KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, August 16, 2012

RIBERY, BENZEMA WABANWA KWA UKAHABA

Frank Ribery

Karim Benzema


PARIS, Ufaransa
WANASOKA nyota wa Ufaransa Franck Ribery na Karim Benzema wanatazamiwa kupandishwa kortini kujibu mashitaka ya kufanya mapenzi na changudoa mwenye umri mdogo.

Nyota hao, ambao jana walitarajia kushuka uwanjani kuchezea Ufaransa dhidi ya Uruguay, walikuwa wanachunguzwa miaka miwili iliyopita.

Wote wanakanusha madai hayo na msichana wanayedaiwa kufanya naye ngono, Zahia Dehar, amesema alikula uroda na wachezaji hao huku wakifahamu fika alikuwa na umri wa miaka 16 wakati huo.

Uchunguzi wa mahakama umewaona Ribery na Benzema wana kesi ya kujibu, lakini tarehe ya kusikilizwa hajapangwa.

Uamuzi wa hakimu Andre Dandot unatofautiana na taarifa ya waendesha mashitaka wa Paris, ambao Novemba 2011 walisema kuwa kesi inapaswa kufutwa kwa sababu wachezaji hao walikula uroda na msichana huyo bila kujua alikuwa na umri mdogo.

Watu sita binafsi walitoa ushahidi na baadhi yao watashitakiwa kwa kutoa kauli za uwongo zilizoikanganya mahakama.

Chini ya sheria za Ufaransa, kujihusisha kimapenzi na kahaba chini ya miaka 18 adhabu yake kufungwa jela miaka mitatu pamoja na kupigwa faini ya dola 55,000.

Sakata la Zahia, lilichomoza, miaka miwili iliyopita na polisi walichunguza madai ya klabu ya Paris iliyoruhusu machangudoa wenye umri mdogo kuingia kujirusha.

Tuhuma hizo ziliibuliwa 2008 na 2009.Mwanasheria anayemwakilisha mshambuliaji huyo wa Real Madrid, Karim Benzema, Sylvain Cormier alisema kuwa mteja wake hana hatia na amejipanga kusimama kidete kumtetea.

Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps alisema sakata hilo lipo mikononi mwa vyombo vya sheria na halitaathiri matokeo ya timu hiyo uwanjani.

No comments:

Post a Comment