KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, December 7, 2012

BWALA KUIONGOZA ZAMBIA DAR


Mshambuliaji gwiji wa zamani wa Zambia, Kalusha Bwalya atauongoza msafara wa timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo wakati itakapokuja nchini kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Tanzania baadaye mwezi huu.
Zambia, ambao wanashikilia ubingwa wa Afrika waliotwaa kwenye fainali zilizopita zilizoandaliwa kwa pamoja na Equatoria Guinea na Gabon, watawasili nchini Desemba 18, 2012 na kucheza mechi hiyo ya kirafiki Desemba 22, 2012 kabla ya kurejea kwao Desemba 23, 2012.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, katibu mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah alisema kuwa Chama cha Mpira wa Miguu cha Zambia (FAZ) kimeiandikia Shirikisho lake barua kikielezea kuwa gwiji huyo ataambatana na timu katika ziara hiyo ya kwanza kwa Zambia nchini tangu ilipotwaa Kombe la Afrika mwaka 2012.
“Kwa mara nyingine Tanzania imebahatika kutembelewa na mmoja wa magwiji wa soka barani Afrika baada ya Abeid Pele (wa Ghana) kutembelea nchini mwezi uliopita,” alisema Osiah. “FAZ wametutaarifu kuwa Bwalya ndiye atakayeongoza msafara wa timu itakapokuja nchini na hivyo Watanzania watapata nafasi nyingine ya kukutana na kuongea na mmoja wa magwiji wa Afrika.
“Tuliona jinsi wachezaji wa Serengeti Boys walivyohamasika kutokana na maneno ya Abedi Pele na tunatarajia ndivyo Bwalya atakavyofanya kwa vijana wetu na wadau wa mpira wa miguu. Tutajitahidi kuandaa program itakayowezesha vijana wetu kuongea naye.”
Bwalya alikuwemo kwenye kikosi cha Zambia, maarufu kama KK Eleven kilichokuwa kinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka 1992, lakini wachezaji wote wakateketea wakati ndege yao ilipoanguka kwenye pwani ya Afrika Magharibi.
Bwalya alinusurika kwenye ajali hiyo kutokana na kupande ndege tofauti. Hata hivyo, akiwa na kikosi kilichojaa damu Changa, gwiji huyo wa Zambia aliiongoza nchi yake kufika fainali. Kalu aliichezea klabu maarufu ya Uholanzi, PSV Einhoven na baadaye kwenda Mexico ambako alistaafia kabla ya kupewa kazi ya ukocha na baadaye kurejea Zambia ambako pia aliifundisha timu ya taifa.
Chini ya uongozi wake, Zambia imefanikiwa kufuta nuksi ya kukosa vikombe barani Afrika baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya pekee mwaka huu

No comments:

Post a Comment