Yanga na kufumua shuti lililompita kipa Ally Mustafa Barthez.

Wakati huo huo, wawakilishi  wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa Afrika, Azam leo wanashuka dimbani mjini Khartoum kurudiana na El Merreikh.

Katika mechi hiyo, Azam inahitaji sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele kufuatia kushinda mechi ya awali mjini Dar es Salaam kwa mabao 2-0.

Thursday, February 26, 2015

NASRY KUJIUNGA NA ASPIRE FOOTBALL DREAM SENEGALKijana Nasry Daudi Aziz aliyezaliwa Agosti 21, 2001 amechaguliwa kujiunga na kituo cha kukuza vipaji cha Aspire Football Dream kilichopo katika mji wa Dakar nchini Senegal.

Mradi wa  Aspire nchini ulianza mchakato wa kusaka vijana mwezi Machi - Mei, 2014 ambapo vijana wengi walijitokeza na kuchaguliwa vijana 14 ambao walikwenda katika mchujo mwingine uliofanyika nchini Uganda uliowashirikisha vijana zaidi ya 50.

Kijana huyo ni miongoni mwa wachezaji 17 waliochaguliwa kati ya vijana 34 walikuwepo nchini Senegal kwa muda wa mwezi mmoja, ambapo kulikuwa na vijana wengi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika na Amerika ya Kusini.

Kituo cha Aspire kilichopo Dakar nchini Senegal ni miongoni mwa vituo viwili vinavyoongozwa na mtoto wa mfalme wa Qatar na timu ya Barcelona, kituo kingine kipo mjini Doha.

Nasry Daud Aziz anatarajiwa kuondoka nchini Februari 28 mwaka huu kuelekea Dakar ambapo atakua kwenye kituo hicho kwa mkataba wa miaka miatano.

 Kutoka nchini Tanzania Nasry anakua ni kijana wa tatu kujiunga na kituo hicho, wengine ni Matine Taganzi na Orgenes Morrel ambaye aliitwa kwenye timu ya Taifa Stars maboresho na kocha Mart Nooj.

STAND NA SIMBA ZAINGIZA MIL 31, MBEYA CITY, YANGA MIL 74
Mchezo uliokuwatanisha wenyeji timu ya Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga dhidi ya timu ya Simba umeingiza jumla ya tsh. milioni 31.

Juma la watazamaji 5,439 waliingia uwanjani kushuhudia mchezo huo, ambao timu ya Stand imepata mgao wa tsh. 6,564,268.22 na Simba wakipata mgao wa tsh. 4,661,581.78.

VAT (18%) tshs. 4,763,135.59 huku FA  mkoa wakipata tsh.665,940.25, FDF tsh. 1,141,611.86, Bodi ya Ligi tsh. 1,522,149.15, Gharama za mchezo tsh. 1,617,283.47, Uwanja tsh. 2,854,029.66, Gharama ya tiketi tsh. 1,593,000,00, FDF tsh. 2,921,000.00, TFF tsh.2,921,000.00

Katika uwanja wa Sokoine mbeya jumla ya tsh. 74,600.000.00, zilipatikana kutokana na watazamaji 14,920 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo,  VAT(18%) tsh.11,379,661.02, CDRB (5%) tsh.3,730.000.00, FDF tsh. 5,222,000,00, TFF tsh. 2,238,000.00, Uwanja tsh. 7,804,550,85, Gharama za mchezo tsh 4,442,578.81, Bodi ya Ligi tsh. 4,162,427,12.

Chama cha soka mkoa (FA) Mbeya kimepata tsh. 1,821,061.86, FDF(TFF) tsh. 3,121,820.34, wenyeji timu ya Mbeya city wakipata tsh. 17,950,466.95 na klabu ya Yanga tsh. 12,747,438.98.

MKUTANO MKUU WA TFF KUFANYIKA MOROGOROKamati ya Utendaji ya Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF iliyokutana jumapili Februari 22 mwaka huu, imefanya mabadiliko ya mahali utakaofanyika Mkutano Mkuu wa mwaka kutoka Mkoa wa Sinigida na kuhamishia mkoa wa Morogoro.

Hatua hiyo imefikiwa na Kamati ya Utendaji kutokana na sababu za kutokukamilika kwa miundombinu ya mkutano mkuu na kuwepo ka shughuli nyingine za kijamii mkoani humo.

Kamati ya Utendaji inamshukuru Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Singida (SIREFA), na uongozi mzima kwa kujitolea kuandaa mkutano huo na huko nyuma waliweza kuandaa mkutano wa makatibu wa vyama vya soka vya mikoa.

TFF itaandaa vikao na matukio mengine mkoani Singida itakapotokea hapo baadae, tarehe ya mkutano mkuu itaendelea kubakia ile ile ya Machi 14, 15 mwaka huu.

Monday, February 23, 2015

MWADUI FC BINGWA LIGI DARAJA LA KWANZA (FDL)


Timu ya Mwadui kutoka mjini Shinyanga,inayofundishwa na Kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio' jana ilitawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kuifunga timu ya African Sports ya jijini Tanga kwa bao 1 - 0, katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Comlex Chamazi jijni Dar es Salaam.

Bao pekee na la ushindi kwa timu ya Mwadui lilifungwa na mshambulaji Kelvin Sabato Kongwe dakika ya 53 ya mchezo na kuihakikishia Mwadui ushindi katika mchezo huo wa fainali.

Mabingwa hao wapya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) walizawadia Kombe la Ubingwa, medali pamoja na hundi ya sh.millioni tatu, huku timu ya African Sports ikipata medali na hundi ya sh. millioni mbili.

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF linaipongeza timu ya Mwadui kwa kuibuka Bingwa mpya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/205.

Jumla ya timu nne zimepanda Ligi Kuu msimu ujao ambazo ni  bingwa Mwadui FC, African Sports, Majimaji na Toto Africans.

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA ALEX

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF amepeleka salamu za rambirambi kwa familia ya Alex Massawe, kufuatia kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Star) na klabu ya Simba SC, Christopher Alex kilichotokea jana mjini Dodoma.

Christopher Alex Massawe aliwahi kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwa mafanikiko makubwa huku pia akiwa tegemeo katika klabu yake ya Simba SC.

Katika salam zake kwa familia ya Massawe, kwa niaba ya TFF, familia ya mpira wa miguu na watanzania, Rais Malinzi amewapa pole wapenzi wa mpira wa miguu nchini  katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo.

MALINZI AIPONGEZA TIMU YA TAIFA SOKA LA UFUKWENIRais wa Shrikisho la Mpira wa miguu nchini –TFF, Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer), Ahmed Mgoyi kwa ushindi wa jumla wa mabao 12- 9 dhidi ya timu ya Taifa kutoka nchini Kenya.

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Sola la Ufukweni, mwishoni mwa wiki iliibuka na ushindi wa mabao 7-6 katika mchezo uliofanyika kwenye Ufukwe wa klabu ya Escape 1 eneo la Msasani Jijini Dar es salaam.

Katika salamu zake Malinzi amesema ushindi walioupata timu ya soka la ufukweni mwishoni mwa wiki, umeitangaza vizuri nchi ya Tanzania na kuwataka Viongozi wa soka la ufukweni, makocha, wachezaji kutobweteka na ushindi huo zaidi kujipanga kwa maandalizi ya mchezo utakaofuata.

Baada ya kuitoa timu ya Taifa ya Kenya, Tanzania watacheza na timu ya Taifa ya Misri mapema mwezi ujao ambapo mchezo wa awali utafanyika jijini Dar es salaam kati ya mwezi Machi 7, 8 na marudiano kufanyika baada ya wiki moja nchini Misri.

Endapo timu ya Taifa ya Tanzania itaiondoa timu ya Taifa ya Misri, moja kwa moja itakata tiketi ya kushiriki Fainali za Mataifa Afrika kwa Soka la Ufukweni 2015 zinazotarajiwa kufanyika Visiwa vya Shelisheli kuanzia April 14 - 19 mwaka huu.

Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), familia ya mpira na watanzania kwa ujumla wanawapa pongezi timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la Ufukweni kwa ushindi huo na kuwatakia maandalizi mema kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Misri.


YANGA CHEREKO, SIMBA YACHINJWA


TIMU ya soka ya Yanga  jana iliendelea kujizatiti kileleni mwa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Mbeya City mabao 3-1.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, mshambuliaji Simon Msuva, aliendelea kudhihirisha ukali wake wa kuzifumania nyavu baada ya kuifungia Yanga bao la kuongoza dakika ya 18. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Mrisho Ngasa aliiongezea Yanga bao la pili dakika ya 59 baada ya kuwahadaa mabeki  wa Mbeya City pamoja na kipa wao.

Mbeya City ilipata bao la kujifariji dakika ya 68 kupitia kwa Abdul Seif baada ya kuunganisha krosi kutoka kwa Deus Kaseke.

Yanga iliendelea kutandaza soka ya kuvutia na hatimaye kupata bao la tatu dakika ya 78 kupitia kwa Haruna Niyonzima.

Wakati huo huo, mambo yameendelea kuwa mabaya kwa Simba baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Stand United ya Shinyanga

Bao pekee na la ushindi la Stand United lilifungwa na Abashim Chidvebede dakika ya 11, akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Abuu Ubwa.

Sunday, February 22, 2015

BEKI NGULI WA ZAMANI WA SIMBA CHRISTOPHER ALEX AFARIKI DUNIA


BEKI wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, Christopher Alex amefariki dunia.

Habari kutoka mkoani Dodoma zimeeleza kuwa, Alex amefariki dunia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kifua.

Wakati huo huo, Chama cha Kandanda mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimeeleza kusikitishwa kwake na kifo cha mchezaji kiungo wa zamani wa klabu ya Simba na Taifa Stars,Christopher Alex,  maarufu kama Masawe, kilichotokea leo (Februari 22), katika Hospitali ya Mirembe, Dodoma.

