KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, July 3, 2017

TAIFA STARS YATINGA NUSU FAINALI MICHUANO YA KOMBE LA COSAFA


TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars jana ilifuzu kucheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la COSAFA Castle baada ya kuwachapa wenyeji Afrika Kusini bao 1-0.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng mjini Rusternburg, Taifa Stars ilijipatia bao hilo la pekee dakika ya 18 kupitia kwa mshambuliaji Elias Maguri.

Maguli alifunga bao hilo kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa kiungo Muzamil Yassin.

Afrika Kusini itabidi ijilaumu kwa kushindwa kutoka uwanjani na ushindi kwani ilitawala sehemu kubwa ya pambano hilo, lakini mabeki wa Taifa Stars walikuwa imara kuondosha hatari hizo.

Kutokana na ushindi huo, Taifa Stars sasa itamenyana na Zambia katika mechi ya nusu fainali itakayopigwa keshokutwa.

No comments:

Post a Comment