KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, January 1, 2013

BREAKING NEWSSSSSS! SAJUKI AFARIKI DUNIA



MSANII nyota wa filamu nchini, Juma Kilowoko, almaarufu kwa jina la Sajuki, amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Sajuki alikuwa amelazwa kwenye hospitali hiyo wiki iliyopita kutokana na matatizo ya tumbo na pumuna hadi mauti yalipomfika, alikuwa amewekewa mashine ya kumsaidia kupumua.

Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Sajuki alifariki dunia saa moja asubuhi na alifikishwa kwenye hospitali hiyo kutokana na kusumbuliwa zaidi na maumivu ya tumbo.

Mdogo huyo wa marehemu alisema madaktari walishauri Sajuki awekewe mashine ya kumsaidia kupumua kwa saa 10 ili itakapoondolewa aweze kuwa katika hali nzuri.

Alisema baada ya kuondolewa kwa mashine hiyo, iwapo Sajuki angeweza kukaa kwa saa 10 bila kutumia kifaa hicho, angeweza kupelekwa India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Sajuki alipelekwa India mapema mwaka jana kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya tumbo na baada ya kurejea nchini, hali yake ilikuwa nzuri, lakini alipaswa kurejea huko kwa matibabu zaidi.

Hivi karibuni, Sajuki aliandaa maonyesho kwa ajili ya kuwashukuru Watanzania kwa kumsaidia kupata matibabu ya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua. Alifanya maonyesho hayo katika miji ya Iringa na
Arusha.

Akiwa katika onyesho la mjini Arusha, msanii huyo alijikuta akiishiwa nguvu na kudondoka stejini kabla ya kusaidiwa na wasanii wenzake na kupelekwa hospitali.

Jumatatu iliyopita, Sajuki alihojiwa na mtangazaji Salama Jabir katika kipindi cha Mkasi kilichorushwa hewani na kituo cha televisheni cha East Africa, ambapo alielezea kwa kirefu kuhusu maisha yake, ugonjwa unaomsumbua na matarajio yake ya baadaye.

No comments:

Post a Comment