KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, December 11, 2012

COASTAL UNION YAANZA VIZURI KOMBE LA UHAI




Coastal Union ya Tanga imeanza vizuri michuano ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuifunga Tanzania Prisons mabao 2-1.
Mechi hiyo ya kundi A ilichezwa jana asubuhi (Desemba 11 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Coastal Union ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa tayari imepachika mabao hayo yaliyofungwa dakika ya 24 na 33 kupitia kwa Ramadhan Same na Yusuf Chuma.
Tanzania Prisons, ambayo itacheza mechi yake pili leo jioni (Desemba 12 mwaka huu) Uwanja wa Azam ulioko Chamazi dhidi ya JKT Ruvu ilipata bao lake dakika moja kabla ya filimbi ya mwisho.
Mechi nyingine za leo ni Toto Africans dhidi ya Coastal Union itakayochezwa saa 2 asubuhi Uwanja wa Azam. Katika kundi B, Simba na African Lyon zitaoneshana kazi asubuhi Uwanja wa Karume wakati Azam na Polisi Morogoro zitacheza saa 10 jioni kwenye uwanja huo huo.
Kundi C leo ni Kagera Sugar vs Oljoro JKT saa 2 asubuhi Uwanja wa Karume, na Yanga na Ruvu Shooting zitaumana saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam.

No comments:

Post a Comment