KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, December 6, 2012

SHINDANO LA MISS EAST AFRICA LASOGEZWA MBELE



SHINDANO la Miss East Africa 2012, ambalo lilitarajiwa kufanyika kesho, limesogezwa mbele hadi Desemba 21, mwaka huu, lengo likiwa ni kuhakikisha linafanyika katika viwango bora zaidi kuliko mashindano mengine.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam, jana na Kampuni ya Rena Events Ltd, inayoandaa shindano hilo, imesema shindano hilo limesogezwa kutokana na maoni ya wadau.

Imesema kuwa maandalizi yote kwa ajili ya shindano hilo yalishakamilika na warembo wote wako kambini na siku chache zilizopita walikuwa wakijivinjari kwenye mbuga za wanyama kwa ajili ya kupiga picha za video vitakazorushwa katika luninga duniani kote.

Warembo watakaochuana kuwania taji hilo wanaendelea kufundwa kwa kupewa mbinu mbalimbali katika kambi iliyopo Hoteli ya White Sands ya Jijini Dae es Salaam, chini ya mwalimu wao Sarah Nyamwenge kutoka Uganda.

Mashindano ya Miss East Africa 2012 yatafanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na yatashirikisha warembo kutoka Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Seychelles, Sudani Kusini na warembo mbalimbali wa Afrika mashariki walioshindana katika nchi mbalimbali za Ulaya ambazo ni Ubelgiji, Ufaransa, na Uholanzi.

Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam na ambapo kwa mwaka huu yanadhaminiwa na Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, TANAPA, Ethiopian Airlines, DTP, Ako Catering, Darlings Hair, Seascape Hotel, Satguru na Clouds Fm

No comments:

Post a Comment