Mwenyekiti wa DRFA,Almas Kasongo,amemuelezea marehemu Christopher kuwa ni mchezaji aliyevuma enzi za uhai wake na kuiletea heshima kubwa klabu yake ya Simba na Taifa kwa ujumla, pale walipofanikiwa kuisukumiza nje ya michuano ya Afrika, klabu ya Zamalek ya Misri na kuivua ubingwa miamba hiyo ya soka ya kaskazini mwaka 2003.

Kiungo huyo aliyeanza kuvuma katika miaka ya 2000, amefariki dunia kutokana na kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kifua kikuu (TB).

Marehemu Christopher Alex, alizaliwa Septemba 12, 1975, na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Uhuru na kumaliza katika shule ya Chamwino huko Dodoma mwaka 1993. Alianza kucheza mpira kwenye timu ya daraja la nne ya Chamwino Utd na baadaye daraja la tatu akiwa na kikosi cha Aston Villa nayo ya Dodoma.

Mwaka 1999-2001, aliitumikia klabu ya CDA ya Dodoma, kabla ya kutimkia klabu ya Reli ya Morogoro mwaka 2002, na baadaye kujiunga na Wekundu wa Msimbazi Simba. Marehemu ameacha mtoto mmoja aitwaye Alex.

Kasongo, kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya DRFA, wametoa ubani wa shilingi laki mbili (200,000/=) kwa familia ya marehemu na kuwataka mashabiki wa soka na watanzania kuungana katika kuifariji familia hiyo kwenye kipindi hiki kigumu cha majonzi.

MTIBWA SUGAR SASA CHOKA MBAYAMABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wameendelea kufanya vibaya licha ya kuanza msimu kwa kishindo, baada ya leo kufungwa bao 1-0 na Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Matokeo hayo, yanaifanya Mgambo itimize pointi 20 baada ya kucheza mechi 15 na kupanda hadi nafasi ya sita kutoka ya 11, wakati Mtibwa inabaki na pointi zake 19 za mechi 16.

Bao pekee la Mgambo JKT jioni ya leo limefungwa na Balimi Busungu dakika ya 27, akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Salim Kapinga.

Wakati huo huo, Kagera Sugar wamepanda hadi nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa bao 1-0 jioni ya leo dhidi ya Polisi Moro Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Kagera wanafikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi 17, wakiwashushia nafasi ya tatu mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 26 za mechi 14. Yanga SC yenye pointi 28 za mechi 14, inaongoza Ligi Kuu.

Bao pekee Kagera leo limefungwa na mshambuliaji wa ‘Taifa Stars Maboresho’, Rashid Mandawa.

Katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, wenyeji Ndanda wameshinda 1-0 dhidi ya Coastal Union, bao pekee la Nassor Kapama

TWIGA STARS WAINGIA KAMBINI


Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars), Rogasian Kaijage ametangaza kikosi cha wachezaji thelathini (30) kitakachoingia kambini leo (Jumapili), kujiandaa na mchezo wa kufuzu Mataifa Afrika dhidi ya Zambia mwezi Machi mwaka huu.

Kaijage ametangaza program yake ya  mazoezi itakayochukua takribani wiki nne (4) ili kuhakikisha wachezaji wanakua tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa kati ya Machi 21, 22 mwaka huu, huku akipanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuelekea Lusaka Zambia kwenye mchezo wa awali.

Twiga Stars ambayo itakua kambini katika Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF zilizopo Karume,  imeingia moja kwa moja katika hatua ya pili kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo wa viwango vya soka la wanawake barani Afrika.

Wachezaji walioitwa ni, Asha Rashid, Esther Chaburuma, Fatuma Bushiri, Fatuma Hassan, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma Abdallah, Sofia mwasikili, Zena Khamis, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Fadhira Hamad, Anastazia Anthony, Shelder Boniface.

Wengine ni Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia Daniel, Fatuma Issa, Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbasi, Stumai Abdallah, Ziada Ramadhani, Zuwena Aziz, Irene Joseph (Mfunzo – Zanzibar), Dawa Haji Vuai (JKU – Zanzibar), Belina Julius na Amina Ramadhani.

Thursday, February 19, 2015

MSUVA AIPAISHA YANGA LIGI KUU, YAICHAPA PRISONS 3-0


YANGA jana iliendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuicharaza Prisons mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Matokeo hayo yameiwezesha Yanga kuendelea kujikita kileleni mwa ligi hiyo, ikiwa na pointi 28 na kuiacha kwa mbali kidogo, Azam, ambayo jana ililazimishwa kutoka suluhu na Ruvu Shooting.

Mshambuliaji Simon Msuva aliibuka shujaa wa Yanga baada ya kuifungia mabao mawili kati ya matatu.

Msuva alifunga bao la kwanza dakika ya tatu alipounganisha wavuni kwa kichwa krosi kutoka kwa Coutinho.

Bao la pili la Yanga lilitokana na uzembe wa mabeki wa Prisons kujifunga wakati wakijaribu kuokoa shuti lililopigwa na Coutinho. Timu hizo zilikwenda mapumziko Yanga ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

Msuva aliihakikishia Yanga ushindi dakika ya 62 baada ya kuifungia bao la tatu, akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Coutinho.

Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa jana, Azam ilibanwa mbavu na Ruvu Shooting baada ya kulazimishwa kutoka nayo suluhu kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo wakati Simba itakapomenyana na Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Tuesday, February 17, 2015

AFRICAN SPORTS, MWADUI FC KUCHEZA FAINALI JUMAPILI


Timu za African Sports ya Tanga na Mwadui FC ya Shinyanga zinatarajiwa kucheza mchezo wa fainali ya kusaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) siku ya Jumapili katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

African Sports waliibuka washindi wa kwanza katika Kundi A na Mwadui FC washindi wa kwanza Kundi B, watacheza mchezo huo wa fainali ambapo bingwa atapewa zawadi ya kombe na medali, hali kadhalika kwa mshindi wa pili.

Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilimalizika mwishoni mwa wiki kwa timu nne kupanda Ligi Kuu kwa kila kundi kutoa timu mbili, Kundi A ni African Sports na Majimaji FC, Kundi B ni timu za Mwadui FC na Toto Africans.

Nazo timu za Green Worriors na Villa Squad zimeteremka daraja la pili baada ya kushika nafasi za mwisho kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza. Villa Squad kutoka Kundi A na Green Warriors Kundi B.

 TFF YAZIPONGEZA AFRICAN SPORTS, MWADUI, MAJIMAJI NA TOTO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Wenyekiti wa klabu ya African Sports (Tanga) , Majimaji (Ruvuma),  Mwadui (Shinyanga) na Toto Africans ya Mwanza kwa timu zao kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

Katika salamu zake Bw. Malinzi amesema vilabu hivyo vinapaswa kujipanga na kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2015/2016, kwani VPL ni ngumu kutokana na timu zote kuwa na ushindani mkubwa wa kutafuta matokeo mazuri kuepeuka kushuka daraja.

Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF, familia ya mpira na watanzania kwa ujumla wanawapa pongezi timu za African Sports, Majimaji, Mwadui na Toto Africans kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom na kuwatakia maandalizi mema ya VPL 2015/2016.

MAHUNDI, BAHANUZI WACHEZAJI BORA LIGI KUUKiungo wa timu ya Coastal Union, John Mahundi amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Disemba 2014 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Mahundi alitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya Coastal Union mwezi Disemba mwaka jana na kuchaguliwa na jopo la makocha linalofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora wa kila mwezi.

Aidha mshambuliaji wa timu ya Polisi Morogoro, Said Bahanuzi amechaguliwa kuwa mchezaji bora mwezi Januari 2015 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi mzunguko wa 15 kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Bahanuzi anayechezea timu ya Polisi Morogoro kwa mkopo akitokea timu ya Young Africans amekua na mchango mkubwa kwa timu yake tangu kujiunga nayo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom nchini.

Kwa kuibuka wachezaji bora, Mahundi na Bahanuzi watazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja kwa kila mmoja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Jopo maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.

Monday, February 16, 2015

TANZANIA YAICHAPA 5-3 KENYA KWENYE BEACH SOCCER.


Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni (Beach Soccer) jana imeibuka na ushindi wa mabao 5- 3 ugenini dhidi wa wenyeji timu ya Taifa ya Kenya kwenye mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa fukwe za Hotel ya Big Tree Pirates jijini Mombasa.

Katika mchezo huo mabao ya Tanzania yalifungwa na Ali Rabbi mabao manne  na Mwalimu Akida bao moja .

Kipindi cha kwanza kilimazika kwa Tanzania kupata mabao 2 Kenya 1, kipindi cha pili kilimalizika Tanzania 4 Kenya 3 na kipindi cha tatu na cha mwishokwa mchezo kimalizika kwa Tanzania kupata mabao 5 Kenya 3.

Mechi ya marudiano inatarajiwa kuchezwa jumamosi wiki hii Februari 21, 2015 jijini Dar es salaam, na endapo timu ya Taifa ya Tanzania itafanikiwa kuwatoa Kenya, itacheza na timu ya Taifa ya Misri katika hatua inayofuata.

Mchezo wa kwanza utafanyika kati ya tarehe 7,8 Machi 2015 jiji Dar es salaam na marudiano yatafanyika nchini Misri kati ya tarehe 13,14 Machi 2015.

Timu inarejea leo jijini Dar es salaam majira ya saa 11 jioni ikitokea jijini Mombasa nchini Kenya.

DRFA YAZIPONGEZA YANGA NA AZAM


Chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimewapongeza wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya vilabu barani afrika klabu ya Azam FC na Yanga SC,kwa kuanza na ushindi katika mechi zao za mkondo wa kwanza mwishoni mwa juma.

Yanga walikuwa wa kwanza kuwapa raha watanzania siku ya jumamosi katika uwanjwa wa taifa jijini,baada ya kuifunga mabao 2-0 timu ya maafande wa Polisi toka Botswana BDF 11,mabao yete hayo yakitupiwa nyavuni na mshambuliaji Amis Tambwe,ikiwa ni mchezo wa kuwania kombe la shirikisho.

