KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, February 4, 2015

YANGA YAISULUBU COASTAL UNION MKWAKWANI


BAO lililofungwa na beki wa kati Nadir Haroub 'Cannavaro' jana liliiwezesha Yanga kukata ngebe za wapinzani wao Coastal Union baada ya kuichapa bao 1-0.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Cannavaro alifunga bao hilo dakika ya 11 kwa kichwa, akiunganisha mpira uliorushwa na beki mwenzake, Mbuyu Twite kutoka pembeni ya uwanja.

Kwa ushindi huo, Yanga sasa imetwaa uongozi wa ligi kuu, ikiwa na pointi 22 na kuwashusha waliokuwa wakiongoza Azam. Timu mbili hizo zinatofautiana kwa pointi moja huku Azam ikiwa na mchezo mmoja kibindoni.

Ikicheza mbele ya maelfu ya mashabiki wake, Coastal Union ililianza pambano hilo kwa kasi na kufanya mashambulizi kadhaa kwenye lango la Yanga, lakini umaliziaji mbovu ulikuwa kikwazo kupata bao.

No comments:

Post a Comment