KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, December 21, 2012

LULU AACHIWA KWA DHAMANA


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo asubuhi imemuachia kwa dhamana msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayetuhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba ‘The Great’.
Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kupitia vifungu vya sheria na kuona kuwa, kwa kosa aliloshtakiwa sasa, msanii huyo anaweza kupata dhamana.
Hatua hiyo inakuja baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kubadilisha mashitaka ya mwanadada huyo kutoka kesi ya mauaji hadi kuua bila kukusudia.
Kutokana na mabadiliko hayo, hata kama Lulu atapatikana na hatia hiyo, hatahukumiwa kunyongwa, badala yake anaweza kufungwa maisha au miaka kadhaa.
Lulu anakabiliwa na tuhuma za kumuua The Great Kanumba aliyefariki dunia, Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwake Vatican, Sinza Dar es Salaam.

1 comment:

  1. ACHA UONGO. KAACHIWA SAA NGAPI NA NANI KAMPATIA DHAMANA?

    ReplyDelete