Kwa upande wa Azam FC,wao waliwafunga wababe wa soka huko Sudan klabu ya El-Merekh kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Didier Kavumbagu pamoja na John Rafael Bocco,katika mchezo wa kuwania kombe la klabu bingwa uliopigwa katika dimba la Azam Cpmplex Chamazi.

Mwenyekiti wa DRFA,Almas Kasongo,amewapongeza wawakilishi hao wa Tanzania kwa hatua hiyo nzuri waliyoanza nayo,na kusema kuwa maandalizi yaliyofanywa na vilabu hivyo kuelekea mashindano hayo ya afrika,pamoja na ubora wa wachezaji na makocha,ni dhahiri kwamba vitafanikiwa kuvuka katika hatua hiyo ya kwanza.

Kasongo,pia amesema DRFA imeridhishwa na muitikio wa mashabiki wa Dar es salaam na maeneo mengine nje ya jiji kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hizo mbili,na kuwapongeza pia viongozi wa vilabu kwa matayarisho waliyoyafanya licha ya dosari ndogo ndogo zilizojitokeza. 

MICHUANO YA LIGI YA MKOA DAR INAENDELEA
Michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam inaendelea tena wiki hii kwa timu 8 kushuka katika viwanja tofauti,kupambana ili kuusaka ubingwa huo pamoja na kupata nafasi ya kuingia katika ligi daraja la pili taifa.

Mechi za leo Februari 16,2015/Azania Ngano watakipiga dhidi ya Yanga U20 (Katika uwanja wa Karume),Stakishari watacheza na FFU (uwanja wa B.Mkapa),Changanyikeni wataumana dhidi ya Tuamoyo (uwanja wa MWL/Nyerere) na New Kunduchi wataoneshana kazi dhidi ya Sinza Stars (uwanja wa Kines).

Kivumbi hicho kitaendelea tena kesho Kutwa Februari 18,2015 kwa Simba U20 kucheza na Ukonga UTD (Uwanja wa karume),Red Coast watacheza dhidi ya Shababi (MWL/Nyerere), Zakhem watacheza na Sifa UTD ( Uwanja wa Bandari) na Beirahotspurs watakipiga dhidi ya Pan African (uwanja wa Kines).

SIMBA YANGURUMA MOROGORO


SIMBA imepoza machungu ya mashabiki wake baada ya jana kuichapa Polisi Moro mabao 2-0 katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Iliwachukua Simba dakika 14 kuhesabu bao la kwanza lililofungwa na mshambuliaji chipukizi Ibrahim Hajibu baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa beki Juuko Murshid na kuwatoka mabeki wa Polisi.

Simba ilipata pigo dakika ya 56 baada ya kipa wake Ivo Mapunda kuzimia uwanjani baada ya kugongana na mchezaji mmoja wa Polisi. Ilibidi kipa huyo atolewe uwanjani na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.Nafasi yake ilichukuliwa na Manyika Peter.

Bao la pili la Simba lilifungwa na Elias Maguri dakika ya 63 baada ya kuwatoka mabeki wa Polisi na kumpiga chenga kipa wao, Tony Kavishe.

Mikosi iliendelea kuiandama Simba dakika ya 81 baada ya beki wake, Kessy Ramadhani kuumia vibaya goti na kutolewa nje ya uwanjani.

Saturday, February 14, 2015

STAND UNITED YAIFANYIZIA MGAMBO SHOOTINGTIMU ya Stand United imeichapa mabao 4-1 Mgambo Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kambarage Shinyanga.

Ushindi huo unakuja siku chache baada ya wachezaji wa timu hiyo kupewa mafundisho na kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya Uholanzi, Patrick Kluivert.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona alizuru Shinyanga wiki hii kufungua cha soka cha watoto katika sekondari ya Com na akapata fursa ya kuhudhuria mazoezi ya Stand United Uwanja wa Kambarage na kuwapa mawaidha

Katika mechi nyingine za Ligi Kuu, Mbeya City imelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Mtibwa Sugar nayo imetoka 0-0 na wenyeji Ndanda, Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

YANGA YAJIWEKA PAZURI MICHUANO YA AFRIKA


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burundi, Amisi Joselyn Tambwe leo ameibuka shujaa, baada ya kuifungia timu yake mabao yote mawili ikishinda 2-0 katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya Botswana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo, unaiweka Yanga SC katika mazingira mazuri ya kuingia hatua ya 32 Bora, ambako itamenyana na mshindi kati ya Sofapaka ya Kenya na Platinum ya Zimbabwe.

Tambwe alifunga bao la kwanza dakika ya kwanza tu kwa kichwa kufuatia krosi maridhawa ya winga Simon Msuva, ambaye alimtoka vizuri beki wa kulia wa BDF, Pelontle Lerole.

Baada ya bao hilo, Yanga SC ilitengeneza nafasi zaidi ya tatu nzuri, lakini ikashindwa kufunga. Kipindi cha pili, Yanga SC walirudi vizuri tena na kuendelea kusukuma mashambulizi langoni mwa BDF.

Hali hiyo ilizaa matunda dakika ya 55 baada ya Tambwe tena kufunga kwa kichwa akimalizia pasi nzuri ya Mrisho Khalfan Ngassa aliyempiga chenga beki wa BDF, Mompati Thuma.

Yanga SC waliendelea kulisakama lango la BDF, ambayo ilikuwa ikifanya mashambulizi ya kushitukiza yasiyo na madhara, lakini hawakufanikiwa kupata mabao zaidi. 

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe/Jerry Tegete dk82, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho/Kpah Sherman dk70.

BDF XI; Tukudzwa Ndoro, Pelontle Lerore, Othusitse Mpharitlhe, Kelegeste Mogomotsi, Mombati Thuma, Mosha Gaolaolwe, Master Masitara, Bonolo Phuduhudu, Vincent Nzombe/Kumbulani Madziba dk76, Thato Ogopotse na Kabelo Seakanyeng.

IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BINZUBEIRY.

Thursday, February 12, 2015

BOBBI KRISTINA AFUNGUA MACHO


NEW YORK, Marekani

HALI ya mtayarishaji wa vipindi vya televisheni na mwanamuziki nchini Marekani, Bobbi Kristina Brown imeanza kutia matumaini.

Bobbi Kristina jana alifumbua macho, baada ya kulazwa kwa zaidi ya wiki moja kwenye chumba cha wagonjwa wenye uangalizi maalumu (ICU).

Taarifa hizo bila shaka ni njema kwa Wamarekani ambao kwa takribani wiki moja wako katika maombezi maalumu ya kumuombea nyota huyo ambaye ni mtoto wa nyota wa zamani wa muziki, Bobby Brown.

Kinda huyo alikutwa ameanguka bafuni na chanzo cha tukio hilo kinafanyiwa uchunguzi na Polisi nchini humo ingawa mumewe, Nick Gordon, anatajwa kuhusika.

Shangazi wa Bobbi, Leolah Brown, amethibitisha taarifa za maendeleo mazuri ya mgonjwa huyo ambaye aliyekuwa mahututi tangu Januari 31 mwaka huu.

Alisema jana alikwenda kumuona katika Hospitali ya Emory University ambapo Bobbi alifumbua macho kwa mara ya kwanza.

Leolah alisema hali yake inaridhisha na familia ina imani nduyu yao atapona ingawa bado wanaendelea na maombi.

“Bado tuna majonzi makubwa lakini, Bobbi anaendelea vizuri na hali yake inatia matumaini kuwa huenda akapona na kurejea katika hali ya kawaida,” alisema shangazi huyo.

Juzi familia ya Bobbi iliwataka madaktari kuzima mashine inayomsaidia kupumua ili aweze kufa katika tarehe kama marehemu mama yake Whitney Houston.

Whitney alifariki dunia Februari 11, 2012 baada ya kukutwa ameanguka bafuni katika Hoteli ya Beverly Hilton na pembeni kukiwa na pakiti za dawa za kulevya.

MAZITO YAIBUKA SAKATA LA MSANII BOBBI KRISTINA

Mumewe apandishwa kizimbani, Yadaiwa alimpiga kabla ya tukio

NEW YORK, Marekani
MUME wa msanii Bobby Kristina, Nick Gordon, anatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu shitaka la makosa ya uzembe barabarani.

Pia mamalaka nchini hapa zinamchunguza kwa tuhuma za kumjeruhi, Bobbi Kristina ambaye ni mtoto wa mwanamuziki nguli wa zamani, Whitney Houston.

Marehemu Whiyney alizaa mtoto huyo na mwanamuziki mwingine mahiri, Boby Brown, ambaye ni gwiji wa kutumia dawa za kulevya.

Mahakama ya Fulton County State, leo inatarajia kutoa kibali cha kukamaktwa kwa Gordon iwapo atashindwa kuhudhuria kesi ya awali inayomkabili.

Mahakama hiyo inatarajia kutoa kibali hicho ikiwa ni wiki moja tangu Bobbi Kristina, alipokutwa amepoteza fahamu bafuni huku kichwa chake kikiwa ndani ya sinki lililokuwa limejaa maji.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali, polisi wa mjini hapa wamesema wana imani Gordon alimjeruhi mkewe kabla ya kutokea tukio hilo.

Tayari polisi wameanza kuchunguza mienendo ya uhusiano wa wawili hao, kabla ya Bobbi Kristina, kukutwa na tukio hilo, Jumamosi wiki iliyopita.

Aidha, mamlaka ya kiuchunguzi zimedai wanandoa hao wamekuwa na historia ya kushambuliana ambapo dakika 15 kabla ya tukio hilo walinaswa wakiwa kwenye malumbano makali.

Max Lomas ambaye ni rafiki wa Bobbi Kristina, alidai Gordon alifuta damu katika eneo la tukio zinazosadikiwa kuwa za mkewe.

Lomas alidokeza kuwa alilazimika kuingia nyumbani kwa Bobbi Kristina, baada ya kugonga mlango kwa muda kabla ya kuingia ndani baada ya kukosa mtu wa kumfungulia na kumkuta rafiki yake akiwa amepoteza fahamu bafuni.

