KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, February 16, 2015

SIMBA YANGURUMA MOROGORO


SIMBA imepoza machungu ya mashabiki wake baada ya jana kuichapa Polisi Moro mabao 2-0 katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Iliwachukua Simba dakika 14 kuhesabu bao la kwanza lililofungwa na mshambuliaji chipukizi Ibrahim Hajibu baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa beki Juuko Murshid na kuwatoka mabeki wa Polisi.

Simba ilipata pigo dakika ya 56 baada ya kipa wake Ivo Mapunda kuzimia uwanjani baada ya kugongana na mchezaji mmoja wa Polisi. Ilibidi kipa huyo atolewe uwanjani na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.Nafasi yake ilichukuliwa na Manyika Peter.

Bao la pili la Simba lilifungwa na Elias Maguri dakika ya 63 baada ya kuwatoka mabeki wa Polisi na kumpiga chenga kipa wao, Tony Kavishe.

Mikosi iliendelea kuiandama Simba dakika ya 81 baada ya beki wake, Kessy Ramadhani kuumia vibaya goti na kutolewa nje ya uwanjani.

No comments:

Post a Comment