KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, July 29, 2017

MALINZI AWATAKIA HERI WAJUMBE WA MKUTANO MKUU TFF



MSUVA ATAMBULISHWA RASMI NA KLABU YAKE YA MOROCCO



Kiungo mshambuliaji wa Tanzania Simon Msuva ametambulishwa rasmi na klabu yake mpya Difaa Hassani El Jadidi ya Morocco baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo.

Msuva aliondoka nchini mwanzoni mwa wiki hii, kwenda Morocco ambako atakuwa na mtanzania mwingine Ramadhani Singano ‘Messi’, ambaye alifika Morocco mapema kuliko Msuva aliyekuwa na majukumu kwenye timu ya taifa.

MASHINDANO YA KIGWANGALLA CUP 2017 YAZINDULIWA JIMBO LA NZEGA VIJIJINI

Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na timu ya Kata ya Mzibaziba wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.

Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wachezaji wa Kata ya Nkiniziwa wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.
Na Mwandishi Wetu

Mashindano ya mpira wa miguu kwa timu za Kata zilizo ndani ya Jimbo la Nzega Vijijini maalufu kama ‘Kigwangalla Cup’ yamezinduliwa rasmi jioni ya Julai 27, 2017 huku miamba 20 ikitarajiwa kuumana kumpata bingwa wa Jimbo hilo kwa mwaka huu.


Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mbunge wa  Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla aliwataka wachezaji wote wanaoshiriki michuano hiyo kuwa na nidhamu iliwaitumie michuano hiyo kama kipimo cha wao cha kuonesha vipaji vyao ili waonekane ngazi za juu.


“Mpambane kweli kweli. Kila mmoja wenu aoneshe uwezo wake wa kusakata kabumbu. Pia muzingatie nidhamu ya hali ya juu kwani michezo inaleta umoja na amani, inaimalisha afya ya miili yetu” alieleza Dk. Kigwangalla wakati akuzungumza na wachezaji katika ufunguzi wa michuano hiyo.


Dk. Kigwangalla pia alipata wasaha wa kukagua timu zilizofungua rasmi michuano hiyo kati ya Mizibaziba dhidi ya Nkiniziwa ambazo hadi kipyenga cha mwisho ziliweza kutoka droo ya bao 1-1.

Dk. Kigwangalla alieleza kuwa, jumla ya Kata 19 za jimbo lake hilo zimeweza kutoa timu ilikushiriki michuano hiyo huku timu maalum ikiingizwa ambayo itajumuisha Madiwani wote kutoka Kata hizo ili kufanya jumla ya timu 20.


Dk. Kigwangalla alizitaja baadhi ya Kata zinazochuana kwenye michuano hiyo ni pamoja na Kata ya Puge, Ndala, Nata, Sanzu,Lusu, Milambo Itobo, Magengati,Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi.


Kata zingine ni Kata za Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe na Mwakanshanhala.
 
Awali kabla ya kuanza rasmi kwa mchezo wa ufunguzi, Madiwani wa Kata zote waliweza kukabidhiwa baadhi ya vifaa kwa timu zao sambamba na hilo wananchi waliweza kufurahia michezo mbalimbali ikiwemo ile ya jadi hasa mchezo wa asili wa bao la Kinyamwezi, kucheza drafti, kukimbiza kuku, michezo ya mbio kwa Wazee huku mchezo wa mbio kwa watu wenye vitambi ukitia fola kwenye ufunguzi huo, uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Nkiniziwa iliyopo kwenye Kata hiyo ya Nkiniziwa.

Monday, July 24, 2017

WAZEE YANGA WAMPA BARAKA MSUVA KWENDA MOROCCO


Baraza la Wazee wa Yanga wamesema kuwa  wanamtakia mafanikio mema kiungo mshambuliaji wake, Simon Msuva anayetarajia kujiunga na Klabu ya Difaa El Jadidi inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.

Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali amesema kuwa kwa upande wao wanatoa baraka zote kwa mchezaji huyo ili aweze kufanikiwa zaidi baada ya kuitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa.

“Leo (jana) tulikuwa na kikao cha Baraza la Wazee wa Yanga na kikubwa ilikuwa ni kujadili suala la kijana wetu Msuva ambaye ameuzwa kwenda kucheza soka Morocco, wazee wa Yanga kwa upande wetu tumeridhia kuondoka kwake.

“Unajua kwa upande wetu ni heshima kubwa kwa klabu yetu kufungua milango ili vijana wetu waweze kucheza soka la kulipwa, mafanikio aliyotuachia ni makubwa na tunayaheshimu kwa sababu siku akiamua kurejea kucheza hapa atarudi kwenye timu yake ambayo imemkuza na kumpa mafanikio,” alisema Akilimali.

Klabu hiyo ya Morocco iliyoshika nafasi ya pili msimu uliopita, imekubali kumlipa Msuva mshahara wa dola 4,000 (Sh 9m), kiasi ambacho awali aligoma akidai ni kidogo kwa sababu anakwenda kuishi ugenini.

Wakati huohuo, Msuva amesema anajua mazingira anayoenda kukutana nayo huku akipanga kuonyesha uwezo wa juu ili kuingia kwenye kikosi cha kwanza.

“Kabla ya kukubali dili la kutimkia Difaa El Jadidi, nilipata muda wa kuitazama ligi yao kubaini aina gani ya mbinu wanazitumia na nimegundua ni kama hapa Tanzania tu yaani hakuna tofauti yoyote ile.

“Kule wanatumia mawinga zaidi kwenye kutengeneza mabao kwa kupiga mipira mirefu pamoja na pasi za haraka, sasa ukiangalia mbinu hiyo mimi nimeicheza sana Yanga na ndiye nilikuwa injini ya kutengeneza mabao, jambo hilo linanipa matumaini ya kuona kwamba sitapata shida ya kufiti na kuingia kwenye mfumo wao,” alisema Msuva.

Sunday, July 23, 2017

SINGIDA UNITED YAMNYAKUA DEUS KASEKE WA YANGA




KOCHA Mkuu wa Singida United, Hans van Pluijm, ameendelea kuibomoa Yanga baada ya kumsajili winga machachari, Deus Kaseke.

Kaseke amekuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Singida United katika kipindi cha wiki moa. Wiki iliyopita, Singida United ilimsajili kipa Ally Mustapha 'Barthez' kutoka Yanga.

Mkurugenzi wa Singida United, Festo Richard Sanga, alisema jana kuwa, wamemsainisha Kaseke mkataba wa miaka miwili.

Kaseke amemaliza mkataba wake wa miaka miwili na Yanga na muda wowote kuanzia leo, atasafiri kwenda Mwanza kuungangana na timu hiyo iliyoweka.

TENGA APEWA ULAJI CAF


Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace John Karia amempongeza Leodegar Chilla Tenga – Rais wa Heshima wa TFF kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Leodegar Chilla Tenga aliteuliwa Ijumaa iliyopita katika Mkutano Mkuu wa CAF uliofanyika mjini Rabat nchini Morocco ambako katika kamati hiyo muhimu, Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zambia (FAZ), Kalusha Bwalya.

“Hii ni sifa kwa nchi. Na ni sifa kwa Mheshimiwa Tenga. Tunajisikia fahari Tanzania kung’ara katika medani za uteuzi katika vyombo vya kimataifa kama CAF. Uteuzi wake ni kwamba anafungua njia kwa nchi na wengine ili kufanya vema,” anasema.

Karia amesema ana imani na Tenga na Bwalya katika kamati yao kwa sababu ni wachezaji na manahodha wa zamani wa timu za taifa. Itakumbukwa kwamba Tenga alikuwa akicheza kama mlinzi Bwalya alikuwa mshambuliaji. “Wote ni wataalamu. wanajua, tutafanikiwa.”

Katika mkutano huo mbali na kuteua akina Tenga na kuunda kamati nyingine, pia ulifanya marekebisho ya muundo wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na sasa yatakuwa yakifanyika katikati ya mwaka badala ya mwanzoni mwa mwaka.