Waaguzi katika hospitali aliyolazwa msanii huyo wa vipindi vya televisheni, wanasema hali yake sio nzuri na mjomba wake ameandika kwenye mtandao wa Instagram kuwa hali ya mpwa wake haileti matumaini.

Mjomba huyo alisema madaktari walimwambia ajiandae kupokea taarifa yoyote kwa kuwa hakuna matumaini Bobbi Kristina, kuokoa uhai wake. 

Hatua ya kupoteza fahamu, Bobbi Kristina, limeushtua ulimwengu kwa kuwa linafanana na tukio la kifo cha Whitney aliyefariki Februari 12, 2012.

Whitney alikutwa amefariki bafuni katika Hoteli ya Beverly Hilton huku kichwa chake kikiwa ndani ya maji.

Katika tukio hilo, polisi walikuta chupa za pombe, vyeti vya hospitali vilivyokuwa vikionyesha kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo na matumizi ya dawa za kulevya aina ya kokein.

Gordon na Bobby Kristina, walifunga ndoa Januari, mwaka jana licha ya ndoa hiyo kupingwa vikali na Bobby Brown kwa kuwa Godon ni mtoto wa kuasili wa Whitney.

Wednesday, February 11, 2015

AZAM YAIPA MTIBWA KIPIGO CHA PAKA MWIZI

MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Azam wamerejea kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Azam ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-1.

Matokeo hayo yameiwezesha Azam kufikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 13, sawa na Yanga, lakini zinatofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Washambuliaji Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu na kiungo Frank Domayo ndio walioiwezesha Azam kwenda mapumziko ikiwa kifua mbele baada ya kuifungia mabao hayo matatu. Bao la Mtibwa lilifungwa na Mussa Nampaka.

Mabao mengine ya Azam katika kipindi cha pili yalifungwa na Domayo na Tchetche wakati bao la pili la Mtibwa lilifungwa na Abdalla Juma.

Tuesday, February 10, 2015

TFF YAFANYA MAREKEBISHO KAMATI NDOGO ZA KISHERIA


 
JUDICIAL AND STANDING COMMITTEES.

Kamati ya Utendaji iliyoketi tarehe 19 Disemba 2014, ilifanya mabadiliko katika kamati ndogo ndogo na zile za kisheria. Kamati hizo ni kama ifuatavyo

KAMATI YA NIDHAMU
1.   Tarimba Abbas (Mwenyekiti)
2.   Advocate Jerome Msemwa ( Makamu mwenyekiti)
3.    Kassim Dau
4.   Nassoro Duduma
5.   Kitwana Manara 

KAMATI YA RUFANI YA NIDHAMU
1.   Advocate Mukirya Nyanduga (Mwenyekiti)
2.   Advocate Revocatus Kuuli (Makamu mwenyekiti)
3.   Abdala Mkumbura
4.   Dr. Franics Michael
5.   Advocate Twaha Mtengela
 
KAMATI YA MAADILI
1.   Advocate Wilson Ogunde (Mwenyekiti)
2.   Advocate Juma Nassoro (Makamu mwenyekiti)
3.   Advocate Ebenezer Mshana
4.   Geroge Rupia
5.   Mh. Said Mtanda

KAMATI YA RUFANI YA MAADILI
1.   Advocate Walter Chipeta (Mwenyekiti)
2.   Magistrate  George Kisagenta (Makamu mwenyekiti)
3.   Lilian Kitomari
4.   Advocate Abdala Gonzi

KAMATI YA UCHAGUZI
1.   Advocate Melchesedeck Lutema
2.   Advocate Adamu Mambi (Makamu mwenyekiti)
3.   Hamidu Mahmoud Omar
4.   Jeremiah John Wambura
5.   John Jembele

KAMATI YA RUFANI TA UCHAGUZI
1.   Advocate Julius Lugaziya (Mwneyekiti)
2.   Advocate Machare Suguta (Makamu Mwenyekiti)
3.   Idrisa Nassor
4.   Paschal Kihanga
5.   Benister Lugora

KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO
1.   Wallace Karia (Mwenyekiti)
2.   Yahya Mohamed (Makamu mwenyekiti)
3.   Goodluck Moshi
4.   Omar Walii
5.   Ellie Mbise
6.    Deo Lubuva

KAMATI YA MASHINDANO
1.   Geofrey Nyange (Mwenyekiti)
2.   Ahmed Mgoyi (Makamu mwenyekiti)
3.   James Mhagama
4.   Stewart Masima
5.   Steven Njowoka
6.   Said Mohamed

KAMATI YA UFUNDI
1.   Kidao Wilfred (Mwenyekiti)
2.   Athumani Kambi (Makamu mwenyekiti)
3.   Vedastus Rufano
4.   Dan Korosso
5.   Pelegriunius Rutahyugwa

KAMATI YA MPIRA WA MIGUU YA VIJANA
1.   Ayoub Nyenzi (Mwenyekiti)
2.    Khalid Abdallah (Makamu mwenyekiti)
3.    Ali Mayay
4.   Mulamu Ngh’ambi
5.   Said Tully

KAMATI YA MPIRA WA MIGUU WANAWAKE
1.   Blassy Kiondo (Mwenyekiti)
2.   Rose Kissiwa (Makamu mwenyekiti)
3.   Zena Chande
4.   Amina Karuma
5.   Zafarani Damoder
6.   Beatrice Mgaya
7.   Sofia Tigalyoma
8.   Ingrid Kimario (Katibu wa Kamati)

KAMATI YA WAAMUZI
1.   Saloum Umande Chama (Mwenyekiti)
2.   Nassoro Said (Makamu mwenyekiti)
3.   Charles Ndagala (Katibu)
4.   Kanali Issaro Chacha
5.   Soud Abdi

KAMATI YA HABARI NA MASOKO
1.   Athuman Kambi (Mwenyekiti)
2.   Alms Kasongo (Makamu Mwenyekiti)
3.   Rose Mwakitangwe
4.   Amir Mhando
5.   Haroub Selemani

KAMATI YA UKAGUZI WA FEDHA
1.   Ramdhan Nassib (Mwenyekiti)
2.   Epaphra Swai (Makamu mwenyekiti)
3.   Jackson Songora
4.   Golden Sanga
5.   Francis Ndulane
6.   Cyprian Kwiyava

KAMATI YA TIBA
1.   Dr. Paul Marealle (Mwenyekiti)
2.   Dr. Fred Limbanga (Makamu mwenyekiti)
3.   Dr. Mwanandi Mwankewa
4.   Dr. Eliezer Ndelema
5.   Asha Mecky Sadik

KAMATI YA FUTSAL NA BEACH SOCCER
1.   Ahmed Idd Mgoyi (Mwenyekiti)
2.   Hussein Mwamba (Makamu mwenyekiti)
3.   Samson Kaliro
4.   Shaffih Dauda
5.   Boniface Pawassa
6.   Apollo Kayugi

PRESIDENTIAL COMMISSION FOR AFFAIRS
1.   Omar Abdulkadir (Mwenyekiti)
2.   Emmanuel Chaula (Makamu mwenyekiti)
3.   Victor Mwandiki
4.   Riziki Majala
5.   Zahra Mohamed
6.   David Nyandu

PRESIDENTIAL COMMISSION ON BUSINESS AND INVESTMENTS
1.   William Erio (Mwenyekiti)
2.   Mbaraka Igangula
3.   Advocate Iman Madega
4.   Lt. Col Charles Mbuge
5.   Philemon Ntalihaja

KIONGOZI VILLA SQUAD APIGWA FAINI 600,000/-


Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imempiga faini ya sh. 600,000 au kifungo cha mwaka mmoja Katibu Mkuu wa Villa Squad, Mbarouk Kassanda kwa kuhusika na uhamisho wa mchezaji Omari Ramadhan ambao haukufuata kanuni za usajili.

Villa Squad iliingiza majina tofauti ya mchezaji huyo wa African Lyon, ambapo badala ya Omari Ramadhan ikaingiza Omari Issa Ibrahim'. Kamati imeona Villa Squad ilifanya hivyo ili kudanganya, kuwezesha mfumo wa usajili wa kielektroniki ukubali jina la mchezaji.

Malalamiko ya kutaka kupewa pointi tatu na mabao matatu kwenye mechi dhidi ya Villa Squad kwa kumchezesha mchezaji huyo, yametupwa na Kamati kwa sababu alikuwa ni mchezaji halali aliyethibitishwa (eligible) na TFF.

Kamati ilimuita mchezaji huyo na kumhoji kama alishiriki au alifahamu udanganyifu wa kubadili majina ili aweze kuingizwa katika mfumo wa eletroniki wa usajili lilibaki kuwa suala la mashaka. Inawezakana alishiriki au hakushiriki; Kamati haikupata ushahidi thabiti. Hivyo, Kamati iliamua kumpa mchezaji faida ya mashaka (benefit of doubts) na hivyo kutompa adhabu yoyote.

Kassanda ameadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 40(11) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) wakati Omari Ramadhan ni mchezaji wa African Lyon kwa vile ana mkataba na klabu hiyo.

JKT MLALE YATAKIWA KUILIPA LYON
Klabu ya JKT Mlale imeamriwa kuilipa African Lyon jumla ya sh. 600,000 ikiwa ni ada ya uhamisho na fidia kwa kumtumia mchezaji Noel Lucas kinyume cha taratibu kwenye mechi.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji baada ya kusikiliza malalamiko ya African Lyon ambapo ilibaini kuwa klabu hiyo ilikubali kulipwa sh. 300,000 ilikwa ni ada ya uhamisho.

Kamati imekataa maombi ya African Lyon kutaka pointi tatu na mabao matatu katika mechi yao ambapo Noel Lucas alicheza, kwa vile mchezaji huyo usajili huo ulithibitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Pia JKT Mlale imetakiwa kuilipa African Lyon sh. 300,000 nyingine za usumbufu wa kufuatilia malipo ya mchezaji huyo. JKT Mlale imetakiwa kulipa fedha hizo kabla ya mechi yake ya mwisho ya ligi

BEKI ALIYEMKABA KOO TAMBWE AFUNGIWA MECHI TATUKamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia mechi tatu beki George Michael Osei wa Ruvu Shooting kutokana na makosa ya kinidhamu aliyoyafanya akiwa uwanjani.

