KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, December 11, 2012

SIMIYU WAFUNGUA TAWI LA YANGA



WANACHAMA wa Yanga waliopo mkoani Simiyu, wamefungua tawi la klabu hiyo lenye makao yake katika mtaa wa stendi ya zamani Bariadi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu wa tawi hilo, Athuman Kihamia ‘Teacher’ mwenye kati ya uanachama ya Yanga namba 001901, alisema kuwa hadi sasa wamepatikana wanachama zaidi ya mia nane waliojiandikisha katika tawili hilo.
Teacher ambaye kabla ya kuhamia Simiyu kikazi alikuwa ni Katibu wa Tawi la Yanga Bomba, Dar es Salaam, alisema kuwa Mwenyekiti wa tawi hilo, ni Bunzili Simanamagu, ambaye ni mmoja wa wanachama maarufu wa Yanga katika mkoa huo uliotokana na mikoa ya Shinyanga na Mwanza.
Mwanachama huyo maarufu wa Yanga ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Tawi la Uhuru Kariakoo, akitoa mchango wake mkubwa kwa timu yao kutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame, alisema kuwa wamejipanga kuifanyia makubwa klabu yao hiyo.
“Huu ni mkoa mpya, hivyo nimeona nitumie uzoefu wangu wa kuitumikia Yanga nilipokuwa Dar es Salaam, kwa kushirikiana na wanachama waliopo mkoani hapa ili kujenga ngome imara ya wanajangwani,” alisema.
Aliongeza: “Moja ya mikakati yetu ni kuhakikisha tawi letu linakuwa moja ya matawi ya Yanga yenye nguvu zaidi hapa nchini kuliko hata ilivyo huko Dar es Salaam, tunaamini hilo linawezekana iwapo wanachama wa Yanga waliopo hapa Shimiyu tutaungana na kushirikiana.”
Teacher alisema wamepanga kulizindua tawi lao mara baada ya mkutano mkuu wa Yanga hapo mwakani, ikiwa ni pamoja na kuanzisha kampeni ya kuhakikisha kila mwenye mapenzi na Yanga mkoani humo, anakuwa na kadi.
“Tuna mipango mingi tuliyopanga kuifanya, hivyo tunawaomba wapenzi wa Yanga waliopo mkoani hapa, kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili waweze kutambulika kama wana-Yanga badala ya kuishia kuwa mashabiki wa kawaida,” alisema.

No comments:

Post a Comment