KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, July 5, 2017

YANGA YAMTAMBULISHA RASMI IBRAHIM AJIB

KLABU ya Yanga leo imemtambulisha rasmi mshambuliaji wake mpya, Ibrahim Ajib, aliyesajiliwa msimu huu kutoka klabu ya Simba.

Uongozi wa Yanga umemtambulisha nyota huyo wa zamani wa Simba katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo, mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.

Ajib alikabidhiwa jezi ya Yanga yenye nembo ya wadhamini wake, Kampuni ya Sport Pesa na Meneja wa timu hiyo, Hafidh Mohamed, mbele ya Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Boniface.




Akizungumza katika hafla hiyo, Boniface alisema wanayo furaha kukamilisha taratibu zote za kumsajili Ajib baada ya kuwa amekamilisha mkataba wake wa kuitumikia Simba.

Boniface alisema Ajib anatarajiwa kuungana na wachezaji wenzake kuanza kambi ya kujiandaa na mechi ya kuwania Ngao ya Hisani kati yao na Simba, itakayochezwa mapema mwezi ujao.

Mbali na Ajib, Yanga pia imefanikiwa kuwaongezea mikataba washambuliaji wake Donard Ngoma kutoka Zimbabwe na Hamisi Tambwe kutoka Burundi.

No comments:

Post a Comment