'
Sunday, December 9, 2012
AZAM YAMWOMBEA NGASA RUHUSA TFF
Azam FC imeandika barua TFF leo ikiwaomba wamruhusu Ngasa kwenda Sudan baada ya mchezo for medical test with Mareikh nakala imeenda kwa simba
Msukumo uliotufanya tuandike barua hii ni kwa kutambua kuwa hii ni nafasi muhimu kwa ngasa na Taifa kwani anakwenda kucheza kwenye timu yenye uwezo na miundombinu kama barani Afrika na inayoshiriki ligi ya mabingwa Afrika karibu kila msimu kitu ambacho kitamuongezea Ngasa kiwango na kuwa na msaada kwa Taifa.
Pia tunapenda kuweka wazi Value ya Signing Fees na Mshahara ambao Ngasa atapewa na Elmereikh ambao ni $4000 (Shilingi Milioni 6 kwa mwezi kwa miaka miwili takribani 144 Milioni) na Signing Fees $ 50,000 Milioni 80 kwa hiyo Ngasa ataweka kibindoni zaidi ya shilingi milioni 230 kwa miezi 24.
Hizi ni pesa nyingi kwa mchezaji wa kitanzania kwa maendeleo ya mchezaji na Familia yake na yatawapa msukumo vijana wengi wenye kipaji kama Ngasa kufanya bidii kwenye soka na kuliletea maendeleo taifa.
Azam FC inaomba TFF imruhusu Ngasa kwenda Sudan akitokea Uganda kwenda kukamilisha vipimo vya Afya na usajili na Azam FC ipo tayari kukaa na simba na kuzungumza juu ya uhamisho huu kwa usimamizi wa TFF.
Hapa ieleweke kuwa ingawa Azam FC inajua haki zake kisheria lakini pia imeamua kupunguza msimamo wake kukubali mazungumzo kwa kuangalia zaidi athari ambazo mchezaji anaweza kupata kimaslahi na kimaendeleo ya uchezaji wake na mpira wa Tanzania kwa ujumla kutokana na mgogoro huu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment