KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, December 5, 2012

AKI, UKWA WACHENGUA MASHABIKI SWAZILAND




MBABANE, Swaziland
WACHEZA filamu nyota wa Nigeria, Chinedu Ikedieze 'Aki' na Osita Iheme 'Ukwa' mwishoni mwa wiki iliyopita walipata mapokezi makubwa walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Matsapha mjini hapa.
Aki na Ukwa wamealikwa nchini Swaziland kwa ajili ya kufanya maonyesho matatu ya vichekesho vitokanavyo na filamu walizowahi kucheza.
Baada ya wasanii hao kutoka nje ya uwanja huo, walipatwa na mshangao mkubwa kukuta mamia ya watu waliokuwa wakiwasubiri kwa shauku kubwa.
Kundi hilo la watu lilivamia kwenye mlango wa kutokea wa eneo la VIP huku kila mmoja akiwa na shauku kubwa ya kuwaona wasanii hao kwa karibu.
Hata maofisa wa polisi waliokuwa wakilinda usalama pamoja na wafanyakazi wa uwanja huo nao walijikuta wakishindwa kujuia kuwasogelea wacheza filamu hao kwa karibu.
Baadhi yao walitumia simu zao za mkononi kuwapiga picha wasanii hao na wengine kuwaomba kupiga nao picha za pamoja.
"Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi usiku wa leo na kesho kuja kutuona kwenye maonyesho yetu. Tunaahidi kuwaletea maonyesho mazuri kwa siku zote mbili,"walisema wasanii hao baada ya kutoka nje ya uwanja huo wa ndege.
Aki aliwaahidi mashabiki hao kwamba, wakati wa monyesho hayo, watatoa nafasi ya kupiga nao picha za pamoja na pia kujumuika nao kufanya mambo mbalimbali.
Wacheza filamu hao walitarajiwa kufanya maonyesho kwenye ukumbi wa Convention Centre na Mavuso Trade Centre.

1 comment: