KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, February 7, 2015

SIMBA YALE YALE DROO KWA KWENDA MBELE AU KUFUNGWA



Mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Simba ya Dar es Salaam leo imegawana pointi na Mbwa Mwitu wa Tanga, Coast Union katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana.

Wanyama hao wa mwituni wamemaliza dakika 90 za kusukuma gozi la ng'ombe bila goli hata la kuotea. Coast Union  siku kadhaa zilizopita iliambulia kichapo cha goli moja kutoka kwa Yanga ya Dar  es Salaam.

Kikosi cha Simba SC kiliwakilishwa dimbani na: Ivo Mapunda, Kessy Ramadhani, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Simon Sserunkuma/Messi dk79, Abdi Banda, Dan Sserunkuma/Ibrahim Hajibu dk88, Elias Maguri na Emmanuel Okwi.

Kikosi cha Coastal Union wao ilikuwa: Shaaban Kado, Mbwana Hamisi, Othman Tamim, Abdallah Mfuko/Hamad Juma dk59, Juma Lui, Abdulhalim Humud, Joseph Mahundi/Itubu Imbem dk86, Godfrey Wambura, Bright Ike Obinna/Mohammed Mtindi dk66, Hussein Sued na Rama Salim.

No comments:

Post a Comment