KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, July 16, 2017

TAIFA STARS YATOKA SARE NA RWANDATIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania Bara, jana ilianza vibaya michuano ya kuwania kufuzu kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), baada ya kulazimishwa kutoka sare ya bao 1-1 na Rwanda.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Rwanda ilikuwa ya kwanza kupata bao kabla ya Tanzania Bara kusawazisha.

Kutokana na matokeo hayo, Tanzania Bara sasa italazimika kucheza kufa na kupona kushinda mechi ya marudiano itakayochezwa Jumamosi mjini Kigali ili iweze kusonga mbele.

Mshindi kati ya Tanzania Bara na Rwanda, atamenyana na mshindi wa mechi kati ya Sudan Kusini na Uganda, ambazo nazo zilitoka suluhu jana mjini Juba.

Bao la Rwanda lilipatikana dakika ya 17 kupitia kwa mshambuliaji wake, Dominique Savio baada ya kupokea krosi kutoka kwa Emmanuel Imanishimwe.

Tanzania Bara ilisawazisha bao hilo dakika ya 34 kwa njia ya penalti iliyopigwa na nahodha Himidi Mao baada ya beki mmoja wa Rwanda kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

No comments:

Post a Comment