Kwa miaka ya nyuma hadi mwaka huu ambako michuano hiyo ilifanyika Gabon, ilikuwa ikifanyika kuanzia katikati ya Januari hadi Februari. Mbali na kuzitoa Fainali za AFCON katikati ya mwaka hadi mwanzoni, pia idadi ya timu za kushiriki zimeongezwa kutoka 16 hadi 24 ambako sasa utakuwa na timu washindwa 10 badala ya mbili kama ilivyokuwa awali.

“Watanzania wasikate tamaa, hata kama kwa mfumo wa sasa unaofutwa au tuseme kubadilishwa, bado tuna malengo yetu yalikuwa ni kufuzu, Tunajipanga kwa hali ya sasa na hatujaanza vibaya na Lesotho. Bado tuna nafasi,” amesema Karia.

Michuano hiyo kuhamishwa kutoka Januari na Februari hadi Juni na Julai kuanzia Fainali za mwaka 2019 nchini Cameroon.

Hii si mara ya kwanza kwa Tenga aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), bali amekuwa akiteuliwa mara kwa mara kuwa Mjumbe wa Kamati mbalimbali za CAF. Hongera sana Rais wa Heshima wa TFF, Leodegar Chilla Tenga.

TAIFA STARS YATUPWA NJE YA RWANDA MICHUANO YA CHAN



TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars imetolewa katika michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani baada ya kulazimishwa kutoka suluhu na Rwanda.

Katika mechi hiyo ya marudiano iliyochezwa mjini Kigali, Taifa Stars ilikuwa ikihitaji ushindi ili iweze kufuzu kucheza fainali za michuano hiyo zitakazofanyika mwakani nchini Kenya.

Rwanda imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini, kufuatia timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya awali iliyochezwa wiki iliyopita mjini Mwanza.

Akizungumzia mechi hiyo, Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania, Fulgence Novatus, amesema kwamba Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti  ya SBL haikuwa na bahati katika mchezo dhidi ya Amavubi ya Rwanda uliofanyika Uwanja wa Kigali ulioko kata ya Nyamirambo.

“Tumecheza vema, tulitafuta nafasi za kutosha. Tumeshambulia sana na kumiliki mpira. Lakini kila tulipojaribu kufunga, bahati haikuwa kwetu,” amesema Novatus mara baada ya mchezo huo.

Matokeo ya sare tasa ya jana yanawapa nafasi ya kusonga mbele Rwanda baada ya sare ya 1-1 katika mchezo uliofanyika Julai 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mchezo huo ni wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) na sasa Rwanda itacheza na Uganda mwezi ujao.

Pamoja na kushindwa kusonge mbele, Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza mechi baada ya kucheza mechi 11 za kimataifa na kushinda mitano; kutoka sare mitano na kufungwa mmoja wa nusu fainali za Cosafa.

ZANZIBAR YAFUTWA UANACHAMA WA CAF

Rais wa soka barani Afrka (CAF ) Ahmad Ahmad.

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limefanya maamuzi ya kuwavua uanachama chama cha soka cha Zanzibar ikiwa ni miezi minne toka  kipewe uanachama na CAF kutoka kwa Rais aliyepita Issa Hayatou.

Rais wa soka barani Afrka (CAF ) Ahmad Ahmad amesema Zanzibar walipewa uanachama kimakosa na kama sheria zingepitiwa vizuri wasingepewa uanachama.

“Walipewa uanachama bila kupitia vizuri kanuni ambazo ziko wazi na zinaeleza kila kitu, kama kanuni na sheria zingepitiwa kiufasaha wasingepewa uanachama”

Sababu kubwa ambayo CAF wameivua uanachama Zanzibar ni kutokana na kisiwa hicho kuwa ndani ya Tanzania ambao nao ni wanachama wa CAF.

“Jina la nchi linatokana na jina linaloandikwa katika umoja wa mataifa UN na Zanzibar katika umoja huo inafahamika ipo ndani ya nchi iitwayo Tanzania ambao ni wanachama wa CAF” alisema Ahmad.

Hilo ni pigo kubwa kwa Wazanzibar kwani wakati huu walikuwa wakipambana kupata uanachama wa FIFA ambao wameukosa na wa CAF nao pia wamekosa.

Kwa maana hiyo ndoto ya kisiwa cha Zanzibar kushiriki michuano ya CAF kama mwanachama zimekufa rasmi na sasa watakuwa wakishiriki michuano hiyo kama Tanzania (Zanzibar na Tanzania bara).

Thursday, July 20, 2017

NYONI, SAIDI MOHAMED WAMWAGA WINO SIMBA, KAMUSOKO AJIFUNGA MIAKA MIWILI YANGA




KLABU ya Simba imetangaza rasmi kuwasajili beki Erasto Nyoni kutoka Azam na kipa Said Mohamed kutoka Mtibwa Sugar kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

Mipango ya Simba kumsajili Nyoni imekuja huku kukiwa na taarifa kuwa, beki huyo alishafanya mazungumzo na klabu ya Yanga na kufikia makubaliano ya kusajiliwa.

Wachezaji hao wawili walioko kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars, walimwaga wino Simba saa chache kabla ya timu hiyo kwenda Rwanda kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya nchi hiyo keshokutwa.

Wakati huo huo, klabu ya Yanga imemsainisha mkataba wa miaka miwili kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe, Thamani Kamusoko.

Kamusoko amekubali kumwaga wino Yanga baada ya mvutano uliodumu kwa miezi kadhaa kuhusu maslahi.

ALLY MUSTAFA 'BARTHEZ' AMWAGA WINO SINGIDA UNITED



Golikipa wa zamani wa Dar es Salaam Young Africans, Ally Mustafa ‘Barthez’,  ametangazwa rasmi kujiunga na klabu ya Singida United, kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania.

Kipa huyo, ambaye pia amewahi kuichezea timu ya Taifa, Taifa Stars na Simba, ametia saini mkataba wa kuichezea Singida United kwa miaka miwili.

Barthez, amejiunga Singida United, ambapo atakuwa katika ‘vita’ ya namba na golikipa wa timu hiyo, Said Lubawa.

Baada ya usajili huo, Mkurugenzi wa Singida United, Festo Richard Sanga, alisema kwa sasa wamebakiwa na nafasi moja kabla ya kukamilisha usajili.

”Kwangu mimi kwanza naona hakuna utofauti kati ya timu kubwa na Singida United. Mimi naona kawaida japo kuna jina kubwa na jina dogo kwa sababu Singida United imepanda daraja msimu huu, lakini Yanga ipo Ligi Kuu muda mrefu na timu kubwa,” alisema Barthez.

TAIFA STARS YAIFUATA RWANDA



Kikosi cha timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kinatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda kesho Jumatano mchana kikitokea Mwanza, Tanzania.
 

Taifa Stars iliyokuwa jijini Mwanza kwa kambi kabla ya kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Rwanda Jumamosi iliyopita, itapitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere kwenda Rwanda.
 

Stars itaondoka Mwanza kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania majira ya saa nne asubuhi na kuwasili Dar es Salaam majira ya saa sita mchana kabla ya kuunganisha ndege ya Rwanda majira ya saa nane alasiri kwenda Kigali, Rwanda.
 

Inakwenda Kigali kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Rwanda maarufu kama Amavubi kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN 2018). Fainali za CHAN mwakani zitafanyika nchini Kenya.
 

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Mshindi wa jumla katika michezo miwili, atakuwa amesonga mbele hivyo kukutana na Uganda mwezi ujao.
 

Katika mchezo huo wa marudiano utakachezwa Kigali Rwanda, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga atamkosa beki wake wa kulia, Shomari Kapombe anayesumbuliwa na mguu alioumia katika mchezo kwanza.
 

