KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, January 22, 2013

MOGELLA, MACHO, NKAMIA WAULA SIMBA

KLABU ya Simba imetangaza kuunda kamati mpya nne, ambazo zitashughulikia masuala ya fedha, ufundi, mashindano na programu za vijana.

Katika kamati hizo, wapo wajumbe wapya kadhaa, wakiwemo wanasoka nyota wa zamani wa timu hiyo, Zamoyoni Mogella, Yussuf Macho na Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia.

Wajumbe wengine wapya walioteuliwa kwenye kamati hizo ni pamoja na wanasoka wa zamani,Bita John, John William, Shaaban Baraza,Wilfred Kidau na mmoja wa wakurugenzi wa kituo cha redio cha Clouds FM, Ruge Mutahaba.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, kamati hizo zitaanza kufanyakazi mara moja na zimetakiwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Alisema kamati ya ufundi itaongozwa na Damian Manembe akisaidiwa na Ibrahim Masoud. Wajumbe ni Crescentius Magori, Khalid Abeid, Said Tully, Dr. Kategile, Mogela, William, Macho, Jeff Lea, Bita na Baraza.

Kamati ya fedha itakuwa chini ya Geofrey Nyange 'Kaburu' (mwenyekiti) na Rahma Al Khaloos (makamu mwenyekiti) wakati wajumbe ni Francis Waya, Zitto Kabwe, Nkamia na Ruge.

Kamwaga alisema kamati ya mashindano itakuwa chini ya Swedy Nkwabi (mwenyekiti) akisaidiwa na Said Pamba (makamu Mwenyekiti). Wajumbe ni Seleman Zeddy, Jerry Yambi, Idd Kajuna, Chaurembo, Gerlad Lukumay, Habbib Nassa, Bundala Kabulwa, Charles Hamkah, Said Rubeya, Abdulfatah Salum, Hatibu Mwinyi, Abdul Mshangama, Humprey Zebedayo, Majaliwa Mbassa, Suleiman Zakazaka, Kesi Mohamed na Mohamed Issa.

Alisema kamati ya programu za vijana inaundwa na Ibrahim Masoud (mwenyekiti) na Mutahaba (makamu mwenyekiti). Wajumbe ni Joseph Itang'are (mjumbe/mlezi), Kidau, Said Tully, Canisius Masombola, Hamis Mrisho, Damas Ndumbaro na Talib Hilal.

No comments:

Post a Comment