KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, August 10, 2012

AIRTEL RISING STAR YAPATA 16 WA MAANA

Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando (kushoto),
akizungumza na Waadishi wa Habari wakati wa kutangaza kikosi
cha timu ya soka cha Airtel Rising Stars, kitakachoshiriki michuano
ya Inter-Continental Jijini Nairobi, Kenya baadaye mwezi huu.
Kulia ni .Ofisa Habari wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Jane
Matinde.


KAMPUNI ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake maalum wa
kuvumbua na kukuza vipaji vya soka nchini ujulikanao kama Airtel
Rising Stars leo wametangaza kikosi cha wachezaji 16
watakaoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ya
vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel yatakayofanyika Nairobi
kuanzia Agosti 19 hadi 25, mwaka huu.

Wachezaji hao walichaguliwa na jopo la makocha kwa
kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Chama cha
Soka Dar es Saalam (DRFA), wakati wa fainali za Taifa za Airtel
Rising Stars zilizofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es
Salaam Juni mwaka huu na kushirikisha timu kutoka mikoa ya Lindi,

Mbeya, Arusha, Ilala, Temeke na Kinondoni.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za TFF jana,
Ofisa Maendeleo wa Soka wa TFF, Salum Madadi aliwataja vijana
watakaowakilisha Tanzania kuwa ni Denis Richard, Juma Hamza,
Abdul Selemani, Ishaka Shekolowa na Bakari Ally kutoka mkoa wa
kisoka wa Temeke.

Wengine ni Abdulatif Mohamed, George Joseph na Badilu Said
(Lindi), Said Kassim, Amos Ikungula, Paul Balama na Goodluck
Mabiku (Ilala), Joel Kasimula na Ibrahim Mtenga (Mbeya),
Sntkony Angelo na Suleiman Yunus (Arusha).

Mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa na ushindani mkali
yatashirikisha wachezaji wengine nyota wa ARS kutoka nchi za
Kenya, Uganda, Malawi, DRC, Congo Brazzaville, Nigeria, Ghana,
Zambia, Niger, Gabon, Burkina Fasso, Sierra Leone, Chad,
Madagascar na Tanzania.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano
Mallya, amesema kuwa lengo la mashindano hayo ya kimataifa ni
kuwapa vijana fursa zaidi ya kuendeleza vipaji vyao na kupata
uzoefu.

“Vile vile Airtel Rising Stars inatoa nafasi kwa wanasoka
hawa chipukizi kuweza kupanua jiografia yao na kujenga urafiki
na vijana wenzao kutoka nchimbali mbali”, alisema Singano.

Michuano hiyo itafuatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa ambayo
pia itafanyika Nairobi chini ya walimu wa soka la vijana kutoka
klabu maarufu duniani ya Manchester United ya Uingereza.

Kliniki kama hii ilifanyika mwaka jana kwenye uwanja wa kisasa

wa soka jijini Dar es Salaam na kushirikisha vijana kutoka Kenya,

Malawi, Sierra Leone na wenyeji Tanzania.

Katika kliniki ya mwaka huu, Tanzania itawakilishwa na wachezaji
sita miongoni mwao ni wavulana watatu na wasichana watatu
ambao walioibuka kuwa wachezaji bora wakati wa fainali za Taifa
jijini Dar es Salaam mwezi Juni.

Airtel Rising Stars ni mpango kabambe wa kuibua na kukuza
vipaji vya wanasoka wanaochipukia barani Afrika. Walengwa ni
wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba
ambao watapata fursa ya pekee ya kuonyesha vipaji vyao mbele
ya waatalum wa mpira wa miguu wa kitaifa na kimataifa.

No comments:

Post a Comment