Osei ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumkaba na kumchezea kibabe mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe ambapo ni kinyume na mchezo wa kiungwana (fair play) ameadhibiwa kwa kuzingatia Ibara ya 48(1)(d) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.

Mlalamikiwa alifika mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi mchezaji Maguri kwa kitendo hicho.

Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa alisema Osei alipopewa nafasi ya kujitetea alikana kufanya kosa hilo na kudai magazeti yametengeneza picha hizo. TFF iliwasilisha ushahidi wa magazeti mawili ya Championi na moja la The Guardian kwa kuzingatia  Ibara ya 96(3) ya Kanuni ya Nidhamu ya TFF Toleo la 2012.

Katika uamuzi wake, Kamati imesema kitendo cha Osei ni kinyume na kanuni ya mchezo wa kiungwana (fair play), na kuongeza kuwa kanuni za TFF kwa makosa kama hayo ni dhaifu, hivyo kuagiza zirekebishwe ili ziweze kuwa kali zaidi.

Katika hatua nyingine Kamati hiyo, imetupa malalamiko yaliyowasilishwa na TFF dhidi Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Mugisha Galibona, na Katibu wa Simiyu (SIFA), Emmanuel Sorogo.

Kwa upande wa Sorogo, Kamati imesema baada ya kupitia vielelezo vya pande zote, hasa upande mlalamikiwa imeridhika kuwa hakushiriki katika kumpiga refa kwenye mechi ya Kombe la Taifa kwa Wanawake kati ya Shinyanga na Simiyu.

Badala yake aliyehusika ni Kocha wa Simiyu, Emmanuel Babu ambaye tayari uongozi umeshachukua hatua dhidi yake kwa kumsimamisha kwanza wakati akisubiri kufikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya SIFA.

Pia barua ya kumsimamisha kocha huyo ilitumwa kwa Katibu Mkuu wa TFF na Mkurugenzi wa Mashindano. Kamati imeyachukulia maneno ya mlalamikiwa kuwa ni sahihi ndiyo maana hayakupingwa na TFF, hivyo malalamiko dhidi ya mlalamikiwa hayana msingi na yametupwa.

Kwa upande wa Galibona ambaye ripoti za Kamishna na refa zilionyesha kuwa alishiriki kuhamasisha marefa kupigwa baada ya mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Polisi Mara FC na Mwadui FC, Kamati imesema mlalamikiwa aliwasilisha vielelezo vinne kuthibitisha kuwa hakuhusika.

Kamati imesema licha ya ripoti ya Saleh Mang'ola kumtaja Galibona, lakini maelezo ya refa huyo na msaidizi wake Rebecca Mulokozi waliyoandika Kituo cha Polisi baada ya tukio hilo hayakumtaja mlalamikiwa mahali popote.

Pia barua ya FAM kwenda TFF kuhusu matukio ya mechi hiyo yanamtoa hatiani mlalamikiwa, hivyo Kamati imeamuru kuwa malalamiko dhidi ya Galibona hayana msingi na yametupiliwa mbali.

KLABU ZATAKIWA KUOMBA LESENI TFF


Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliketi jana Jumapili tarehe 08 Februari, 2015 katika kikao chake cha kawaida.  Pamoja na kujadili maandalizi ya Mkutano Mkuu wa kawaida utakaofanyika Machi 14 na 15 mjini Singida, Kamati ilijadili na kuamua yafuatayo:-

1.Zoezi la utoaji leseni kwa vilabu litaanza kabla ya msimu wa ligi 2015/16.  Vilabu vitatumiwa fomu za maombi mapema iwezekanavyo ili viweke nyumba zao sawa na kuleta maombi.  Leseni za vilabu (club licence) ni agizo la CAF na FIFA katika kuhakikisha vilabu vinaendeshwa kwa weledi.  Baadhi ya maeneo yanayoagaliwa katika utoaji wa leseni ni pamoja na kuwepo kwa Sekretarieti, miundo mbinu ya mazoezi na mashindano, hadhi za kisheria (legal status) mikataba ya ajira n.k.

2.   Kamati ya Utendaji imeazimia kufanyika kwa mashindano ya Taifa Cup kwa upande wa
wanaume.  Sekretarieti ya TFF imetakiwa kufanya juhudi ili mashindao hayo yaweze kufanyika.

3.   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limetoa pongezi kwa Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii
(NSSF) kwa juhudi zake za kukuza soka la vijana kupitia mradi wake wa kuanzisha shule ya soka
(Academy) kwa ushirikiano na klabu ya Real Madrid ya Hispania.  Aidha Kamati ya Utendaji ya
TFF imeipongeza Kampuni ya Symbion na klabu ya Sunderland ya Uingereza kwa juhudi zao za
kuchangia maendeleo ya soka la vijana na mpira wa miguu kwa ujumla ikiwa ni kupitia mpango
wa kujenga shule ya soka (academy) uwezeshaji wa mashindano ya vijana chini ya miaka 13
(U-13) yatakayofanyika mwezi April, 2015 mjini Mwanza na ujenzi wa miundo mbinu ya soka na
michezo kwa ujumla.

Kamati ya Utendaji imewaomba wadau wengine kufuata mifano hiyo na kuchangia maendeleo ya
soka kwani kazi hii inategemeana ni kwa faida ya wadau mbali mbali.

4.   Kamati ya Utendaji ilipokea mabadiliko ya uwakilishi wa Chama cha Soka la Wanawake nchini (TWFA) yaliyotokana na kuondoka kwa Bi. Lina Kessy aliyekuwa Mwenyekiti wake.  Bi. Lina ameajiriwa kama Afisa michezo wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia.  Nafasi ya Mwenyekiti inachukuliwa na Bi. Rose Kisiwa ambaye hapo kabla alikuwa Makamu Mwenyekiti wa TWFA ataendelea kuwa Mwenyekiti mpaka hapo utakapokaa Mkutano Mkuu wa kawaida wa TWFA.

5.   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kuwepo kwa vitendo vya vurugu na utovu wa nidhamu katika mashindano mbalimbali yanayoendelea nchini.  TFF inatoa wito kwa wadau wote wa mpira wa miguu hususani viongozi wa vilabu kutilia mkazo elimu ya kujitambua ili wachezaji wajue kuwa wao ni hazina ya Taifa na kioo (taswira) cha jamii, hivyo waepuke vitendo vya utovu wa nidhamu ndani na nje ya uwanja.  Vitendo hivi si tu vinakwamisha maendeleo, bali pia vinawadharirisha wao, mpira wa miguu na jamii kwa ujumla.

Kufuatia matukio ya hivi karibuni na kuzingatia umuhimu wa kushughulikia masuala ya kinidhamu
kwa haraka na weredi, Kamati ya Utendaji imeteua ya Kamati ya kuangalia na kusimamia kanuni
za uendeshaji Ligi. Kamati hiyo itaundwa na wajumbe kutoka Bodi ya Ligi, Kurugenzi ya
mashindano, Kamati ya mashindano na kamati ya waamuzi.

                                                                                              
TFF YATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA FIF
Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TFF,  Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Rais Sidy Diallo wa Shirikisho la soka nchini Ivory  Coast (FIF) kwa kutwaa Ubingwa wa Mataifa Afrika.
Katika salam zake Bw. Malinzi amesema mafanikio hayo ya kutwaa Ubingwa wa Afrika
yametokana na juhudi za Rais huyo pamoja na Kamati yake ya Utendaji.

Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), familia ya mpira na watanzania kwa
ujumla wanawapa pongezi Shirikisho la mpira wa Miguu la Ivory Coast kwa kutwaa Ubingwa
huo wa Afrika kwa mara pili.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF amepeleka salamu za
rambirambi kwa Rais Mohamed Gamal wa Chama cha mpira wa miguu nchnii Misri (EFA ),kufuatia vifo vya mashabiki vilivyotokea mwishoni wa wiki katika mchezo uliowakutanisha  Zamalek na ENPPI.

Mashabiki wapatao ishirini na moja (22)  wameripotiwa kupoteza maisha katika vurugu hizo
zilizowahusisha mashabiki wa Zamalek na ENPPI na kupelekea Shirikisho la Soka nchini Misri
kuisimamisha michezo ya Ligi nchini humo.

Katika salam zake, kwa niaba ya TFF, familia ya mpira wa miguu na watanzania Rais Malinzi amewaomba wapenzi wa soka nchini Misri kuwa wavumilivu  katika kipindi hiki cha maombelezo ya vifo vya mashabiki hao.

TFF YAIPONGEZA CAF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za pongezi Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Bw Issa Hayatou kwa kufanikiwa kuandaa salama fainali za Mataifa Afika nchini  Equatorial Guinea bila ya kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola.

Katika salamu hizo kwenda kwa Bw Haytou na nakala yake kupitia Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) Bw Hicham El Amrani, Bw Malinzi amesema kwa pamoja analipongeza Shirikisho hilo na wenyeji wa michuano kwa kufanikiwa kuandaa mashindano hayo na kumalizika salama.

RATIBA YA MECHI ZIJAZO ZA LIGI KUUMECHI ZIJAZO LIGI KUU  
Feb 11, 2P15
Azam vs Mtibwa Sugar

Feb 14, 2015
Ndanda vs Mtibwa Sugar
Coastal Union vs Mbeya City
Stand United vs Mgambo Shooting

Feb 15, 2015
Polisi Morogoro vs Simba
Kagera Sugar vs JKT Ruvu

Feb 21, 2015
Mbeya City vs Yanga
Kagera Sugar vs JKT Ruvu
Ndanda vs Coastal Union
Mgambo Shooting vs Mtibwa Sugar

Feb 22, 2015
Stand United vs Simba
Azam vs Tanzania Prisons

Feb 25, 2015
Mbeya City vs Ruvu Shooting

BARCELONA NAO KUTUA BONGO, KUCHEZA NA MAGWIJI WA BONGO


KIKOSI cha magwiji wa Barcelona kitazuru Dar es Salaa Machi 28 mwaka huu kwa ajili ya mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya wachezaji nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, maarufu Tanzania Eleven.

