KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, August 16, 2012

RITA: SIAMINI KAMA BADO NATESA NOLLYWOOD

LAGOS, Nigeria
BAADA ya ukimya wa muda mrefu, mcheza filamu nyota wa Nigeria, Rita Dominic ameibuka na kusema haamini kuona kwamba bado anatesa katika Nollywood.
Rita alisema hayo wiki hii alipohojiwa na mtandao wa naijerules kuhusu mwenendo wa uigizaji filamu ulivyo hivi sasa nchini Nigeria.
Mwanadada huyo mwenye sura jamali alisema, yapo mabadiliko makubwa katika fani hiyo ikilinganishwa na miaka michache iliyopita.
Rita, ambaye alishinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike wa Nigeria 2012 alisema, anaona fahari kuwa sehemu ya mabadiliko hayo katika uigizaji filamu.
“Kwa kweli siamini kuona kuwa, bado nakubalika katika fani ya uigizaji Nollywood,”alisema mwanadada huyo mwenye jisimu lenye mvuto.
“Yapo mabadiliko makubwa hivi sasa. Siamini kama ningekuwepo hapa kushuhudia mabadiliko haya, lakini bado nipo. Fani ya uigizaji imepiga hatua kubwa kimaendeleo,”alisema.
Rita ni mmoja wa waigizaji, ambao fani hiyo imewapa mafanikio makubwa kimaisha. Dada huyo ni mmoja wa waigizaji matajiri wa kike nchini Nigeria.
Hivi karibuni, Rita alikuwa bize akishiriki kucheza filamu mpya, ambayo picha zake zilipigwa katika mjini wa Ibadan uliopo kwenye jimbo la Oyo kabla ya kurejea Lagos siku chache zilizopita.

No comments:

Post a Comment