KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, August 11, 2012

SIMBA YATISHIA KUMSHTAKI TWITE, BIN KLEB ATAMBA WAMEMALIZA KAZI



KLABU ya Simba imesema itamfikisha mahakamani mchezaji Mbuyu Twite wa klabu ya APR kwa kosa la kuwatapeli na kukubali kusajiliwa na Yanga.

Akizungumza mjini Dar es Salaam leo, mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zakaria Hanspope alisema, Twite alishapokea fedha za Simba na kukubali kuingia nayo mkataba, hivyo hawezi kwenda kinyume.

Hanspope alisema kilichofanywa na Yanga kumshawishi mchezaji huyo arejeshe fedha za Simba na kupokea fedha zao ni cha kihuni na hawawezi kukivumilia.

Alisema kama ni kurejesha fedha zao, anayepaswa kufanya hivyo ni Twite mwenyewe na si klabu ya Yanga.

Hanspope alisema wao waliingia mkataba na Twite kupitia klabu yake ya APR na Shirikisho la Soka la Rwanda, hivyo walipaswa kuomba hati ya uhamisho kutoka Rwanda na si Congo.

"Haya mambo lazima ufike wakati yafikie mwisho. Haiwezekani klabu imesikia kwamba mchezaji amesajiliwa na klabu fulani na yenyewe inamfuata kuzungumza naye,"alisema.

Hanspope alisema bado wanaamini kwamba Twite ni mchezaji wao na kama itatokea vinginevyo, watapambana hadi haki yao ipatikane.

Naye mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, Abdalla Bin Kleb alijigamba kuwa, hawana mjadala wowote na Simba kuhusu Twite kwa vile wamefuata taratibu zote katika kumsajili.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Rwanda leo, Bin Kleb alisema anaashukuru kwamba amekamilisha vyema kazi aliyotumwa na viongozi wenzake na kwamba Twite sasa ni mali ya Yanga.

No comments:

Post a Comment