KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, December 3, 2012

KILIMANJARO STARS, ZANZIBAR HEROES ZATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA CHALENJI


Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakishangilia baada ya kumaliza mechi ya robo fainali ya Kombe la Chalenji dhidi ya Burundi kwenye uwanja wa Lugogo mjini Kampala, Uganda. Zanzibar ilishinda kwa penalti 6-5 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90. (Picha kwa hisani ya blogu ya Bin Zubeiry)


TIMU za soka za Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars na Zanzibar, Zanzibar Heroes zimefuzu kucheza nusu fainali ya michuano ya soka ya Kombe la Chalenji baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Rwanda na Burundi.
Katika mechi hizo za robo fainali zilizochezwa kwenye uwanja wa Lugogo mjini Kampala, Uganda, Kilimanjaro Stars iliichapa Rwanda mabao 2-0 wakati Zanzibar Heroes iliitoa Burundi kwa penalti 6-5.
Kwa matokeo hayo, Zanzibar sasa itacheza na mshindi wa mechi nyingine ya robo fainali kati ya Kenya na Malawi itakayochezwa kesho wakati Kilimanjaro Stars itamenyana na mshindi kati ya wenyeji Uganda na Ethiopia.
Mshambuliaji Abdallah Othman aliibuka shujaa wa Zanzibar Heroes baada ya kuifungia penalti ya mwisho, baada ya kipa Mwadini Ally kupangua penalti ya Abdul Fiston wa Burundi.
Manahodha wa timu zote mbili, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Zanzibar Heroes na Suleiman Ndikumana wa Burundin walipoteza penalti zao leo.
Wafungaji wa penalti za Zanzibar Heroes walikuwa Khamis Mcha ‘Vialli’, Adeyom Saleh Mohamed, Jaku Juma, Samir Hajji Nuhu na Aggrey Morris.
Katika mechi ya kwanza, Kilimanjaro Stars ilijipatia mabao yake kupitia kwa Amri Kiemba kipindi cha kwanza na John Boko katika kipindi cha pili.
Kilimanjaro Stars iliwakilishwa na Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Amri Kiemba, Salum Abubakar/ Athumani Iddi , Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa na John Bocco/Shaaban Nditi.

No comments:

Post a Comment