KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, January 22, 2013

WAREMBO MISS UTALII WATEMBELEA UPL

WAREMBO 31 watakaoshiriki katika shindano la kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2013, jana walitembelea katika ofisi za Kampuni ya Uhuru Publications Limited (UPL), inayochapisha magazeti ya Uhuru, Burudani na Mzalendo.

Katika ziara hiyo, warembo hao walijionea kazi mbalimbali za za utayarishaji wa magazeti hayo, zinavyofanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kabla ya kuwafikia wasomaji.

Wakizungumza baada ya ziara hiyo ya mafunzo, warembo hao walisema wamefurahi kutembelea ofisi za UPL kwa vile ndiyo kampuni pekee kongwe ya habari nchini.

Wakati wa ziara hiyo, Msanifu wa Habari wa gazeti la Uhuru, Lilian Timbuka aliwaeleza warembo hao kuwa, gazeti la Uhuru lilianzishwa Desemba 9, 1961.

Lilian pia aliwaeleza warembo hao kuwa, maktaba ya UPL ndiyo kongwe kuliko zote nchini na imekuwa ikihifadhi magazeti ya kampuni hiyo tangu mwaka 1961.

"Hata kwa kuzalisha waandishi wa habari nchini, UPL ndio chimbuko na wanahabari wengi waliopo kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini," Lilian aliwaeleza warembo hao.

Warembo hao ni Rose Edwin, Beatrice Idd, Sophia Yusufu, Ivony Steven, Irene Thomas, Erica Elibariki, Hamisa Jabir, Debora Jacob, Jania Abdul, Mulky Huda, Asha Ramadhan, Zena Alkly, Rosemary Emmanuel.

Wengine ni Ana Posialy, Idan John, Doreen Bukoli, Diana Joachim, Hadija Said, Jesica Peter, Mary Lutta, Halima Hamis, Pauline Mgeni, Anganile Rodgers, Furaha Kinyunyu, Neema Julius, Chrisina Daudi, Lightness Kitua, Flora Msangi, Saraphina Jackson, Magreth Michael na Irene Richard.

Shindano la Miss Utalii limepangwa kufanyika Februari 16 mwaka huu kwenye hoteli ya Lamada mjini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment