KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, December 4, 2012

KENYA YAIFUATA ZANZIBAR HEROES, UGANDA YAIITA KILIMANJARO STARS




MABINGWA watetezi Uganda na jirani zao wa Kenya leo wamefuzu kucheza nusu fainali ya michuano ya soka ya Kombe la Chalenji baada ya kuzitoa Ethiopia na Malawi.
Katika mechi hizo zilizochezwa kwenye Uwanja wa Namboole mjini Kampala, Kenya iliichapa Malawi bao 1-0 wakati Uganda iliicharaza Ethiopia mabao 2-0.
Kwa matokeo hayo, Kenya sasa itakutana na Zanzibar Heroes katika mechi ya kwanza ya nusu fainali itakayochezwa keshokutwa na kufuatiwa na pambano kati ya Uganda na Kilimanjaro Heroes.
Mshambuliaji Mike Barasa ndiye aliyeivusha Kenya hatua ya nusu fainali baada ya kuifungia bao la pekee na la ushindi dakika ya 56,
Wakati huo huo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ametuma salamu za pongezi kwa timu ya Zanzibar Heroes kwa kufanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya kombe la challenge.
Zanzibar Heroes imeingia hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Burundi kwa mikwaju ya penalti (6-5) kwenye uwanja wa Lugogo mjini Kampala, Uganda kufuatia timu hizo kutoka sare ya bila kufungana katika dakika zote 90 za mchezo.
Katika salamu hizo, Maalim Seif alisema Zanzibar Heroes wanaendelea kudhihirisha uwezo wa Zanzibar wa kushiriki katika mashindano ya kimataifa.
Ameitaka timu ya Zanzibar Heroes kuongeza juhudi katika mchezo wake wa nusu fainali ili kuendeleza ushindi wake na hatimaye kuweza kutwaa Kombe hilo la Challenge katika msimu huu.

No comments:

Post a Comment