KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, August 20, 2012

SONG ATUA RASMI BARCELONA





KIUNGO wa kimataifa wa Cameroon na klabu ya Arsenal ya England, Alexander Song amejiunga rasmi na klabu ya Barcelona ya Hispania.

Song aliwasili katika mji wa Barcelona leo baada ya taratibu za uhamisho wake kukamilika, ambapo klabu hiyo imelipa ada ya uhamisho ya pauni milioni 15.

Arsenal haikuwa na kipingamizi kuhusu kuhama kwa kiungo huyo, ambaye ameshafanyiwa vipimo vya afya yake na kufuzu.

Kocha Mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger amekubali kumuuza Song kwa kile anachoamini kuwa, kutoonyesha uwezo mkubwa msimu uliopita.

Hata hivyo, kuna habari kuwa, uamuzi wa Song kuhama umetokana na kushindwa kwake kuelewana na viongozi katika suala la kuboresha mkataba wake.

Song, ambaye alikuwa akilipwa mshahara wa pauni 55,000 kwa wiki, alikuwa amebakiza miaka mitatu kwenye mkataba wake na Arsenal.

No comments:

Post a Comment