KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, December 9, 2012

POULSEN KUTANGAZA KIKOSI CHA TAIFA STARS KESHO


Kilimanjaro Stars iliyokuwa inashiriki michuano ya Kombe la Chalenji jijini Kampala, inarejea Dar es Salaam leo Jumapili (Desemba 9, 2012). Timu hiyo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 11 kamili jioni kwa ndege ya PrecisionAir.

Baada ya Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes kumaliza kushiriki mashindano ya Kombe la Chalenji jijini Kampala, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen kesho Jumatatu (Desemba 10, 2012) saa 6 kamili mchana ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) atatangaza kikosi chake kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12, 2012 jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22, 2012 katika Uwanja wa Taifa.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment