KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, August 23, 2013

LULU ATANGAZA VIINGILIO VYA FOOLISH AGE



MSANII Elizabeth Michael 'Lulu' ametangaza viingilio katika onyesho la uzinduzi wa filamu yake mpya, inayokwenda kwa jina la Foolish Age. Filamu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 30 mwaka huu kwenye ukumbi wa VIP wa Mlimani City mjini Dar es Salaam. Lulu ameeleza kupitia mtandao wa facebook kuwa, kiingilio kitakuwa sh. 30,000 kwa mtu mmoja na sh. 300,000 kwa watu watakaolipia meza maalumu. Kwa mujibu wa Lulu, uzinduzi wa filamu hiyo utapambwa na burudani ya muziki kutoka kwa bendi ya Machozi, inayoongozwa na Judith Wambura 'LadyJaydee' na wasanii Barnaba Elias na Amin kutoka kundi la THT. Filamu hiyo ni ya kwanza tangu Lulu alipotoka gerezani na imetengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited ya Dar es Salaam. "Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu.. Ninayo furaha ya kuwafahamisha kuwa Agosti 30 ndiyo siku nitakayozindua movie yangu mpya iitwayo Foolish Age. Hatimaye narudi kazini,"ameeleza Lulu. "Nahitaji sapoti ya mashabiki wote wa Lulu na wale wa Bongo Movi,"ameongeza msanii huyo mwenye mvuto mbele ya luninga.

No comments:

Post a Comment