KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, August 4, 2013

YANGA YAILOWESHA MTIBWA



MABINGWA wa soka wa Tanzania Bara, Yanga jana walidhihirisha nia yao ya kutetea taji hilo msimu ujao baada ya kuitandika Mtibwa Sugar mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkali, Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0. Bao hilo lilifungwa na Saidi Bahanuzi dakika ya 26 baaa ya kutokea piga nikupige kwenye lango la Mtibwa.

Mtibwa ilipata bao la kusawazisha dakika ya 57 kupitia kwa Shabani Kisiga. Alifunga bao hilo kwa njia ya penati baada ya beki Rajabu Zahir wa Mtibwa kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Jerry Tegete aliifungia Yanga bao la pili dakika ya 81 kwa njia ya penalti baada ya kuangushwa na beki mmoja wa Mtibwa ndani ya eneo la hatari.

Hussein Javu aliiongezea Yanga bao la tatu dakikaya 87 baada ya kipa Hussein Sharrifu wa Mtibwa kutema shuti la Tegete.

No comments:

Post a Comment