KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, February 11, 2015

AZAM YAIPA MTIBWA KIPIGO CHA PAKA MWIZI

MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Azam wamerejea kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Azam ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-1.

Matokeo hayo yameiwezesha Azam kufikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 13, sawa na Yanga, lakini zinatofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Washambuliaji Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu na kiungo Frank Domayo ndio walioiwezesha Azam kwenda mapumziko ikiwa kifua mbele baada ya kuifungia mabao hayo matatu. Bao la Mtibwa lilifungwa na Mussa Nampaka.

Mabao mengine ya Azam katika kipindi cha pili yalifungwa na Domayo na Tchetche wakati bao la pili la Mtibwa lilifungwa na Abdalla Juma.

No comments:

Post a Comment