TAARIFA YA KAMATI YA UCHAGUZI TASMA
 

Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Wataalamu wa Tiba za Michezo (TASMA), kimetangaza majina ya waliochukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Agosti 5, mwaka huu.
 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya chama hicho, Leslie Liunda wanaowania uenyekiti ni Joakim Mshanga, Usubene Kisongo na Biyondo Mgome ilihali kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti, amejitokeza Magreth Mtaki pekee.
 

Wale wanaotaka ukatibu mkuu wa chama hicho ni Suphian Juma na Nassoro Matuzya waliojitokeza huku nafasi ya ukatibu msaidizi inawaniwa na Alfred Mchinamnamba.

Nafasi Mweka Hazina inawaniwa Alex Gongwa huku Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF inawaniwa Richard Yomba na Cosmas Kapinga ilihali Ujumbe wa Kamati ya Utendaji wamo   Paschal Itonge na Mwanandi Mwankemwa.

Kwa mujibu wa ratiba ya mchakato wa uchaguzi huo kuanza leo na kesho (Julai 18, 2017 na Julai 19, mwaka huu) watapokea pingamizi katika ofisi za Omlipiki Maalumu (Special Olympic) zilizopo jirani na Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kipindi cha usaili kimepangwa kuanza Julai 20, 2017 hivyo wagombea wote wanatakiwa kufika mbele ya kamati ili kusailiwa.
 

“Mgombea ambaye atashindwa kuhudhuria atakuwa amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi utafanyika Agosti 5, mwaka huu katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam,” amesema Liunda.

Tuesday, July 18, 2017

SIKINDE KUFANYA MAONYESHO KENYA WIKI IJAYO


BENDI ya muziki wa dansi ya Mlimani Park Orchestra (Sikinde), inatarajiwa kuondoka nchini wiki ijayo kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya maonyesho mawili ya muziki.

Kiongozi wa bendi hiyo, Abdalla Hemba, alisema mjini Dar es Salaam, jana kuwa, bendi hiyo itakwenda Kenya kwa mwaliko uongozi wa Hoteli ya Deepwest Resort.

Hemba alisema bendi hiyo itaondoka nchini Jumatatu ijayo kwa basi, ikiwa na kundi la wanamuziki 14, ambao hakuwa tayari kutaja majina yao kwa madai kuwa ni mapema kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa Hemba, onyesho la kwanza la bendi hiyo limepangwa kufanyika Julai 28 wakati onyesho la pili litafanyika Julai 29, mwaka huu, kwenye ukumbi wa hoteli hiyo.

Hemba alisema kutokana na maelezo waliyopatiwa na mratibu wa onyesho hilo, Abuu Omar, ukumbi wa Deepwest Resort upo jirani na jengo la T-Mall, barabara ya Lang'ata, Jijini Nairobi.

Tayari baadhi ya vyombo vya habari nchini Kenya, vimeshaanza kuitangaza ziara hiyo, ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa muziki nchini humo.

Baadhi ya vyombo hivyo vya habari, likiwemo gazeti la Daily Nation,  vimeielezea bendi hiyo kuwa ni miongoni mwa zilizotamba kimuziki katika ukanda wa Afrika Mashariki miaka ya 1980.

Ziara hiyo itakuwa ya tatu kwa Mlimani Park Orchestra nchini Kenya. Ilikwenda huko kwa mara ya kwanza mwaka 1988, ambako ilirekodi albamu ya Kisonoko na kutumbuiza kwenye sherehe za maadhimisho ya kutimiza miaka 10 madarakani, Rais wa zamani wa nchi hiyo, Daniel Arap Moi.

Sikinde ilikwenda tena Kenya mwaka 2006, ambapo ilifanya maonyesho mawili katika ukumbi wa Carnivores ulioko mjini Nairobi.

MALINZI AENDELEA KUSOKA KEKO


NA FURAHA OMARY

VIGOGO watatu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),  akiwemo Rais wake Jamal Malinzi na Katibu Mkuu, Mwesigwa Selestine, wataendelea kusota mahabusu kwa kuwa upelelezi wa shauri lao haujakamilika.

Malinzi (57) na Mwesigwa (46) ambao wako mahabusu katika gereza la Keko na mhasibu Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga (27), aliyeko gereza la Segerea, walipanda kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washitakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri, ambapo upande wa jamhuri ulikuwa ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Leonard Swai.

Kwa upande wa washitakiwa, Malinzi na Mwesigwa walikuwa wakiwakilishwa na jopo la mawakili  wapya akiwemo Richard Rweyongeza, Nehemiah Nkoko na Jacquline Rweyongeza. 

Mawakili wengine waliotambulishwa kuwawakilisha Malinzi na Mwesigwa ni James Bwana, Rwegeshora, Kashinje Thabit huku Nsiande akiwakilishwa na wakili Senguji Abraham.

Upande wa jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo waliomba shauri lao liahirishwe hadi tarehe nyingine kwa kutajwa huku wakili Abraham akiomba kupatiwa hati ya mashitaka na maelezo ya mlalamikaji kwenye kesi hiyo.

Hata hivyo, Swai alidai wakili huyo atapatiwa hati ya mashitaka lakini hawezi kupewa maelezo ya mlalamikaji kwa kuwa shauri hilo halijaanza kusikilizwa.

Hata hivyo, wakili Abraham aliendelea kusisitiza kupatiwa maelezo hayo kwa madai kuwa yatamsaidia mteja wake kufahamu tuhuma zinazomkabili.

Hakimu Mashauri alikubaliana na hoja za upande wa jamhuri kwamba wakili huyo atapatiwa hati ya mashitaka lakini hawezi kupatiwa maelezo ya mlalamikaji kwa kuwa si wakati wake.

Baada ya kusema hayo, Hakimu Mashauri aliahirisha shauri hilo hadi Julai 31, mwaka huu kwa kutajwa na kusema washitakiwa wataendelea kubaki rumande.

Vigogo hao wa TFF walifikishwa mahakamani  kwa mara ya kwanza Julai 26, mwaka huu na TAKUKURU  wakikabiliwa na mashitaka 28 yakiwemo ya kutakatisha fedha makosa ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

Katika hati hiyo ya mashitaka, Malinzi anakabiliwa na mashitaka 26 yakiwemo ya kughushi risiti mbalimbali zikionesha ameikopesha TFF fedha huku Selestine akiwa na mashitaka manne na Nsiande mashitaka mawili.

Shitaka la kwanza, Malinzi na Selestine wanadaiwa Juni 5, mwaka jana jijini Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya kwa pamoja walighushi nyaraka ambayo  maazimio ya kamati ya utendaji ya tarehe hiyo ikionesha kuwa kamati iliamua kubadilisha mtu wa kutia saini wa akaunti zake za benki kutoka Edgar Leonard Masoud na kuwa Nsiande  Isawafo Mwanga.

Selestine anadaiwa Septemba Mosi, mwaka jana katika benki ya Stanbic Tanzania Limited tawi la  Kinondoni, Dar es Salaam  kwa nia ya udanganyifu aliwasilisha nyaraka ya kughushi ambayo ni maazimio ya kamati yautendaji ya TFF ya kubadilisha jina la mtia saini wa akaunti zake.

Shitaka la tatu hadi la 25 linamkabili  Malinzi ambaye anadaiwa  katika tarehe tofauti kati ya Novemba 6,  2013 hadi Septemba 22, 2016 kwenye shirikisho hilo alikuwa akighushi risiti zikiwa na kiwango tofauti cha Dola za Marekani akionesha amelikopesha shirikisho hilo.

Malinzi anadaiwa Novemba 6, 2013, alighushi risiti kuonesha ameikopesha TFF Dola za Marekani 9300, Desemba 17, 2013 aliikopesha  Dola za Marekani 10,000 na Dola 18,000, Dola 500 na Dola 1,032.

Pia  Malinzi anadaiwa Machi 26, 2014, katika shirikisho hilo alighushi risiti zikionesha amelikopesha  Dola 40,000, Machi 13, 2014 amekopesha Dola 5,000. Dola 40,000, Machi 16, 2014 alilikopesha Dola 10,000, Julai 11, 2014 alilikopesha Dola 3,000, Julai 15, 2014 alilikopesha mkopo wa Dola 14,000.

