KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, August 14, 2013

STEWART ALALAMIKIA RATIBA LIGI KUU



KOCHA Mkuu wa Azam, Stewart Hall ameilalamikia ratiba ya michuano ya soka ya ligi kuu ya Tanzania Bara kwa madai kuwa haikutenda haki kwa timu yake.

Stewart ameueleza mtandao wa Bin Zubeiry akiwa Afrika Kusini juzi kuwa, ratiba hiyo itaifanya timu yake icheze mechi nyingi kwa muda mfupi na hivyo kuikosesha muda wa kupumzika.

"Tunacheza Agosti 24 na 28, mechi zote ugenini. Hii ni mbaya," alisema kocha huyo kutoka Uingereza.

"Halafu kuna mapumziko ya kupisha kambi ya Taifa Stars kwa siku 14. Taratibu za FIFA hazisemi hivyo, ni siku saba tu. Ligi inaumia kwa ajili hii. Tupo nje ya Kombe la CHAN, kwa nini timu ikae kambini siku zote hizo? " alihoji kocha huyo.

Stewart pia alilalamikia uchezeshaji mbovu wa mechi za ligi hiyo, unaofanywa na baadhi ya waamuzi, ambao ameuelezea kuwa umelenga kuzibeba baadhi ya timu.

Pamoja na kuwepo kwa kasoro hizo, kocha huyo alisema matumaini ya timu yake kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu ni makubwa.

"Lazima tupambane kutimiza ndoto huku tukijua marefa si wazuri,"alisema kocha huyo mwenye makeke.

Stewart alisema baadhi ya waamuzi wa Tanzania wanahitaji msaada, ikiwa ni pamoja na kuongezewa mishahara, posho na kutengenezewa mazingira mazuri ya kazi.

Alisema iwapo hayo hayatafanyika, waamuzi wengi wataendelea kushawishika na rushwa na kuziumiza timu bora kwa kuzipendelea baadhi ya timu zinazowahonga.

No comments:

Post a Comment