KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, August 7, 2013

LIGI KUU YAZIDI KUPATA NEEMA

WAKATI kituo cha televisheni cha Azam kimeingia mkataba wa kuonyesha laivu mechi za ligi kuu ya Tanzania Bara, kampuni nyingine zaidi huenda ikajitokeza kuidhamini kamati ya ligi hiyo.

Habari zilizopatikana jana kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zimeeleza kuwa, tayari kamati hiyo imeshaanza kufanya mazungumzo ya awali na kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa habari hizo, kampuni hiyo inajihusisha na utengenezaji wa vinywaji baridi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, wanatarajia kuitangaza kampuni hiyo wiki ijayo baada ya mazungumzo kati yao kukamilika.

Karia alisema lengo la udhamini huo ni kuiwezesha kamati yake kufanyakazi zake kwa ufanisi wakati wa kusimamia ligi hiyo, inayotarajiwa kuanza Agosti 24 mwaka huu, ikizishirikisha timu 14.

"Tunataka kwenda na wakati na kuiga mfano wa CAF (Shirikisho la Soka Afrika) na FIFA (Shirikisho la Soka la Dunia) ili kamati na TFF nazo ziweze kuwa na wadhamini wake kwa lengo la kufanikisha utendaji wa kazi za kila siku,"alisema.

No comments:

Post a Comment