Malinzi anadaiwa Julai 15, 2014 alighushi risiti kuonesha alilikopesha shirikisho hilo Dola 4,000, Julai 25, 2014 alilikopesha Dola 1,000, Agosti 19, 2014 alilikopesha Dola 5,000, Oktoba 11, 2014 alilikopesha mkopo wa Dola 1,200, Agosti 17, 2015 alilikopesha Dola 5,000, Julai 22, 2015 alilikopesha shirikisho hilo Dola 2,000 na Mei 9, mwaka jana, alilikopesha mkopo wa Dola 7,000.

Mashitaka mengine, Malinzi anadaiwa Juni 16, 2016 alighushi risiti akidai kwamba alilikopesha shirikisho hilo Dola 10,000, Agosti 2, mwaka jana, alilikopesha Dola 1,000, Septemba 19, mwaka jana, alilikopesha Dola 1,000 na Septemba 22, mwaka jana, alilikopesha shirikisho hilo mkopo wa Dola 15,000 wakati akijua si kweli.

Malinzi, Selestine na Nsiande wanadaiwa tarehe tofauti kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19, 2016 jijini Dar es Salaam  kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la kutakatisha fedha na kujipatia Dola za Marekani 375,418 wakati wakijua fedha hizo ni zao la kosa la uhalifu la kughushi.

Rais huyo wa TFF na Selestine wanadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19, mwaka jana kwenye benki ya Stanbic tawi la Kinondoni, Dar es Salaam  kwa pamoja walijipatia Dola za Marekani 375,418 kutoka kwenye benki hiyo wakati wakijua upatikanaji wa fedha hizo ni  zao la kosa la kughushi.

Nsiande anadaiwa katika kipindi hicho, kwenye ofisi za TFF  aliwasaidia Malinzi na Selestine kujipatia fedha kutoka benki ya Stanbic ambazo ni Dola za Marekani 375,418 huku akijua zimepatikana kwa udanganyifu kwa kosa la kughushi nyaraka ya kuhamisha fedha.

Washitakiwa hao waliposomewa mashitaka yao waliyakana.

KAMATI YA NIDHAMU TFF YAMTOA KIFUNGONI HAJI MANARA


Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefuta adhabu dhidi ya wanafamilia wanne waliofungiwa kushiriki masuala la soka
kwa mwaka mmoja.
 

Wanafamilia hao ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa, James Mwakwinya; Mwenyekiti wa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA), Blassy Kiondo; Kaimu Katibu wake, Ayoub Nyaulingo pamoja na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.

Haji Manara alitiwa hatiani Aprili 23, mwaka huu kwa makosa ya lugha chafu na za chuki kwa viongozi wa TFF na kupotosha umma dhidi ya kadi njano ya
mchezaji Mohammed Fakhi wa Kagera Sugar ambako alifungiwa kushiriki masuala ya mpira kwa mwaka mmoja na faini ya Sh milioni tisa.

Viongozi wa RUREFA walifungiwa kwa mwaka mmoja na faini ya Sh. milioni mbili kwa kila mmoja kwa makosa ya kukiuka maagizo ya viongozi wa Kamati
ya Uchaguzi ya TFF iliyotaka wasitishe mchakato wa uchaguzi mkoa kwa kuwa kulikuwa na rufaa iliyokatwa TFF.

Akizungumza na Wanahabari leo Julai 17, 2017 Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas, alisema viongozi hao wamesamehewa
adhabu zao kwa kuwa waliomba kupitiwa upya kwa mashauri yao na kamati imeona ni bora kuwaachia huru ili kuendeleza masuala ya soka.

“Wapo wengi waliofungiwa wengine maisha na wengine adhabu fupi, msamaha huu ni kwa wale ambao wameomba tu kupitiwa upya kwa adhabu
zao, pia milango ipo wazi kwa wengine ambao wanataka kupitiwa kwa mashauri yao, lakini si kwa wale waliopanga matokeo uwanjani,” alisema
Tarimba.

Kadhalika, Tarimba aliwaomba viongozi wa TFF kuandaa semina ya Maofisa Habari na Viongozi wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ili kuepuka
maneno machafu ambayo yanasababisha wao kufungiwa.

“Inaonekana viongozi na Maofisa Habari hawana maneno mazuri ya kuongea na wadau wa soka na ndio maana matatizo ya kufungiwa yanajitokeza mara
kwa mara, naamini wakipata semina hiyo itawasaidia kujirekebisha na kupunguza kesi kama hizo,” alisema Tarimba.

Sunday, July 16, 2017

TAIFA STARS YATOKA SARE NA RWANDA



TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania Bara, jana ilianza vibaya michuano ya kuwania kufuzu kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), baada ya kulazimishwa kutoka sare ya bao 1-1 na Rwanda.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Rwanda ilikuwa ya kwanza kupata bao kabla ya Tanzania Bara kusawazisha.

Kutokana na matokeo hayo, Tanzania Bara sasa italazimika kucheza kufa na kupona kushinda mechi ya marudiano itakayochezwa Jumamosi mjini Kigali ili iweze kusonga mbele.

Mshindi kati ya Tanzania Bara na Rwanda, atamenyana na mshindi wa mechi kati ya Sudan Kusini na Uganda, ambazo nazo zilitoka suluhu jana mjini Juba.

Bao la Rwanda lilipatikana dakika ya 17 kupitia kwa mshambuliaji wake, Dominique Savio baada ya kupokea krosi kutoka kwa Emmanuel Imanishimwe.

Tanzania Bara ilisawazisha bao hilo dakika ya 34 kwa njia ya penalti iliyopigwa na nahodha Himidi Mao baada ya beki mmoja wa Rwanda kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

SIMBA YAENDA KUWEKA KAMBI AFRIKA KUSINI


TIMU ya soka ya Simba inatarajiwa kuondoka nchini Jumanne kwenda Afrika Kusini kwa ziara ya wiki mbili, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kwa vyombo vya habari jana ilisema kuwa, kikosi kitakachoondoka Jumanne hakitakuwa na wachezaji waliomo kwenye timu ya Taifa ya Tanzania Bara.

Wachezaji hao bado wapo kwenye kikosi cha Tanzania Bara, wakijiandaa na mchezo wa marudiano wa michuano ya Kombe la CHAN dhidi ya Rwanda, Jumamosi ijayo. Katika mechi ya awali iliyochezwa jana mjini Mwanza, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wachezaji hao, kipa Aishi Manula, mabeki Shomari Kapombe, Salim Mbonde, viungo Muzamil Yassin, Said Ndemla na Shiza Kichuya na mshambuliaji John Bocco, wataungana na Simba baada ya mchezo huo wa marudiano dhidi ya Rwanda.

Ikiwa Afrika Kusini, mbali ya kufanya mazoezi chini ya kocha wake, Joseph Omog, Simba itacheza mechi kadhaa za kujipima nguvu.

Baada ya ziara hiyo ya Afrika Kusini, Simba itarejea nchini kwa ajili ya tamasha lake la kila mwaka la Simba Day, litakalofanyika Agosti 8, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba imekuwa ikilitumia tamasha hilo kutambulisha wachezaji wake wapya na pia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu kutoka nje ya nchi.


Friday, July 14, 2017

MAZOEZI AZAM DOZI MWANZO MWISHO



DOZI mwanzo mwisho! Hivyo ndivyo unavyoweza kuyaelezea mazoezi ya Azam FC ya kujiandaa na msimu ujao, ambapo imeanza kujifua kwa staili ya aina yake kwa wachezaji kupewa dozi mara tatu kwa siku.

Huo ni mwendelezo wa mazoezi ya Azam FC tokea ilipoanza maandalizi ya msimu mpya Mei 28 mwaka huu, ikiwa na kikosi chenye sura mpya za wachezaji wengi vijana wenye vipaji vya hali ya juu na baadhi wakiwa ni wazoefu.