Almasi Kasongo, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam, wanaoandaa ziara hiyo kwa ushirikiano na kampuni ya Prime Time Promotions amesema hayo leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari ukumbi wa City Sports Lounge, Dar es Salaam.

Mkutano huo, ulihudhuriwa na mkali wa zamani wa mabao wa Barcelona, Mholanzi Patrick Kluviert ambaye amethibitisha ujio wa nyota waliotaka Camp Nou miaka ya nyuma kidogo.

Ziara hiyo ni matunda ya ziara ya magwiji wa wapinzani wa Barcelona, Real Madrid Agosti mwaka jana, ambao pia walicheza na magwiji wa Tanzania na kushinda 3-1 Dar es Salaam.

WARUNDI, WASOMALI KUZICHEZESHA YANGA, AZAMMAREFA kutoka nchi jirani za Burundi na Somalia, ndio watachezesha mechi za kwanza za Raundi ya Awali ya michuano ya Afrika za timu za Tanzania mwishoni mwa wiki.

Yanga SC itamenyana na BDF XI Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Azam FC watakuwa wenyeji wa El Merreikh ya Sudan Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji.

Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Azam na El Merreikh refa atakuwa Hassan Mohamed Hagi, wasaidizi wake namba moja Bashir Sh Abdi Sule na namba mbili Salah Omar Abubakar wakati mezani atakuwa Kidane Melles Terfe, wote wa Somalia.Kamisaa wa mchezo huo atakuwa M.CHaileyesus Bazezew Beleti kutoka Ethiopia.

Mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Yanga SC na BDF XI, refa atakuwa Thierry Nkurunziza, wasaidizi wake Ramadhani Nijimbere namba moja, Herve Kakunze namba mbili na mezani George Gatogato, wote wa Burundi wakati Kamisaa atakuwa Joseph Nkole wa Zambia.

Monday, February 9, 2015

IVORY COAST MABINGWA WAPYA AFRIKA


IVORY Coast jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa soka barani Afrika baada ya kuichapa Ghana kwa penalti 9-8 katika mechi ya fainali iliyochezwa mjini Malabo, Equatorial Guinea.

Mshindi wa pambano hilo ilibidi apatikane kwa njia ya penalti tano tano baada ya timu hizo kumaliza dakika 120 zikiwa suluhu.

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Ivory Coast kutwaa taji hilo tangu 1992, ilipoishinda Ghana kwa staili hiyo hiyo ya penalti tano tano.

Kipa Boubacar Barry aliibuka shujaa wa Ivory Coast baada ya kufunga penalti ya mwisho na kisha kuokoa shuti la kipa mwenzake wa Ghana, Razak Braimah.

Pambano hilo lilikuwa na ushindani mkali kutokana na timu zote mbili kucheza kwa kasi na
nguvu, kila moja ikipania kutoka uwanjani na ushindi.

Sunday, February 8, 2015

YANGA MWENDO MDUNDOMSHAMBULIAJI Mrisho Ngasa jana aliibuka shujaa wa Yanga baada ya kuifungia mabao mawili katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga iliichapa Mtibwa Sugar mabao 2-0 na kurejea kileleni mwa ligi hiyo.

Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Ngasa tangu aliporejea nchini kutoka Afrika Kusini, alikokwenda kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa.

Ngasa alifunga mabao hayo katika kipindi cha pili baada ya kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya Kpah Sherman.

Mshambuliaji huyo aliyewahi kuzichezea Azam na Simba, alifunga bao la kwanza dakika ya 55 baada ya kupokea pasi maridhawa kutoka kwa Simon Msuva.

Nyota huyo wa timu ya taifa, Taifa Stars, aliongeza bao la pili dakika ya 62 baada ya kuwachambua mabeki wa Mtibwa kabla ya kufumua shuti lililompita kipa Said Mohamed.

Ushindi huo wa Yanga ni wa pili mfululizo na umekuja siku chache baada ya kuichapa Coastal Union bao 1-0 wiki iliyopita mjini Tanga.

Saturday, February 7, 2015

SIMBA YALE YALE DROO KWA KWENDA MBELE AU KUFUNGWAMabingwa wa kombe la Mapinduzi, Simba ya Dar es Salaam leo imegawana pointi na Mbwa Mwitu wa Tanga, Coast Union katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana.

Wanyama hao wa mwituni wamemaliza dakika 90 za kusukuma gozi la ng'ombe bila goli hata la kuotea. Coast Union  siku kadhaa zilizopita iliambulia kichapo cha goli moja kutoka kwa Yanga ya Dar  es Salaam.

Kikosi cha Simba SC kiliwakilishwa dimbani na: Ivo Mapunda, Kessy Ramadhani, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Simon Sserunkuma/Messi dk79, Abdi Banda, Dan Sserunkuma/Ibrahim Hajibu dk88, Elias Maguri na Emmanuel Okwi.

Kikosi cha Coastal Union wao ilikuwa: Shaaban Kado, Mbwana Hamisi, Othman Tamim, Abdallah Mfuko/Hamad Juma dk59, Juma Lui, Abdulhalim Humud, Joseph Mahundi/Itubu Imbem dk86, Godfrey Wambura, Bright Ike Obinna/Mohammed Mtindi dk66, Hussein Sued na Rama Salim.

DRFA YATAJA RATIBA 18 BORAChama cha soka mkoa wa Dar es Salaam DRFA,kimetaja makundi ya timu zitakazoshiriki kucheza hatua ya 18 bora (hatua ya pili) ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam,inayotarajia kuanza kutimua vumbi mapema mwezi huu.
Katika kundi (A) limepangwa kuwa na timu za Simba U20,Red Coast,Sifa UTD,Shababi,Ukonga UTD,Zakhem,Ugimbi,Beirahotspurs na Pan Africa.
Katika kundi (B) litakuwa na timu za Yanga U20,Stakishari,FFU,New Kunduchi,Sinza Stars,Changanyikeni,Tuamoyo,Sifapilitan na Azania Unga.
Ligi hiyo ya mkoa wa Dar es Salaam iliyokuwa na jumla ya timu 36,imeingia katika hatua ya pili,ambayo  itaanza Februari 11 mwaka huu katika viwanja mbalimbali ,ambapo kwa upande wa kundi (A)

Simba U20    vs    Red Coast       (Karume)
Sifa UTD         vs   Shababi           (Mwl/Nyerere)
Ukonga UTD  vs   Zakhem           (Airwing)
Ugimbi           vs   Beirahospurs  (Bandari)
KATIKA KUNDI (B) Februari 12
Yanga U20    vs   Stakishari          (Karume)
FFU                vs  New Kunduchi   (Benjamini Mkapa)
Sinza Stars    vs  Changanyikeni   (Kines)
Tuamoyo      vs  Sifapolitan          (Bandari)
Viongozi wa DRFA bado wanatoa wito kwa viongozi wa vilabu mbalimbali,mashabiki na wakazi wa jiji pamoja na maeneo ya jirani,kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya wachezaji.

NYOSO, MORRIS WAPEWA ADHABU KALI


 Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
 imewafungia kati ya mechi tatu na nane wachezaji Juma Nyoso wa Mbeya City
 na Aggrey Morris wa Azam kutokana na makosa ya kinidhamu waliyoyafanya
 wakiwa uwanjani.

Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji
 mshambuliaji Elias Maguri wa Simba amefungiwa mechi nane za Ligi Kuu ya
 Vodacom (VPL). Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 57 na Ibara ya
 11 (f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.

 Akiwa mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 5 mwaka huu) jijini Dar es
 Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi
 mchezaji Maguri kwa kitendo hicho.

Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa
 alisema kitendo kilichofanywa na Nyoso ni kosa kubwa, kudhalilisha utu wa
 mtu, na ni mfano mbaya kwa watoto na jamii nzima ya mpira wa miguu. Naye Morris amefungiwa mechi tatu za VPL baada ya kutiwa hatiani kwa
 kumpiga mshambuliaji Emmanuel Okwi wakati timu hizo zilipopambana kwenye
 mechi ya ligi iliyochezwa Januari 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
 Salaam. Kabla ya kusoma uamuzi, Wakili Msemwa alisema mlalamikiwa Morris alikiri
 kugongana na Okwi, kwa maelezo kuwa aliingia kwenye 'reli' ndiyo ukatokea
 mgongano huo.

Kamati baada ya kupitia malalamiko ya klabu ya Simba, ripoti za Brain CT
 scan kutoka Besta Diagnostic Centre na nyingine kutoka Taasisi ya Mifupa
 Muhimbili (MOI), taarifa za madaktari zilionyesha Okwi aligongwa kichwani
 akiwa anacheza mpira na kuzimia kwa dakika tano, pia mkanda wa video
 uliowasilishwa na TFF imeona kulikuwa na kugongana kati ya wachezaji hao.

 Hivyo, Kamati ikamtia hatiani Morris kwa kutumia Ibara ya 48(1)(d) ya
 Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012 kwa kumfungia mechi hizo tatu na
 kumpa onyo kali.

 Pia Kamati hiyo imemfungia miezi sita na kumpiga faini ya sh. 200,000
 Meneja Vifaa (Kit Manager) wa timu ya Polisi Mara, Clement Kajeri kwa
 kuhamamisha vurugu na kuwapiga waamuzi kwenye mechi dhidi ya Mwadui
 iliyochezwa Uwanja wa Karume mjini Musoma. Adhabu hiyo imetolewa kwa
 kuzingatia kanuni ya 40(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.

 Wachezaji watatu wa Friends Rangers; Mahmoud Othman, Khalid Twahil na John
 Alexander wamefungia miezi sita na faini ya sh. 500,000 kila mmoja kwa
 kumpiga mwamuzi kwenye mechi ya Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Majimaji.

