KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, August 16, 2012

YAMETIMIA, ROBIN VAN PERSIE ATUA MAN UTD, WENGER ASEMA HAWAKUWA NA UWEZO WA KUMZUIA

Huu ndio utakaokuwa mwonekano mpya wa Robin Van Persie baada ya kutua Man Utd



LONDON, England
KOCHA Mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa, hawakuwa na uwezo ama nguvu ya kumzuia mshambuliaji Robin van Persie kujiunga na Manchester United.
Arsenal ilimuuza Van Persie kwa Manchester United juzi usiku baada ya kufikia makubaliano na Arsenal ya kumuuza kwa kitita cha pauni milioni 24.
Man United imefanikiwa kumnasa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi baada ya majadiliano ya wiki kadhaa na Arsenal pamoja na mchezaji huyo.
Kwa kumsajili Van Persie, Manchester United imezipiku Manchester City na Juventus, ambazo pia zilikuwa zikimwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.
Van Persie alitarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya yake leo kabla ya kumwaga wino kwenye klabu hiyo.
Wenger anatarajiwa kutumia pesa za mauzo ya mchezaji huyo kusajili wachezaji wengine wapya kabla ya kufungwa kwa msimu wa usajili.
Akihojiwa na kituo cha televisheni cha Ufaransa jana, Wenger alisema inasikitisha kupoteza mchezaji mzuri na mwenye kiwango cha juu kama Van Persie, ambaye alikuwa amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake.
Alipoulizwa atasajili wachezaji gani wapya kwa ajili ya kuziba pengo la mchezaji huyo, Wenger aliwataja Lukas Podolski na Olivier Giroud.
Van Persie anakuwa mchezaji wa kwanza wa Arsenal kuhamia Manchester United tangu Viv Anderson alipofanya hivyo mwaka 1987.

No comments:

Post a Comment