Mazoezi hayo ni maalumu kabisa katika kipindi hiki cha maandalizi ya msimu ujao, ambapo Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, amepanga kutengeneza kikosi kikali kitakachoweza kufanya makubwa katika siku za usoni.

Kikosi hicho leo kimeshafanya mazoezi mara mbili, saa 1.00 asubuhi na 3.30 asubuhi na kitamalizia dozi ya mwisho saa 11.00 jioni ndani ya viunga vya Azam Complex, Chamazi.

Cioaba amesema faida kubwa ya kufanya mazoezi makali hivi sasa ni kuwajenga wachezaji kwenye maeneo mbalimbali, kiufundi uwanjani, stamina na ustahimilivu kwenye kupambana.

Baada ya kumaliza programu hiyo ya mazoezi, Azam FC itasafiri Julai 20, mwaka huu kuelekea kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ikienda kucheza mechi tatu za kirafiki, ya kwanza ikiwa ya mwaliko dhidi ya Mbeya City, itakayofanyika Julai 22 katika siku watakayokuwa wakisherehekea Mbeya City Day.

Mechi nyingine za kirafiki itacheza na timu mbili zilizopanda daraja. Njombe Mji Julai 24 mwaka huu mjini Njombe na ikimaliza ziara hiyo kwa kukipiga na Lipuli ya Iringa Julai 26 kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam Julai 27.

EVERTON ILIPOICHAPA GOR MAHIA MABAO 2-1 DAR






EVERTON YAWASHUKURU WATANZANIA KWA UKARIMU



Wayne Rooney (wa tatu kushoto) kushoto akiwa na wachezaji wenzake walipokuwa Jijini Dar es Salaam ambapo timu ya Everton ilicheza na timu ya Gor Mahia katika mchezo wa kirafiki ulichezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Na. Mwandishi Wetu-MAELEZO

Timu ya Soka ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uiungereza imemaliza ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania na kuelezwa kufurahishwa na namna Watanzania walivyoipokea timu hiyo.

Timu ya Everton iliwasili Tanzania siku ya Jumatano wiki hii ambapo jana ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.

“Imekuwa ni uzoefu mpya kwangu kuja hapa (Tanzania) na nina tumaini sasa Makamu wa Rais atakuwa akiishabikia Everton”, alieleza Wayne Rooney kupitia tovuti ya timu hiyo.

Pia katika akaunti yake ya mtandao wa tweeter, Rooney aliwashukuru washabikji wa Tanzania kwa kuiunga mkono Everton katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.

“Great start to the pre-season. Special thanks to the fans supporting us in Tanzania”, aliandika Rooney akitoa shukrani za pekee kwa washabiki wa Tanzania.

Kwa upande wa Kocha wa timu hiyo, Ronald Koeman alielezea kufarahia ziara ya kuja Tanzania na zaidi ni kutokana na hali ya urafiki iliyooneshwa na washabiki wa soka nchini.

Rooney pia aliungana na wachezaji wengine kama Morgan Schneiderlin, Jonjoe Kenny na Kevin Mirallas wa timu hiyo walipata fursa ya kujifunza tamaduni za kimsai, kujifunza kupika chakula cha asili, kutembelea shule yenye wanafunzi wenye mahutaji maalum na pia kufanya mazoezi na timu ya vijana wenye ulemavu wa ngozi (Albino United).

Timu ya soka ya Everton ilifanya ziara nchni Tanzania ambapo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, Marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na wageni mbalimbali kutoka ndani na nche ya nchi.

EVERTON YARIDHISHWA NA MATIBABU YA MABUSHA NA MATENDE


Mtangazaji wa Televisheni ya Everton, Darren Griffiths akizungumza katika hafla hiyo iliyowakutanisha wagonjwa waliotibiwa na wanaotibiwa ugonjwa wa Matende na Mabusha na baadhi ya wachezaji wa timu ya Everton ambayo imekuwa ikifadhili matibabu hayo kushoto ni Graham Stuart na Leon Osman wachezaji wa zamani wa Everton.

NA WAMJW-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa timu ya mpira wa miguu ya Everton kutoka nchini Uingereza imeridhishwa na huduma inayotolewa kwa wagonjwa  wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo mabusha na matende hapa nchini.

Hayo yamezungumzwa na mmoja wa viongozi wa Everton Bw. Darren Griffiths ambao ni washiriki katika kuchangia huduma ya magonjwa hayo hapa nchini  ambaye ameongozana na timu yake ili kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Gor Mahia kutoka chini Kenya.

“Tunayo furaha kuona wagonjwa wengi waliokuwa wanaumwa mabusha na metende nchini Tanzania kwa sasa wamepona kabisa na tunahaidi kuwa na Wizara ya afya bega kwa bega katika kutokomeza magonjwa haya” alisema Bw. Darren Griffiths

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt.  Vida Mmbaga amesema kuwa kutokana na ushiriki wa Everton katika kuchangia utoaji wa Huduma ya kutibu ugonjwa huo wamefanikiwa kupata ujuzi wa upasuaji hasa kwa wagonjwa wa mabusha na matende hapa nchini.

Aidha Dkt. Vida  amesema kuwa Serikali ikishirikiana vyema na wananchi na mashirika mbalimbali ya afya magonjwa hayo yatatokomea kwa kiasi kikubwa hapa nchini mpaka kufikia mwaka 2025.

Mbali na Hayo Dkt. Vida amesema kuwa anawashukuru watu wa Everton kwa kupitia ushirikiano wao katika sekta ya afya kwa kutoa huduma  pamoja na mafunzo kwa wataalamu ambapo imesaidia kuwafanyia upasuaji wagonjwa  elfu moja.

Kwa upande wake Bw. Yahya Ally Kidege mkazi wa pugu stesheni amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwajali wananchi wake kwani amepata upasuaji wa ugonjwa wake wa busha na amepona kabisa kwan alikua na ugonjwa huo takribani miaka 20.

Wednesday, July 12, 2017

EVERTON YATUA NCHINI

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na mshambuliaji Wayne Rooney wa timu ya Everton ya England, baada ya kuwasili nchini leo asubuhi kwa ziara ya siku tatu. Everton inatarajiwa kucheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

WACHEZAJI wa Everton wakishuka kwenye ndege iliyowaleta nchini leo asubuhi

WACHEZAJI wa Everton wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili nchini

Tuesday, July 11, 2017

WAYNE ROONEY KUTUA BONGO KESHO AKIWA NA EVERTON



Siku moja baada ya Wayne Rooney kutangazwa kujiunga na Everton FC ambayo ni timu yake ya utotoni akitokea Man United kama mchezaji huru, baadhi ya mashabiki wa soka Tanzania walikuwa wakihisi kwamba huenda Rooney asije Tanzania katika mchezo dhidi ya Gor Mahia.

Wengi walihisi hivyo na kudhani kuwa Rooney anaweza akapewa mapumziko au asije mechi ya Tanzania akaungana na wenzake katika mechi ya pili ya Everton ya maandalizi ya msimu dhidi ya FC Twente ya Uholanzi lakini leo imethibitika kuwa Rooney anakuja Tanzania.

Rooney, juzi alifanya mazoezi na Everton kwa mara ya kwanza, akiwa mchezaji wa timu hiyo baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na kueleza kuwa ziara ya Everton nchini Tanzania, itamfanya hawajue vizuri wachezaji wenzake.

“Hii trip naiangalia kwa uzuri na itakuwa safari sana kwetu na natumaini nitapata nafasi ya kucheza, huwa ni vizuri sana kusafiri na wachezaji wenzako na kutembea sehemu tofauti tofauti, kiukweli sijawahi kufika Tanzania”

TAIFA STARS YAPAA KWENDA MWANZA


Hivi sasa majira ya saa moja usiku - Julai 10, mwaka huu kikosi cha timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kinasafiri kwenda jijini Mwanza kwa Ndege ya Fast Jet, ikiwa na ongezeko la wachezaji wapya saba. 