 Licha ya wachezaji hao kuitikia mwito wa Kamati, wachezaji hao walizuiwa na
 viongozi wa kuingia ukumbini wakati malalamiko dhidi yao yalipoanza
 kusikilizwa. Hatua hiyo iliifanya Kamati ifanye uamuzi baada ya kuusikiliza
 upande wa walalamikaji pekee.

 Shauri dhidi ya mchezaji George Michael wa Ruvu Shooting kwa kumchezea
 ubabe Amisi Tambwe wa Yanga, Kamati imeliahirisha baada ya mlalamikiwa
 kupata udhuru uliosababisha asiwepo.

 Pia Kamati ya Nidhamu imeelekeza malalamiko ya timu ya Friends Rangers
 kupinga refa kuchezesha mechi yao dhidi ya Majimaji kwenye mvua kubwa,
 kutoa maamuzi yasiyo halali na kutokuwepo na ukweli kwenye ripoti ya
 Kamishna yakasikilizwe na Bodi ya Ligi kwa vile si masuala ya kinidhamu.

Wednesday, February 4, 2015

YANGA YAISULUBU COASTAL UNION MKWAKWANI


BAO lililofungwa na beki wa kati Nadir Haroub 'Cannavaro' jana liliiwezesha Yanga kukata ngebe za wapinzani wao Coastal Union baada ya kuichapa bao 1-0.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Cannavaro alifunga bao hilo dakika ya 11 kwa kichwa, akiunganisha mpira uliorushwa na beki mwenzake, Mbuyu Twite kutoka pembeni ya uwanja.

Kwa ushindi huo, Yanga sasa imetwaa uongozi wa ligi kuu, ikiwa na pointi 22 na kuwashusha waliokuwa wakiongoza Azam. Timu mbili hizo zinatofautiana kwa pointi moja huku Azam ikiwa na mchezo mmoja kibindoni.

Ikicheza mbele ya maelfu ya mashabiki wake, Coastal Union ililianza pambano hilo kwa kasi na kufanya mashambulizi kadhaa kwenye lango la Yanga, lakini umaliziaji mbovu ulikuwa kikwazo kupata bao.

Monday, February 2, 2015

USAJILI WA DIRISHA DOGO LIGI KUU YA ENGLAND HUU HAPA


Arsenal yamnyakua kiungo mkabaji kinda wa miaka 17,  Krystian Bielik na beki wa kati, Gabriel Paulista
Manchester United yamsajili kipa Victor Valdes
Sunderland yaimarisha kikosi chake kwa kumsajili Jermain Defoe
Liverpool haijafanya usajili wowote wa dirisha dogo
West Brom yamnyakua Callum McManaman kutoka Wigan
Yaya Sanogo ajiunga na Crystal Palace

ARSENAL
WALIOSAJILIWA

Gabriel Paulista (Villarreal, £11.2m)
Krystian Bielik (Legia Warsaw, £2.5m) 

WALIOONDOKA
Benik Afobe (Wolves, ada haikutajwa)
Lukas Podolski (Inter Milan, mkopo)
Yaya Sanogo (Crystal Palace, mkopo)
Joel Campbell (Villarreal, mkopo) 

ASTON VILLA
WALIOSAJILIWA

Carles Gil (Valencia, £3.25m)
Scott Sinclair (Manchester City, mkopo)

WALIOONDOKA
Darren Bent (Derby, mkopo)
Gary Gardner (Nottingham Forest, mkopo)
Chris Herd (Wigan, mkopo)
Callum Robinson (Preston, mkopo)

BURNLEY
WAlIOSAJILIWA

Michael Keane (Manchester United, ada haikutajwa)

WALIOONDOKA
Hakuna

CHELSEA
WALIOSAJILIWA

Juan Cuadrado (Fiorentina, £27m)

WALIOONDOKA
Andre Schurrle (Wolfsburg, £24m)
Ryan Bertrand (Southampton, £10m)
Mark Schwarzer (Leicester, huru)
Thomas Kalas (Middlesbrough, mkopo)
John Swift (Swindon, mkopo)
Lewis Baker (Sheffield Wednesday, mkopo)
Marko Marin (Anderlecht, mkopo)
Mohamed Salah (Fiorentina, mkopo)

CRYSTAL PALACE
WALIOSAJILIWA

Wilfried Zaha (Manchester United £6m)
Jordon Mutch (QPR, £5.75m)
Lee Chung-yong (Bolton, ada haikutajwa)
Keshi Anderson (Barton Rovers, £35,000)
Shola Ameobi (Gaziantep, huru)
Pape Souare (Lille, ada haikutajwa)
Yaya Sanogo (Arsenal, mkopo)

WALIOONDOKA
Stuart O'Keefe (Cardiff, ada haikutajwa)
Alex Wynter (Colchester, ada haikutajwa)
Zeki Fryers (Rotherham, mkopo)
Lewis Price (Crawley, mkopo)
Jake Gray (Cheltenham, mkopo) 
Barry Bannan (Bolton, mkopo)
Jimmy Kebe (huru)

EVERTON
WALIOSAJILIWA

Aaron Lennon (Tottenham, mkopo)

WALIOONDOKA
Samuel Eto'o (Sampdoria, huru)
Chris Long (Brentford, mkopo) 
Conor McAleny (Cardiff, mkopo)

HULL CITY
WALIOSAJILIWA

Dame N'Doye (Lokomotov Moscow, £3m)

WALIOONDOKA
Tom Ince (Derby County, mkopo)

LEICESTER CITY
WALIOSAJILIWA

Andrej Kramaric (Rijeka, £9.5m)
Mark Schwarzer (Chelsea, huru)
Robert Huth (Stoke City, mkopo)

WALIOONDOKA
Tom Hopper (Scunthorpe, mkopo)

LIVERPOOL
WALIOSAJILIWA

Hakuna

WALIOONDOKA
Oussama Assaidi (Al Ahli, £4.7m)
Suso (AC Milan, £1m) 

MANCHESTER CITY
WALIOSAJILIWA
 
Wilfried Bony (Swansea, £28m)

WALIOONDOKA
Matija Nastasic (Schalke, mkopo)
Scott Sinclair (Aston Villa, mkopo) 

MANCHESTER UNITED
WALIOSAJILIWA

Victor Valdes ( huru)
Sadiq El Fitouri (Salford City, huru)
Andy Kellett (Bolton, mkopo)

WALIOONDOKA
Wilfried Zaha (Manchester United, £6m)
Michael Keane (Burnley, £3m)
Darren Fletcher (West Brom, huru)
Will Keane (Sheffield Wednesday, mkopo)
Ben Amos (Bolton, mkopo)
Jesse Lingard (Derby County, mkopo)

NEWCASTLE UNITED
WALIOSAJILIWA

Hakuna

WALIOONDOKA
Mapou Yanga-Mbiwa (Roma, £5.2m)
Hatem Ben Arfa (huru)
Gael Bigirimana (Rangers, mkopo)
Haris Vuckic (Rangers, mkopo)
Shane Ferguson (Rangers, mkopo)
Davide Santon (Inter Milan, mkopo)

QUEENS PARK RANGERS
WALIOSAJILIWA
 
Mauro Zarate (West Ham, mkopo)
Ryan Manning (Galway United, huru)

WALIOONDOKA
Jordon Mutch (Crystal Palace, £5.75m)
Bruno Andrade (Stevenage, mkopo)

SOUTHAMPTON
WALIOSAJILIWA

Ryan Bertrand (Chelsea, £10m)
Eljero Elia (Werder Bremen, mkopo)
Filip Djuricic (Benfica, mkopo)

WALIOONDOKA
Jack Cork (Swansea, £3m)
Jos Hooiveld (Millwall, mkopo)
Artur Boruc (Bournemouth, mkopo)

STOKE CITY
WALIOSAJILIWA

Philipp Wollscheid (Bayer Leverkusen, mkopo)

WALIOONDOKA
Ryan Shotton (Derby, ada haikutajwa)
Maurice Edu (Philadelphia Union, ada haikutajwa)
Robert Huth (Leicester City, mkopo)

SUNDERLAND
WALIOSAJILIWA

Jermain Defoe (Toronto, ada haikutajwa)

WALIOONDOKA

Jozy Altidore (Toronto, ada haikutajwa)
Mikael Mandron (Shrewsbury, mkopo)
Charis Mavrias (Panathinaikos, mkopo)
Cabral (huru)

SWANSEA CITY
WALIOSAJILIWA
 
Kyle Naughton (Tottenham, £5m)
Jack Cork (Southampton, £3m)
Matt Grimes (Exeter City, £1.75m)
Nelson Oliveira (Benfica, mkopo) 

WALIOONDOKA
Wilfried Bony (Manchester City, £28m)
Rory Donnelly (Tranmere, mkopo)
Jazz Richards (Fulham, mkopo)

TOTTENHAM HOTSPUR 
WALIOSAJILIWA

Dele Alli (MK Dons, £5m)

WALIOONDOKA
Kyle Naughton (Swansea, £5m)
Aaron Lennon (Everton, mkopo)
Milos Veljkovic (Charlton, mkopo)
Benoit Assou-Ekotto (huru)
Dele Alli (MK Dons, mkopo)

WEST BROMWICH ALBION
WALIOSAJILIWA 

Callum McManaman (Wigan, £4.75m)
Darren Fletcher (Manchester United, huru)

WALIOONDOKA

Luke Daniels (Scunthorpe, ada haikutajwa)

WEST HAM UNITED
WALIOSAJILIWA

Doneil Henry (Apollon Limassol, ada haikutajwa)

WALIOONDOKA

Mauro Zarate (QPR, mkopo)
Ricardo Vaz Te (huru)

FRANCIS CHEKA AFUNGWA JELA


NA LATIFA GANZEL, MOROGORO,

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro, imemhukumu bondia nguli nchini, Francis  Cheka, kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela, baada ya kumtia hatiani kwa kosa  la shambulio  na  kudhuru mwili.

