KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, December 27, 2012

YANGA YAPIGWA KIMOJA NA TUSKER



WENYEJI Yanga jana walipigwa mweleka wa bao 1-0 na mabingwa wa soka wa Kenya, Tusker katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo ilikuwa ya kuwaaga mashabiki kwa Yanga, ambayo keshokutwa inatarajiwa kukwaa pipa kwenda Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya mechi za mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

Bao pekee na la ushindi la Tusker lilifungwa na mshambuliaji Ismail Dunga kwa njia ya penalti dakika ya 44 baada ya kiungo, Nurdin Bakari wa Yanga kumuangusha Khalid Aucho ndani ya eneo la hatari.

Katika mechi hiyo iliyohudhuriwa na mashabiki wachache, Yanga ilicheza vizuri vipindi vyote viwili na kufanya mabadiliko kadhaa ya wachezaji, lakini ilishindwa kutengeneza nafasi za kufunga mabao.



No comments:

Post a Comment