Kati ya hao ambao Kocha Mkuu Salum Mayanga amewaita, wamo  wale aliowatangaza juma lililopita ambao ni John Bocco, Kevin Sabato pamoja na kinda Athanas Mdamu ambaye anacheza Alliance ya Mwanza inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
 

Katika kikosi chake kabla ya kuivaa Rwanda Jumamosi ijayo, wachezaji wengine ambao Kocha Mayanga amewatangaza leo ni pamoja na Kipa wa Serengeti Boys - timu ya taifa a vijana ya Tanzania, Ramadhan Kabwili.
 

Mbali ya hao wamo pia Boniface Maganga kutoka Mbao FC, Joseph Mahundi kutoka Azam FC na pia amemrejesha tena Said Ndemla wa Simba SC ambaye awali alikuwa kwenye uangalizi wa majeraha.
 

Kikosi hicho kinakwenda kujiandaa na mchezo dhidi ya Rwanda utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Jumamosi ya Julai 15, mwaka huu  
 

Kipa Benno Kakolanya, Shaban Idd Chilunda na Mbaraka Yussuf hao wamepumzishwa kwa sababu ya majeraha waliyoyapata kwa nyakati tofauti wakiwa na Taifa Stars huko Afrika Kusini kwenye michuano ya Kombe la Castle la Cosafa - inayoandaliwa na Baraza la Soka kwa nchi za Kusini mwa Afrika.
 

Pia wachezaji wa kimataifa ambao hawahusiki na mechi za CHAN ambao ni Thomas Ulimwengu na Elius Maguri, hawakuongozana na timu.
 

Timu hiyo ilishika nafasi ya tatu katika michuano ya Castle Cosafa kwa kuishinda Lesotho kwa mapigo 4-2 ya penalti katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Moruleng nchini Afrika Kusini Ijumaa iliyopita.
 

Mwanza inajiandaa na mchezo dhidi ya Rwanda unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Julai 15, mwaka huu kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN).

Timu hiyo ambayo kwa mwaka huu imecheza mechi tisa za kimataifa na kushinda mitano; kutoka sare miwili na kufungwa mmoja wa nusu fainali za Cosafa, itakuwa na kikosi cha wachezaji 24.

Monday, July 10, 2017

KESI YA WEMA SEPETU YAPIGWA TENA KALENDA



KESI ya kukutwa na dawa za kulevya inayomkabili mwigizaji Wema Sepetu na wenzake, imeahirishwa hadi Agosti Mosi, mwaka huu.

Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa, baada ya Wakili wa Serikali, Estezia Wilson, kusema hakimu anayesikiliza kesi hiyo hayupo.

Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 1, mwaka huu, kwa ajili ya kusikilizwa.

DK. MWAKYEMBE ASITISHA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BMT, DIONIZ MALINZI


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe,ametangaza kusitisha uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dionis Malinzi.

Dk. Mwakyembe alitangaza uamuzi huo jana, alipokutana na kuzungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dar es Salaam.

Uamuzi huo umekuja siku chache baada ya agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuitaka wizara hiyo kupitia upya utekelezaji wa BMT.

Kufuatia agizo hilo la Majaliwa, Waziri Mwakyembe amesitisha uteuzi huo ili kujiridhisha kuhusu utendaji wa baraza hilo.

Julai 5, mwaka huu, wakati akiahirisha kikao cha bunge mjini Dodoma,
Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza Waziri Mwakyembe kufanya mapitio ya uteuzi wa baraza hilo.

SIMBA YAMSAJILI MBONDE WA MTIBWA, YANGA YAMNASA KIPA WA CAMEROON



Klabu ya Yanga imemsainisha mkataba wa miaka miwili, golikipa wa African Lyon, Youthe Rostand, ambaye ni raia wa Cameroon baada ya kufanya vizuri msimu uliopita licha ya klabu yake kushuka daraja.

Yanga imesajili Rostand huku kukiwa na tetesi kwamba, golikipa wake,
Deogratius Munishi ‘Dida’, anafanya mipango ya kujiunga na klabu ya moja ya Afrika Kusini.

Rostand amesajiliwa Yanga ili kusaidiana na Beno Kakolanya baada ya kuwepo na taarifa kuwa, akitajwa kuondoka kwenye kikosi hicho cha Jangwani na amekuwa akihusishwa kujiunga na Singida United.

Wakati huo huo, klabu ya Simba, imemsajili beki wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde, kwa mkataba wa miaka miwili ili kuziba pengo la Abdi Banda anayehamia Afrika Kusini.

Mbonde amesaini saa chache baada ya kuwasili Dar es Salaam, akitokea Afrika Kusini, ambako aliiongoza timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kushika nafasi ya tatu kwenye michuano ya Kombe la COSAFA.

Taarifa zimeeleza kuwa, Mbonde amesaini mkataba huo mbele ya mfadhili wa klabu hiyo, Mohammed ‘Mo’ Dewji, ambaye kwa sasa ndiye anayeihudumia timu.

Sunday, July 9, 2017

JULIO, MALIMA WAKATWA UCHAGUZI MKUU WA TFF, VYETI VYA WALIOPITISHWA VYAPELEKWA KUKAGULIWA


Kamati mpya ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), tayari imekutana kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa mapema wiki iliyopita na Kamati ya Utendaji ya TFF.

Mara baada ya kikao hicho cha jana Jumamosi, Kamati imeweka hadharani majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uchaguzi, kinyang'anyiro kinachotarajia kufanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma.

Katika kinyang'anyiro hicho, wagombea watatu wa nafasi ya urais hawakupitishwa akiwemo Jamal Malinzi ambaye alikatwa kutokana na kutohudhuria usaili kinyume cha kanuni ya 11 (7) ya kanuni za uchaguzi za TFF.

Mgombea mwingine ambaye hajapitishwa kuwania nafasi hiyo ni Fredrick Masolwa ambaye hajapitishwa kwa kukosa uzoefu kwa mujibu wa kanuni ya 9 (3) ya kanuni za uchaguzi za TFF.

John Kijumbe aliondolewa katika kinyang'anyiro hicho kwa kukosa uzoefu huku Athumani Nyamlani alijitoa kuwania uongozi wa Shirikisho hilo.

Waliopitishwa kuwania urais na Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi, Wakili Revocatus Kuuli ni Imani Madega, Fredrick Mwakalebela, Wallace Karia, Ally Mayay, Shija Richard na Emmanuel Kimbe.

Nafasi ya Makamu wa Rais aliyejitoa ni Geofrey Nyange Kaburu ambaye anakabiliwa na tuhuma ya makosa matano yakiwemo ya utakatishaji fedha kwa klabu ya Simba huku waliopitishwa ni Mulamu Ng'ambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.

Kwa mujibu wa Kuuli, zoezi linalofuata kwa sasa ni kuhakiki kwa vyeti vya kidato cha nne kwa kila mgombea baada ya kupitisha majina.

Kanda namba 1 ya Mikoa ya Kagera na Geita: waliopitishwa ni Saloum Chama, Leopold Mukebezi na Kaliro Samson huku Abdallah Mussa aliondolewa katika hatua za awali kwa kutoambatanisha cheti cha elimu ya sekondari.

Kanda namba 2 inayounganisha mikoa ya Mara na Mwanza: Vedastus Lufano, Ephraim Majinge, Samwel Daniel na Aaron Nyanda (Wamepitishwa) huku Kanda namba 3 (Mikoa ya Shinyanga na Simiyu) Stanslaus Nyongo, Mbasha Matutu na Bannista Rugora (wamepitishwa).

Kanda namba 4 (Mikoa ya Arusha na Manyara) waliopitishwa ni Omar Walii, Sarah Chao na Peter Temu (wamepitishwa), Kanda namba tano inayounganisha mikoa ya Kigoma na Tabora waliopitishwa ni John Kadutu, Issa Bukuku, Abubakar Zebo na Francis Michael.