Cheka alihukumiwa kifungo hicho jana baada ya Hakimu Mkazi, Said Msuya, kumtia hatiani kwa kosa la kumshambulia na kumdhuru mwili aliyekuwa  Meneja wa baa yake, Bahati Kabanda.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Cheka anadaiwa kutenda  kosa  hilo  Julai  2,  mwaka  jana,  katika  eneo  la kata  ya  Uwanja  wa Taifa,  Manispaa  ya Morogoro.

Bondia huyo anadaiwa   kumpiga aliyekuwa  meneja wa  baa   yake   ilijulikanayo   kwa  jina  la  Vijana Social Hall  na kusababisha  kumdhuru sehemu mbalimbali za   mwili.

Akisoma hukumu hiyo, Hakima  Msuya alisema mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela na baada ya kumaliza kutumikia adhabu hiyo,  atatakiwa  kumlipa mlalamikaji gharama ya sh. milioni moja ya matibabu alizojitibia  baada  ya kupigwa  na  bondia huyo.

Akizungumza baada ya kupewa adhabu hiyo, Cheka alidai  kuna mkono wa   watu  wenye  lengo  la  kutaka  kuchafua  jina  lake   na maisha  yake .

Cheka alidai kushangazwa  kusomewa  kuwa  alikiri  kosa  la  kumpiga  mlalamikaji wakati  yeye  katika maelezo  yake  alikana shitaka.

"Ni  wazi kesi  yangu  ilipangwa  kuvurugwa  ili nifungwe na  kunipoteza  katika  ulimwengu wa  masumbwi," alidai.

Kocha wa bondia huyo, Abdallah  Komando, alidai  kuwa  kifungo cha  bondia  wake  kimemtia  simanzi  kubwa,   kwa kuwa kesi hiyo ingeweza kumalizika mezani.

Komando alisema kifungo cha bondia wake ni matokeo ya fitna za  kimichezo.

MANJI AONYESHA JEURI YA FEDHA, KUDHAMINI KOMBE LA EBOLA KWA DOLA 500,000 ZA MAREKANI

MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji ametenga kiasi cha dola 500,000 kwa ajili ya michuano ya Ebola  Cup itakayoshirikisha timu 108 za Afrika.

Katika michuano hiyo Tanzania itawakilishwa na Yanga pamoja na mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Azam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Yanga, Katibu Mkuu wa klabu hiyo Jonas Tibohora  alisema hatua za kuanza michuano hizo zipo kwenye hatua nzuri.

Alisema michuano hiyo imeandaliwa kwa ajili ya  kuchangisha fedha  zitakazowasaidia waafrika walioathirika na ugonjwa wa Ebola.

Alisema michuano hiyo itasimamiwa na Chama cha Soka Afrika (CAF), na kwamba kwa sasa kamati ya michuano hiyo yenye wajumbe mchanganyiko kutoka nchi wanachama wa CAF itakaa na kupanga tarehe ya michuano hiyo.

Alisema michuano hiyo itachezwa kwa mtindo wa makundi ambapo kutakuwa na makundi 16 na kila kundi litakuwa na timu kati ya nne na saba.

Alisema michuano hiyo itashirikisha timu zote kutoka Afrika ambazo ni mwanachama wa CAF ambapo kila nchi itatoa timu mbili na michuano itachezwa nyumbani na ugenini.

Alisema  kila timu zitachangia kiasi cha dola 100,000 kama ada ya ushiriki ambazo zitaingizwa moja kwa moja katika mfuko wa kusaidia waathirika hao.

"Mpango huu yatari umepitishwa na kinachofuata ni kupangwa kwa tarehe ya michuano ambapo kamati ya mashindano inayoongozwa na Mwenyekiti wake Machache Shipanda kutoka Zambia itakutana na kutoa ratiba,"alisema Tibohora.

Alisema pia mpango huo umeungwa mkona na umoja wa Afrika (AU) ambao watashirikiana kwa pamoja kuhakikisha michuano hiyo inafanyika kwa manufaa makubwa.

DRFA YAIFAGILIA TEMEKE KUTWAA KOMBE LA TAIFA LA WANAWAKE


 Chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA, kimeipongeza timu ya Temeke kwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Taifa la Wanawake,baada ya kuifunga Pwani kwa bao 1-0,kwenye mchezo wa fainali uliopigwa Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Azam Complez, Chamazi.

Katika fainali hiyo iliyohudhuriwa na Waziri mwenye dhamana ya michezo Dk.Fenella Mukangara,Temeke ilijipatia bao lake dakika ya  66 kupitia kwa mchezaji wao Neema Paul.

Temeke walifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuwafunga ndugu zao Ilala kwa mabao 4-0,huku Pwani wakitinga hatua hiyo kwa kuifunga Kigoma mabao 3-2.

Mshindi amejinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu, makamu bingwa sh. milioni mbili, wakati mshindi wa tatu ameondoka na sh. milioni moja.

Mbali na Temeke kubeba ubingwa,pia imefanikiwa kutoa mlinda mlango bora, Belina Julius aliyezawadiwa kitita cha shilingi 500,000/-.

Mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliwakutanisha, Ilala dhidi ya Kigoma, ambapo Ilala ilifanikiwa kuchukua nafasi ya tatu baada ya kushinda mabao  3-0.

Uongozi wa DRFA,unatoa shukurani kwa mashabiki wa mkoa wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani,ambao wamejitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo na kuwaomba waendelee kuwa na moyo huo ili kuongeza hamasa kwa wachezaji.

TFF YATUMA RAMBIRAMBI MSIBA WA KATIBU IRFAShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya msiba wa Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA), John Ambwene Mwakalobo uliotokea jana (Februari 1 mwaka huu) mkoani Iringa baada ya kuanguka akiwa nyumbani kwake.

Msiba huo ni pigo kwa wadau wa mpira wa mpira wa miguu kwani wakati wa uhai wake, Mwakalobo alitoa mchango mkubwa akiwa kiongozi. Mwaka 2011 alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa IRFA, kabla ya 2012 kushinda nafasi ya Katibu Msaidizi.

Alizaliwa Februari 4, 1954 na kupata elimu ya sekondari katika shule ya Azania, Dar es Salaam na baadaye mafunzo ya ualimu kwenye Chuo cha Ualimu Mpwapwa mkoani Dodoma. Alianzia kazi ya ualimu Newala mkoani Mtwara kabla ya kuhamia mkoani Iringa mwaka 1981. Alistaafu mwaka 2013.

TFF inatoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu kwa msiba huo.

Marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho (Februari 3 mwaka huu) kwao Kyela mkoani Mbeya. Ameacha mke, watoto wanne na mjukuu mmoja. Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

MECHI ZA MWISHO FDL SASA FEB 8 NA 10

 Mechi za raundi mbili za mwisho za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa makundi yote mawili zimerudishwa nyuma kutokana na maombi ya klabu hizo kupungaza gharama za kuendelea kuziweka kambini timu zao.

Hivyo, Februari 8 mwaka huu kundi A litacheza mechi zake za raundi ya 21 wakati zile za raundi 22 ambayo ndiyo ya mwisho zitafanyika Februari 13 mwaka huu. Mechi za Februari 8 ni KMC vs African Lyon, Kurugenzi vs African Sports, Majimaji vs JKT Mlale, Kimondo vs Friends Rangers, Ashanti United vs Villa Squad, Polisi Dar vs Lipuli.

Februari 13 mwaka huu ni African Lyon vs Polisi Dar, Kurugenzi vs Lipuli, Kimondo vs Majimaji, JKT Mlale vs Ashanti United, Friends Rangers vs African Sports, na Villa Squad vs KMC.

Kwa upande wa kundi B wataanza mechi za raundi 22 Februari 10 mwaka huu ili kupisha mechi za viporo za Polisi Mara zinazomalizika Februari 5 mwaka huu. Hivyo, Februari 10 mwaka huu itakuwa ni Burkina Faso vs JKT Kanembwa, Mwadui vs Polisi Tabora, Polisi Dodoma vs Green Warriors, Rhino Rangers vs JKT Oljoro, Panone vs Polisi Mara, Geita Gold vs Toto Africans.

Raundi ya 22 itachezwa Februari 15 mwaka huu kwa mechi kati ya JKT Kanembwa vs Green Warriors, Mwadui vs Burkina Faso, Polisi Tabora vs JKT Oljoro, Polisi Dodoma vs Panone, Toto Africans vs Rhino Rangers, na Geita Gold vs Polisi Mara.  

KIPA BORA WANAWAKE AZAWADIWA 500,000/-

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Temeke baada ya kuibuka washindi wa mashindano ya Proin Women Taifa Cup, ambayo yalichezwa katika Dimba la Azam huku Proin Promotions na Azam wakidhamini mashindano hayo.


Nahodha wa Timu ya Pwani akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni mbili ambazo ni zawadi ya mshindi wa pili katika Mashindano ya Proin Women Taifa Cup na kumalizika kwa Temeke kuwa mabingwa kwa kuifunga Pwani goli 1- 0.
Nahodha wa Timu ya Ilala ambao ni washindi wa tatu akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja ambayo mshindi wa tatu katika mashindano hayo ni Ilala
 Na Mwandishi Wetu
Kipa bora wa michuano ya Kombe la Taifa la Wanawake, Belina Julius wa Temeke amezawadiwa sh. 500,000 na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara.

Dk Mukangara alitoa zawadi hiyo baada ya mechi ya fainali ya michuano iliyomalizika jana kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam. Dk Mukangara alikuwa mgeni rasmi kwenye fainali hiyo.

Temeke ndiyo walioibuka mabingwa wa michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini baada ya kuilaza Pwani bao 1-0 katika fainali iliyoonyeshwa moja kwa moja (live) na televisheni ya Azam.

Ilala ilifanikiwa kutwaa baada ya kuichapa Kigoma mabao 3-0. Bingwa amepata sh. milioni tatu, makamu bingwa sh. milioni mbili wakati mshindi wa tatu ameondoka na sh. milioni moja katika michuano hiyo iliyodhaminiwa na kampuni ya Proin.