KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, August 7, 2013

MGOSI ATUA MTIBWA SUGAR



MSHAMBULIAJI wa zamani wa klabu ya Simba, Mussa Hassan 'Mgosi' amejiunga na klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

Mgosi, ambaye msimu uliopita aliichezea JKT Ruvu ya mkoani Pwani, amejiunga na Mtibwa kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Kocha Mkuu wa Mtibwa, Mecky Maxime alisema kwa njia ya simu jana kutoka Morogoro kuwa, wameamua kumsajili Mgosi kutokana na uwezo wake kisoka bado kuwa juu.

Maxime alisema pia kuwa, uamuzi wao wa kumsajili Mgosi umelenga kuziba pengo la mshambuliaji wao, Hassan Javu aliyejiunga na Yanga hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Maxime, mshambuliaji huyo nyota wa zamani wa Simba ametia saini mkataba wa kuichezea Mtibwa kwa mwaka mmoja na anatarajiwa kujiunga na kikosi hicho hivi karibuni.

Katika hatua nyingine, kiungo wa kimataifa wa Uganda, Patrick Ochan ametemwa kwenye kikosi cha mabingwa wa zamani wa Afrika, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mtandao wa TP Mazembe umeripoti wiki hii kuwa, Ochan ametemwa kwenye kikosi cha timu hiyo kutokana na kutokidhi mahitaji ya klabu.

Mbali na Ochan, mtandao huo umemtaja mchezaji mwingine aliyetemwa kwenye kikosi hicho kuwa ni Mike Mutyaba wa Uganda na tayari wote wawili wamesharejea nchini kwao.

No comments:

Post a Comment