Kanda namba 6 yenye mikoa ya Katavi na Rukwa Keneth Pesambili na Baraka Mazengo – wote wamepitishwa huku Kanda namba 7 Mbeya na Iringa waliopitishwa ni Cyprian Kuyava, Elias Mwanjala na Erick Ambakisye ilhali Abdusuphyan Sillah hajapitishwa kwa kukosa uzoefu.

Kanda namba 8 mikoa ya Njombe na Ruvuma waliopitishwa ni Golden Sanga, James Mhagama, Vicent Majili na Yono Kevela huku Kanda namba 9 Lindi na Mtwara Athumani Kambi na Dunstan Mkundi (wamepitishwa).

Kanda namba 10 Dodoma na Singida waliopitishwa ni Hussein Mwamba, Steward Masima, Mohamed Aden, Ally Suru na George Komba (wamepitishwa) huku Mussa Sima hajapitishwa kwa kukosa uzoefu.

Kanda namba 11 Pwani na Morogoro waliopitishwa ni Charles Mwakambaya, Gabriel Mkwawee na Francis Ndulane huku Hassan Othuman hajapitishwa kwa kukosa uadilifu huku Kanda namba 12 Kilimanjaro na Tanga waliopitishwa ni Khalid Mohamed na Godluck Moshi wamepitishwa wakati Thabity Kandoro hajapitishwa kwa kukosa uzoefu.

Kanda namba 13 Dar es Salaam: waliopitishwa ni Abdul Sauko, Emmanuel Kazimoto, Ayoub Nyenzi, Shaffih Dauda, Peter Mhinzi, Lameck Nyambaya, Mussa Kissoky, Said Tulliy, Ally Kamtande, Aziz Khalfan, Ramadhani Nassib na Saad Kawemba.

Wakati Saleh Abdallah hajapitishwa kwa kukosa uzoefu, Jamhuri Kihwelu na Bakari Malima (hawajapitishwa kwa kushindwa kuwasilisha vyeti vya elimu ya sekondari).

MCHAKATO WA UCHAGUZI RUREFA NA LIPULI


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyokutana Julai 8, mwaka huu pamoja na mambo mengine pia ilijadili mchakato wa chaguzi za Mkoa wa Rukwa (RUREFA) na timu ya Lipuli inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.

Kuhusu mchakato wa uchaguzi Mkoa wa Rukwa (RUREFA), Kamati ya Uchaguzi inayoongozwa na Mwenyekiti Msomi Wakili Revocatus Kuuli, imeagiza zoezi hilo liendelee na inamtuma Mjumbe wake siku ya usaili, Msomi Wakili Thadeus Karua kwa ajili ya kushuhudia.

“Na pia Kamati ya Uchaguzi itawatuma wajumbe siku ya uchaguzi tarehe 5 Agosti, 2017,” imesema kamati hiyo ilipoagiza kuhusu kuendelea kwa uchaguzi huo.

Kuhusu uchaguzi wa Lipuli,  Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Msomi Wakili Kuuli, imemwagiza Katibu Mkuu wa klabu hiyo, kuendelea na maandalizi ya uchaguzi kama ilivyoelekezwa na kamati kwamba ufanyike Agosti 5, mwaka huu.

“Na Kamati inamtuma mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi Msomi Wakili Mohamed Ally Mchungahela kwa ajili ya uangalizi siku ya uchaguzi,” imesema sehemu ya taarifa ya kamati kwa uongozi wa Lipuli.

Kamati imesisitiza, “Na wanachama waendelee kulipia ada za uanachama kwa kuwa watakaoruhusiwa kupiga kura ni wanachama hai tu.”

AMINA, SOMOYE, ZENA WAREJESHWA KUIONGOZA TWFA



Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amewapa kongole viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA), waliochaguliwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Chichi, Dar es Salaam.

Katika uchaguzi huo uliopata uwakilishi wa theluthi mbili ya mikoa yote ya Tanzania, Amina Karuma alitetea kiti chake kwa kupata kura 47 kati ya 52 za wapigakura wote huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikichukuliwa na Rose Kissiwa ambaye aliyepata kura 42.

Mwanahabari Mkongwe wa Gazeti la Nipashe kutoka Jumba la Magazeti la The Guardian, Somoe Ng’itu alishinda nafasi ya Katibu Mkuu kwa kuvuna kura 49 ilihali Theresia Mung’ong’o alishinda nafasi ya Katibu Msaidizi.

Hilda Masanche alishinda nafasi ya Mweka Hazina wa TWFA kwa kupata kura 25 wakati Mwanahabari mwingine Zenna Chande alishinda nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa kupata kura 44.

Wajumbe Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmine Soudy na Chichi Mwidege hawakushinda baada ya wagombea wote wanne kutopata zaidi ya nusu ya kura kulingana na idadi ya wapigakura kwa mujibu wa katiba ya TWFA.

Uchaguzi huo ulisimamiwa na Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Msomi Wakili George Mushumba, ambaye pia aliwapongeza washindi.

Awali akifungua mkutano huo wa uchaguzi, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Salum Madadi aliwataka wajumbe hao kuwa makini katika kuchagua na kwamba si wakati wa kufanya mzaha katika soka la wanawake.

MBARAKA YUSSUFU ABAKI AFRIKA KUSINI, MWAKYEMBE AIMWAGIA SIFA TAIFA STARS



MSHAMBULIAJI Mbaraka Yussuf wa Taifa Stars, amebaki nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Mbaraka, mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar, ambaye inasemekana amejiunga na Azam kwa ajili ya msimu ujao, hakuweza kumaliza michuano hiyo kutokana na kuumia.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga, alisema juzi usiku baada ya timu hiyo kurejea kutoka Afrika Kusini kuwa, bado hawajaelewa kipi kinachomsumbua mchezaji huyo.

“Tuliyemuacha Afrika Kusini ni Mbaraka Yusuph na taarifa ya nini kinamsumbua na anarudi lini, madaktari watatuambia,” alisema Mayanga.

Wakati huo huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameipongeza Taifa Stars kwa kumaliza michuano ya Kombe la COSAFA ikiwa ya tatu.

“Nchi nzima ilitamani kuwepo hapa kuwapokea, tupo hapa tunawahakikishia vijana wa Taifa Stars kuwa, kazi waliyoifanya ni nzuri,” alisema Dk. Mwakyembe.

HATIMAYE ABDI BANDA APATA TIMU AFRIKA KUSINI


SAA chache ya kuwasili nchini, beki wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Abdi Banda, akitokea Afrika Kusini, alikokuwa akishiriki katika michuano ya Kombe la COSAFA, ameweka wazi kuwa sasa ni rasmi hatoendelea kuitumikia Simba SC msimu ujao.

Banda amejiunga na klabu ya Baroka ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu na amerudi Tanzania kwa ajili ya kuaga kabla ya Julai 12, mwakahuu, kurejea Afrika Kusini kuungana na timu yake hiyo mpya inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini.

“Ni ishu ambayo imekuwa rasmi kwa sasa hivi, lakini ya muda mrefu kwa hiyo nimekuja tu nyumbani mara moja kupata baraka za nyumbani, kwani nimekuja kuaga kwa viongozi wangu wa zamani wa Simba ambao nimekuwa nao muda mrefu," alisema Banda.

TFF YAIPONGEZA TAIFA STARS KUSHIKA NAFASI YA TATU KOMBE LA COSAFA


Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, ameipongeza Taifa Stars kwa mafanikio ya kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Castle la Cosafa - inayoandaliwa na Baraza la Soka kwa nchi za Kusini mwa Afrika.

“Haya ni matunda ambayo tunayaota kila wakati kwa timu kupata ushindi. Tunawapongeza wachezaji, benchi nzima la ufundi likiongozwa na Kocha Salum Mayanga, pamoja na watendaji wote kwa mafanikio ya timu yetu ya Taifa Stars,” amesema Karia alipozungumza na TFF TV online.
 

