KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, December 1, 2012

KILIMANJARO STARS YAFANYA MAUAJI CHALENJI



TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars jana ilifuzu kucheza robo fainali ya michuano ya soka ya Kombe la Chalenji kwa kishindo baada ya kuibugiza Somalia mabao 7-0 katika mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Lugogo mjini Kampala.
Mshambuliaji Mrisho Ngasa ndiye aliyeibuka shujaa wa Kilimanjaro Stars baada ya kuifungia mabao matano kati ya saba. Mabao mengine mawili yalifungwa na John Boco.
Ngasa sasa anaongoza kwa ufungaji mabao katika michuano hiyo, akiwa na mabao matano, akifuatiwa na Boko mwenye mabao manne na Selemani Ndikumana wa Burundi mwenye mabao matatu.
Kutokana na ushindi huo, Kilimanjaro Stars sasa itakutana na Rwanda katika mechi ya robo fainali itakayopigwa kesho kuanzia saa nane mchana na kufuatiwa na mechi nyingine kati ya Zanzibar na Burundi, itakayochezwa kuanzia saa 10 jioni.
Zanzibar imetinga hatua hiyo kama best looser kutoka katika kundi C baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Malawi.
Kwa mujibu wa ratiba, mechi zingine za robo fainali zitachezwa Jumanne kayi ya Kenya na Malawi kuanzia saa 10 jioni na kati ya Uganda na Eritrea kuanzia saa moja usiku.

No comments:

Post a Comment