
Akizungumza na tovuti ya Simba, Matola alisema lengo lake kwa sasa ni kuhakikisha kwamba anatengeneza vipaji vingi zaidi ili vitumike katika timu ya wakubwa na hivyo kupunguza gharama za usajili.
"Msimu uliopita, wachezaji kama Ramadhani Singano, Edward Christopher, Hassan Khatib, Abdallah Seseme na Frank Sekule walitoka katika kikosi cha vijana na kujiunga na timu ya wakubwa. Mwaka huu, Haruna Chanongo naye amepandishwa na hivyo sisi tuna jukumu la kutafuta wa kuziba nafasi zao," alisema.
Matola ambaye ni miongoni mwa manahodha wa Simba waliotwaa makombe mengi zaidi akiwa mchezaji, sasa ametwaa mataji matatu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita akiwa na kikosi hicho. Vikombe hivyo ni Uhai, Kinesi na Banc ABC
No comments:
Post a Comment