Amesema kwamba timu hiyo imeonyesha uzalendo wa hali ya juu katika kutafuta mafanikio na ana imani kwamba Tanzania itashiriki michuano mingi ya kimataifa kwa kuwa ina wachezaji wengi makinda huku TFF ikiendelea kuwakuza wengine kwa ajili ya kutimiza ndoto za furaha ya Watanzania kwa sasa na hapo baadaye.
 

Taifa Stars jana usiku Julai 7, mwaka huu iliifunga Lesotho katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Castle Cosafa kwa mapigo 4-2 ya penalti katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Moruleng nchini Afrika Kusini.
 

Katika mchezo huo wa jana, mabao ya Taifa Stars jana yalifungwa na Himid Mao, Abdi Banda, Simon Msuva na Raphael Alpha. Taifa Stars walikosa mkwaju mmoja wa penalti uliopigwa na Shiza Kichuya kwa kugongesga mwamba wa juu, lakini Lesotho walikosa mapigo mawili - moja likiwa limegonga mwamba wa pembeni na jingine likipanguliwa na Kipa Said Mohammed.
 

Taifa Stars inatarajiwa kurejea usiku wa kuamkia kesho Jumapili Julai 9, mwaka huu saa 9.30 usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda ambako itajipanga kwenda Mwanza siku ya Jumatatu saa 12.00 jioni kwa ndege ya Shirika la Ndege la Fast Jet.
 

Itakwenda Mwanza kujiandaa na mchezo dhidi ya Rwanda unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Julai 15, mwaka huu katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN).
 

Timu hiyo ambayo kwa mwaka huu imecheza mechi tisa za kimataifa na kushinda mitano; kutoka sare miwili na kufungwa mmoja wa nusu fainali za Cosafa, itakuwa na kikosi cha wachezaji 20.
 

Wachezaji wanne hawatakuwako kwenye kikosi ambao ni majeruhi Mbaraka Yussuf na Shaban Idd Chilunda kadhalika nyota wa kimataifa ambao hawahusiki na mechi za CHAN ambao ni Thomas Ulimwengu na Elius Maguri.
 

Tayari Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga amewaongeza nyota wawili katika kikosi hicho ambao ni John Bocco na Kelvin Sabato kutoka Majimaji ya Songea kujaza nafasi za Chilunda na Mbaraka.
 

Pia amemwita  kinda Athanas Mdamu ambaye ni mchezaji mwanafunzi kutoka Shule ya kukuza vipaji ya Alliance ya Mwanza ili kumpatia uzoefu kwenye timu ya taifa ya wakubwa. Mdamu ataungana na timu huko Mwanza yaliko makazi yake.

Friday, July 7, 2017

UCHAGUZI TWFA KUFANYIKA DAR ES SALAAM


Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA), sasa utafanyika Dar es Salaam badala ya Dodoma na Morogoro - mikoa iliyotangazwa awali.
 

Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Msomi Wakili George Mushumba, amesema kwamba taratibu zote zimekamilika na kwamba siku ya uchaguzi ni Jumamosi Julai 8, mwaka huu.


Wakili Mushumba ametoa wito kwa wajumbe wote kufika Dar es Salaam Ijumaa Julai 7, mwaka huu kwa ajili ya kufahamu tararibu za awali za uchaguzi.


Tayari Kamati ya Mushumba ilitangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu.


Majina ambayo yamepitishwa ni Amina Karuma, Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Theresia Mung’ong’o, Hilda Masanche, Salma Wajeso, Zena Chande, Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmine Soudy na Chichi Mwidege.


Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.


FOMU ZA KUWANIA UONGOZI TAFCA


Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA), Ramadhani Mambosasa ametoa wito wa walimu wa soka kujitokeza kwa wingi kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi - ngazi ya taifa.


Mambosasa ametoa wito huo ikiwa zimebaki siku mbili tu kwa mujibu wa kanuni kukamilisha hatua hiyo. Fomu hizo zinazopatikana ofisi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam, zilianza kutolewa juzi Julai 3, 2017 na mwisho ni Julai 7, mwaka huu.


“Wanaojitokeza wachache. Wengine wanadai hawafahamu zilizo ofisi za DRFA. Tunatoa wito wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali,” amesema Mambosasa.


Nafasi zilizotangazwa kuwaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina ambao fomu zao zinapatikana kwa Sh 200,000 wakati nafasi za wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu zao zinapatikana kwa Sh 100,000.


UCHAGUZI CHAMA CHA WATAALAMU WA TIBA ZA MICHEZO


Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Wataalamu wa Tiba za Michezo (TASMA), kimetangaza Uchaguzi Mkuu wa chama hicho kwamba utafanyika Agosti 5, mwaka huu katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.


“Wanachama wote wanakaribishwa kushiriki kwa namna moja au nyingine katika zoezi hili muhimu sana,” amesema Mwenyekiti wa kamati hiyo, Leslie Liunda alipokuwa anatangaza ramani ya mchakato wa uchaguzi huo leo Alhamis Julai 06, 2017.


Amesema: Mwanachama ye yote anayependa kukiongoza chama hiki anaombwa kuchukua fomu katika ofisi za Olimpiki Maalumu, zilizoko jirani na Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa ajili ya kugombea nafasi anayoona kuwa anaweza kuimudu.”


Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina ambao fomu zao zinapatikana kwa Sh 200,000 wakati nafasi za wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu zao zinapatikana kwa Sh 100,000.

KAMATI YA UCHAGUZI TFF YAVUNJWA NA KUUNDWA UPYA


Kamati ya Utendaji (EXCOMM) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, imekutana tena leo Jumanne Julai 4, 2017 katika kikao cha dharura ambako ilijadili mgawanyiko katika Kamati ya Uchaguzi ya TFF.


Kamati hiyo ya utendaji inakutana kwa dharura kwa mujibu wa Ibara ya 35 (1) ya Katiba ya TFF inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6). Kikao cha Kamati hiyo kilianza saa 8.58 alasiri hadi saa 10.51 jioni.


Katika kikao chake kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za shirikisho, Karume jijini Dar es Salaam Kamati iliamua kufanya mabadiliko madogo katika Kamati zake za Kisheria na Kamati za uchaguzi kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 44 (7) na Ibara ya 52 inayotoa mamlaka ya kufanya mabaduiliko hayo.


Katika Kamati ya Uchaguzi, EXCOMM imeteua Mawakili kuongoza kamati hiyo wakiongozwa na Msomi Wakili Revocatus Kuuli; Mheshimiwa Wakili Mohammed Mchengelwa; Msomi Wakili Malangwe Mchungahela; Msomi Wakili Kiomoni Kibamba na Msomi Wakili Thadeus Karua.


Katika Kamati ya Rufaa Uchaguzi, EXCOMM imeteua Msomi Wakili, Abdi Kagomba kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Msomi Wakili Kenneth Mwenda na wajumbe ni Msomi Wakili  Rashid Sadalla, Mhe. Jabir Shekimweri na Mohammed Gombati.


Kadhalika katika kamati za kisheria za TFF, ikianzia Kamati ya Maadili, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Hamidu Mbwezeleni kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Msomi Wakili Steven Zangira na wajumbe ni Mhe. Glorius Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhressa.


Kamati ya Rufaa na Maadili, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Ebenezer Mshana kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Naibu Kamisha katika Jeshi la Polisi (DCP), Mohammed Mpinga na Wajumbe ni Msomi Wakili Benjamin Karume; Dk. Lisobine Kisongo na Mrakibu Msaidizi wa Polisi - ASP Benedict Nyagabona.


Kamati ya Nidhamu ya TFF, EXCOMM imeteua Tarimba Abbas kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Peter Hella huku Wajumbe wakiwa ni Boniface Lyamwike, Dk. Billy Haonga na Kassim Dau.


Kamati ya Rufaa ya Nidhamu, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Rahim Shaban kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Siza Chenja huku Wajumbe wakiwa ni Abbas Mtemvu; Amani Mulika, Amin Bakhressa na Stella Mwakingwe.