KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, August 20, 2012

MANCHESTER UNITED SASA YAMNYEMELEA KAKA

SIKU chache baada ya kumsajili mshambuliaji Robin Van Persie kutoka Arsenal, klabu ya Manchester United inajiandaa kumsajili kwa mkopo wa muda mrefu mshambuliaji Ricardo Kaka wa Real Madrid ya Hispania.

Real Madrid ipo tayari kumuuza Kaka kwa mkopo wakati ikiwa inajiandaa kumsajili mshambuliaji Luka Modric.

Mbali na Manchester United, klabu zingine zilizoonyesha nia ya kumsajili Kaka ni Galatasaray ya Uturuki na AC Milan ya Italia.

Kocha Mkuu wa Manchester United, Sir Alex Ferguson anampa nafasi kubwa Kaka, lakini pia ameonyesha wasiwasi wake kuhusu kiwango chake na majeruhi, ambayo yamekuwa yakimuandama mara kwa mara.

Manchester United wiki iliyopita ilimsajili Robin Van Persie kutoka Arsenal na jana ilimsajili beki mwingine mpya wa kushoto, Alexander Buttner kutoka Vitesse Arnhem ya Uholanzi kwa uhamisho wa pauni milioni 3.9.

Kaka alikuwa benchi jana wakati Real Madrid ilipolazimishwa kutoka sare ya bao 1-1 na Valencia katika mechi ya ufunguzi ya ligi kuu ya Hispania, La liga.

No comments:

Post a Comment