KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, December 11, 2012

TAIFA QUEENS WAPOKEWA KIFALME



Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi akiwa Mwenyekiti wa wake za viongozi, Germina Lukuvi mara baada ya timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Queens) iliporejea nchini na Kombe la Michiuano ya Kimataifa iliyofanyika nchini Siangapore

Wachezaji na viongozi wa timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Quees) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao baada ya kuwasili jana kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea nchini Singapore.


TIMU ya taifa ya Netiboli ya Tanzania ‘Taifa Queens’ imerejea kwa kishindo jana baada ya kushiriki na kutwaa Kombe la michuano ya Kimataifa iliyokuwa ikifanyikia Singapore barani Asia.
Taifa Queens ilitwaaa ubingwa huo baada ya kuingia fainali ikiwa na pointi 10 ikicheza na timu ya Malasia iliyokuwa na pointi 4 ambapo ilifanikiwa kuifunga magoli 45-38.
Akizungumza baada ya kurejea, Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi alisema maandalizi ni kitu kizuri sana, anaamini kocha aliwapa wachezaji mbinu za kutosha hadi kupelekea ubingwa huo.
“Hii imetusaidia sana maana kocha mwenyewe ni kijana hivyo anambinu za kisasa kitu kilichotusaidia wakati tukiwa ugenini, hakuna kitu kizuri kama kupigiwa wimbo wa taifa lako ukiwa ugenini huku wazungu ambao ni wenyeji wa mashindano hayo wakiwa penbeni,” alisema Bayi.
Kwa upande wake Kocha wa Taifa Queens, Mary Waya alisema mashindano yalikuwa ni magumu anawapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo ambao umemuweka pazuri yeye pamoja na Watanzania wote kwa ujumla.
“Kila kitu unatakiwa umtangulize mungu, akili, na nguvu ndio zinafuata naimani wachezaji wangu walikuwa makini na kujua nini wamekifuata huko, akili ni kitu cha muhimu ukiwa mchezoni hivyo mimi sina la kusema zaidi ni kumshukuru mungu kwa ushindi tulioupata,” alisema Kocha huyo ambaye ni Mmalawi.
Kocha huyo alisema amefurahishwa na ushindi huo na kwamba kwasasa anajipanga kuifua timu hiyo kwaajili ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia.
Naye Nahodha wa timu hiyo, Lilian Sadolin alisema anamshukuru mungu kwa ubingwa huo pia Watanzania wanatakiwa kuendelea kuwapa sapoti katika mashindano mbalimbali.
“Wakati tunaondoka niliwaahidi Watanzania lazima turudi na ushindi, sisi ubingwa tushaapata kabla hatujaenda kule tulienda kutimiza wajibu, naimani tuliwazidi mbinu unapokuwa uwanjani unatakiwa kuwa na mbinu za ziada hivyo tunamshukuru Mungu kwa ushindi tulioupata,” alisema Lilian

No comments:

Post a Comment