KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, February 23, 2015

MWADUI FC BINGWA LIGI DARAJA LA KWANZA (FDL)


Timu ya Mwadui kutoka mjini Shinyanga,inayofundishwa na Kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio' jana ilitawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kuifunga timu ya African Sports ya jijini Tanga kwa bao 1 - 0, katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Comlex Chamazi jijni Dar es Salaam.

Bao pekee na la ushindi kwa timu ya Mwadui lilifungwa na mshambulaji Kelvin Sabato Kongwe dakika ya 53 ya mchezo na kuihakikishia Mwadui ushindi katika mchezo huo wa fainali.

Mabingwa hao wapya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) walizawadia Kombe la Ubingwa, medali pamoja na hundi ya sh.millioni tatu, huku timu ya African Sports ikipata medali na hundi ya sh. millioni mbili.

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF linaipongeza timu ya Mwadui kwa kuibuka Bingwa mpya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/205.

Jumla ya timu nne zimepanda Ligi Kuu msimu ujao ambazo ni  bingwa Mwadui FC, African Sports, Majimaji na Toto Africans.

No comments:

Post a Comment